Hoja ya Shossi juu ya sh. 500/- ya babu

Hoja ya Shossi juu ya sh. 500/- ya babu

basi maadamu mimi na wewe hatufahamu yaliyo moyoni mwake, na wala hatupaswi kumhukumu ili tusihukumiwe muacheni babu afanye kazi yake kwa wanaoamini watapona kwa uwezo wake aliopewa na mungu.
Muacheni babu ahudumie watu, msimzushie yasiyo na msingi kwamba eti hatawaponya masikini, au wasio na hiyo 500/- aliwahi kutamka hivyo???

Acheni afanye kazi yake bwana, wasio na hiyo hela waende pia tuone kama hawatapewa huduma, sio kuzusha tu

huku tukiomba kwa bidiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Kwahiyo mkuu unasema kuwa gharama ya dawa ni 500/- ila ukiwa na pungufu unatiwa?
Wewe unao ushuhuda kuwa mtu alienda bila ya pesa au alienda na pesa pungufu ya 500/- akatibiwa?
Kama ni hivyo mbona babu hajatwambia kuwa Mungu alimuotesha bei ya dawa ni sh 500/- ila kwa asiye na hiko kiasi pia anatibiwa? alishasema hivyo?

Maswali mazuri sana
Kama mimi na wewe hatuna ushuhuda wowote wa wasio na 500/- kutibiwa au la basi atupaswi kuinua vinywa vyetu kumnyooshea kidole babu, maana hata malalamiko ya wagonjwa kusema hiyo 500/- ni kubwa pia hatujayasikia. Tuache Babu afanye kazi yake mpaka pale tutakapo pata ushuhuda tofauti. Sawa???
 
Kwahiyo mkuu unasema kuwa gharama ya dawa ni 500/- ila ukiwa na pungufu unatiwa?
....
Mtumishi, hebu nyoosha hiyo sentensi. Inaleta ukakasi kiaina (ingawa naelewa unataka kusema nini)!
 
huku tukiomba kwa bidiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii

Ndio maana hata Babu anatekeleza wajibu wake wa kuwaombea wote wanaokwenda kwake kutibiwa
Amen
 
Mungu ataka tuponywe roho kwanza ndipo baadae mwili, (matayo 6:33) tatizo linakuja babu (ambaye ni mchungaji) hafanyi hivyo? kama angesema yeye ni mganga wala kusingekuwa na tatizo.

Hapana ila masharti yake ya kwamba lazima uwe pale ili upate uponyaji yanasumbua kidogo. Mungu wa kweli hana mipaka na katika agano jipya Yesu alisema imekwisha (yohana 19:30) akimaanisha mambo ya torati (agano la Musa kwa wana waisraeli) limekwisha.

Baada ya hapo roho mtakatifu ndiye anaye tawala, ambaye hana mipaka na wala haina haja ya kutumia "media". Ndiyo maana hata mimi natatizo kuamini kwamba Babu anafanya hayo kutokana na maandiko.

Alipoza wale waliomsikiliza neno.

Tofauti ya hapa mwalimu ni kwamba wanotengeneza hizo dawa siyo wachungaji/padre ni wanasayansi wao wapo katika kuponya miili tuu. Mtumishi wa mungu anatakiwa kuhubiri neno ili watu waponywe roho ndipo wapate uponyaji

Ifahamike tu babu alianza kutibu like two or three years back lakini kuna watu walikwenda wakapona ndo wakamtangaza babu so sio yeye anayetumia media.

Mwataka babu ahubiri waende kanisaful;ani kama wengine?
Simpingi babu wala sina sababu ya kumkosoa, na sina ushuhuda wa aliyepona ninayemfahamu lakini sitaki kuwa kama TOMASO vilevile.
Naacha kazi ya Mungu itende kazi kama ni roho zile tulizoambiwa zitakuja kwa jina lake naamini Babu kuna adhabu yake itamfika na kama ni kazi ya mungu na indelee kutenda kazi na kwa dunia nzima.
 
