Nadhani tunaangalia kinadharia zaidi, point ya Judith ni pale babu anapoweka kiwango cha pesa. Kama kweli watu 'wanapona' watatoa huna haja ya kumwambia mtu atoe shs,ngapi. Wewe unaweka kapu la sadaka, mtu atatoa kwa jinsi anavyoguswa na kama ni cha Mungu utaguswa tu kutoa.
Kuna incidence imetokea dada mmoja alikuwa ananieleza alikuwa huko, mama mmoja alikuja na shs 10,000 tu maana mtu hupati picha halisi ya gharama mpaka ufike huko au alikuwa na uwezo mdogo. Katika pilikapilika za hapa na pale pesa ikaanguka. Alipofika kwa babu, akaambiwa bila shs 500 hawezi kupata kikombe. Ndipo msamaria mwema akajitolea kumlipia. Sasa najiuliza kweli binadamu anaweza kuwa na huruma kuliko Mungu.
Hebu tutafakari!