Exposure ni kuona tu au ni kuona na kujifunza? Mbona tunasafiri sana, tunaona mazuri ya wenzetu, lakini hatujifunzi na hatubadiliki? Tumeridhika?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,499
113,610
Wanabodi

Kuna huu msemo kuona ni kuamini na ni kujifunza!. Je, Tanzania sasa tuanze kuwa tunajifunza mambo mazuri ya wenzetu tunayoyaona kupitia exposure mbalimbali kwenye ziara za Mhe Rais wetu, nje ya nchi?. Je tuige mazuri ya wenzetu yatatusaidia au sisi ni sisi na wao ni wao?

Hoja hii ni kufuatia ziara ya Rais Samia nchini Indonesia ambapo JF imekuwa ndio media ya kwanza kutuletea live ya ziara hiyo kabla hata ya TV yoyote ya Tanzania, kabla hata ya Ikulu Mawasiliano

Mimi ni miongoni mwa waandishi wa habari tulioshiriki ziara nyingi za rais wetu nje ya nchi. Moja ya faida kubwa za kusafiri ni kupata kitu kinachoitwa exposure, mtu unakuwa exposed kwenye mazingira tofauti tofauti, na hii exposure inapatikaka kwa kutembelea eneo husika, na kuona, ambapo sio tuu kuona ni kuamini bali kuona ni kujifunza.

Kwenye ziara za wenzetu tunaona jinsi wenzetu wana ongoza misafara ya viongozi, hakuna mambo ya kufunga barabara saa nzima rais anapita au kuna msafara wa viongozi, Misafara ya viongozi inachosha, inatesa na kurudisha nyuma maendeleo, IGP Sirro peleka Traffic Sweden kujifunza misafara ya wenzetu, Time is Money!

Tukiwa nchini Sweden, Rais Mkapa na msafara wake wote tukiwemo sisi waandishi wa habari, tulipandishwa basi moja!, Hakuna ubaya wowote wala ajabu yoyote Marais kupanda pamoja! Tulipanda basi moja na Rais Mkapa nchini Sweden sisi ikifanyika event mahali, Waziri, KM, Wakurugenzi, kila mmoja anakuja na VX lake na dereva wake!

Marais wetu huwa wakuwa na walinzi na ADC na msafara wa watu kibao, leo nchi Indonesia, nimemshuhudia Rais Samia na mwenyeji wake tuu, wao peke yao, hakuna cha mlinzi wale ADC!.

Viongozi wetu wawapo kwenye security cleared area kama Ikulu, walinzi na ADC wanamzonga wa nini?!.

Hebu Shuhudia

726477d8-86eb-445c-a00c-303a87abfc89.jpeg

Shuhudia Mgeni na mwenyeji tu, hakuna majeshi nyuma wala ADC!

603864d5-d68a-4022-a691-0edf739f73ce.jpeg

Wawili peke yao!
e9d87279-6960-4676-9a2c-40c8c9bab991.jpeg

Wawili pekee yao
eb71c696-c522-48b2-9e8d-645423ee7dc9.jpeg

Wawili pekee yao
67c079cf-fd0c-4ac4-b290-db4c5148ddd1.jpeg

Wawili pekee yao

Kiti kingine nimekinote Ikulu ya Indonesia ni wingi wa wanyama mwetu, zoo!. Nilimpongeza Rais Magufuli kuipendezesha Ikulu yetu Hongera Rais Magufuli kuipendezesha Ikulu yetu kuliko enzi za Nyerere, Ikulu iwe kivutio cha utalii, restrictions ziondolewe watalii wafurike hapo nililaumu wanyama ni wengi!, nilichoshuhudia Ikulu ya Indonesia, kiukweli Ikulu yetu ni kama haina mnyama!

Hitimisho
Je, Tanzania sasa tuanze kuwa tunajifunza mambo mazuri ya wenzetu tunayoyaona kupitia exposure mbalimbali kwenye ziara za Mhe Rais wetu, nje ya nchi? Je, tuige mazuri ya wenzetu yatatusaidia au sisi ni sisi na wao ni wao? Tuendelee kusafiri na kuyaona mazuri ya wenzetu, na kuacha huko huko, tukirudi tuendelee na yetu kwasababu wao ni wao na sisi ni sisi kila mtu kivyake vyake?

Hiki kitu kinachoitwa exposure faida yake ni kuona tu au ni kuona na kujifunza? Mbona tunasafiri sana, tunapata exposure kubwa, tunaona mazuri ya wenzetu na the way they do things, lakini mbona ni kama hatujifunzi? na kama tuna jifunza, mbona kama bado hatubadiliki the way we do some of our things?au sisi tumeridhika hivi ndivyo sisi tulivyo, wao ni wao na sisi ni sisi?

Paskali
 
Wao ni wao na sisi ni sisi.
Sometimes kutojifunza vitu ni strategy nzuri ya ku survive au kuto survive.