Naona hii thread sasa ni useless imeshageuzwa kuwa ni mkutano wa injili ( miracle crusade ). hii haijatulia kumbukeni humu kuna watu wa dini mbalimbali, ila tu nawaonya biblia imeshaandika wazi kwamba si wote waniitao bwana, bwana, kwamba watauona ufalme wa mbinguni, noooo.
sisi tunawaangalia mnavyojifanya mabingwa wa maandiko, kati yenu nyinyi hakuna alie shujaa na kumpenda Yesu kuliko Simon Petro, lakini ni huyo huyo alimkana mara tatu. Hii thread imeshakuwa kichefuchefu.
 
Nilikuwa sijaelewa.
Nikuulize suala la niongeza basi. Unajua kuwa hadi miaka hii ya sasa kuna makabila ambayo hayajawahi kusikia Neno la Mungu. Hawa wameonewa na Mungu? (in the Amazon and other places)

Kama unakubali kuwa Neno halijafika huko, huduma ya Yesu utasemaje imeponya watu wote duniani?

Ni kweli huduma ya Yesu, inaweza kuwa haijafika huko, Lakini Mungu aliyewaumba kwa sura na Mfano wake, bado anawahifadhi na kuwaponya kwa jinsi yao.
Na kwa neema ya Mungu wanaweza wakifikiwa na neno Vile vile, maadamu, neno la Mungu linasafiri.
Na hapa ujue kuna tofauti ya neno na KIKOMBE.
Kikombe kile hakitembei, na navyosikia hapaswi mtu mwingine kukitoa, dunia nzima inabidi Iende LOLIONDO,
Hakuna watumishi wanaoandaliwa kwa ajili ya huduma ili ifike hata hapo Kilimanjaro tu, akichemsha mti mtu mwingine unakuwa sumu.
Lakini neno la MUNGU, hata miti inaweza ikanena, na mtu akapata uzima ndani yake.
Mtu anaweza akilisikia hata kwenye redio, au kwa njia ya nyimbo akaokolewa.
 
Ni mungu huyuhuyu aliyewataka wanawaisrael wamgeukie nyoka wa shaba wa MUSA pindi watakapoumwa na nyoka wataka kusema walewalioshindwa hawakupendwa na mungu hapo pia palikuwa na sharti, ni mungu huyuhuyu aliye waaambia watu imani yako imekuponya na sehemu nyingine aliwataka watu wajipake matope nasehemu nyingine aliwaambia wataka takasika tasika na wengine iliwabidi wakajichovywe mtoni tena kwenye maji macha je wasema hapa mungu alikuwa na upendeleo????????

Hivi leo nimlaumu mungu kwa kuwaacha ndugu zangu wafe kwa ukimwi na kisukari nawalikwenda kuombewa na hawakupona? nimlaumu aliwaacha wafe mapema bila kusubiri kikombe cha babu ambacho kinge waponya? Nami nije kusema mungu ana upendeleo?
Ni wangapi wamekufa kwa magonjwa kama malaria, ukimwi,pepo punda na mengineyo ina maana mungu ana upendeleo?
Ni mwenye imani yupi leo hii hanywi dawa ya malaria na kusubiri maombi na hupona? je mungu ana upendeleo maana dawa hazipatikani bure ati?

Naona unachanganya vipindi viwili vya biblia, kipindi cha Musa ni tofauti na kipindi cha matendo ya mitume (baada ya yule msaidizi) ambapo hakuhitajika media ili kufanya uponyaji. Baada ya kushukiwa roho mtakatifu mitume waliweza kufanya yale Yesu aliyoyafanya na zaidi (Matendo 2:1-4)
 
asante kwa kuongeza sauti.

zama za makuhani ndio hiyo 10% iliamuriwa na labda hili nalo lahitaji mjadala wake unaojitegemea.

