Hoja ya Shossi juu ya sh. 500/- ya babu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hoja ya Shossi juu ya sh. 500/- ya babu

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Ms Judith, Mar 21, 2011.

 1. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #1
  Mar 21, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  nianze kwa kuweka wazi kuwa sina hakika na imani ya huyu ndugu yetu Mohamedi Shossi, sijui kama ni mwislamu, mkristo ama muumini wa dini nyinginezo.

  aliweka wazi kuwa babu si size ya Yesu na alisema kuwa Yesu ni "world icon" na babu hawezi kulinganishwa naye hata kidogo. baadhi walimkosoa kumwita Yesu "world icon" na walikuwa na sababu zao. pia ametoa michango mingi tu mingine ila hapa nataka niungane naye na kumpongeza kwa kuhoji hiyo bei ya babu.

  Mungu wetu afikie mahali apange bei!! tena ya huduma itokanayo na karama aliyotoa mwenyewe? kweli hapo pagumu kuingia akilini. tena mungu wake huyo akampa na mchanganuo wa namna atakavyozigawa hizo pesa, eti 300/- kwakanisa, yatima na wajane na 200/- za wahudumu wanaomsaidia kazi! kwa kweli naona kama hizi ni kashfa kwa Mungu wetu.

  neema ya Mungu wetu ni kubwa na pana sana, na kamwe huyu babu asiichezee kiasi hiki. yeye atangaze kuwa ni mganga aliyekuja na dawa ya mti wa mrigariga, afuate taratibu za serikali za kujisajili kisheria ili serikali itambue kazi zake na aweke bei yake kama wawekavyo waganga wengine na tutamchukulia kama tunavyowachukulia waganga wengine.

  hongera tena Mohamed Shossi, hoja yako ni njema na ya kweli. Mungu wetu hahitaji hata senti yetu moja. karama zake hutoa bure. michango kwa ajili ya kazi ya Bwana ni ya hiyari na kadiri mtu alivyojaaliwa kutoa.

  ukishaweka bei (hata kama ni sh.10/-) maana yake ni kwamba asiye nayo hapati huduma! kumbuka madukani kuna pipi za sh.10/- na usipokuwa na hiyo sh.10/- hupati hiyo pipi. ndiyo maana ya bei. sasa babu anasema kama huna sh. 500/- kaa pembeni mwenye hela aje apate kikombe! hata akiamua kuwasamehe wengine kulipa, manake atakuwa kakiuka utaratibu wa huyo mungu wake anayedhibiti bei! sasa hii nayo bado ni huduma ya kiroho kweli kwa mujibu wa dini ya kikristo? mungu gani huyu anayepanga hesabu hivi?

  tuendelee kutafakari na kuliombea kanisa

  Mungu akubariki sana ndugu Mohamedi Shossi,

  Glory to God!
   
 2. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #2
  Mar 21, 2011
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Mungu alimtuma yesu, wayahudi wakamuua , amemtuma babu hamtaki kuamini dawa yake.. Mnataka amtume nani?
  Dada nenda kanywe dawa kwa babu inatibu. iwe mia au 100,000 uponyaji upo watu wanapona
   
 3. daughter

  daughter JF-Expert Member

  #3
  Mar 21, 2011
  Joined: Jun 22, 2009
  Messages: 1,275
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Miss Judith,thank you very much for this useful thread. But for as long as nimeshafika kwa babu na kupata kikombe kinachonipa ahueni kubwa ya maradhi 'niliyokuwa' nayo, sitahoji lolote kuhusu hiyo mia tano. Infact natamani ningeweza kulipa zaidi
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Mar 21, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Ni hadithi za Abunuwas na kufuru kubwa na kulinganisha pipi ya shiing 10 dukani, na Malignant cancer, au Chronic Asthma, au HIV/Aids, Au Blood Pressure!
  Ukiona mtu yeyote anaongea commedies ujue wazi hajaugua!...Hivi mnayajua hayo magonjwa niliyotaja hapo juu....mnajua usumbufu wake?
  Msicheze na ufundi wa kuongea maneno bana!
   
