Naomba niweke wazi kitu kimoja hiyo mia tano inayoonekana kama tunaipinga kwa wivu si kweli kwani kama matumizi yake ni kusaidia wajane na masikini biblia imesema "[FONT=Bookman Old Style, Times New Roman, Times Roman, Serif]Uzeni mali yenu mkawape maskini misaada. Jifanyieni mifuko isiyochakaa, na jiwekeeni hazina mbinguni ambako haitapungua. Huko wezi hawakaribii, wala nondo hawaharibu, [/FONT][FONT=Bookman Old Style, Times New Roman, Times Roman, Serif]Pale ilipo hazina yako, ndipo pia utakapokuwa moyo wako.[/FONT][FONT=Bookman Old Style, Times New Roman, Times Roman, Serif]" Luka 12:32-33[/FONT]
Mimi na wewe Miss Judith tunachokipinga ni kuwapa "kikombe" bila kuwapa neno la Mungu hata biblia imesema [FONT=Bookman Old Style, Times New Roman, Times Roman, Serif]"Mtumishi ambaye anajua matakwa ya bwana wake lakini hajiweki tayari kufanya anavyotakiwa, atapigwa sana".[/FONT] Luka 12:34 ndio maana mimi na wewe tunampinga babu si kwa kuwa anapokea mia tano ila kwakuwa hawapi watu chakula cha roho hafanyi anavyotakiwa kufanya!
Naona tatizo la wachangiaji wengi wa mada hii ni kuchangia bila kufanya ufuatiliaji au hata ka utafit kadogo ka kufika kwa babu physically hata kama si kwa kunywa dawa.
Kila asubuhi saa moja babu hutoa briefing kwa wanaokuwepo. Nilishuhudia watu wakitoka kwenye magari hata yaliyokuwa umbali wa kilometa 8 kuja kusikiliza briefing ya babu. Kwa kifupi siku ya tarehe 18/3/2011 katika briefing alisema yafuatayo (mimi nilikuwepo):
Dawa hiyo ameoteshwa kutibu magonjwa matano yasiyo na dawa za kawaida nayo ni Ukimwi, kisukari, kansa, pumu, na kifafa. Lakini alisema kuna watu wametoa ushuhuda kuwa wamepona magonjwa tofauti na hayo; kuna waliokuja na kipofu akapona na wengine kiwete akatembea. Huo ni ushuhuda wa watu
Kwa wenye HIV, ndani ya muda wa siku saba vidudu vitakuwa vimefungwa na haviwezi kukushambulia, na baada ya mwezi mmoja vitakuwa havipo tena, hivyo aliwashauri wanaopima baada ya kunywa kikombe wasiwe na waswasi ikiwa watapima ndani ya siku 7 na wakaambiwa vidudu bado vimo. Alitoa tahadhari ya kutokwenda kuendekeza tena kale kamchezo kwani dawa inanywewa mara moja tu; hivyo ukipata tena ugonjwa haitakusaidia.
Dawa si ya dhehebu wala dini fulani; hivyo aliwaasa viongozi wa makanisa mbalimbali na dini mbalimbali wasiwazuie waumini wao kuja kuponywa.
Kuhusu watu wanaotafuta hiyo mizizi ya mti huo ili waondoke nayo, alisema haitawasaidia kwani ameoteshwa dawa aitoe yeye mwenyewe kwa mkono wake na inywewe pale pale. Akasema hajui kama Mungu kamteua mtu mwingine wa kutoa dawa hiyo.
Alisema yeye si mganga na hivyo yeye hatibu; kinachotibu ni neno la Mungu aliloweka kwenye huo mti, yeye ni wakala tu wa kuunganisha mgonjwa na neno hilo.
Kuhusu watu wanaochakachua foleni kuwa wakinywa wanakunywa juisi au maji alisema yeye hajasema hayo, yeye anachotoa ni dawa, ila hiyo isiwe kigezo cha kuvuruga foleni kwani nyote miacha magari yenu mkajirundika hapa, hamtaweza kuhudumiwa.
