Hoja ya Shossi juu ya sh. 500/- ya babu

Hoja ya Shossi juu ya sh. 500/- ya babu

Haina maana mimi tu ndio nitumie hapana.
Wala hatutakiwi kumkubali kirahisi tu kwa sababu alikuwa Mchungaji na Wachungaji wamemkubali.
Atumie jina la Yesu, lakini afundishe watu, waelewe na kumkubali Bwana Yesu, kama bwana na Mwokozi wa Maisha yao.
Awafundishe kuabudu katika jina la Yesu, halafu awape dawa wa pone.
Inakuwaje unamwambia mtu nimekuponya kwa jina Yesu anaondoka wala hasemi habari za Yesu anasema habari za Kikombe na Babu mwenyewe.

Hayo ni maswli ambayo yananifanya nishindwe kuikubali na kuiamnini.
Kwa upande mwingine, Njia za Mungu zipo nyingi, kutokana na hilo ndo maana na sema TUOMBE UKWELI UJULIKANE.
Yawezekana mmenilewa vibaya au nimejieleza vibaya hapo juu, ila lengo langu ni kwamba. NIngemwelewa Babu kama asingemhusisha Mungu kwa Jina la Yesu, katika hiyo dawa yake, ikajulikana tu kuna Dawa imegunduliwa na babu inaponya watu, wa DINI zote, kabila zote, na Rangi zote, iwe unamwamini Yesu au humwamini pia. We amini kikombe na Babu mwenyewe basi.

Unaposema Kikombe kina ponya kwa jina La Yesu, wakati kuna watu hawataki kulisikia hata hilo jina la Yesu, lakini wanakwenda kwa sababu ya magonjwa na Mateso tu, mimi nakuwa sielewe. Ndio maana nikasema Basi yeye atibu tu, kwa mti na maji kama hana nafasi ya kufundisha habari za Yesu aache kulitumia hilo jina.

Tuendelee kuweka Imani yetu, kwenye Hayo maji na huo mti.
Mbarikiwe.

Babu hawezi kuacha kulitumia jina la YESU kwakuwa tu kuna watu hawapendi kulisikia, na wasiopenda kusikia jina la YESU likitajwa wakokila mahali si kwa babu wa loiondo pekee.

Isitoshe watu wasiopenda kulisikia jina la YESU likitajwa na babu wa loliodo ni pamoja na wewe. Yesu alipomuamuru mkoma akajitose mto jordani mara saba hakuacha kulitaja jina la Mungu baba,vinginevyo YESU angeendelea tu kuponya watu pasipo kutaja jina la Mungu kwa kuwa wengine walikuwa hawamjui Mungu bali walisukumwa na mateso ya magonjwa waliyokuwa nayo.
 
  • Thanks
Reactions: CPU
Nimesema hivyo ktk msingi na mtazamo huo hapo juu.
Si unajua kuwa 50/50 eeh, sasa ndo mimi!!! Labda niseme hivyo.

Kama uko 50/50 uko kwenye hatari kubwa sana, kwa maana nyingine wewe ni vuguvugu.

Nadhani unakumbuka maandiko matakatifu yanatuonya tusiwe vugu vugu, ni bora kuwa baridi au moto, vinginevyo utatapikwa,.........
 
Hili lakutenda dhambi linawahusu ambao hawajamjua Mungu ukisha kuwa mtoto wa Mungu trait ya dhambi inaondoka unabaki kuwa sawa na Mungu yaani born again in spirit,

Tunakuwa watoto wa Mungu (Joh 1:12). Mungu atabakia kuwa Mungu pekee hakuna mwingine kama yeye. Amen

dhambi haina tena dominion juu yako na neema ya kuishinda ni kubwa sana kama vile mtu mzima kula mavi haiwezekani na akiweza ujue basi akili ishamruka. Kama uko born again na bado dhambi inakutawala rudi magotini omba neema ya Mungu akujaze roho mtakatifu maana unajidanganya wala Yesu hakujui maana wote waliompokea aliwapa nguvu ya kuwa wana wamungu na hivyo ndivyo tulivyo. Je Mungu anatenda dhambi? Je Yesu alishawahi kutenda dhambi?

