Hoja ya Shossi juu ya sh. 500/- ya babu

Hoja ya Shossi juu ya sh. 500/- ya babu

ndugu pakajimmy,

hatukejeli wanaopata faraja huko kwa babu kutokana na magonjwa na madhaifu mbalimbali, la hasha. tunawashauri wapendwa wetu wasome na kufahamu ukweli juu ya nini yaliyo mapenzi na makusudi ya Mungu kama yalivyobainishwa ndani ya biblia na wapime na kujaribu kila roho kama inatokana na Mungu.

hivi kuna mtu huko samunge aliyepata majaribu kumshinda ayubu? mbona ayubu alikataa kumkufuru Mungu? iweje maelfu huko samunge wawe tayari kumdhihaki Mungu kwa sababu ya BP, cancer, ukimwi nk, eti kwa kupokea kikombe cha mchungaji mstaafu!

mwenye imani ya kweli na iliyojengwa kwenye neno (siyo iliyojengwa kwenye miujiza) atamtukuza Mungu hata apate mateso kiasi gani. atamtukuza Mungu hata katikati ya mateso, naam hata kama atamiminwa damu na kufa kama shahidi (martyr). imani yenu iko wapi sasa?

mimi niko tayri kuishi na majaribu ya ukimwi na mengineyo sugu lakini sio kumkufuru Mungu kiasi hicho cha samunge. ee Mwenyezi Mungu naomba nisaidie

Glory to God

Hujui ulisemalo wewe kaa kimya upesi!
 
Hatuwezi kunyamaza na lazima tuseme ukweli kwasababu kama kuna uwalakini kwanini tukae kimya? Hii mada si kwaajili ya babu bali ni kwaajili ya wana JF ili waweze kutambua kwamba si vyote vin'gaavyo ni dhahabu.

Sawa Mwingira nakupata
Endelea kueneza Utume na Unabii wako
Unanichekesha sana, unaongea utafikiri wanaJF ndio wanaongoza kwenda kupata kikombe kwa babu. Nenda loliondo na hao wenzako kama kweli unania hiyo, maana kule ndio kuna maelfu ya watu wanaenda kila siku, acha kubangaiza na keyboard hapa JF.
Hilo somo lako litakuwa majungu tu kama hujaenda kusema kwa wanaoenda loliondo.
Au unataka kubadili imani zetu sisi tuliowapinga ili ziwe kama zenu?? He he he . . .
 
Kumbe umegundua CPU!

Wanapiga kelele hapa mjini wakati wahusika wapo kwenye foleni kijijini.
Ungemtarajia mwenye uchungu naoaende Loliondo ili awahubirie waenda kwa babu. Inaonekana kila anayekwenda Loliondo hamjui Mungu vizuri. Hapa ndipo wengine wanajiona ni wakristo "first class" wengi tuko daraja la tatu.

Inachekesha saaaaaaana!
 
ndugu pakajimmy,

hatukejeli wanaopata faraja huko kwa babu kutokana na magonjwa na madhaifu mbalimbali, la hasha. tunawashauri wapendwa wetu wasome na kufahamu ukweli juu ya nini yaliyo mapenzi na makusudi ya Mungu kama yalivyobainishwa ndani ya biblia na wapime na kujaribu kila roho kama inatokana na Mungu.

hivi kuna mtu huko samunge aliyepata majaribu kumshinda ayubu? mbona ayubu alikataa kumkufuru Mungu? iweje maelfu huko samunge wawe tayari kumdhihaki Mungu kwa sababu ya BP, cancer, ukimwi nk, eti kwa kupokea kikombe cha mchungaji mstaafu!

mwenye imani ya kweli na iliyojengwa kwenye neno (siyo iliyojengwa kwenye miujiza) atamtukuza Mungu hata apate mateso kiasi gani. atamtukuza Mungu hata katikati ya mateso, naam hata kama atamiminwa damu na kufa kama shahidi (martyr). imani yenu iko wapi sasa?

mimi niko tayri kuishi na majaribu ya ukimwi na mengineyo sugu lakini sio kumkufuru Mungu kiasi hicho cha samunge. ee Mwenyezi Mungu naomba nisaidie

Glory to God

Tatizo ninyi wafuasi wa akina Kakobe, Mwingira, Lusekelo, Prof Dr Mh Mch Rwakatare mnasumbua sana na tiba zenu za vitu visivyoonekana eti utasikia kulikuwa kuna vitu vinatembea mwilini lakni sasa sivisikii! Sijawahi one mlemavu wa viungo, kipofu ameenda huko akarudi ametupa magongo yake! Maombezi yenu ni vichwa, maumivu ya tumbo nk. Wewe ulitaka Mch Babu awe wa rangi gani? Eti unakebehi kwa kusema "kikombe cha mch Msitaafu" wewe unataka kumpangia mungu watu wa kuwatumia.
Kanisani tunatoa zaka na sadaka je Mungu ni masikini mpaka tumchangie moja ya 10! Hasha! Zipo shuhuda za watu waliopona! Utawaweka wapi watu hawa! Halafu ni wapi mchungaji amekosea au kwa sababu ni dawa ya miti shamba!
 
yaani kuna wa2 humu kama MS! wana talent ya ku provoke wengine.
 