lakini kwa siku zetu kutoa ni hiyari na kulingana na uwezo na moyo wako unavyojisikia. kumyima mgonjwa huduma kwa vile tu hela aliyonayo haifiki aliyoamuru mungu fulani, huo ni uganga tu kama wa wengine wanaodai kiasi fixed cha pesa ama mifugo kama kuku, mbuzi nk. Mungu wetu hawezi kutunyima rehema na uponyaji wake kwa kuwa kaweka bei na tumeshindwa kuimudu.

mbarikiwe sana

Glory to God

Kama hayo mambo ya utoaji yaliyoonyeshwa agano la kale yanahusu zama za makuhani itamaanisha:
1. Yesu alikuja kuitangua torati
2. Zama hizi hakuna makuhani tena
3. Hatuna haja ya kusoma agano la kale

Tukirejea kwenye hoja ya msingi ambapo babu anapingwa kwa kutoza fixed amount yet nobody is telling us wapi Mungu alikataza hilo.
 
Ila tunatakiwa kuzipima roho (1 Joh 4:1 )

Kuzipima Roho ni ruksa na wala huwezi zipima roho JF, yatubidi kufunga na kuomba na kupata majibu ya kiroho, wapima roho kiroho wala sio kwa uelewa wa kimwili utapata majibu ya kiroho.

Na si jambo jema kuwatangazia watu eti Babu hajatumwa na Mungu halafu unakwenda kufunga na kuomba wakati tayari upo subjective and u have an answer from ur own view.

Kama hujapata jibu la kiroho basi huna haki ya kutangaza babu hajatumwa na mungu.
 
  • Thanks
Reactions: CPU
Naona hii thread sasa ni useless imeshageuzwa kuwa ni mkutano wa injili ( miracle crusade ). hii haijatulia kumbukeni humu kuna watu wa dini mbalimbali, ila tu nawaonya biblia imeshaandika wazi kwamba si wote waniitao bwana, bwana, kwamba watauona ufalme wa mbinguni, noooo.
sisi tunawaangalia mnavyojifanya mabingwa wa maandiko, kati yenu nyinyi hakuna alie shujaa na kumpenda Yesu kuliko Simon Petro, lakini ni huyo huyo alimkana mara tatu. Hii thread imeshakuwa kichefuchefu.

Sasa mpendwa wewe unataka nini kwa kusema hivo??
Pole lakini, hata kama tunasema Bwana bwana tukiwa wachafu, hiyo haimzui Mungu, wa haibadilishi uwepo wa Mungu.
Mungu yupo pale pale, na hakuna Intermediate Conection kati yako na MUNGU wetu.
Wewe angalia kile unachokiamini, kiamini hicho. Sasa tuache kusema kwa sababu kuna watu watasema/wanasema bwana bwana lkn ni wachafu???
 
Kwa kigezo kipi??

Nadhani ukisoma vizuri nilichoandika usingeuliza swali jepesi namna hii.
Kweli ni kitu cha kuuliza Mtumishi wa Mungu ana kigezo kipi??
Kuombea watu wenye magonjwa sugu na matatizo mbalimbali tayari ni SIFA KUU ya kuitwa MTUMISHI WA MUNGU
Au unakataa??

Hata kama unajua kuchambua Biblia na vifungu vyake, kama husaidii wenzako wewe kweli ni Mtumishi wa Mungu???
Ni kazi bure!!
Hata uwe na uwezo wa kuhamisha milima, kunena kwa lugha za malaika n.k. kama huwezi kusaidia watu (ambapo lazima uongozwe na UPENDO) wewe ni Mtumishi kweli??
 
Ila tunatakiwa kuzipima roho (1 Joh 4:1 )

Tunapima kila roho kwa maandiko na sio hisia au maelekzo ya viongozi wa dini.
Babu kapotoka wapi???? Tupeni maandiko jamani!!!!!!!!
 
