Mwita Maranya
JF-Expert Member
- Jul 1, 2008
- 10,565
- 7,993
kuna post nyingi sana nimetoa majibu mengi sana tofauti. tatizo kuna mtu hukurupuka kuweka post bila kusoma zilizotangulia. kwa hiyo kama hoja fulani imejirudia na mimi nilishaijibu silazimiki kujijibu upya.
pia kuna wale wanaoniuliza wakinitaka nisemee mfano madhehebu yangu ya KKKT ama huduma zinazojitegemea kama za akina rwakatale, mwingira, kakobe, mwakasege, lusekelo nk, mimi si msemaji wa KKKT wala huduma nyingine yoyote ila nikiona kitu hakiendi kama maandiko yanavyosema mimi hufafanua namna maandiko yanavyotaka na si kusemea kanisa. hata huyu babu naye ni m-KKKT kama mimi, ninamkosoa kwa kuwa shughuli zake zina maswali mengi sana kwa mujibu wa maandiko.
kuna wengine wananishambulia mimi binafsi. naweza kuafafanua pale ninapoona kuna haja ya kufanya hivyo, vinginevyo naziacha tu hoja zao waendelee wenyewe.
halafu mmeona wengine wameanza kuchat na marafiki zao hapa kwenye thread kama wafanyavyo kwenye thread za jukwaa la MMU, sijui watu watabadilika lini!?
we jadili hoja nami nipo kufafanua hoja.
you are welcome.
kwa neema ya Mungu nitazikabili hoja zenu zote
Glory to God
Heshima kwako Judith,
Kwanza kabisa nataka nikukumbushe kwamba Mungu hana kigeugeu, wala njia zake hazichunguziki, akili yake na uwezo wake ukilinganisha na sisi binadamu ni sawa na umbali kati ya mbingu na ardhi.
Umesema kwamba wewe ni mlutheri lakini pia umekiri kwamba si msemaji wa KKKT, na inafahamika kwamba babu ni mchungaji mstaafu wa KKKT na huduma yake imeidhinishwa na kubarikiwa na uongozi wa kanisa la KKKT, Askofu Thomas Laizer ndiye mkuu wa KKKT dayosisi ya kaskazini alipo babu wa loliondo na ametolea tamko huduma ya babu. Sasa kama mkuu wa kanisa unalolitumikia ameshatoa kauli ya kuunga mkono huduma ya babu na wewe unakuja hapa kuipinga, basi unakwenda kinyume na msimamo wa kanisa lako ambalo msemaji wake amethibitisha kanisa lako KKKT kuunga mkono huduma hiyo. Kwa lugha nyepesi kabisa wewe ni muasi ama unataka kuanzisha uasi ndani ya kanisa la KKKT.
Kama unajiamini na unaamini kwamba unachokisema na kukisimamia ni cha ukweli, hukupaswa kuja hapa kumshambulia babu wa loliondo, ulitakiwa kwenda kuonana na uongozi wa kanisa lako na kuwaeleza dukuduku lako, kinyume na hapo naogopa kukuita msaliti.
Kitu kingine ninachokiona kwako, kama tukikubaliana na mtazamo wako kwamba huduma ya babu ni ya kishetani, si mpango ama huduma ya kiMungu,basi tutalazimika kukutazama vizuri katika angle hiyo hiyo ya unyoofu wa moyo wako na matendo yako. Tukijaribu kukumbuka kwamba Kimtokacho mtu mdomoni ndicho kiujazacho moyo wake,basi nataka turudi nyuma kidogo tu kwenye lile darasa lako la mbinu za kutongoza. Kwa jinsi ulivyoendesha lile darasa la kutongoza bila shaka wewe ni mzoefu wa kuwavua wanaume, huwezi kuwa mtaalamu wa kutongoza halafu uje kutamba kwamba wewe ni bikira, labda unataka kutufanya tufikirie hatua moja mbele kwamba unatumia mtandao wa nusu shilingi.
Lakini pia nikibaki hapo hapo kwenye mbiu za kutongoza na uaminifu wako mbele za Mungu, ninapenda nikukumbushe kwamba aliyesema usizini ndiye huyo huyo aliyesema usishuhudie uongo na ndiy huyo huyo Mungu aliyesema usiue. Maandiko matakatifu yanatukumbusha na kutufundisha kuwa ukimuangalia mwanamke/mwanamme na kumtamani moyoni mwako tayari umeshazini naye, kwahiyo unakuwa hatiani kwa kuzini. Kwahiyo kama unthubutu kutongoza wanaume kwa mujibu wa maelezo yako mwenyewe basi tayari umemtamani huyo mwanaume na kwahiyo hata kama haufiki kwenye hatua ya kuukalia mtalimbo basi tayari umeshazini na huyo mwanaume na kwahiyo unakuwa umetenda dhambi kwa kwenda kinyume na amri ya Mungu.
Kutokana na ukweli huu, sitaki kuamini kabisa kwamba unaweza kuja kujikweza hapa kwamba ni mkamilifu kwakuwa bado bikra bila kukumbuka unashiriki uzinzi myoni mwako.
Mwisho kabisa nikukumbushe kwamba Kakobe, Mwingira, Mama rwakatare na wengine tunaowafahamu wanafanya show za vipindi vya kuhubiri injili kwenye runinga kila siku na watu wanamiminika kwao kupata uponyaji, na hawa wananchi wanaokwenda kutafuta uponyaji huko nio wanaotoa sadaka na michango mbali mbali kwa majina ya sadaka ya shukrani n.k, tunashuhudia watu wakitoa shuhuda kwamba wamesafiri kutoka kona zote za nchi hii hata nje ya nchi kuja dsm kutafuta uponyaji kwa kakobe, mwigira, mama rwakatare, mzee wa upako na wengine lakini hilo halikushughulishi isipokuwa unashughulika na huduma ya babu ambayo hajawahi kuwa na kipindi cha runinga ama radio kujitangaza bali walioponywa ndio waliosambaza habari za uponywaji wao na hatimaye media zikaamua kumpa babu promo bila yeye kulipia.Kwanini hujahoji watumishi wa show za runinga kwenda kutoa uponyaji mioani badala yake wamejikita dsm tu?? kwani hao wananchi wanapokuja dar wanakuja bila kulipia nauli? au makanisa hayo ndiyo yanayowasafirisha kuja dsm?? hebu kuwa mkweli katika hili, chuki, wivu na husda ndo zinakusumbua.
Nakuomba ukatubu kwanza dhambi yako ya uzinzi na nuendelee kumtumikia Mungu pasipo kujikweza ili usije ukashushwa chini na kuaibika.
Nilikuwa napita tu kuelekea mugumu nikaona ni vizuri kukuachia ujumbe huu muhimu kwa ustawi wa imani yako.