Wapendwa katika Bwana,

Naamini kila mmoja wetu anaufahamu vizuri mjadala unaoendelea juu ya Mch. Mwasapile. Maelezo ya baadhi ya mambo yalijitokeza katika mada yangu ile ni kama ifuatavyo:
1. Ni bora tukamwacha babu aendelee na kazi zake
kimsingi mimi na wote tunaohoji shughuli za uganga wa babu hatuna nia ya kumzuia babu kufanya shughuli zake hizo za kutibu kwa mitishamba, bali tunahoji uhalali wa madai yake kuwa shughuli hizo zimetokana na ufunuo wa Mungu. Na hii ni kwa sababu tukimpima kimaandiko, tunapata kila sababu ya kusema kuwa kama ni kweli kafunuliwa na Mungu, basi si Mungu huyu tunayemuabudu wakristo na aliyemtuma Bwana Yesu kuja duniani kutuokoa dhambini (kumbukeni kuwa kuna miungu mingine ya uongo hujiinua na kudai kuabudiwa kama Mungu aliye hai). Sababu zetu ni pamoja na kuwa
· Babu hafundishi neno la Mungu na hivyo hiyo huduma yake imelenga kuponya mwili pekee na si roho
· uponyaji wake umefungamana na mti Fulani na siyo Yesu Kristo %3

kwahiyo ulikua unafanya research? ha ha ha ha ha mbavu zangu jamani.
 
Da Judith nadhani unahitaji kurudi kwenye kamusi ili utambue tofauti ya MAJUMUISHO na UTETEZI.
Umejitetea zaidi badala ya kuleta majumuisho.

Cha kushukuru ni kwamba tumejua yale yajazayo mioyo wa watu!!

Anyway; "Better is not Good Enough and the Best is Yet to Come"
 
nianze kwa kuweka wazi kuwa sina hakika na imani ya huyu ndugu yetu Mohamedi Shossi, sijui kama ni mwislamu, mkristo ama muumini wa dini nyinginezo.

aliweka wazi kuwa babu si size ya Yesu na alisema kuwa Yesu ni "world icon" na babu hawezi kulinganishwa naye hata kidogo. baadhi walimkosoa kumwita Yesu "world icon" na walikuwa na sababu zao. pia ametoa michango mingi tu mingine ila hapa nataka niungane naye na kumpongeza kwa kuhoji hiyo bei ya babu.

Mungu wetu afikie mahali apange bei!! tena ya huduma itokanayo na karama aliyotoa mwenyewe? kweli hapo pagumu kuingia akilini. tena mungu wake huyo akampa na mchanganuo wa namna atakavyozigawa hizo pesa, eti 300/- kwakanisa, yatima na wajane na 200/- za wahudumu wanaomsaidia kazi! kwa kweli naona kama hizi ni kashfa kwa Mungu wetu.

neema ya Mungu wetu ni kubwa na pana sana, na kamwe huyu babu asiichezee kiasi hiki. yeye atangaze kuwa ni mganga aliyekuja na dawa ya mti wa mrigariga, afuate taratibu za serikali za kujisajili kisheria ili serikali itambue kazi zake na aweke bei yake kama wawekavyo waganga wengine na tutamchukulia kama tunavyowachukulia waganga wengine.

hongera tena Mohamed Shossi, hoja yako ni njema na ya kweli. Mungu wetu hahitaji hata senti yetu moja. karama zake hutoa bure. michango kwa ajili ya kazi ya Bwana ni ya hiyari na kadiri mtu alivyojaaliwa kutoa.

ukishaweka bei (hata kama ni sh.10/-) maana yake ni kwamba asiye nayo hapati huduma! kumbuka madukani kuna pipi za sh.10/- na usipokuwa na hiyo sh.10/- hupati hiyo pipi. ndiyo maana ya bei. sasa babu anasema kama huna sh. 500/- kaa pembeni mwenye hela aje apate kikombe! hata akiamua kuwasamehe wengine kulipa, manake atakuwa kakiuka utaratibu wa huyo mungu wake anayedhibiti bei! sasa hii nayo bado ni huduma ya kiroho kweli kwa mujibu wa dini ya kikristo? mungu gani huyu anayepanga hesabu hivi?

tuendelee kutafakari na kuliombea kanisa

Mungu akubariki sana ndugu Mohamedi Shossi,

Glory to God!

Wakati mwingine muwe mnatumia akili!! yaani yule mchungaji angekuwa anaenda porini kuchimba miziziz, anakuja anachemsha kwa ajili ya mamilioni ya watu peke yake!!! inaingia akilini!!?
Asingeweza kufanya kazi, isingewezekana kabisa labda kama ingekuwa anawawekea mikono watu ndiyo tunge sema....Lakini kuna kazi kubwa tena kuubwa sana angewezaje bure bure!!! then nani nchi hii kalalamika kuwa hiyo mia tano ni kubwa!? zaidi ya makafi wachache tu?
 
