Hoja ya Shossi juu ya sh. 500/- ya babu

Hoja ya Shossi juu ya sh. 500/- ya babu

Chamoto kama umesoma post zangu kabla nilisema "Binafsi sina uhakika na dawa anayotoa babu lakini sitotenda haki kuisema negatively kwa vile isije ikawa kwa kufanya hivyo ukawa unashindana na Mungu mwenyewe".

Ninapinga watu ku-conclude kwamba anachofanya yule babu si cha Mungu bila kuonyesha kimaandiko kwamba si cha Mungu. Binadamu tunadhani tunaweza kumchagulia Mungu nani amtumikie na amtumikie vipi. Ni vipi kama kweli mtu akinywa dawa na akapona undhani sifa atampa Mungu yupi hata kama hakuhubiriwa injili siku hiyo??? Kama Rahabu kahaba alikuwa ni mtumishi wa Mungu, Mchungaji mstaafu je??

Tuseme tu kwamba TUSIHUKUMU maana nani ajuaye kama afanyacho babu ni Kazi ya Mungu, ni nani yuko tayari kushindana na Muumba wake?? Eti chungu kimwambie mfinyanzi hujui kazi yako wewee... thubutuuuuu!!!!!!!!!!!!!!!!

Tupo pamoja ndugu ila tunatakiwa tuhoji kwa maandiko (mfano kwanini hawaambi walioponywa wamtukuze Mungu) na kuomba na Mungu ni mwema atatuwezeka kutambua kweli.
 
hahahaha!
UEFA CUP hiyo.....

lakini nimepata storiiz chini ya carpet kwamba BABU NI FREEMASONS live...

nasikia hata dawa wanakunywa watu watano watano....
Hommie kwa hiyo mtu ukiinywa hiyo dawa baadae unaanza kutenda kinyume na matakwa ya Mungu? au inakuwaje hapa? huu ufreemansons unafaidikaje hapa?
 
Mkuu

Tatizo LD ameanza kuiona hii thread huku mwishoni, hajui chanzo cha watu kuzungumzia hiyo bikira.
Halafu tukieleza ukweli wa mienendo yake hapa JF wanasema tunamshambulia yeye binafsi.
Sasa sielewi mtu mwenye kujiita anauelewa mzuri wa neno la Mungu na maandiko yake anajitenganisha vipi na mienendo yake????
ANAEJIONA MSAFI AWE WA KWANZA KUMRUSHIA JIWE BABU

Maandiko matakatifu yanatutaka wakristo kuwa barua zinazosomeka vizuri kwa watu wengine, unaposema wewe ni mkristo lazima uenende na matakwa na matendo ya kristo. Hakuna mahali popote tunaposoma YESU Kristo aliwahi kufundisha watu mambo yaliyo kinyume na mapenzi ya baba Mungu.
Tunataka wanaoipinga huduma ya babu waje na uthibitisho, aidha wameoteshwa ndoto ama vinginevyo watueleze ni kwa namna gani babu amegeuka kuwa agent wa shetani wakati uongozi wa kanisa analolitumikia wametambua na kuikubali huduma yake.

Pia tusisahau kwamba roho mtakatifu anagawa karama/vipawa kadri atakavyo yeye, sasa nashindwa kuwashangaa wanaolazimisha babu ahubiri injili wakati hiyo ndio kazi ameifanya maisha yake yote, na isitoshe hata kutoa huduma ya tiba kwa hayo magonjwa sugu nayo ni injili kwa kuwa watakaoponywa na kikombe cha babu watautambua uwezo wa Mungu na hatimaye kukata shauri na jhapo tayari babu amehubiri injili.
Kuna siku nimemshuhudia babu anwaonya wale wanaokwenda kupata kikombe pasipokuwa na ugonjwa, wakiwa wanafanya hivyo kama kutafuta kinga, babu aliwaonya kwamba dawa yake sio kinga bali ni kwa ajili ya kutibu wagonjwa ili wakipona wakamshukuru Mungu kwa uponyaji huo.
 
Hapana SMU si hacra zangu...............naona jamvi hapa la moto ndo nangoja kwanza lipoe!

Pole sana my dia

Mungu akuwezeshe ushushe hizo hasira na kuzimaliza kabisa
Mimi imenishangaza sana mtu anajiita Mkristo Mkamilifu, badala ya kumuombea Babu na uponyaji wake uwe na nguvu zaidi ili watu wengi zaidi wapone (kama tunavyofundishwa wakristo kuombeana na kutakiana heri na mema) hata kama haziponyi magonjwa yote aliyosema, anaanza kuhoji ka shilingi 500/- anakopata kwa upendo na huruma yake kwa binadamu wenzake kutibu magonjwa sugu???
 
A second time they summoned the man who had been blind. "Give glory to God by telling the truth," they said. "We know this man is a sinner."

He replied, "Whether he is a sinner or not, I don't know. One thing I do know. I was blind but now I see!"
 