kama unaamini Mungu wala Yesu hawawezi tenda vipi basi mtoto wa Mungu atende dhambi? Yesu ni mtoto wa kwanza wa Mungu na baadaye kina Paulo na mitume kumi na mbili na wenginewaliokuwa Yerusalem siku ya Pentekoste wakawa wazaliwa wa pili nasi tukazaliwa baadaye na bado wengine wanaendelea kuzaliwa kila siku wanapoyatoa maisha yao kwa kristo.

Ubarikiwe mpendwa kasome tena kitabu cha matendo ya mitume na waraka wa Paulo kwa warumi then soma waraka wa Petro uone nini nazungumza.

Ni kweli tukisha mkaribisha Yesu (yaani kumkubali kuwa bwana na mwokozi wetu) dhambi haina nguvu kwasababu roho wa Mungu anakaa ndani yetu. Mungu akuzidishie.
 
Kama uko 50/50 uko kwenye hatari kubwa sana, kwa maana nyingine wewe ni vuguvugu.

Nadhani unakumbuka maandiko matakatifu yanatuonya tusiwe vugu vugu, ni bora kuwa baridi au moto, vinginevyo utatapikwa,.........

Ndio maana naomba kwa bidii ili Mungu anipe kuifahamu kweli na hiyo kweli iniweke huru.
Mungu sio dhalimu, na ameruhusi tuhojiane naye, kwa hiyo sina mashaka na Mungu. Najua wakati wake ukifika atahukumu kwa haki,
Nitajua ukweli ni upi katika mambo haya.
Barikiwa sana!!!
 
Sorry to take you guys back to the Title of the thread.

In my opinion MOH'D SHOSSI'S VIEWS were meant TO MOCK THE VERY BELIEVERS WHO ARE ARGUING HERE.

It is ridiculous for true believers to keep arguing over the mockery for several pages.

Spiritually, the time spent arguing in here could have been better spent praying for the sick, non-believers and people who are suffering all over the world.
 
Acha hizo CPU,
Vita vyetu si vya DAMU NA NYAMA.
We omba tu.

LD kuna sehemu nimesema hivyo vita ni vya Damu na Nyama?? Au unapindisha makusudi??
Mimi nitaendelea kuomba na kumwombea na Babu pia hata kama wewe hauna imani na uchungaji wake, aendelee kuwezeshwa na Mungu ktk kazi yake. Sitabagua wa kumuombea.

Sisi tutaendelea kumuombea awezeshwe zaidi na hata waliopata dawa yake nao waponywe magonjwa yao
 
Babu hawezi kuacha kulitumia jina la YESU kwakuwa tu kuna watu hawapendi kulisikia, na wasiopenda kusikia jina la YESU likitajwa wakokila mahali si kwa babu wa loiondo pekee.

Isitoshe watu wasiopenda kulisikia jina la YESU likitajwa na babu wa loliodo ni pamoja na wewe. Yesu alipomuamuru mkoma akajitose mto jordani mara saba hakuacha kulitaja jina la Mungu baba,vinginevyo YESU angeendelea tu kuponya watu pasipo kutaja jina la Mungu kwa kuwa wengine walikuwa hawamjui Mungu bali walisukumwa na mateso ya magonjwa waliyokuwa nayo.

Nena Mkuu watu wapate kuelewa kwamba
Hakuna binadamu mwenye mamlaka ya kuzuia mwenzake asitumie jina la Yesu.
 
Haina maana mimi tu ndio nitumie hapana.
Wala hatutakiwi kumkubali kirahisi tu kwa sababu alikuwa Mchungaji na Wachungaji wamemkubali.
Atumie jina la Yesu, lakini afundishe watu, waelewe na kumkubali Bwana Yesu, kama bwana na Mwokozi wa Maisha yao.
Awafundishe kuabudu katika jina la Yesu, halafu awape dawa wa pone.
Inakuwaje unamwambia mtu nimekuponya kwa jina Yesu anaondoka wala hasemi habari za Yesu anasema habari za Kikombe na Babu mwenyewe.

