Hongera Rais Magufuli kuipendezesha Ikulu yetu kuliko enzi za Nyerere, Ikulu iwe kivutio cha utalii, restrictions ziondolewe watalii wafurike

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,498
113,601
Wanabodi,

Leo kuna video clip ya Ikulu yetu ya Magogoni imepandisha humu, kiukweli nimekuwa very impressed na ile zoo ya Ikulu na jinsi wanyama walivyopendezea.

Kwenye mazuri wajameni tupongeze: Wanyama pori waipamba Ikulu, Hongera sana Rais Magufuli

Nimesema kwa upande wa wanyama pori, rais Magufuli, ameipendezesha sana Ikulu yetu kuliko hata enzi za Nyerere, kwasababu wanyama Ikulu walikuwepo tangu enzi za Nyerere, kufuatia Ikulu kuwa na a limited surface area na wild animals natural habitat yao ni wilderness, ikaamuliwa wawepo wanyama wachache tuu for leisure kwa rais na wageni wake wakiwemo ndege tausi ambao sasa Ikulu ndio natural habitat yao.

Wild animals enjoys wilderness, bila kuwa na mazingira ya natural habitat yao, wild animals hawawezi ku breed, hivyo kuweka idadi kubwa hivyo ya wanyama kwenye kieneo kidogo kile ni furaha pendeza macho lakini mateso kwa baadhi yao, maana matting ni moja ya haki za msingi za wanyama, sijui. kama Tanzanzia bado chama kinachoitwa TSPCA!, kumbe domestication of wild animals sasa sio just for leisure, sasa ni kuonyeshea!, hivyo na kwa vile serikali imehamia Dodoma, napendekeza Ikulu iwe Magogoni Zoo, na kwa heshima ya Magufuli, napendekeza Rais Magufuli akae Ikulu muda kama wa Nyerere au zaidi hadi pale Mungu atakapoamua!.

Tena unaweza kukuta uamuzi wa kufuga wanyama wengi hivyo kwenye eneo dogo lile, umefanyika bila EIA, kama tulivyoamua kununua ndege kwa cash huku hatuna business plan!. Sasa tuifanye Ikulu yetu kuwa kivutio cha utalii, vile vizuizi viondolewe, waweke nominal fee watalii hadi wa ndani tutafurika.

Ni muhimu sana rais Magufuli afanye safari muhimu za nje sio tuu kukutana na wenzake, bali pia kupata exposure, akaone Ikulu za wenzake, mfano Ikulu ya South inavyofurika, watalii. Pia aende Ikulu ya White House tena akiandamana na Makonda ili kumkomoa beberu Pompeo!, akaone jinsi wageni wanavyo jivinjari kwenye Ikulu ya White house ya Marekani. Hao wanyama na all the beauty ni bure kama watu hawatatembelea na kuchangia the upkeep cost. JPM angekuwa na exposure kubwa, asinge jenga Ikulu mpya ya Chamwino kwa replica ya magofu ya makao makuu ya Uislamu!. Kwa vile ni modern building, angejenga kitu ultra modern structures watu waseme wow!. JPM angeijua historia halisi ya majengo ya Ikulu ya Magogoni, asingethubutu kurudia kosa hilo Ikulu ya Chamwino, kuna karma ya majengo, itaifanya Ikulu ya Chamwino kuwa a haunted house bila yeye kujijua!. Siku zote matokeo ya kuishi a hounted house bila kujijua, hao invisible occupants wa hauted house, from time to time, huhitaji kuwekewa chakula fulani mezani kwao, ikitokea mpangaji wa nyumba hiyo akashindwa kupeleka chakula yao, mezani kwao, then huwezi hata kumgeza yeye ndio chakula hivyo kuletwa mezani, kwa hao majamaa kula kichwa cha the occupier!.
There must ne a good reasons besides fish smell iliyomfanya Mwalimu Nyerere kulikimbia lile mansion pale Ikulu na kuishi kwenye ile humble residence yake ya Msasani!.

Na kama hoja ya restrictions ni usalama wa rais, maana naona ulizi wake wa sasa, unakaribiana na ulinzi wa Mu7!, then Ikulu Zoo iwe open to public zile siku rais yuko Dodoma ambapo pia I hope kutakuwa na Chamwino Zoo. Kiukweli ita-make a lot of sense kuliko hata ile ikulu ya Chato!.

Hongera sana Rais Magufuli kwa kuendelea kumuishi Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere kwa maneno na matendo, pia tunakuombea utawale kwa muda kama wa Nyerere au kwa kukaribiana tu japo vipindi viwili vya miaka 10/10.

P
 
Orodha ya Maraisi wa JMTZ kwa ubora;

1.Mzee Mwinyi
1.Raisi Magufuli
2.Mwalimu Nyerere
3.Mzee Kikwete
4.Mzee Mkapa ( Mkapa ameshuka kuwa wa mwisho sababu ya ubinafsishwaji wa mashirika yetu, kuuza nyumba zetu, Mikataba mibovu ya Madini, Mke wake ktk KLM, mauaji ya Mwembechai na Pemba, ... vinginevyo angeweza kupanda)
 
Pongezi ni nzuri lkn ukakasi unakuja pale unasema kuliko enzi za fulani. Kila enzi huwa na maboresho yake ,hata enzi za mawe hazikufanana, kulikuwa na early stone age, middle na baadaye late stone age.
Katika zote hizo kila moja ilikuwa bora zaidi ya iliyotangulia.

Huu ukakasi una implications za biasness, that's not good at all.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii clip si bure kuna namna....unatumwa ujumbe mahali!! Nawapongeza wahusika wa ikulu kwa kushirikiana na wizara ya maliasili na utalii bila kuisahau wizara ya mambo ya usafirishaji kwa kufanikisha jambo hili.
 
Ikulu bado ipo Dar?kuna kuhama kweli ? Kama ndo na Zebra,swala wameletwa Dar. Hii serikali ina vituko sijawahi ona. Ikulu imekuwa Zoo sasa.
Mkuu ukweli kama umekulia Dar au umeishi miaka mingi utajua Ikulu kuna wanyama miaka mingi kabla ya Magufuli kuwa raisi au pengine kabla ya kuwa Mbunge.

Sema raisi waliomtangulia hatukuwaona wakiwa ktk picha wanahudumia wanyama au wana watazama kama kujifurahisha wakiwa pale Ikulu.
 
Back
Top Bottom