Basi asiseme ameoteshwa na Mungu kwasababu maandiko yanatufundisha kuhubiri neno. (Matayo 28:19)

Chamoto binadamu tunaota ndoto karibu kila tulalapo, Babu kaota ndoto ya dawa ya magonjwa sugu akaonyeshwa mti ambao wam,asai wanatumia kutengenezea sumu ya kuwekea kwenye mishale na mikuki yao leo huyo huyo binadamu anakunywa na kuponya magonjwa.

SASA KAMA BABU ALIOTA NDOTO YA DAWA HIYO ASEME ALIOTESHWA NA NANI? KAMA BABU HANA NIA MBAYA JUU YA HILO AMTANGAZE NANI?
LEO MIMI NIKIWA NATAFUTA KAZI NA NIKAOTA NIMEAPPLY LET SAY BOT OR UN. KESHO NIKAAPPLY BAADA YA SIKU KADHAA NIKAPATA KAZI AMBAYO NILIITAFUTA KWA MUDA NIMTANGAZE NANI ALINIOTESHA HIYO NDOTO
 
Hommie kwa hiyo mtu ukiinywa hiyo dawa baadae unaanza kutenda kinyume na matakwa ya Mungu? au inakuwaje hapa? huu ufreemansons unafaidikaje hapa?
mi mwenyewe sielewi kwakweli....!

wenyewe wanasema babu ni freemasons
na ule mti MRIGARIGA nao ni freemasons
which means na twiga wote nao ni FREEMASONS
 
Nimeshakuelewa cpu, ubarikiwe na nisamehe kwa kukuambia umefika kumbe hujafika. Ila pia nashukuru kwa sababu sasa nimekuelewa vizuri sana.

Ubarikiwe
 
Mkuu sipiyuuu shida mi mwenyewe nashindwa kuelewa, yeye anaamini kabisa yesu ni mungu, ila haamini mtu akiponywa kwa jina la mungu ila tu mpaka utamke Yesu!

Kaka kuna Mungu wengi ujue, kuna watu wakisikia unaomba kwa jina la Yesu wanakuona wa ajabu. Leo unaenda kuwaambia nimepona kwa jina la Yesu, na unashuhudia Yesu anaponya. Watakuelewa kweli? Lakini ukisema nimekunywa kikombe kwa babu watakuelewa.

Mi sina shida na huduma ya babu lakini asimhusishe Mungu tena kwa jina la Yesu. Tuamini tu kuna mti akikupa yy peke yake unapona. Ukichemsha ww unakuwa sumu.

CPU nimekuelewa kaka angu!!!
 
Pole sana my dia

Mungu akuwezeshe ushushe hizo hasira na kuzimaliza kabisa
Mimi imenishangaza sana mtu anajiita Mkristo Mkamilifu, badala ya kumuombea Babu na uponyaji wake uwe na nguvu zaidi ili watu wengi zaidi wapone (kama tunavyofundishwa wakristo kuombeana na kutakiana heri na mema) hata kama haziponyi magonjwa yote aliyosema, anaanza kuhoji ka shilingi 500/- anakopata kwa upendo na huruma yake kwa binadamu wenzake kutibu magonjwa sugu???
Kuna swali niliuza toka mwanzo kabisa na mpaka sasa sijapata jibu, hivi mtu akinywa kikombe cha babu ataanza kutenda mabaya yamchukizae mungu? maana mi najua kazi ya shetani ni kupotosha watu wa mungu......Maana babu alishasema imani yako ndo itakuponywa, kama kweli wewe unamuamini Mungu!
 
mi mwenyewe sielewi kwakweli....!

wenyewe wanasema babu ni freemasons
na ule mti MRIGARIGA nao ni freemasons
which means na twiga wote nao ni FREEMASONS

Daaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaah! Sasa kwa mwenendo huu, kuna kiumbe kweli ambacho sio freemasons??
 
Tupo pamoja ndugu ila tunatakiwa tuhoji kwa maandiko (mfano kwanini hawaambi walioponywa wamtukuze Mungu) na kuomba na Mungu ni mwema atatuwezeka kutambua kweli.

nadhani utakuwa hufuatilii sana habari za nyumbani kupitia runinga zetu za bongo, na wengi wanasema huwa hawaangalii tbc1 kwakuwa inachuja sana habari. Kwa kukufahamisha tu ni kwamba nimemshuhudia babu kupitia tbc1 kwenye taarifa ya habari(sikumbuki siku) alikuwa anatoa onyo kwa wanaokwenda kwake kupata dawa kwa ajili ya kinga. Aliwaonya kwamba dawa yake ni kwa ajili ya kutibu waginjwa ili wakipona wakamshukuru Mungu kwa uponyaji. Kwa mantiki hiyo naamini kwamba babu anawaambia watu wamtukuze Mungu kupitia uponyaji wake, labda kama una jingine kiongozi.
 