Hayo ni maswli ambayo yananifanya nishindwe kuikubali na kuiamnini.
Kwa upande mwingine, Njia za Mungu zipo nyingi, kutokana na hilo ndo maana na sema TUOMBE UKWELI UJULIKANE.
Yawezekana mmenilewa vibaya au nimejieleza vibaya hapo juu, ila lengo langu ni kwamba. NIngemwelewa Babu kama asingemhusisha Mungu kwa Jina la Yesu, katika hiyo dawa yake, ikajulikana tu kuna Dawa imegunduliwa na babu inaponya watu, wa DINI zote, kabila zote, na Rangi zote, iwe unamwamini Yesu au humwamini pia. We amini kikombe na Babu mwenyewe basi.

Unaposema Kikombe kina ponya kwa jina La Yesu, wakati kuna watu hawataki kulisikia hata hilo jina la Yesu, lakini wanakwenda kwa sababu ya magonjwa na Mateso tu, mimi nakuwa sielewe. Ndio maana nikasema Basi yeye atibu tu, kwa mti na maji kama hana nafasi ya kufundisha habari za Yesu aache kulitumia hilo jina.

Tuendelee kuweka Imani yetu, kwenye Hayo maji na huo mti.
Mbarikiwe.

Dadangu unakubali na kukataa at the same time.
Lakini afundishe watu.....Halafu awape dawa wapone = unataka afanye tulivyozoea kana kwamba job description yake tulimtengenezea sisi na sio aliyemtuma. Uzuri unakumbuka kwamba Kwa upande mwingine njia za Mungu zipo nyingi.

Kuna muhubiri mmoja yupo Marekani anaitwa Bill Graham yeye anahubiri tu haombei wagonjwa hata siku moja. Yeye anasema hakupewa karama hiyo sasa si kila uponyaji unatakiwa uambatane na formal preaching.
Yule kipofu aliyeponywa na Yesu hakuhubiriwa kwanza lakini alisema "Kwamba ni mwenye dhambi mimi sijui lakini kitu kimoja najua: Nilikuwa kipofu lakini sasa naona. (John 9:25).

Kama kuna wanaopona kisha wanatukuza kitu other than God then we should wary, otherwise njia za Mungu zipo nyingi tujipe subira wenye kuomba na waombe si kwa hili la babu tu bali Mungu awashughulikie na mafisadi wote pia maana hospitali zetu zingekuwa kama Aga Khan imani yetu kwa Mungu pengine tungeitumia kuvumbua mambo mengine makuu zaidi.
 
Ninachoona hapa ni kwamba
LD anataka Babu pia awadhibiti watu waseme wameponywa na Yesu.
Na ni wazi anakerwa na watu kutamka NIMEPATA KIKOMBE KWA BABU na badala yake anataka kila mtu kule aseme NIMEPATA YESU au NIMEPONYWA NA YESU sio ndio hivyo unavyotaka LD?????
 
Babu hawezi kuacha kulitumia jina la YESU kwakuwa tu kuna watu hawapendi kulisikia, na wasiopenda kusikia jina la YESU likitajwa wakokila mahali si kwa babu wa loiondo pekee.

Isitoshe watu wasiopenda kulisikia jina la YESU likitajwa na babu wa loliodo ni pamoja na wewe. Yesu alipomuamuru mkoma akajitose mto jordani mara saba hakuacha kulitaja jina la Mungu baba,vinginevyo YESU angeendelea tu kuponya watu pasipo kutaja jina la Mungu kwa kuwa wengine walikuwa hawamjui Mungu bali walisukumwa na mateso ya magonjwa waliyokuwa nayo.