Kusema kweli Kwa spidi ya Dunia na technology inavoenda Kwa kasi na madhara yake yashaonekana mi sometimes naona Bora tanzania tuishi hivi hivi na tuwe washamba hivi hivi tu kama tupo Karne ya 20 kuliko kukimbilia hiyo UTopian world tunayoaminishwa.

Kwa kutembea sana I learn to appreciate ushamba wetu na umaskini wetu mybe huo Ushamba na ujinga wetu unaweza ukatusaidia siku Moja.
 
Unapoweka akili yako tumboni huwezi kujifunza kwa kuwa kila wakati unawaza kumfurahisha na kumwimbia mapambio huyo mfadhili wako.

Wengi wa wanaoambatana na viongozi katika ziara zao ni machawa ambao kwao critical thinking ni mbingu na ardhi. Hivyo hawawezi kutoa ushauri wala kupinga hoja yo yote kutoka kwa viongozi.

Tanzania tuna safari ndefu sana katika kujikomboa kifikra na bahati mbaya watoto na vijana wetu wanapata mafunzo kutoka kwa hao machawa kwa kuwaaminisha uzalendo ni kuwaamini viongozi bila ukomo.
 
Sisi hatuna viongozi tuna Wanasiasa. Wanasiasa huwa wanawaza uchaguzi na siyo maendeleo.Kwaiyo Wanasiasa wa Tanzania huwa wanaenda kutalii kwasababu starehe ni moja ya vitu vinavyovipenda sana. Viongozi tuliobahatika kuwapata tangu Uhuru ni Mwalimu Nyerere na Dkt. Magufuli; hawa walikuwa na vision na ndiyo maana ata waliyoyafanya yanaonekana wala uhitaji kuoneshwa!
 
Siku zote anayejifunza ni yule anayejishusha mbele ya mwalimu, ukienda kwa mbwembwe mbele ya mwalimu hautajifunza lolote zaidi ya mwalimu kukujazia sifa zisizo na maana. Simama mbele ya mwalimu wako akuone ni mtu mwenye shida umekwenda kwake akueleze siri ya mafanikio yake, usisimame mbele yake ukimwambia mtabadilishana ujuzi! Indonesia na Tanzania tulikuwa darasa moja deski moja mwalimu mmoja, thamani ya pesa yao yetu na ya uingereza miaka mpaka miaka ya sitini ilikuwa moja lakini walijifunza kutoka kwa wajuzi na wakafanikiwa maradufu huku sisi tukijisifu kwa mafanikio zaidi yao! Tumeupiga mwingi.

Kwa mfumo wetu wa kutopenda kuitumia katiba na kuamua kuiendesha nchi kichama tukipendana kwa wanaoharibu mambo kisa tu ni wenzetu tutamaliza awamu zote za dunia bila mafanikio zaidi ya kupeana udakitari pasipo kutibu maradhi.
 
Unapoweka akili yako tumboni huwezi kujifunza kwa kuwa kila wakati unawaza kumfurahisha na kumwimbia mapambio huyo mfadhili wako.

Wengi wa wanaoambatana na viongozi katika ziara zao ni machawa ambao kwao critical thinking ni mbingu na ardhi. Hivyo hawawezi kutoa ushauri wala kupinga hoja yo yote kutoka kwa viongozi.

Tanzania tuna safari ndefu sana katika kujikomboa kifikra na bahati mbaya watoto na vijana wetu wanapata mafunzo kutoka kwa hao machawa kwa kuwaaminisha uzalendo ni kuwaamini viongozi bila ukomo.
Zamani nilikua nataka Tanzania tujikomboe kifikra ila Kwa Sasa nimeamua kuipenda hivo hivo bila kutamani chochote kutoka kwake,ni kama uzae mtoto mlemavu ambae yupo kitandani mda wote mwisho wa siku hutamani Tena apone unajifunza kumkubali Hali yake na kumpenda hivo hivo.
 
Siku zote anayejifunza ni yule anayejishusha mbele ya mwalimu, ukienda kwa mbwembwe mbele ya mwalimu hautajifunza lolote zaidi ya mwalimu kukujazia sifa zisizo na maana. Simama mbele ya mwalimu wako akuone ni mtu mwenye shida umekwenda kwake akueleze siri ya mafanikio yake, usisimame mbele yake ukimwambia mtabadilishana ujuzi! Indonesia na Tanzania tulikuwa darasa moja deski moja mwalimu mmoja, thamani ya pesa yao yetu na ya uingereza miaka mpaka miaka ya sitini ilikuwa moja lakini walijifunza kutoka kwa wajuzi na wakafanikiwa maradufu huku sisi tukijisifu kwa mafanikio zaidi yao! Tumeupiga mwingi.
Kwa mfumo wetu wa kutopenda kuitumia katiba na kuamua kuiendesha nchi kichama tukipendana kwa wanaoharibu mambo kisa tu ni wenzetu tutamaliza awamu zote za dunia bila mafanikio zaidi ya kupeana udakitari pasipo kutibu maradhi.

