Hoja ya Shossi juu ya sh. 500/- ya babu

Hoja ya Shossi juu ya sh. 500/- ya babu

Kwa hiyo LD watu wote wanaohubiri kwa jina la Yesu unawakubali sio?
Yaani hii hukumu unayoitoa hapa kua babu asitibu kwa kumusisha mungu sijui unaitoa wapi?

Sio wote nina wakubali na ndio maana hata huyu sina vigezo vya kumkubali mpaka sasa hivi. Simkumu mtu hata kidogo, na wala hoja ya kwamba tumwamini kwa sababu alikuwa Mchungaji wa KKKT siikubali. Mkuu hapo juu sijui ni wapi ninaenda mbele na rudi nyuma lkn nachosema mimi, sina vigezo thabiti vya kumkubali wala kumkataa, namuomba Mungu, atajibu kwa wakati wake. So wakati utaamua mambo hapa. Haijalishi viongozi wa Kanisa wamemkubali cha msingi ni kuomba tu.

CPU hapo juu nashukuru sana kwa kunielewa.ASOMAE NA AFAHAMU!!!
 
Kimey

LD mara aseme hana elimu ya kujua kama Babu anasema ukweli au la mara atoe hukumu kuwa Babu asitumie Jina la Mungu!

Kweli Babu katuchanganya
Acha tu Mwalimu mi nilishawaambia toka mwanzo kama huwezi kudhibitisha uyaseamyo bora ukae kimya tu kuliko kutaka kulazimisha hoja!! Mtu anasema babu hajatumwa na Mungu, unaomba udhibitsho wa kile alichokisema anashindwa kueleza!
Mi ntkubaliana na yule tu atakaye sema kua amefunga na kuomba kwa Mungu akamwambia kua kweli huduma aitoayo babu sio sahihi, nitakubaliana nae kwa sababu yeye na babu hawatakua tofauti, kwani wote wanadai wameambiwa na Mungu! Ila asitake kulazimisha nimuamini kile anachokisema kwa kua hawezi kunidhibitishia!
 
  • Thanks
Reactions: CPU
Mkuu LD amejaa utata mtupu, mwanzoni alikuwa against huduma ya babu,

Baada ya kumpa darasa la kutosha akageuka, tena akakiri kwamba amekuelewa kumbe alikuwa anataka kukuchuuza.

Ghafla bilamkutarajia amerudi kule kule alikokuwa, kimsingi hajakuelewa kama alivyodai hapo mwanzo, wasiwasi wangu ni kwamba amelewa injili uliyompa!!

Mkuu
dada LD amenielewa KUSHOTO, maana si unaona hata hiyo NIMEKUELEWA KAKA ANGU anavyoisisitiza huku maelezo yake pia yakionyesha uelewa mwingine.
 
Sio wote nina wakubali na ndio maana hata huyu sina vigezo vya kumkubali mpaka sasa hivi. Simkumu mtu hata kidogo, na wala hoja ya kwamba tumwamini kwa sababu alikuwa Mchungaji wa KKKT siikubali. Mkuu hapo juu sijui ni wapi ninaenda mbele na rudi nyuma lkn nachosema mimi, sina vigezo thabiti vya kumkubali wala kumkataa, namuomba Mungu, atajibu kwa wakati wake. So wakati utaamua mambo hapa. Haijalishi viongozi wa Kanisa wamemkubali cha msingi ni kuomba tu.

CPU hapo juu nashukuru sana kwa kunielewa.ASOMAE NA AFAHAMU!!!
Mshiki unajichanganya sana, Unasema huna Vigezo vya kudhibitisha huduma ya babu kua ni kweli au si kweli, then hapo hapo unakuja kusema babu atibu ila Asilihusishe Jina la Yesu na Mungu!! mi ndo maana sikuelewi msimamo wako!
 
ni hivi punde tu nilikuwa naongea na mtu toka Eritrea akanipa ushuhuda wa mtu mwenye shughuli kama za babu huko kwao, ngoja nimdadisi zaidi, nikipata maelezo mazuri nitakuja kuwadokeza hapa jamvini.

by the way, nafurahi sana jinsi mjadala huu unavyokwenda. bahati mbaya nimebanwa na majukumu, but baada ya 30 minutes nitakuwa free, ntarudi kujibu hoja zote za msingi zinazonihusu. kipekee niwashukuru wote mnaoendelea kuitetea injili ya kweli na msingi wa manepo ya Mungu. kwa neema ya Mungu tutazishinda hila za shetani. amina

mbarikiwe sana wapendwa.