Lakini ukumbuke aliweka msisitizo kwenye kuhubiri neno na si miujiza. Pale alipolisha maelfu ya watu kesho yake wakaja mara mia ya kundi lilokuwepo na ndipo akawageukia mmekuja kufanya nini? Kula mikate au na kuwaambia Mimi ni mkate ushukao kutoka mbinguni kwahiyo leo mtaenda kunila mimi na kunywa damu yangu. Je wangapi walibaki kumla Yesu/neno la Mungu? je hakuwageukia na wale mitume na kuwauliza na wao je wako tayari kula au na wao wanataka kufuata wengi maana luga ya duniani ni sauti ta wengi ndiyo ukweli na siyo neno la Mungu. Je Petro alimjibu je? Hii pekee inamaliza ubishi wote. Hakuna mbingu wala ukweli wala uzima pasipo kula/kujua neno la Mungu ambaye ni Yesu naye amesema straight and forward 'mimi(YESU/NENO) ndimi njia kweli na uzima mtu haji kwa baba ila kwakupitia mimi' Ndiyo maana kila injili inayopinga consistence ya haya maneno ndiyo mpinga kristo mwenye! Maana ameweka mhuri wa milele kwamba mbingu na dunia zitapita lakini neno langu halitapita milele nami hulituma neno nalo halirudi pasipo kufanya kusudi la moyo wangu.

Wapendwa no short cut mtaijua kweli (Yesu/Neno la Mungu) nalo litawaweka huru na mtu akiwekwa huru na neno amekuwa huru kweli kweli. Kama mtaitafuta thread ya Mzee Mwanakijiji mtaona he was very smart na alisema kiakili ili asikwaze watu nami na mnukuu without direct quatations...thousands come to be healed of their diseases though its not said if they drink the cup they will never become sick again...Hiyo ndiyo tofauti ya uponyaji wa Babu na ule wa Neno/Kristo maana ukila mwili wa kristo huugui tena its a permanent solution to all diseases. Mtasema hiyo siyo practical then here I am testifing for you I myself have never been sick for years pamoja na kuwa was suppose to be dead if science was to be true about my condition. I had all my kidneys destroyed by medications and on top I had an intestinal canser which started as ulcers this was later on found a result of helico bacteria ambao according to Drs wanapatikana kwenye mahindi yasiyokobolewa. So mine is not a theoratical knowledge is a life experience. Ninawafahamu watu wengi sana ambao hawakumbuki lini walimeza vidonge, lakini wengi hawapendi kuamini.

Here is the preaching for ur reference http://www.pastorchrisonline.org/channel/watch/cha1936492a2ed
 
Mungu alimtuma yesu, wayahudi wakamuua , amemtuma babu hamtaki kuamini dawa yake.. Mnataka amtume nani?
Dada nenda kanywe dawa kwa babu inatibu. iwe mia au 100,000 uponyaji upo watu wanapona

babu katumwa na mungu gani..?
 
Lakini ukumbuke aliweka msisitizo kwenye kuhubiri neno na si miujiza. Pale alipolisha maelfu ya watu kesho yake wakaja mara mia ya kundi lilokuwepo na ndipo akawageukia mmekuja kufanya nini? Kula mikate au na kuwaambia Mimi ni mkate ushukao kutoka mbinguni kwahiyo leo mtaenda kunila mimi na kunywa damu yangu. Je wangapi walibaki kumla Yesu/neno la Mungu? je hakuwageukia na wale mitume na kuwauliza na wao je wako tayari kula au na wao wanataka kufuata wengi maana luga ya duniani ni sauti ta wengi ndiyo ukweli na siyo neno la Mungu. Je Petro alimjibu je? Hii pekee inamaliza ubishi wote. Hakuna mbingu wala ukweli wala uzima pasipo kula/kujua neno la Mungu ambaye ni Yesu naye amesema straight and forward 'mimi(YESU/NENO) ndimi njia kweli na uzima mtu haji kwa baba ila kwakupitia mimi' Ndiyo maana kila injili inayopinga consistence ya haya maneno ndiyo mpinga kristo mwenye! Maana ameweka mhuri wa milele kwamba mbingu na dunia zitapita lakini neno langu halitapita milele nami hulituma neno nalo halirudi pasipo kufanya kusudi la moyo wangu.