Wapendwa katika Bwana,

Naamini kila mmoja wetu anaufahamu vizuri mjadala unaoendelea juu ya Mch. Mwasapile. Maelezo ya baadhi ya mambo yalijitokeza katika mada yangu ile ni kama ifuatavyo:
1. Ni bora tukamwacha babu aendelee na kazi zake
kimsingi mimi na wote tunaohoji shughuli za uganga wa babu hatuna nia ya kumzuia babu kufanya shughuli zake hizo za kutibu kwa mitishamba, bali tunahoji uhalali wa madai yake kuwa shughuli hizo zimetokana na ufunuo wa Mungu. Na hii ni kwa sababu tukimpima kimaandiko, tunapata kila sababu ya kusema kuwa kama ni kweli kafunuliwa na Mungu, basi si Mungu huyu tunayemuabudu wakristo na aliyemtuma Bwana Yesu kuja duniani kutuokoa dhambini (kumbukeni kuwa kuna miungu mingine ya uongo hujiinua na kudai kuabudiwa kama Mungu aliye hai). Sababu zetu ni pamoja na kuwa
· Babu hafundishi neno la Mungu na hivyo hiyo huduma yake imelenga kuponya mwili pekee na si roho
· uponyaji wake umefungamana na mti Fulani na siyo Yesu Kristo %3
Hivi kuna aliyewahi kudhibitisha iwapo ni kweli Mwingira wa Efatha aliota ndoto kuagizwa akaanzishe ile huduma yake? Nadhani ni bora kukaa kimya badala ya kupinga jambo usilolielewa.
 
Mungu alimtuma yesu, wayahudi wakamuua , amemtuma babu hamtaki kuamini dawa yake.. Mnataka amtume nani?
Dada nenda kanywe dawa kwa babu inatibu. iwe mia au 100,000 uponyaji upo watu wanapona
Nilikuwa naamini yesu ndio Mungu, kumbe yeye alitumwa na Mungu, kwamaana yesu ni Mtume tu sio?.
 
Kwa kweli hayo magonjwa ni mazito na yanatisha sana. Lakini kuna ushahidi kuwa babu anayatibu? Nani kapona kansa au ukimwi mtusaidie wanaJF hapa barazani. Mimi namutazamia Lyatonga kama atapona nitajifariji kidogo kwamba walau mtu mmoja wa kisukari amepona lakini wa kansa na ukimwi je? Mwisho wa babu ni mbaya!!!
:embarassed2:
 
wapendwa samahani,

hata sijui kimetokea nini. ngoja nirudie kupost tena manake naona post imefika imekatika , lol

ooh, my God
 
Wapendwa katika Bwana,

Naamini kila mmoja wetu anaufahamu vizuri mjadala unaoendelea juu ya Mch. Mwasapile. Maelezo ya baadhi ya mambo yalijitokeza katika mada yangu ile ni kama ifuatavyo:
1. Ni bora tukamwacha babu aendelee na kazi zake
kimsingi mimi na wote tunaohoji shughuli za uganga wa babu hatuna nia ya kumzuia babu kufanya shughuli zake hizo za kutibu kwa mitishamba, bali tunahoji uhalali wa madai yake kuwa shughuli hizo zimetokana na ufunuo wa Mungu. Na hii ni kwa sababu tukimpima kimaandiko, tunapata kila sababu ya kusema kuwa kama ni kweli kafunuliwa na Mungu, basi si Mungu huyu tunayemuabudu wakristo na aliyemtuma Bwana Yesu kuja duniani kutuokoa dhambini (kumbukeni kuwa kuna miungu mingine ya uongo hujiinua na kudai kuabudiwa kama Mungu aliye hai). Sababu zetu ni pamoja na kuwa
· Babu hafundishi neno la Mungu na hivyo hiyo huduma yake imelenga kuponya mwili pekee na si roho
· uponyaji wake umefungamana na mti Fulani na siyo Yesu Kristo
· Tiba yake imo ndani ya mipaka ya kijiji cha samunge pekee

· tiba yake haimuinui na kumtukuza Mungu bali anajiinua yeye mwenyewe na mti wake wa mrigariga
· Maono yake yaliambatana na agizo la kutoza sh.500/- kwa kila atakayehitaji uponyaji (Mungu wetu hatozi wala hahitaji hata senti yetu moja)
· Anataka dunia nzima isafiri kwenda kijijini kwake kupata hiyo huduma yake
Majibu ya haya yote yametolewa kwa kina kwenye thread husika

2. Tumwache kila mtu afuate imani yake
Kama wakristo, ni wajibu wetu kupima kila roho na kujiridhisha kuwa imetokana na Mungu (1Watehsalonike 5:18 na 1 Yohana 4:1). Katika Ezekiel 33:8-9 tunaambiwa ukimwona mtu anapotea nawe usiseme neno kumuokoa, ataangamia lakini damu yake itadaiwa mkono mwako. Kwa hiyo ni wajibu utokanao na upendo wa undugu katika mwili wa Kristo kuwa tusiwaache watu waelekee upotevuni. Kama mitume wa Bwana na wamissionari wangeacha kila mtu afuate imani yake, hakika hakuna mtu angemjua Yesu na kuzijua Baraka za Mungu za rohoni nje ya Galilaya, Samaria na Yudea, mikoa alikohudumu Bwana enzi za huduma yake hapa duniani.

Kamwe hatutanyamaza wala kumwacha kila mtu afuate imani yake. Bali katika kila neno, kila ndoto na kila ishara/muujiza, tutachunguza na kupima kama liko sawa na limetokana na injili ya Bwana na kuonya, kukaripia na kufundisha njia sahihi bila kuchoka (2 Timotheo 4:1-5).