Glory to God
 
Sio wote nina wakubali na ndio maana hata huyu sina vigezo vya kumkubali mpaka sasa hivi. Simkumu mtu hata kidogo, na wala hoja ya kwamba tumwamini kwa sababu alikuwa Mchungaji wa KKKT siikubali. Mkuu hapo juu sijui ni wapi ninaenda mbele na rudi nyuma lkn nachosema mimi, sina vigezo thabiti vya kumkubali wala kumkataa, namuomba Mungu, atajibu kwa wakati wake. So wakati utaamua mambo hapa. Haijalishi viongozi wa Kanisa wamemkubali cha msingi ni kuomba tu.

CPU hapo juu nashukuru sana kwa kunielewa. ASOMAE NA AFAHAMU!!!

Bila shaka kama huna imani kwamba Mungu anaweza kumtumia Babu kufanya kazi yake basi tuache aendelee na wenye imani na Mungu kupitia kwa Babu, maana huna vigezo vya KUKUBALI wala KUKATAA. Basi tusimwamuru aache kutumia Jina la Yesu.

Nashukuru kwa KUNIELEWA dada angu, wala huna sababu ya kuisisitiza hiyo elewa, maana hata mimi NAKUELEWA sasa.
Nimesoma na KUFAHAMU
 
My conclusion ni kwamba
SAUTI YA WENGI NI SAUTI YA MUNGU
Na umeona sauti ya wengi ilivyokupinga kwa nguvu zote. Hii thread lazima itakuwa imekuharibia siku yako kwa namna fulani.

Kama sauti ya wengi ni sauti ya Mungu basi vipi aje Yesu pekee kuikomboa dunia yenye mamilioni ya wanadamu? Kina Musa, Elia, Elisha, Yohana wangetosha kutuelekeza mbinguni wala tusingepotea. Kumbuka kwenye imani hakuna democrasia neno la Mungu litabaki hata dunia na mbingu zitapita. Kwahiyo usije ukawa una commite communal sin bila kujua ni vyema ukaji nyenyekeza kwa Roho mtakatifu akufunulie na akisha kupa reveletion kama babu alivyo pewa na roho anayoijua yeye basi ungekuwa na haki ya kuhukumu lakini kwa kufuata wanadamu utapotea ndugu yangu.
 
kaaaaaaaaaaazi kweli kweli hapa hata ashuke nani hatoeleweka bora kusubiri tu wakati uamue
 
Mkuu LD amejaa utata mtupu, mwanzoni alikuwa against huduma ya babu,

Baada ya kumpa darasa la kutosha akageuka, tena akakiri kwamba amekuelewa kumbe alikuwa anataka kukuchuuza.

Ghafla bilamkutarajia amerudi kule kule alikokuwa, kimsingi hajakuelewa kama alivyodai hapo mwanzo, wasiwasi wangu ni kwamba amelewa injili uliyompa!!

Nimemwelewa CPU, jinsi anavyoipeleka Imani yake.
Sikutaka kuendeleza mjadala mrefu kwenye hiyo,
Na ndio maana , kuna sehemu anasema yeye mwenyewe,
Katafakari halafu kaelewa ninachokimaanisha.
Kwa maana hiyo kama ni kweli amenielewa, ataelewa ni kwa nini na mimi nilisema nilimwelewa kule juu.
 
Mara Yesu asitumike kuombea,mara 500 nyingi basi tu vurugu tupu.Mods close this thread watu watatoboana macho maana imepoteza mvuto wa kuitetea
 
Mbona mambo mema na maovu yanajulikana wazi tuu, yaani wewe unataka kuniambia ukifanya kosa dhamira yako haikuhukumu?
Kuhusu babu mimi sina haki ya kumuhumumu na siwezi fanya hivyo kwasababu wote tumetenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu (warumi 3:23) ila tuu nunatakiwa tuwe waangalifu.

Hili lakutenda dhambi linawahusu ambao hawajamjua Mungu ukisha kuwa mtoto wa Mungu trait ya dhambi inaondoka unabaki kuwa sawa na Mungu yaani born again in spirit, dhambi haina tena dominion juu yako na neema ya kuishinda ni kubwa sana kama vile mtu mzima kula mavi haiwezekani na akiweza ujue basi akili ishamruka. Kama uko born again na bado dhambi inakutawala rudi magotini omba neema ya Mungu akujaze roho mtakatifu maana unajidanganya wala Yesu hakujui maana wote waliompokea aliwapa nguvu ya kuwa wana wamungu na hivyo ndivyo tulivyo. Je Mungu anatenda dhambi? Je Yesu alishawahi kutenda dhambi?

kama unaamini Mungu wala Yesu hawawezi tenda vipi basi mtoto wa Mungu atende dhambi? Yesu ni mtoto wa kwanza wa Mungu na baadaye kina Paulo na mitume kumi na mbili na wenginewaliokuwa Yerusalem siku ya Pentekoste wakawa wazaliwa wa pili nasi tukazaliwa baadaye na bado wengine wanaendelea kuzaliwa kila siku wanapoyatoa maisha yao kwa kristo.