Na Bado hatujifunzi,it's like tumeumbwa hivo,it's on our DNA. Huwezi kutubadilisha ni impossible.

Yaani matatizo yetu waTz ni sio sisi au viongozi wetu. Ndio tulivoumbwa na hakuna mtu au kiongozi atatubadilsha. Mybe itokee mbeleni technogia ya kubadilisha DNA ya mtu halafu watanzania wote tubadilishwe ndio tutabadilika.
 
Mkuu

Katiba mbovu inayompa mamlaka makubwa Rais inamfanya Raise kufanya maovu ikiwemo mikataba ya wizi na ubadhirifu kwahio Raise anakua na hofu kubwa sana unaotokana na wasiwasi wa uovu wake lazima awe na ulinzi na kampany ya watu wengi!!

Sasa bas,katiba mpya ikipatikana tu Rais atakuwa chini ya uangalizi was kila kitu na uadilifu hatokua na hofu ya uovu wake kwasababu haupo kabisa!!

Utaona hayo unayoshuhudia huko ughaibuni!!
 
low IQ haina uwezo wa kujifunza chochote na ndiyo maana IQ test ilikuwa developed ili kuchuja, maadamu tanzagiza haifwati meritocracy hakuna kitakachobadilka mtaishi kuwinda wanyarwanda tu kwa wivu, linchi likuubwa linaogopa kanchi kama mkoa …
 
Wao ni wao na sisi ni sisi.
Sometimes kutojifunza vitu ni strategy nzuri ya ku survive au kuto survive.

Kusema kweli Kwa spidi ya Dunia na technology inavoenda Kwa kasi na madhara yake yashaonekana mi sometimes naona Bora tanzania tuishi hivi hivi na tuwe washamba hivi hivi tu kama tupo Karne ya 20 kuliko kukimbilia hiyo UTopian world tunayoaminishwa.

Kwa kutembea sana I learn to appreciate ushamba wetu na umaskini wetu mybe huo Ushamba na ujinga wetu unaweza ukatusaidia siku Moja.
Sio kweli. Ndio maana tunaona fahari kujiibia wenyewe na kufikiria tunamuibia mtu mwingine. Ndio maana tunafikiria tuaajiriwe ili tukapige deals badala ya kufanya kazi za kuleta maendeleo.
Ndio maana mpaka leo kipindupindu na unyafuzi ni magonjwa yanayosumbua jamii yetu. Anayedharau elimu rasmi au mbadala ni mtu wa chini kabisa ambaye anatakiwa aogopwe kama ukoma
 
Na Bado hatujifunzi,it's like tumeumbwa hivo,it's on our DNA. Huwezi kutubadilisha ni impossible.

Yaani matatizo yetu waTz ni sio sisi au viongozi wetu. Ndio tulivoumbwa na hakuna mtu au kiongozi atatubadilsha. Mybe itokee mbeleni technogia ya kubadilisha DNA ya mtu halafu watanzania wote tubadilishwe ndio tutabadilika.
Hebu Waweke mbele yako viongozi wote wa CCM anza kumpima kila mmoja uwezo wake kisiasa na kielimu. Angalizo, usihusishe undugu au uchama, utapata jibu kwanini hatuendelei.
 
Sio kweli. Ndio maana tunaona fahari kujiibia wenyewe na kufikiria tunamuibia mtu mwingine. Ndio maana tunafikiria tuaajiriwe ili tukapige deals badala ya kufanya kazi za kuleta maendeleo.
Ndio maana mpaka leo kipindupindu na unyafuzi ni magonjwa yanayosumbua jamii yetu. Anayedharau elimu rasmi au mbadala ni mtu wa chini kabisa ambaye anatakiwa aogopwe kama ukoma
Ni vitu ambavo tumeshindwa kujibadilisha. Tushaongea na kupambana navyo sana mwisho wa siku unaamua kukubali kua ujinga wetu ni vitu nje ya uwezo wetu,it's on our DNA bro! You can't change it and nobody can. The universe before being created mungu alikua anajua Kuna a small part in the world people will be dumb, incompetent and lazy and it's obvious. waTz Wana trauma nyingi na wenyewe washaridhika nazo na kuzikubali kama part of their life.
 
Viongozi tuliobahatika kuwapata tangu Uhuru ni Mwalimu Nyerere na Dkt.Magufuli;hawa walikuwa na vision na ndiyo maana ata waliyoyafanya yanaonekana wala uhitaji kuoneshwa!
Acheni dharau. sijui umri wako. Yaani Magufuli alikuwa na vision kumzidi Mkapa? Hivi unajuwa kuwa Tanzania Development Vision 2025 iliandikwa mwaka 2000 wakati Mkapa ndiye Rais? hivi unajuwa kuwa takriban 90% ya projects na mambo yaliyotekelezwa na Kikwette, Magufuli na sasa Samia yanatoka kwenye hiyo Blueprint? Nimeamini Magufuli alwapumbaza sana wajinga
 
Back
Top Bottom