3. Tusihukumu tusije tukahukumiwa
kupima na kuhoji aina ya roho aitumiayo babu kuponya na kama imetokana na Mungu au la, sio kuhukumu. Kuhoji tunakofanya ni kwa mujibu wa maandiko matakatifu na sio nje yake. Ndugu yako akiwa na mwenendo usiofaa na ukamkanya au kumpa angalizo ili abadili mwenendo wake sio kumhukumu.
Babu ni ndugu yangu katika Bwana na kama kuna shaka yoyote katika shughuli zake, ni wajibu wangu na wa mkristo yoyote kumrejeza katika kweli yote. Hatutaacha kufundisha, kuonya, kukemea na kazi nyingine za mhubiri wa injili (2 Timotheo 4:1-5)

4. Mambo ya imani magumu kueleweka
imani chanzo chake ni kusikia na kusikia huja kwa neno la Kristo. Kwa maneno mengine, imani isiyotokana na uelewa wa injili si imani ya Kikristo. Imani ya kikristo lazima itokane na neno na hupimwa kwa neno na hivyo twaweza kusema kwa hakika kabisa kuwa imani fulani ni sahihi au sio sahihi kwa kuzingatia msingi wa neno la Mungu.
Ugumu wengi wanaousema ni wa imani tofauti na za kikriso kwa sababu hazijafunuliwa. Zimefumbwa na kuachwa kama MYSTERY, ila ya kikristo iko wazi na ITS NO LONGER A MYSTERY. Nawashauri wapengwa tusiwe wazito kusoma neno la Mungu lenye ufunuo wa kila kitu tunachopaswa kujua kuhusu imani yetu.

5. Tuiache huduma ya babu itajidhihirisha mbele ya safari kwani kama ni ya uongo atakwama tu
Wale wanaojua misingi ya Total Quality Management, hawawezi kusema kauli kama hii. Ni sawa na kusema tuache ndege iruke na abiria angani bila kujiridhisha kama ina mafuta ya kutosha kwa safari ili kama haina mafuta ya kutosha itaanguka na ndipo tutakapojua ukweli kama ilikuwa na mafuta ya kutosha au la! Haya ni mawazo mabaya sana na kwa kweli ni ya ajabu! Learning from mistake doesnt always work!

Kama nilivyosema katika namba 2, 3 na 4 hapo juu haiwezekani kumuacha babu aendelee tu na huduma yake bila kuhoji uhalali wake kimaandiko. Kama asingedai kuwa ni ufunuo wa Mungu uliokuwa juu yake, basi ingeeleweka kuwa ni mganga wa mitishamba kama wengine na tungemchukulia hivyo. Kwa kuwa kasema ni ufunuo wa Mungu basi tunawajibu wa kuupima ufunuo wenyewe na kuhoji usahihi wake kimaandiko kabla ya kuuamini. Isitoshe kama ni wa uongo, atawadanganya na kuwapoteza watu wengi sana na anaweza hata kusababisha mauti ya kutisha hata kuzidi ya kibwetere wa Uganda na mwisho enzi kuangamiza ndugu zetu wengi zaidi katika jehanamu.

6. Hata Yesu aliponya watu kwa kutumia tope, naaman aliponywa kwa kujichovya mara saba mto yordani
hatuna shina na mti autumiao kuponya, bali chanzo cha ufunuo wake na utaratibu mzima wa tiba yake vinatia shaka kwani haviendani na imani ya kikristo kwa mujibu wa maandiko. Bwana wetu ni Bwana wa vitu vyote. Alipokuwa duniani alidhihirisha mambo mengi sana kwa namna ya kipekee sana na ilikuwa inalenga kuonyesha kuwa alikuwa na malaka juu ya kila kitu na kuwa ndiye atokaye kwa Baba. Kila miujiza aliyoifanya ilikuwa unique na ishara kuwa yeye ndiye. Aliweza hata kufufua wafu na kusamehe dhambi na aliweka wazi kuwa ana mamlaka ya kusamehe dhambi (Mathayo 9:6).
Kwa nyakati zote miujiza ilikuwa si kwa kila mtu aliyekuwa dhaifu. Enzi za naaman kulikuwa na wakoma wengi sana duniani, lakini ni naaman pekee aliyeponywa, enzi za Yesu kulikuwa na wagonjwa wengi sana wa kila aina, lakini ni hakuwaponya wote. Miujiza ya huyu babu inamtukuza mwenyewe na mti wake na si Mungu.

7. uponyaji ni suala la imani ya mponywaji
Yesu aliposema kuwa “imani yako imekuponya” alikuwa anadokeza tu nini kilichoponya. Naomba nieleweke hapa kuwa
· si mara zote Yesu alikuwa akisema kilichoponya
· si kila uponyaji ni kwa sababu ya imani ya mponywaji
· Imani ya mponyaji pia yaweza kuponya hata kama mponywaji hana imani
Kitabu cha matendo ya mitume kina mifano mingi sana ju ya ukweli huu.

8. Watu wameteseka sana na maradhi na Mungu amekuja kuwafariji na kuwarejeshea matumaini ya afya njema
lengo kubwa la Mungu ni kuokoa kutoka katika dhambi na sio kuondoa mateso ya mwili na faraja ya Bwana iko rohoni zaidi na sio mwilini.
Hata waganga watumiao pepo wachafu nao huwapa faraja wateja wao kwa hiyo, faraja pekee wapatayo wateja wa babu haituzuii kuhoji usahihi wa roho atumiayo babu kuponya.