Miss Judith, ni mnafiki mkubwa na nakushangaa kuleta post kama hii na kama ulitaka kumpongeza Shossi ungem PM halafu najua watu wenye mawazo na fikra kama za Shossi juu ya hili suala ni wengi tu huku mtaani na wewe nadhani umetumwa kuja kuleta wivu wa kishetani na hao manabii na mitume wanajiona wao wana uzima kumbe ni matapeli wa kutupwa, na elewa kwamba mazingira aliyokua nayo Yesu huwezi linganisha na mazingira ya sasa kila kitu kinahitaji gharama, infact umenichefua sana kwa kujifanya wewe ni mtu wa rohoni kumbe ni KIBURI CHA UZIMA ambacho mnafundishwa katika makanisa yenu. Na usiwakejeli wanaoenda kwa babu acha watu wakapokee uzima hata kama ni wa mwili na sio roho na imani wakitoka pale watamsifu na kumtukuza Mungu jinsi alivyo waponya. NAKUOMBA URUDI HAPA JAMVINI UTUAMBIE WEWE NI MUUMINI WA KANISA GANI. Ili nisikuone mnafiki maana umejipambanua kuwa wewe ni mtakatifu sana please njoo hapa utueleza vinginevyo.......
Ahsante sana mkuu!..... Huyu dada hii ni post ya 3 ya kumponda babu. Siku moja nilitofautiana kimtazamo kuhusiana na babu,lakini alinishambulia kwa hasira na kashifa kibao!. Leo naingia tena jamvini nakutana na post yake nyingine ya kumsema babu. Binafsi nashindwa kumwelewa huyu Dada......Ila nashukuru most of wachangiaji ikiwemo wewe'mmegundua kuwa hoja zake hazina mashiko kwa hapa Duniani hadi Mbinguni
 
Kuzipima Roho ni ruksa na wala huwezi zipima roho JF, yatubidi kufunga na kuomba na kupata majibu ya kiroho, wapima roho kiroho wala sio kwa uelewa wa kimwili utapata majibu ya kiroho.

Na si jambo jema kuwatangazia watu eti Babu hajatumwa na Mungu halafu unakwenda kufunga na kuomba wakati tayari upo subjective and u have an answer from ur own view.

Kama hujapata jibu la kiroho basi huna haki ya kutangaza babu hajatumwa na mungu
.

Ahsante kwa majibu murua, sina la kumuongezea huyu ndugu yetu

The Following User Says Thank You to Diehard For This Useful Post:

CPU (Today)​
 
Kama kweli wewe unamjua Mungu nakupongeza mama yangu. Lakini nina mashaka kwa sababu kwa umri wangu sijasoma mahali po pote ambapo Mungu ametaja gharama ya neema yake. Kifupu Neema ya Mungu ni bure.

Mchanganuo wa 500 za babu kama ulivyoutoa, ni kuwa yeye ni mmoja wa wahudumu na kama walivyo wahudumu wanakula kutokana na huduma. Kinyume chake hawatakiwi watajirike kutokana na huduma kwa sababu watamkufuru Mungu. Kinatosha hakitoshi siyo issue. Kama ni kwa neema ya Mungu yeye ndiye anajua inatosha.

Sijaisoma hiyo hoja ya Shossi lakini ni upofu wa jicho la roho kulinganisha gharama ya huduma kwa watu na kiwango cho chote cha fedha.
 
Ndio maana hata Babu anatekeleza wajibu wake wa kuwaombea wote wanaokwenda kwake kutibiwa
Amen

CPU inaonekana wewe umefika kwa babu, hebu niambie kidogo hivi anaombea kwa jina la YESU?
Watu wa dini zote wanafika pale, anawafundisha Imani ya kupona ktk jina la Yesu, wanakubali na kuamini,
Halafu anachukua maji anayaombea kwa jina la Yesu, halafu anawapa watu wanakunywa kwa Imani ya Bwana Yesu,
Halafu wanarudi, wakiwa wapepona kwenye dini zao kwa Imani ya kupona kwa JINa la YESU?
Wanaendelea na Dini zao kama kawaida, kama mpagani, anarudi kwenye upagani wake, lakini amepona kwa jina la YESU?

