Hoja ya Shossi juu ya sh. 500/- ya babu

CPU haahhaa. Ndio point ya Judith kuwa sio kila ndoto ni ufunuo wala miujiza. Mengine ni shetani.

Sasa wewe utajaza kuwa Loliondo ni Ufunuo au Shetani na vile utajaza kuwa kuchorachora ni Ufunuo au Shetani

Mwalimu
Mimi nilikuwa naambiwa tu kwamba UTACHORWA CHORWA kifuani, sijui utafanyiwa nini (mbinu zingine nimezisahau) sasa nikashindwa kuelewa ikitokea hivyo ndio nayo ni miujiza au ufunuo?? Maadamu mleta mada hii ndio aliyeleta na hiyo ya kuchorana, basi na wewe yapaswa uwe mwanafunzi kwake ili akufundishe. Atakupangia ratiba nadhani, kutwa mara 3 kama sikosei
 
Hahah nyie watu mmenichekesha kweli. CPU ukishakuvuka under 18 hurudi tena. :)

Ati mtu anatoka kipovu kwa dhambi ya mwenziwe! Hapo tu ndo walipokuchosha wewe Kimey....lol

Wawaacheni walioamini waendelee nako na kama ni makosa Mungu ni mwingi wa kusamehe.

btw Dhambi zote zina uzito sawa mbele ya Mungu. Sasa jukwaa la wakubwa kama dhambi tujuwe kuwa ni sawa na dhambi ya Babu Loliondo kama dhambi :)

Mwalimu
Nifundishe basi cha kufanya pale inapotokea mtu anafanya MASHAMBULIZI YAKE kwa Babu na huduma zake akakimbilia kudai ni HOJA, ila anapoambiwa yeye alivyojikoroga na mienendo yake anasema ni MASHAMBULIZI BINAFSI ???!!!:ballchain:

Saidia Mwalimu please!
 
Mpendwa ungeachana na huu mjadala,naona unashambuliwa zaidi wewe kama wewe badala ya hoja husika,inasikitisha sana.

umeona eeeeee

unafikiri aliyesema great minds discuss issues, poor mind discuss people alikosea?

sasa tumetibitisha wenyewe hapa JF

kwa kweli inasikitisha sana, kukimbia mjadala sitakimbia, kwa neema ya Mungu nitasema chochote ninachoona kinafaa kusemwa hata kama dunia nzima itanishukia. sishangai kuona kuwa wengi wako kinyume na mimi, ni ukweli ulio wazi kuwa njia ielekeayo upotevuni ni pana sana na waiendayo ni wengi.

nakushukuru kwa ushauri mzuri, kukutana na majaribu ni sehemu ya maisha mpendwa.

Mungu akubariki

Glory to God
 
Kaka
Hapo ambapo wewe unaona kuna utata basi ni bora ungeanza kujiuliza hizo 10% za kipato chako zilizotamkwa utoe kanisani alipanga nani?? Mungu au Binadamu???
Kama alipanga binadamu, mbona haitui-challenge makanisani kama hii 500/- ya babu??
Biblia ina tangaza na kueneza neno la Mungu, lakin inauzwa kwa fixed price, tafakari????!!!
Kanisani huko huko tuahimizwa kutoa sadaka ya jengo na sare za wanakwaya ambapo tuaambiwa ni lazima zifike kiasi fulani, tafakari????!
Tunaenda ktk mahospitali ya makanisa, tunachangia fixed amount kupata huduma fulani, tafakari?????!!!

Baada ya kutafakari hayo yote, then uje kwenye 500/- ya babu ili utibiwe magonjwa sugu
Kwanza tukubaliane, kutoa sadaka sio lazima yaani kama huna kipato sio lazima kutoa.
Na sadaka pia sio lazima kutoa pesa(nirekebishwe kama nimekosea)
Na pia hiyo 10% uliyoitaja hapo nayo pia inategemea na kipato cha mtu(tunarudi pale palee)
Kama kuna askofu, padri au mchungaji anayesema sadaka ni lazima utoe kiasi fulani huyo ANAKOSEA.
Kuhusu biblia;
Kesi ya biblia hapa ni tofauti kabisa.
wapo wanaouza biblia kwa bei ya juu, wapo wanouza kwa bei ya chini na wapo pia wanaotoa bure.
Hawa wote hawajaoteshwa na Mungu.

Turudi kwenye tiba ya babu.
Mungu anapoagiza mtu anayetaka tiba yake ni lazma atoe sh 500/- ili apone na asiyekuwa nayo je?
Tiba iliyoelekezwa na Mungu!!
kama mimi uwezo wangu ni sh 100/- je inamaana nife? Mungu yupo fea kweli hapo?
Ndio maana hata kwenye kutoa sadaka Mungu alielekeza kutoa kadiri ya uwezo wako, hakusema fixed amount.
 
Mpendwa ungeachana na huu mjadala,naona unashambuliwa zaidi wewe kama wewe badala ya hoja husika,inasikitisha sana.
Ajibiwe mara ngapi? wewe ukiangalia yeye hujibu post ile tu inayomsapoti ila zile zinazoelezea hoja yake wala haangaiki nazo! kwa hiyo ishu ya kujibu hoja hapa naona inakosa mshiko!
 