 5. Kunta Kinte

  Kunta Kinte JF-Expert Member

  #5
  Mar 21, 2011
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 3,660
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Umenipa jambo la kufikiria, mungu ameelekeza na mgao wa mapato!!!
   
 6. daughter

  daughter JF-Expert Member

  #6
  Mar 21, 2011
  Joined: Jun 22, 2009
  Messages: 1,275
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Nimekupa thanx kaka. Watu wanaongea tu na kutunga hadithi hayajawafika bado. Sioni tu vile unaweza compare 500 na kisukari cha zaidi ya miaka 10
   
 7. S

  Strategizt Senior Member

  #7
  Mar 21, 2011
  Joined: Oct 16, 2009
  Messages: 176
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Ni kweli kabisa wanaongea kwa nia ya kujifurahisha! Ila waendelee kumuomba Mungu yasiwapate maradhi hayo maana watamkumbuka Babu na wakati huo sidhani kama atakuwepo bado au la
   
 8. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #8
  Mar 21, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  ndugu pakajimmy,

  hatukejeli wanaopata faraja huko kwa babu kutokana na magonjwa na madhaifu mbalimbali, la hasha. tunawashauri wapendwa wetu wasome na kufahamu ukweli juu ya nini yaliyo mapenzi na makusudi ya Mungu kama yalivyobainishwa ndani ya biblia na wapime na kujaribu kila roho kama inatokana na Mungu.

  hivi kuna mtu huko samunge aliyepata majaribu kumshinda ayubu? mbona ayubu alikataa kumkufuru Mungu? iweje maelfu huko samunge wawe tayari kumdhihaki Mungu kwa sababu ya BP, cancer, ukimwi nk, eti kwa kupokea kikombe cha mchungaji mstaafu!

  mwenye imani ya kweli na iliyojengwa kwenye neno (siyo iliyojengwa kwenye miujiza) atamtukuza Mungu hata apate mateso kiasi gani. atamtukuza Mungu hata katikati ya mateso, naam hata kama atamiminwa damu na kufa kama shahidi (martyr). imani yenu iko wapi sasa?

  mimi niko tayri kuishi na majaribu ya ukimwi na mengineyo sugu lakini sio kumkufuru Mungu kiasi hicho cha samunge. ee Mwenyezi Mungu naomba nisaidie

  Glory to God
   
 9. Nanren

  Nanren JF-Expert Member

  #9
  Mar 21, 2011
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 1,739
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Hivi na zile sadaka zinazotolewa kanisani (sadaka maalum, sadaka ya kawaida ya mkristo, ahadi ya mkristo, Sadaka ya jengo, Fungu la kumi, n.k) nazo zitakuwa na kasoro kama ilivyo 500 ya babu? Au zile sadaka zinazotolewa kwenye makongamano/mikutano ya injili na uponyaji, hazipokelewi?
   
 10. bmx

  bmx Member

  #10
  Mar 21, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 67
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  huna iman hiyo dada, sema matatizo hayajakufika,,
   
 11. Ngorunde

  Ngorunde JF-Expert Member

  #11
  Mar 21, 2011
  Joined: Nov 17, 2006
  Messages: 1,128
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  Miss Judith hujaumwa, hutajua machungu ya ugonjwa. Eti uko tayari kuishi na magonjwa sugu..!!? Mwombe Mungu aendelee kukupa afya ila usiwadhihaki wenye kuhitaji tiba.
   
 12. Susy

  Susy JF-Expert Member

  #12
  Mar 21, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 1,450
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  :peace:
   
 13. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #13
  Mar 21, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Kwa kweli hayo magonjwa ni mazito na yanatisha sana. Lakini kuna ushahidi kuwa babu anayatibu? Nani kapona kansa au ukimwi mtusaidie wanaJF hapa barazani. Mimi namutazamia Lyatonga kama atapona nitajifariji kidogo kwamba walau mtu mmoja wa kisukari amepona lakini wa kansa na ukimwi je? Mwisho wa babu ni mbaya!!!
   