Au ni aje hapo? CPU nisaidie tafadhali.
 
Naona hii thread sasa ni useless imeshageuzwa kuwa ni mkutano wa injili ( miracle crusade ). hii haijatulia kumbukeni humu kuna watu wa dini mbalimbali, ila tu nawaonya biblia imeshaandika wazi kwamba si wote waniitao bwana, bwana, kwamba watauona ufalme wa mbinguni, noooo.
sisi tunawaangalia mnavyojifanya mabingwa wa maandiko, kati yenu nyinyi hakuna alie shujaa na kumpenda Yesu kuliko Simon Petro, lakini ni huyo huyo alimkana mara tatu. Hii thread imeshakuwa kichefuchefu.

Siyo hivyo ndugu mimi ni mkosaji pia na siwezi kusema ni wa haki hata kidogo na ukinichunguza maisha yangu utaona nimekosea sana ila tuu ni neema yake ndiyo inayotuponya.

Sikiliza ndugu hii mada (na nyingine nyingi) nimefuatilia lakini niliona ni malumbano tuu na personal attack kwahiyo sikutaka kujiingiza lakini baadae ikazidi na ukweli ukawa unapindishwa ndipo nikaamua kujibu baadhi ya maswali. Kama umesoma mada zote zinazo onyesha utata wa huduma ya babu utaelewa kwanini ninasema hivyo.

Mungu akubariki.
 
Naona unachanganya vipindi viwili vya biblia, kipindi cha Musa ni tofauti na kipindi cha matendo ya mitume (baada ya yule msaidizi) ambapo hakuhitajika media ili kufanya uponyaji. Baada ya kushukiwa roho mtakatifu mitume waliweza kufanya yale Yesu aliyoyafanya na zaidi (Matendo 2:1-4)

Nakubali usemayo lakini hata leo hii wapo watumishi wanaoponya kwa kuwawekea wagonjwa mikono na wengine wanasema watu walete nguo au vitambaa wakawagusishe au wavike wagonjwa wao majumbani na wana pona.
Wapo watokao jasho wanapoomba na kutumia nguvu na wapo wanaoomba kwa kurelax na miujiza yaja.
Lakini leo hii KIKOMBE CHA BABU watu hawataki kuamini na na hawana vithibitisho au hawajafunuliwa kama babu ni wa mungu au la lna wanajaribu tu kutangaza babu siye.
Nipo kujaribu kujua ipi ni busara kama watu hawana uhakika wa haya ni haki kwao au ni dhambi kumtangaza babu vibaya au kukaa kimya?
Ikumbukwe Mungu katujalia hekima ya kupambanua mambo na kutafuta namna ya kuyapresent na kujua namana ya kucounter act na reaction za watu.
 
Nadhani ukisoma vizuri nilichoandika usingeuliza swali jepesi namna hii.
Kweli ni kitu cha kuuliza Mtumishi wa Mungu ana kigezo kipi??
Kuombea watu wenye magonjwa sugu na matatizo mbalimbali tayari ni SIFA KUU ya kuitwa MTUMISHI WA MUNGU
Au unakataa??

Hata kama unajua kuchambua Biblia na vifungu vyake, kama husaidii wenzako wewe kweli ni Mtumishi wa Mungu???
Ni kazi bure!!
Hata uwe na uwezo wa kuhamisha milima, kunena kwa lugha za malaika n.k. kama huwezi kusaidia watu (ambapo lazima uongozwe na UPENDO) wewe ni Mtumishi kweli??

Sawa sawa CPU kaka angu.
Ni mtumishi kwa sababu anaombea sio.
Sawa kaka angu nimekuelewa nijibu hayo maswali, hapo juu kwa kunisaidia nielewe zaidi tafadhali.
 
Back
Top Bottom