9. Sh. 500/- anazotoza babu si kitu ukilinganisha na baraka na faraja ya uponyaji wa magonjwa sugu kama ukimwi, kansa, kisukari, shinikizo la damu nk wanayopata. tena wengi wako tayari kutoa zaidi ila babu ndiye anawazuia
Karama ya Mungu ni bure na haitozwi hata senti moja, tumepewa bure na tutoe bure . Watumishi wanaweza kuomba au kuchagiza sadaka na michango mingine ya hiyari kulingana na uwezo na mapenzi ya mtoaji.
Huduma a neno la Mungu ni bure kabisa, yoyote atozae fedha (nyingi au chache, awe babu, mwakasege, judith au nani mwingine) yuko kinyume na injili.

10. Kwa nini hatupingi huduma za wengine?
Inafahamika kuwa akina kakobe, mwingira, rwakatale, fernandes, lusekelo, gwajima gamnywa nk hutoza pesa nyingi sana kwa kisingizio cha sadaka na michango mbalimbali kama mafungu ya kumi, ujenzi, shukrani nk. Hapa ikumbukwe kuwa hawa hawakuwa mada na hakuna aliyeleta mada juu yao tukakataa kuchangia au tukachangia kwa kuwaunga mkono na ilipofika kwa babu tu ndiyo tukageukia kumlaumu babu.
hapa sitasema juu yao na kama kuna haja basi mimi mwenyewe au yoyote mwingine alete mada inayowahusu nitachangia na naamini na wapendwa wote wanaolitumaini neno la uzima wachangia kwa kadiri ya neema ya Mungu.
Ila napenda kusema kwa kifupi kuwa babu hawezi kuwa sawa kwa vile tu wengine hao tuliotaja nao wanafanya. Huduma ya Mungu haina cha kufuata mkumbo na wala hatuwezi kuipima roho ya babu na shughuli zake kwa roho na shughuli za watu wengine. Kila roho na shughuli ya kiroho hupimwa kwa maandiko matakatifu pekee ambayo ni maneno ya Mungu mwenyewe, basi.

11. Sisi tunaotilia shaka huduma hii tuna wivu.
Hapa hakuna wivu, kuna neno la Mungu na shughuli za babu, basi. Kama zisingepingana na maandiko, tungepata wapi sababu ya kuihoji au kuipinga huduma yake? Mimi sio kiongozi wala wakala wa huduma yoyote pinzani ya kiroho bali ni mkristo wa kawaida.

12. Tunatilia shaka huduma hii kwa sababu hatujapatwa na magonjwa sugu na kujua jinsi yanavyowatesa watu
nadhani nimeishaafafnua kwa kirefu ni kwa nini tunahoji hii huduma ya babu na si vyema ku-duplicate material bila sababu za msingi. Tunalopinga ni jinsi huduma yenyewe ilivyo kwa msingi wa neno la Mungu. Ayubu alipata mateso makubwa sana ya kufilisika mali, misiba nyumbani kwake, majipu nk lakini hakumkufuru Mungu wala kugeukia imani zisizo sahihi.

Kwa hiyo na sisi hatuna sababu ya kuacha kuwahimiza hata wapendwa wetu wenye mateso ya magonjwa kuendelea kumuamini Mungu wa kweli hata ikibidi kumtukuza Mungu kwa njia ya kifo bila kuikana imani. HUU NDIO UKRISTO NINAOUFAHAMU MMI.
Ukristo wa kumwamini Mungu wakati wa afya na raha peke yake na ujapo wakati wa maradhi na shida nyingine ukaruhusu kujishirikisha na roho zisizoeleweka vyema tena bila kuzipima eti kwa sababu tu “umeteseka sana na wanahitaji uponyaji”, hakika sio ukristo wa kweli uliojengwa juu ya neno la Mungu na mimi si MMOJA WAO.

13. Muhimu ni kupona na sio zaidi
ni kweli muhimu ni kupona, tena kupona roho sio mwili. Ni heri tuingie mbinguni na chongo au vilema kuliko kutupwa jehanum tukiwa na macho wakamilifu wa mwili. Kwa hiyo watu watafute kupona roho zao kabla ya kitu kingine chochote.
Mwenye ukimwi, kansa, kisukari, pumu, BP nk atafute kwanza uponyajiwa roho yake na atakuwa amepata faida kubwa sana ya kuingia mbinguni hata akifa kutokana na maradhi yake hayo, kuliko aponywe hayo maradhi bila kutengeneza maisha yeke na Mungu na hatimaye kuishia jehanum.

14. Ubikira wa Miss Judith
hii haikuwa mada lakini iliingizwa kwenye mjadala baada ya mimi mwenyewe kulazimika kujieleza baada ya watu kuhusisha AVATAR yangu na maisha yangu binafsi wakidai kuwa kama avatar inavyoonekana inawezekana na mimi ni mhuni tu na mambo mengine mengi.