Kaka kuna Mungu wengi ujue, kuna watu wakisikia unaomba kwa jina la Yesu wanakuona wa ajabu. Leo unaenda kuwaambia nimepona kwa jina la Yesu, na unashuhudia Yesu anaponya. Watakuelewa kweli? Lakini ukisema nimekunywa kikombe kwa babu watakuelewa.

Mi sina shida na huduma ya babu lakini asimhusishe Mungu tena kwa jina la Yesu. Tuamini tu kuna mti akikupa yy peke yake unapona. Ukichemsha ww unakuwa sumu.

CPU nimekuelewa kaka angu!!!

Mi hapa sijakuelewa kabisaaaaaaaa???!!!!!
Au wewe mwenzetu una wasiwasi na Mungu anaetumiwa na Babu, na ambaye ndie huyo huyo viongozi wa KKKT wanamuabudu???
 
una uhakika gani kama uponyaji ni mambo ya kimwili (mkate tu). Tatizo tunaweka tafsiri zetu, kwa matamanio yetu au ya wale waliotufunza. Tunasahau kuwa hatujui yote ya Mungu, hatujui nani mwovu na nani mwema, hatujui nani anafanya ya Mungu na nani anafanya ya shetani. Tumeemegemea kuhukumu.

Tukeshe tukiomba.

Mbona mambo mema na maovu yanajulikana wazi tuu, yaani wewe unataka kuniambia ukifanya kosa dhamira yako haikuhukumu?
Kuhusu babu mimi sina haki ya kumuhumumu na siwezi fanya hivyo kwasababu wote tumetenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu (warumi 3:23) ila tuu nunatakiwa tuwe waangalifu.
 
Kaka kuna Mungu wengi ujue, kuna watu wakisikia unaomba kwa jina la Yesu wanakuona wa ajabu. Leo unaenda kuwaambia nimepona kwa jina la Yesu, na unashuhudia Yesu anaponya. Watakuelewa kweli? Lakini ukisema nimekunywa kikombe kwa babu watakuelewa.

Mi sina shida na huduma ya babu lakini asimhusishe Mungu tena kwa jina la Yesu. Tuamini tu kuna mti akikupa yy peke yake unapona. Ukichemsha ww unakuwa sumu.

CPU nimekuelewa kaka angu!!!

Baada ya kutafakali kwa kina maelezo yako, hata mimi sasa "NAANZA KUKUELEWA" dada angu, usijali
 
Kwahiyo wewe tu ndo unaruhusiwa kulitumia jina la YESU lakini mchungaji mstaafu aliyetumia muda wa maisha yake kumhubiri YESU kristo sasa haruhusiwi tena kulitaja jina kla YESU kwenye huduma yake kwa kuwa tu hupendi?? kazi bado mbichi kwa kweli, unakwenda mbele hatua tano kisha unarudi nyuma hatua kumi!!
 
Kwa hiyo LD watu wote wanaohubiri kwa jina la Yesu unawakubali sio?
Yaani hii hukumu unayoitoa hapa kua babu asitibu kwa kumusisha mungu sijui unaitoa wapi?
 
Baada ya kutafakali kwa kina maelezo yako, hata mimi sasa "NAANZA KUKUELEWA" dada angu, usijali

Mkuu LD amejaa utata mtupu, mwanzoni alikuwa against huduma ya babu,

Baada ya kumpa darasa la kutosha akageuka, tena akakiri kwamba amekuelewa kumbe alikuwa anataka kukuchuuza.

Ghafla bilamkutarajia amerudi kule kule alikokuwa, kimsingi hajakuelewa kama alivyodai hapo mwanzo, wasiwasi wangu ni kwamba amelewa injili uliyompa!!
 
Kwa hiyo LD watu wote wanaohubiri kwa jina la Yesu unawakubali sio?
Yaani hii hukumu unayoitoa hapa kua babu asitibu kwa kumusisha mungu sijui unaitoa wapi?

Kwahiyo wewe tu ndo unaruhusiwa kulitumia jina la YESU lakini mchungaji mstaafu aliyetumia muda wa maisha yake kumhubiri YESU kristo sasa haruhusiwi tena kulitaja jina kla YESU kwenye huduma yake kwa kuwa tu hupendi?? kazi bado mbichi kwa kweli, unakwenda mbele hatua tano kisha unarudi nyuma hatua kumi!!

Wakuu
Mi nishamuelewa anapokwenda huyu dada yetu
Ametoa hukumu tayari kwa Babu kwamba pamoja na kufanya kazi miaka zaidi ya 40 akinena mara kadhaa kuhudumia kwa jina la Yesu (ambaye ndie Mungu huyo huyo) leo ASILIGUSE KABISA JINA LA YESU!!!!!
Inasikitisha sana! Tena sana!
Kwa maana nyingine hana imani na Babu wala huduma zake maana kashasema aache kutumia Jina la Yesu!
Masikini daaaaaah!
 
Kimey

LD mara aseme hana elimu ya kujua kama Babu anasema ukweli au la mara atoe hukumu kuwa Babu asitumie Jina la Mungu!

Kweli Babu katuchanganya
 
Back
Top Bottom