Wapendwa no short cut mtaijua kweli (Yesu/Neno la Mungu) nalo litawaweka huru na mtu akiwekwa huru na neno amekuwa huru kweli kweli. Kama mtaitafuta thread ya Mzee Mwanakijiji mtaona he was very smart na alisema kiakili ili asikwaze watu nami na mnukuu without direct quatations...thousands come to be healed of their diseases though its not said if they drink the cup they will never become sick again...Hiyo ndiyo tofauti ya uponyaji wa Babu na ule wa Neno/Kristo maana ukila mwili wa kristo huugui tena its a permanent solution to all diseases. Mtasema hiyo siyo practical then here I am testifing for you I myself have never been sick for years pamoja na kuwa was suppose to be dead if science was to be true about my condition. I had all my kidneys destroyed by medications and on top I had an intestinal canser which started as ulcers this was later on found a result of helico bacteria ambao according to Drs wanapatikana kwenye mahindi yasiyokobolewa. So mine is not a theoratical knowledge is a life experience. Ninawafahamu watu wengi sana ambao hawakumbuki lini walimeza vidonge, lakini wengi hawapendi kuamini.

Here is the preaching for ur reference || Pastor Chris Online - Channel ||

great testimony dear brother!

nashukuru pia kwa maelezo mazuri ya kufafanua nafasi ya neno la Mungu kwenye imani na maisha yetu. neno ni kubwa na lenye nguvu kuliko miujiza. haleluya!

ubarikiwe sana

Glory to God
 
ni hivi punde tu nilikuwa naongea na mtu toka Eritrea akanipa ushuhuda wa mtu mwenye shughuli kama za babu huko kwao, ngoja nimdadisi zaidi, nikipata maelezo mazuri nitakuja kuwadokeza hapa jamvini.

by the way, nafurahi sana jinsi mjadala huu unavyokwenda. bahati mbaya nimebanwa na majukumu, but baada ya 30 minutes nitakuwa free, ntarudi kujibu hoja zote za msingi zinazonihusu. kipekee niwashukuru wote mnaoendelea kuitetea injili ya kweli na msingi wa manepo ya Mungu. kwa neema ya Mungu tutazishinda hila za shetani. amina

mbarikiwe sana wapendwa.

Glory to God

wapendwa, ile habari ya Eritrea inapatikana hapa kwenye link hiyo hapo chini. niliifungulia thread yake kwa sababu thread hii ilipelekwa service kwa kitambo, so mods wanaweza kuziunganisha pamoja na hii kwa sasa.

https://www.jamiiforums.com/jf-chit-chat/120225-kutana-na-babu-wa-eritrea.html

pia kama muonavyo imehamishiwa chit-chat forum, hiyo ni busara za mods, lakini jukwaa kwangu mimi sioni kama ni issue japo watu wakiishiwa hoja watakurupuka kuwa "ndio maana iko chit-chat" lakini Mungu aweza kutumia hata mambo manyonge na kuyafanya ujumbe mkuu wa wokovu wa kweli.

source ya habari hii ni rafiki yangu na tumezungumza naye jana ofisini baada ya kazi na yalikuwa mazungumzo ya mdomo kwa mdomo. kwa hiyo wale wanaokimbilia kuuliza "source?" habari ndiyo hiyo.

i will be back soon

What is.."SOURCE NI RAFIKI YANGU?"...Huu ni Uswahili huu, and i call it grapevine woman to woman talk!
Mwishowe utatuletea habari za kumchuna mtu au kumfanya ATM, maana tayari ushaleta ishu za kuTONGOZANA!...HUH!
Naanza kuwaamini waliosema kuwa weweni GETRUDE Rwakatare, au watchdog wake!..kubalini tu kuwa watu wamestukia huduma zenu za kitapeli makanisani kwenu!
 