Kwa magonjwa mengine (yale manne) alisema matokeo utayaona mapema zaidi kama pumu, kisukari, kifafa na kansa. wa kansa kama iko kwa nje utaona mabadiliko ndani ya siku tatu tu!
(Alitulaumu eti tumezuia vyombo vya kuchemshia dawa kwani kuna gari limevibeba lakini tunainyima njia ya kupita)
Kama kawaida, aliruhusu maswali:
Wa kwanza aliuliza juu ya mwanae kuwa na kisukari kwa miaka 6; umati ulihamaki na kumjibu kuwa huyo atapona usiwe na hofu. Niliona babu akiongea naye kwa sauti ya chini sikusikia alichomweleza.
wa pili alisema niko katika ndoa kwa muda mrefu lakini sijapata mtoto; je dawa itanisaidia? Babu alianza kwa kumpa pole; kisha akamwambia - watoto hutoka kwa Mungu na dawa imetoka kwa Mungu, hivyo kunywa dawa huku ukiomba bila shaka Mungu atakusaidia.
Swali lililofuata lilihusu wagonjwa mahututi, au wasio na uwezo wa kufika hapo alipo babu kwamba anaonaje akiwapa hiyo dawa wakawapelekea ali mradi yeye ameshaibariki? Aliwajibu kuwa yeye ameelelezwa kuwa dawa itanywewa pale na hajaelekezwa vinginevyo, hivyo wafanye bidii wawalete. "Kama nitaelekezwa vinginevyo basi nitafanya kulingana na maelekezo"
Mimi nilimuuliza swali: Kwa mfano nimekuja hapo nina ukimwi, nimekunywa dawa na kupona, nimerudi nyumbani lakini kwa bahati mbaya nikapata kisukari, je naweza kuja kunywa dawa mara ya pili kwa ugonjwa huu mpya? Alisema "sina jibu" Kwa kadri nilivyooteshwa mtu atakunywa dawa hii mara moja tu; kwamba sasa uje mara ya pili kwa ugonjwa tofauti - sina jibu. Lakini Mungu si wa hivyo - yaani leo uje na ugonjwa sugu unywe dawa upone halafu upate tena ugonjwa mwingine sugu? Hakika Mungu si wa hivyo - ila ikitokea hivyo - sina jibu!
Mama mmoja aliuliza kuwa mwanae haeleweki - mara ni wa kike mara ni wa kiume. Kwa kweli wengi au labda niseme mimi sikumwelewa alimaanisha nini, ila babu alimweleza hivi - hakika Mungu hushinda nguvu zote za giza.
Baada ya hapo yalianza maswali ya kurudia ikionekana kuwa wanouliza walichelewa - Babu alifunga kipindi hicho kwa sala fupi akituombea wote tuliosafiri kuja pale ili tuweza kuponywa hayo mateso tuliyokuja nayo na hatimaye turudi nyumbani salama tukimtukuza Mungu kwani ndiye muweza wa yote.
umati uliomba tutawanyike ili tuweze kupewa dawa. Tulirudu kwenye mgari yetu na kuendelea kupokea kikombe na kuondoka.
Kati ya watu 10 tuliokuwa kwenye gari, aliyepata nafuu ya haraka ni wa pumu. Wakati tuanaenda alikuwa amevaa jaketi na khanga ili asidhurike sana lakini baada ya kunywa dawa aliweza kuachia jaketi kuvaa nguo za kuacha mabega nje licha ya mawingu, mvua na baridi iliyokuwepo! Wengine matatizo yetu yatachukua muda zaidi ili kuthibitisha uponaji wetu.
Huyo ndiye babu - nisingeweza kuandika neno kwa neno kwa yote aliyosema; hayo ni kwa ufupi tu. Safari yetu tulifika kijijini Samunge jumatano saa 12.05 jioni, tukapata kikombe ijumaa saa 2 asubuhi. Mvua iliyonyesha kwa wingi siku ya alhamisi ililowesha kuni na hivyo dawa kuchemshwa kidogo mchana na kuisha saa moja jioni ambapo babu alisitisha huduma yake hadi kesho yake. Kama angetoa dawa kama kawaida hadi saa tatu usiku, tungekunywa siku hiyo.