 14. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #14
  Mar 21, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,278
  Trophy Points: 280
  Hii thread yako dada unatutafutia ban wakati hata keki ya birthday yangu sijaikata. naomba unijibu maswali madogo, kama kazi za mungu zote ni bure, ni kwa nini biblia tunauziwa? pili, ni kwa nini mapadri na wachungaji wanalipwa mishahara/ posho kwa kazi za mungu? je umesahau ya kwamba mtu hawezi kuishi kwa mkate tu ila kwa kila neno anenalo toka ndani ya kinywa chake? je zile sadaka zinazotolewa kwa mamilioni makanisani, huwa kuna ndege inakuja kuzichukuwa zile sadaka na kuzipeleka mbinguni kwa sir God?
  Ni hayo tu machache naomba unijibu kabla sijaanza kuchangia hii thread yako. kumbuka hiyo ni dibaji tu.
   
 15. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #15
  Mar 21, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 935
  Trophy Points: 280
  Kama sikosei Miss Judith ni muumini wa lile kanisa la mahubiri ya vipaja vya kuku kwenye friji a.k.a kanisani kwa Mama Mikocheni B. Uzandiki mtupu....
   
 16. KIWAVI

  KIWAVI JF-Expert Member

  #16
  Mar 21, 2011
  Joined: Jan 12, 2010
  Messages: 1,748
  Likes Received: 379
  Trophy Points: 180
  nIJUAVYO MIMI... Miss Judith atapata shughuli yake muda si muda, watoto wa mjini wanasema Mungu wa sasa kijana

  tic-tac
   
 17. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #17
  Mar 21, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Watu kama hao akiuguliwa na nduguye au kuugua mwenyewe wala hahoji mara ya pili!..
  Ni rahisi sana kuandika kwenye keyboard...Lakini unapokuwa na mgonjwa ndani, wa kuanikwa na kuanuliwa, unatamani atokee mtu yeyote akupe altenative!..
  Miss Judith, ubarikiwe uzidi kuwa na afya njemA ili uyaishi maneno yako!...Wewe una muda wa kutosha wa kupima na kujaribu roho, lakini elewa kuna mwenzio ambaye yuko na miaka 5 kitandani hajasimama...
  Its easy said than done...always!
   
 18. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #18
  Mar 21, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Hakuna neno sahihi ninaloweza kuliweka hapa zaidi ya wivu na hii sasa imekuwa ugonjwa mbaya unaolitafuna taifa letu Tanzania.Fuatilia matamko ya viongozi wa dini hasa yale madhehebu yanayojitangaza sana through TV utagundua wanasumbuliwa na wivu bahati mbaya hata wewe Miss Judith unaangukia kwenye kundi hilo.

  Binafsi nimekutana na wagonjwa waliokuwa wakisumbuliwa na ugonjwa wa kisukari hakika wangebahatika kukutana na wewe wangekutupia mayai viza kama siyo kukutemea mate.
   
 19. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #19
  Mar 21, 2011
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,012
  Trophy Points: 280
  .
  Hivi aliyepanga zaka. 10% ya kila unachopata sii mali yako ni ya Mungu ni nani?
  Na hata kama utaamua kuikopa hiyo zaka, irudi na riba ya 5%. Haya ni mahesabu ama sio mahesabu? Na ni nani anakabidhiwa hili fungu na kwa kazi gani?
  Miss judi, tusaidiane hapa tunatafuta maarifa ya kimungu.
  .
   
 20. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #20
  Mar 21, 2011
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Nenda kasome biblia uone mahali kibao Mungu anatoa vipimo kamili! Kwa mfano, 10%, wakati wanajenga hema la kuabudu, nk. Utasema hapo sio Mungu kupanga kila kitu? Point yako haina nguvu hata kidogo!
   
Loading...