Ni heri kuwa baridi au moto .kuliko kuwa vuguvugu..

this is one of the greatest statements here!

kama kwa Yesu, you are welcome, yaangalieni wenyewe hayo. ila huwezi kuwa kotekote. hakika Mungu hadhihakiwi

Glory to God
 
wakuu tusimpinge kwa bezo miss judy....Hivi ni kwa kiasi gani tunaweza kumtambua mtumishi/nabii/mhubiri wa uongo?
 
Heshima kwenu wanajamvi,

Si kawaida yangu kurejea kwenye mada niliyoichangia lakini baada ya kuipitia tena na kusikiliza maneno ya mitaani nimeona si vibaya nikarejea tena kuchangia hii mada.

Mwanzo nilisema wanaopinga huduma ya Babu wa Loliondo wa wanasumbuliwa na wivu hawana hoja za maana za kumshawishi mtu mwenye akili zake ambaye hajawahi kusumbuliwa na magonjwa ya akili kuacha kufuata huduma ya Babu.

Nimegundua mambo mengi kwanini wapo wapinzani wengi wa huduma ya Babu.

[1] Tofauti za kimadhehebu ni sababu kubwa inayotumuiwa na baadhi ya viongozi wa madhehebu ya kikristo kuwatisha waumini wao wasiende kupata tiba ya Babu.Madhehebu mengi hasa Assambless of God waumini wake wengi walikuwa wakiabudu aidha Catholic,Lutheran au Anglican.Waumini wamejazwa ujinga kwamba uponyaji kamwe hauwezi kupatikana nje ya dhehebu lao yaani Pentecoste/Assembless of God.kwakuwa Babu wa Loliondo ni mchungaji mstaafu wa Kilutheri dhana kwamba hakuna upako au uponyaji inaendelezwa sana na kukuzwa.

Nitatoa mfano mmoja kukazia hoja yangu,Mwalimu C Mwakasege ni muumini wa kanisa la Lutherani wakati anaanzisha huduma yake [Maana] alikumbana na upinzania mkali kweli kwanini hajahama dhehebu la Lutheran ambako hakuna upako /Yesu na nk.Mwalimu Mwakasege alikuwa akiwajibu vizuri sana baadhi ya wakosoaji wake wakubwa kwamba Yesu hakai kwenye Madhehebu wala hakuna dhehebu liloanzishwa na Yesu kila mtu anayeokoka abaki kwenye dhehebu lake.Ukishangaa kwanini Askofu Mtume na Nabii Mwingira anamwandama Babu utakuta ni dhana ile ile ya haya madhehebu kudhani Mungu yuko kwenye madhebu yao tu mengine ni wasindikizaji tu.

Nilihudhuria mkutano wa Injili wiki iliyopita nilishangaa mhubiri alikuwa akitumia muda mwingi kumkosoa Babu badala ya kumuubiri Kristo.Kila kipengele kuhusiana na babu kilichambuliwa kwa namna ya ushabiki wa ajabu kiasi waumini/wasikilizaji wakakosa amani ya kuendelea kumsikiliza mhubiri.Shilingi mia tano anayotoza Babu ilijadiliwa kiasi kwamba hata wenye sadaka ya 500 walishindwa kutoa eg ina alama ya nyoka na nk.

Mwisho Babu wa Loliondo hajamlazimisha mtu au watu wamfuate ikiwa moyo wako unakukataza kwenda kupata tiba sawa lakini habari za kumzushia Babu ni vyema zikaachwa kabisa watu,ndugu na jamaa wamekwenda wamepata tiba/kikombe wamepona magonjwa sugu yaliyowasumbua na kuwatesa kwa muda mrefu chuki za nini mbona mlikuwa mnanunua vitambaa vya Mama G Lwakatare,Mlikuwa mkombewa na Mzee wa Upako mkatia fedha nyingi kwenye A/C yake binafsi haikuwa nongwa.Babu habagui anatoa kikombe kwa watu wote Waislamu kwa wakristo bila kukulazimisha kufuata dini anayoiamini punguzeni chuki maana najua kuacha kabisa haiwezekani.

Wiki ijayo mvua ikipungua nakwenda kupata kikombe cha Babu !!!!!!!.
 
Back
Top Bottom