Ubarikiwe mpendwa kasome tena kitabu cha matendo ya mitume na waraka wa Paulo kwa warumi then soma waraka wa Petro uone nini nazungumza.
 
kaaaaaaaaaaazi kweli kweli hapa hata ashuke nani hatoeleweka bora kusubiri tu wakati uamue
Yaani we acha tuu ila afadhali sasa kwasababu wale waliokuwa wanaleta kejeli na kuleta personal attack badala ya hoja za maana wamewekwa sawa.
 
Acha tu Mwalimu mi nilishawaambia toka mwanzo kama huwezi kudhibitisha uyaseamyo bora ukae kimya tu kuliko kutaka kulazimisha hoja!! Mtu anasema babu hajatumwa na Mungu, unaomba udhibitsho wa kile alichokisema anashindwa kueleza!
Mi ntkubaliana na yule tu atakaye sema kua amefunga na kuomba kwa Mungu akamwambia kua kweli huduma aitoayo babu sio sahihi, nitakubaliana nae kwa sababu yeye na babu hawatakua tofauti, kwani wote wanadai wameambiwa na Mungu! Ila asitake kulazimisha nimuamini kile anachokisema kwa kua hawezi kunidhibitishia!

thumbs_up_large.png
 
Nimemwelewa CPU, jinsi anavyoipeleka Imani yake.
Sikutaka kuendeleza mjadala mrefu kwenye hiyo,
Na ndio maana , kuna sehemu anasema yeye mwenyewe,
Katafakari halafu kaelewa ninachokimaanisha.
Kwa maana hiyo kama ni kweli amenielewa, ataelewa ni kwa nini na mimi nilisema nilimwelewa kule juu.

Naona CPU amekugusa sana leo, lakin huyo huyo CPU hana tofauti na misimamo ya akina Kimey, Gaijin, Mwita Maranya, PakaJimmy, Dena Amsi, Realman na wengine kibao. Nashukuru kwa kunielewa tofauti na hao wengine
 
Sio wote nina wakubali na ndio maana hata huyu sina vigezo vya kumkubali mpaka sasa hivi. Simkumu mtu hata kidogo, na wala hoja ya kwamba tumwamini kwa sababu alikuwa Mchungaji wa KKKT siikubali. Mkuu hapo juu sijui ni wapi ninaenda mbele na rudi nyuma lkn nachosema mimi, sina vigezo thabiti vya kumkubali wala kumkataa, namuomba Mungu, atajibu kwa wakati wake. So wakati utaamua mambo hapa. Haijalishi viongozi wa Kanisa wamemkubali cha msingi ni kuomba tu.

CPU hapo juu nashukuru sana kwa kunielewa.ASOMAE NA AFAHAMU!!!

LD, kama huna vigezo vya kumkubali wala kumkata babu hapo ndipo umepiga hatu kwa kujiepusha kumhukumu mtu ili usije ukahukumiwa.

Mara ulipogeuka na kumtaka babu asilitaje jina la YESU kwenye huduma yake hapo ndipo uliporudi nyuma, kwa kuwa umekubali kunaswa na mtego ule ule uliojaribu kujinasua.
 
Pia fahamu kwamba njia za Mungu (nakushauri uwe unaanza na herufi kubwa kila unapoandika jina la Muumba wako) hazina cha kuwa great thinker wala thin thinker, sisi sote ni mali yake. Hata babu nae ni mali ya Bwana.
Mbele za Mungu hakuna anaefanana nae kwa kufikiri wala kumkaribia. Uwe great thinker wa JF, mimi nisiwe sote tuko sawa mbele za Mungu.
Kwa imani yako kwamba huenda babu anafanya kazi za shetani, fanya maombi basi ili babu aanguke na ashindwe ktk kazi zake, kuja hapa hapa kumpongeza Shossi hakusaidii kumzuia babu asifanye kazi yake (ambayo wewe unaiona kama ya kishetani)

HAKUNA BINADAMU ANAEWEZA CHUNGUZA NJIA ZA MUNGU WETU
USIHUKUMU USIJE UKAHUKUMIWA

Hayo yalisemwa na Isaya enzi zile roho mtakatifu alipokuwa hajawa released. In this era mawazo yetu yana fanana na ya Mungu ndiyo maana tunaambiwa tuukulie wokovu maana mwana wa mfalme/mrithi akiwa mtoto hatofautishwi na mtumwa/kijakazi. Tena tunaambiwa vita vyetu si vya damu na nyama bali katika mawazo yetu hadi tutakapo angusha kila elimu na wazo linalopingana na mawazo na understanding ya kristo. Akatuambia hakuna awezaye kujua mawazo ya roho iwe ya mtu au mnyama isipokuwa roho mwenye hiyo roho na ndivyo kusema mambo ya Mungu ayajua roho wa Mungu maana yumo ndani ya Mungu. Akaendelea kusema kama roho ya Mungu iko ndani yenu basi mmefanyika kuwa Miungu/watoto wa Mungu maana paka hawezi zaa panya; wala mbwa kuzaa ng'ombe kama ndivyo Mungu anazaa nini? Swali ni je umezaliwa na Mungu kwa nguvu ya Roho wa Mungu? Kama bado yes mawazo ya Mungu huwezi kuyajua katu ni mbingu na dunia na wala hutawahi kuyajua na hatima yake ni wewe kuingia shimoni maana kweli yake haimo ndani yako.
 