Ubikira wangu unatokana na neema ya Mungu pamoja na kutembea katika mwanga wa neno la Mungu toka nikiwa mdogo. SIWEZI KUONA HAYA KUSHUHUDIA JAMBO HILI. Kama waasherati hawaoni haya kujisifia ufundi wao wa kufanya uzinzi, kwa nini mie nione haya kuliinua neno la Mungu? Huu ni ushahidi mwingine kuwa neno la Mungu lina nguvu na linaweza kubadili mienendo yetu na tukaishi maisha yenye Baraka za Mungu kama tutaliamini na kuliacha liongoze maisha yetu.

Ni vizuri wote (hata waliobeza) wakajua kuwa ubikira ni jambo la kawaida kimaumbile lakini jiulize kuwa ukiitisha mabikira wenye umri wa miaka 26 kutoka mtaa unaoishi utapata wangapi? Sijasema hawapo, nauliza unategemea kupata wangapi? Najua hamjasahau, juzijuzi tu hapa JF ilikuwa inajadiliwa mada ya watu kutamani wangerudi kuwa mabikira!

Ni kizazi kilichopotoka tu ndicho kitakachoweza kuchefuliwa na ubikira. Bikira Maria alipotokewa na malaika na kupewa ujumbe kuwa atapata mimba, alisema bila haya wala kutafuna maneno kuwa yeye yu bikira. Huko uyahudi enzi zile kila atajwapo mwanamke ama binti ambaye hajamjua mume bado ilikuwa ni kawaida kusisitiza kuwa yu bikira. Hata baba akiwatambulisha wabinti zake ilikuwa kawaida kusema, mwanangu huyu ni bikira anaitwa Fulani.

Mtu akijisifia hapa masuala ya ufundi wa mapenzi halaumiwi kuwa ana-attract attention. Kuna mtu aliwahi kuanzisha thread kuwa anatafuta infidelity na ilichangamkiwa na watu wengi na ilipita kurasa 150! Wapendwa tutafakari kwa pamoja haja ya kuyarudia maneno ya Mungu na kuyategemea yatuongoze njia zetu.

15. Mwenendo wa Miss Judith hapa JF kikristo unatia shaka
Hebu kuweni positive. Kutongoza si lazima kuishie kwenye ngono, bali kunalenga kuanzisha urafiki na mawasiliano. Mimi ni mpenzi na mwerevu wa saikolojia na sosholojia. Baadhi ya majukumu yangu yanahusisha utafiti wa masuala yanayoangukia katika Nyanja hizo. Sanaa nzima ya kutongoza na kila kitu kinachoendelea huko “at your own risk” ninakifahamu vizuri japo sijawahi ku-practice ngono maishani mwangu. Kama kuna mtu ana swali akaulize kwenye ile thread inayohusika nitamjibu kadiri nitakavyoweza.
Sioni tatizo la kutembelea huko“at your own risk”, kwani yaliyoko huko ndiyo yanayofanyika kila siku hapa duniani. Pia kwa nafasi yangu kikazi na kijamii, nawajibika kuyajua kiundani, kisayansi na kwa ufasaha na ninayafanyia kazi kila siku.

16. Thread kuhamishiwa chit-chat forum
Japo sikuwaunga mkono moderators katika hili lakini naamini walijitahidi kuwa wavumilivu manake kuna kila dalili kuwa baadhi ya members humu wana nguvu ya ajabu juu ya moderators na inawezekana nao ni moderators pia. Dada yangu Michele amewahi kutofautiana na baadhi ya watu hapa tena kwa jambo la kawaida kabisa kwa watu kutofautiana akaishia kupewa ban. So hata mimi najua naweza kukabiliwa na hatari ya ban.
Siwezi kunyamaza nikaacha kusema neno la kweli iwe juu ya babu au mtu mwingine yoyote eti kwa kuogopa ban. Mungu ndiye Muweza wa yote na hatimaye Kweli itashinda.

poleni kwa maelezo marefu japo nimeedit sana hadi nikachelewa kupost. Nimalizie kwa kusema kuwa kwa neema ya Mungu nimekuwa hivi nilivyo (1Wakorintho 15:10)

Mungu awabariki nyote

Glory to God
 
Miss Judy nimesoma thread zako na kuona ni wazi umeisoma bible na huenda ulipata malezi ya ukristo.elimu yako pia si haba.shida inakuja kwenye kila kitu kinapozidi huwa harmful.

hata wale waislamu wa al shabab wanatetea uislamu uliopitiliza hadi kuzuia taarifa za habari zisianze na mlio wowote kama ngoma au muziki,pia simu yako ikiita ringtone ya muziki wewe adhabu ni kifo.humu mitaani wapo pia wanaovaa visuruali kama vipedal..dont touch my shoes au never come down na videvu vyao kama beberu,walikuwepo wale wasabato masalia waliokaa airport wakitarajia kusafiri kimiujiza na hao wote ni zao la imani iliyopitiliza..

kwa dunia hii ya karne hii ya sayansi na technologia na pia maisha ya kiwango endelevu na muingiliano mkubwa ni vigumu kuishi kama zile enzi za before christ or mtume muhammad SAW ama miaka michache iliyofuata baada ya vifo vyao.kumbuka pia kuwa vingi vizuri havidumu ndo maana hata uwepo wake messiah ulidumu kwa miaka 33 japo miaka hiyo watu waliishi kwa mamia ya miaka na hiyo ni kwa sababu kuu ya kupingwa..

nimeshakuwa na walimu chuoni ambao ni wasomi bingwa lakini wasioweza kuwa na ubora katika maisha mengine ya kawaida jambo ambalo ni hatari sana..

