Sina uhakika kama unafahamu kwamba Dr Wilbroad Slaa alikuwa Padri wa Kanisa Katoliki, na kwa miaka 10 au zaidi alikuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC). Hiyo PhD aliyo nayo ni ya sheria za Kanisa (Canon Law). Ukifuatilia hatua za kupata upadri katika Kanisa Katoliki utakubaliana nami kwamba Kanisa hili lina utaratibu wa kujikusanyia hazina kubwa ya watu wenye uwezo mkubwa kiakili, na wote wanaofikia hatua ya kuwa Padri wana uwezo wa kufanya PhD na zaidi. Masomo wanayofanya katika Seminari Kuu (Philosophy na Theology) ni sawa kabisa na universities kwa shahada ya kwanza na ya pili, ingawa baadhi ya seminari hizo huwa haziwapi shahada hizo (kwa sababu za ukiritimba na kuogopa kuwa wakipata sifa kubwa watatoroka, labda). Sababu nyingine za kuwanyima shahada japo wamesoma sawa na (au zaidi ya) wenye shahada ni lile dai la kwamba kitu cha muhimu kwa Padri ni lile daraja/sakramenti ya upadrisho ambayo hutolewa na Askofu, na wala si cheti kikubwa! Na kwa kuwa mapadri huweka nadhiri (vows) ya utii, inabidi wakubaliane na hali hiyo. Lakini akishafanya kazi na kuaminiwa zaidi na Askofu, basi hapo Padri anaweza kupewa nafasi ya kwenda kupata shahada zake, na huwa wanafanya masomo kuendana na kipaji chake na mahitaji ya Kanisa kwa wakati huo kama itakavyoamuliwa na Askofu, na ndipo atakaposoma hadi kufanya hizo PhD nk. Kwa kufuata nadhiri ya utii, Padri hata mwenye PhD anaweza kupangiwa kazi yoyote na Askofu wake, na haruhusiwi kukataa. Kwa mfano, Askofu anaweza kumpangia padri huyo kazi ya kutunza accounts, na kama atasema hana taaluma hiyo, atatumwa akasome(ndio maana unaweza kumkuta Padri mwenye umri wa miaka 50 au zaidi, anasomea cheti cha accounts technician, na usishangae ukakuta huyo ana PhD ya fani fulani, labda Lingustics au Sociology) .
Hiyo inaweza kuwa possible explanation ya Dr Slaa kusoma Advanced Diploma (sijui ya nini) wakati alishafanya PhD. Wanaomfahamu zaidi (au yeye mwenyewe) wanaweza kutoa maelezo specific zaidi, lakini mimi nimetoa maelezo ya jumla yanayowahusu watu walioko au waliopitia mkondo huo wa Upadri katika Kanisa Katoliki. Natumaini kwa kiasi fulani nimekidhi kiu ama shauku yako ndugu Kingwele.