Mimi naona watu waache wivu, waliozoea kujizolea sifa kwa ajili ya kuponya watu sasa wanamuona babu kama threat, wengine ambao walikuwa wanatibu kisukari kwa shilling milion 3 kupitia mgongo wa kanisa wanaona hawana future. Wale waliozoea kutangaza bank account zao na M-pesa ndo wanaotusumbua humu. Babu aendelee kusaidia watu na kama yeye Judith atenda kwa imani ya shetani basi atatibiwa kwa nguvu za shetani lakini kama anaamini kuwa mungu anamtumia babu kuponya watu wake basi atakuwa ameponywa na Mungu. Je hawa watu walitaka hizi nguvu apewe mzungu? au Tortoise pekee? Mbona wengine wanaponya kwa vitambaa na hamuwasemi?
 
Kwahiyo wewe tu ndo unaruhusiwa kulitumia jina la YESU lakini mchungaji mstaafu aliyetumia muda wa maisha yake kumhubiri YESU kristo sasa haruhusiwi tena kulitaja jina kla YESU kwenye huduma yake kwa kuwa tu hupendi?? kazi bado mbichi kwa kweli, unakwenda mbele hatua tano kisha unarudi nyuma hatua kumi!!

Haina maana mimi tu ndio nitumie hapana.
Wala hatutakiwi kumkubali kirahisi tu kwa sababu alikuwa Mchungaji na Wachungaji wamemkubali.
Atumie jina la Yesu, lakini afundishe watu, waelewe na kumkubali Bwana Yesu, kama bwana na Mwokozi wa Maisha yao.
Awafundishe kuabudu katika jina la Yesu, halafu awape dawa wa pone.
Inakuwaje unamwambia mtu nimekuponya kwa jina Yesu anaondoka wala hasemi habari za Yesu anasema habari za Kikombe na Babu mwenyewe.

Hayo ni maswli ambayo yananifanya nishindwe kuikubali na kuiamnini.
Kwa upande mwingine, Njia za Mungu zipo nyingi, kutokana na hilo ndo maana na sema TUOMBE UKWELI UJULIKANE.
Yawezekana mmenilewa vibaya au nimejieleza vibaya hapo juu, ila lengo langu ni kwamba. NIngemwelewa Babu kama asingemhusisha Mungu kwa Jina la Yesu, katika hiyo dawa yake, ikajulikana tu kuna Dawa imegunduliwa na babu inaponya watu, wa DINI zote, kabila zote, na Rangi zote, iwe unamwamini Yesu au humwamini pia. We amini kikombe na Babu mwenyewe basi.

Unaposema Kikombe kina ponya kwa jina La Yesu, wakati kuna watu hawataki kulisikia hata hilo jina la Yesu, lakini wanakwenda kwa sababu ya magonjwa na Mateso tu, mimi nakuwa sielewe. Ndio maana nikasema Basi yeye atibu tu, kwa mti na maji kama hana nafasi ya kufundisha habari za Yesu aache kulitumia hilo jina.

Tuendelee kuweka Imani yetu, kwenye Hayo maji na huo mti.
Mbarikiwe.
 
LD, kama huna vigezo vya kumkubali wala kumkata babu hapo ndipo umepiga hatu kwa kujiepusha kumhukumu mtu ili usije ukahukumiwa.

Mara ulipogeuka na kumtaka babu asilitaje jina la YESU kwenye huduma yake hapo ndipo uliporudi nyuma, kwa kuwa umekubali kunaswa na mtego ule ule uliojaribu kujinasua.

Nimesema hivyo ktk msingi na mtazamo huo hapo juu.
Si unajua kuwa 50/50 eeh, sasa ndo mimi!!! Labda niseme hivyo.
 
Naona CPU amekugusa sana leo, lakin huyo huyo CPU hana tofauti na misimamo ya akina Kimey, Gaijin, Mwita Maranya, PakaJimmy, Dena Amsi, Realman na wengine kibao. Nashukuru kwa kunielewa tofauti na hao wengine

Acha hizo CPU,
Vita vyetu si vya DAMU NA NYAMA.
We omba tu.
 
Back
Top Bottom