Jaribu kuchukulia hali halisi na si ubishani wa neno kwa neno la injili,injili ni pana na kila mtu anaielewa kimtazamo wake ndio maana hata kulizaliwa madhehebu ya kiprotestant,sababu kuu ni mitizamo tofauti

hata wasabato wanapingana nawe mluteri katika siku ya kuabudu nk, hivyo nadhani ni bora kujisemea wewe na si kuwasemea wao..

kumbuka wapo wala kitimoto na wasiokula lakini wote wanaishi dunia moja na unachat nao humu thru yr pc..hata hii invention ya computer ingekuwa instantly na ikakukuta huna elimu yoyote zaidi ya injili ungeweza kuipinga na kusema ni uchawi,ama technology ya simu ungekataa na kusema ni mungu pekee anayeweza kuongea na binadamu from distant location apart

lakini ni mungu ndiye huwafunulia wanadamu njia za kufanya ambazo ni uwezo wake kupitia kwa binadamu..
mfano alimuwezesha edison kuvumbua taa ya umeme je ungekuwapo ungesema kwa nini avumbue yeye na si wengine?

Tuwe wakweli na pia tumatch uhalisia
 
Mungu Yu Mwema. Natumaini BABU atampa asiye na ya kulipa kikombe FREE OF CHARGE yaani bure. Mungu angependa iwe hivyo. AMEN.
 
Mungu Yu Mwema. Natumaini BABU atampa asiye na ya kulipa kikombe FREE OF CHARGE yaani bure. Mungu angependa iwe hivyo. AMEN.
Mungu wa Yakobo na Isaka na Daudi yu "mwema" hawezi kumwotesha mtu ndoto wagonjwa wakateseke kwenye foleni na kujisaidia maporini kupata tiba!
 
ndugu pakajimmy,

hatukejeli wanaopata faraja huko kwa babu kutokana na magonjwa na madhaifu mbalimbali, la hasha. tunawashauri wapendwa wetu wasome na kufahamu ukweli juu ya nini yaliyo mapenzi na makusudi ya Mungu kama yalivyobainishwa ndani ya biblia na wapime na kujaribu kila roho kama inatokana na Mungu.

hivi kuna mtu huko samunge aliyepata majaribu kumshinda ayubu? mbona ayubu alikataa kumkufuru Mungu? iweje maelfu huko samunge wawe tayari kumdhihaki Mungu kwa sababu ya BP, cancer, ukimwi nk, eti kwa kupokea kikombe cha mchungaji mstaafu!

mwenye imani ya kweli na iliyojengwa kwenye neno (siyo iliyojengwa kwenye miujiza) atamtukuza Mungu hata apate mateso kiasi gani. atamtukuza Mungu hata katikati ya mateso, naam hata kama atamiminwa damu na kufa kama shahidi (martyr). imani yenu iko wapi sasa?

mimi niko tayri kuishi na majaribu ya ukimwi na mengineyo sugu lakini sio kumkufuru Mungu kiasi hicho cha samunge. ee Mwenyezi Mungu naomba nisaidie

Glory to God

Wangu usicheze na mungu......atakupa hicho unachotaka
 
pole sana mpendwa kwa misukosuko ya samunge.

Bwana anasema njooni kwangu wote wenye kulemewa na mizigo ya dhambi nami nitawapumzisha. jifunzeni kwangu kwa maana mimi ni mpole na myenyekevu wa moyo, nira yangu ni laini na mzigo wangu ni mwepesi. ulihangaika hivyo kwa kuwa ulienda kwa Babu samunge, hakika kwa Bwana Yesu aliye mahali pote, usingeteseka kiasi hicho. ukiijiua kweli, hiyo itakuweka huru

nakuombea afya njema na ubarikiwe sana na Bwana

Glory to God
Kwenda kwa bwana kuna maana nyingi; mimi nimeenda kwa babu kupata lile neno ambalo Mungu ameliweka kwenye huo mti; ni kama wewe unavyoenda kanisani; si kuna siku mvua inakunyeshea lakini hukati tamaa!
Miss Judith, nakushukuru kwa kunipa pole ila nasikitika kuona katika thread nyingi unaonekana kumpinga babu, licha kukueleza kwa ufupi ile briefing ya asubuhi. Kwa bahati nzuri nimeownload ile video ya the loliondo wonder part 2, babu anasema, unapokunywa dawa mtizame Mungu usimtizame mwanadamu! Je Mnataka aseme nini zaidi? Kwenye hiyo video sikiliza anavyomjibu yule mama aliyeuliza juu ya kufunguliwa njia za uzazi! Ni wapi aliposema tumtizame yeye kama mganga?
 
Wapendwa katika Bwana,

Naamini kila mmoja wetu anaufahamu vizuri mjadala unaoendelea juu ya Mch. Mwasapile. Maelezo ya baadhi ya mambo yalijitokeza katika mada yangu ile ni kama ifuatavyo:
1. Ni bora tukamwacha babu aendelee na kazi zake
kimsingi mimi na wote tunaohoji shughuli za uganga wa babu hatuna nia ya kumzuia babu kufanya shughuli zake hizo za kutibu kwa mitishamba, bali tunahoji uhalali wa madai yake kuwa shughuli hizo zimetokana na ufunuo wa Mungu. Na hii ni kwa sababu tukimpima kimaandiko, tunapata kila sababu ya kusema kuwa kama ni kweli kafunuliwa na Mungu, basi si Mungu huyu tunayemuabudu wakristo na aliyemtuma Bwana Yesu kuja duniani kutuokoa dhambini (kumbukeni kuwa kuna miungu mingine ya uongo hujiinua na kudai kuabudiwa kama Mungu aliye hai). Sababu zetu ni pamoja na kuwa
· Babu hafundishi neno la Mungu na hivyo hiyo huduma yake imelenga kuponya mwili pekee na si roho
· uponyaji wake umefungamana na mti Fulani na siyo Yesu Kristo
· Tiba yake imo ndani ya mipaka ya kijiji cha samunge pekee

· tiba yake haimuinui na kumtukuza Mungu bali anajiinua yeye mwenyewe na mti wake wa mrigariga

Hapa ndipo sikubaliani nawe:
Babu kabla ya kutoa huduma kila asubuhi huongea na watu na kuwaimarisha kiimani na kiroho. Anasema unapokunywa dawa mtizame Mungu, usimtizame binadamu - unataka aseme nini zaidi? Kumbuka hana muda wa kuhubiri muda mrefu.
Kwamba uponyaji wake umefungamana na mti fulani na si Yesu Kristo; babu anasema, kinachoponya si mti bali neno la Mungu lililowekwa na Mungu kwenye huo mti - hao utasema uponyaji umefungamana na mti? au neno!. Kwamba uponyaji wake haufungamani na Yesu Kristo, labda ni kweli kwa kuwa uponyaji wake umeelekezwa kwa watu wote hata wasiomwamini Kristo; Ndiyo maana yeye anamtaja Mungu ili wote waaminio kuwepo kwa Mungu waponywe kwa hilo neno lake. Ni wazi kama akisema naponya kwa njia ya Yesu Kristo - waislamu, wahindu, nk wasingeamini.
Kwamba Tiba iko ndani ya Samunge tu - jamani hata Yesu si alianzia kwa waislaeli kwanza? Huyu kaanzia Samunge na kila mwenye imani aende samunge. Mbona hata watu walitoka sehemu za mbali kumfuata Kristo? Kumbuka aliyetoka ethiopia!
Babu anamtukuza Mungu na si mti, nimeshaeleza hapo juu.
Nilisafiri na hivyo nikachelewa kusoma maneno haya.
 
Kwenda kwa bwana kuna maana nyingi; mimi nimeenda kwa babu kupata lile neno ambalo Mungu ameliweka kwenye huo mti; ni kama wewe unavyoenda kanisani; si kuna siku mvua inakunyeshea lakini hukati tamaa!
Miss Judith, nakushukuru kwa kunipa pole ila nasikitika kuona katika thread nyingi unaonekana kumpinga babu, licha kukueleza kwa ufupi ile briefing ya asubuhi. Kwa bahati nzuri nimeownload ile video ya the loliondo wonder part 2, babu anasema, unapokunywa dawa mtizame Mungu usimtizame mwanadamu! Je Mnataka aseme nini zaidi? Kwenye hiyo video sikiliza anavyomjibu yule mama aliyeuliza juu ya kufunguliwa njia za uzazi! Ni wapi aliposema tumtizame yeye kama mganga?

Hapa ndipo sikubaliani nawe:
Babu kabla ya kutoa huduma kila asubuhi huongea na watu na kuwaimarisha kiimani na kiroho. Anasema unapokunywa dawa mtizame Mungu, usimtizame binadamu - unataka aseme nini zaidi? Kumbuka hana muda wa kuhubiri muda mrefu.
Kwamba uponyaji wake umefungamana na mti fulani na si Yesu Kristo; babu anasema, kinachoponya si mti bali neno la Mungu lililowekwa na Mungu kwenye huo mti - hao utasema uponyaji umefungamana na mti? au neno!. Kwamba uponyaji wake haufungamani na Yesu Kristo, labda ni kweli kwa kuwa uponyaji wake umeelekezwa kwa watu wote hata wasiomwamini Kristo; Ndiyo maana yeye anamtaja Mungu ili wote waaminio kuwepo kwa Mungu waponywe kwa hilo neno lake. Ni wazi kama akisema naponya kwa njia ya Yesu Kristo - waislamu, wahindu, nk wasingeamini.
Kwamba Tiba iko ndani ya Samunge tu - jamani hata Yesu si alianzia kwa waislaeli kwanza? Huyu kaanzia Samunge na kila mwenye imani aende samunge. Mbona hata watu walitoka sehemu za mbali kumfuata Kristo? Kumbuka aliyetoka ethiopia!
Babu anamtukuza Mungu na si mti, nimeshaeleza hapo juu.
Nilisafiri na hivyo nikachelewa kusoma maneno haya.

ndugu, angalia maneno ya Mungu, usiangalie babu anasema nini. mengi ya maelezo yako yalishajibiwa humu kwenye thread hii, ukipitia post hizi kwa makini utaona almost kla jibu limo.

ubarikiwe sana

utukufu una Yeye Bwana hata milele
 
Back
Top Bottom