Nisaidieni kidogo. Kuna mtu alienda akawa hana 500 akakataliwa kupewa huduma?

Na kuna sehemu babu amesema ameoteshwa kutoza 500?

Kwanza tukubaliane, kutoa sadaka sio lazima yaani kama huna kipato sio lazima kutoa.
Na sadaka pia sio lazima kutoa pesa(nirekebishwe kama nimekosea)
Na pia hiyo 10% uliyoitaja hapo nayo pia inategemea na kipato cha mtu(tunarudi pale palee)
Kama kuna askofu, padri au mchungaji anayesema sadaka ni lazima utoe kiasi fulani huyo ANAKOSEA.
Kuhusu biblia;
Kesi ya biblia hapa ni tofauti kabisa.
wapo wanaouza biblia kwa bei ya juu, wapo wanouza kwa bei ya chini na wapo pia wanaotoa bure.
Hawa wote hawajaoteshwa na Mungu.

Turudi kwenye tiba ya babu.
Mungu anapoagiza mtu anayetaka tiba yake ni lazma atoe sh 500/- ili apone na asiyekuwa nayo je?
Tiba iliyoelekezwa na Mungu!!
kama mimi uwezo wangu ni sh 100/- je inamaana nife? Mungu yupo fea kweli hapo?
Ndio maana hata kwenye kutoa sadaka Mungu alielekeza kutoa kadiri ya uwezo wako, hakusema fixed amount.
 
Hahaha CPU bwana unanichekesha kweli.

Lakini mambo ya imani magumu sana. Watu wanatake offense mara moja wanapotajiwa Imani zao. Tustahamiliane tu, ni jambo la kupita.

Mwalimu
Nifundishe basi cha kufanya pale inapotokea mtu anafanya MASHAMBULIZI YAKE kwa Babu na huduma zake akakimbilia kudai ni HOJA, ila anapoambiwa yeye alivyojikoroga na mienendo yake anasema ni MASHAMBULIZI BINAFSI ???!!!:ballchain:

Saidia Mwalimu please!
 
umeona eeeeee

unafikiri aliyesema great minds discuss issues, poor mind discuss people alikosea?

sasa tumetibitisha wenyewe hapa JF

kwa kweli inasikitisha sana, kukimbia mjadala sitakimbia, kwa neema ya Mungu nitasema chochote ninachoona kinafaa kusemwa hata kama dunia nzima itanishukia. sishangai kuona kuwa wengi wako kinyume na mimi, ni ukweli ulio wazi kuwa njia ielekeayo upotevuni ni pana sana na waiendayo ni wengi.

nakushukuru kwa ushauri mzuri, kukutana na majaribu ni sehemu ya maisha mpendwa.

Mungu akubariki

Glory to God

Ni kweli ndugu

Endelea kusema tu, usiogope chochote wala lolote.
Ukipata njia nyingine za UTONGOZAJI usisite kutuhabarisha
Ukipata mada nyingine AT YOUR OWN RISK pia usisite kutuambia, hata kama sisi tutasema ni kinyume na kazi ya Mungu
Na ni kweli hiyo njia ya UPOTEVUNI ni pana mno kama zilivyopana mbinu zako za utongozaji, utaipita kwa kujidai bila kusongwa songwa wala kusukumwa sukumwa.
Tunashukuru pia
 
ubarikiwe sana mpendwa.

usemayo yanadhihirisha mengi sana. kama ningesema hapa kuwa "niliyabeba madume kumi kwa siku moja" nafikiri thread yangu ingepitiliza kurasa 100! hii ndiyo dunia tunayoishi, kuwa bikira ni aibu, ila kuwa malaya, msagaji nk. unapata maswahiba kedekede. nakuombea baraka na Mungu asikupite anapozuru wengine. amina

Glory to God

Kuwa Bikra ni heshima sana Mungu akubariki na akupe haja ya moyo wako akupe Mume mwema kwenye maisha yako. Ukweli uko wazi na unaonekana una ufahamu mzuri wa maandiko, Babu anaweza kua sahihi au asiwe kwakuwa ni binadamu maana hata Musa aliambiwa auambie mwamba utoe maji yeye kaupiga mwamba mara mbili, babu anaweza kuharibiwa pia na watu maana mioyo hugeuzwa na watu.
 
Judith

Tafadhali nisaidie unipe quote inayoonyesha Babu kusema kuwa kwenye ndoto aliona pia bei ya huduma na mchanganuo wake.

Kwani inaweza kuwa alioteshwa dawa tu, bei akapanga mwenyewe.

Na ikiwa ni hivyo tutasema dawa haitoki kwa Mungu kama Babu mwenyewe aliamua kujipangia bei? Na jee tunaushahidi kuwa asiye na pesa hapatiki huduma?
 
Ajibiwe mara ngapi? wewe ukiangalia yeye hujibu post ile tu inayomsapoti ila zile zinazoelezea hoja yake wala haangaiki nazo! kwa hiyo ishu ya kujibu hoja hapa naona inakosa mshiko!

kuna post nyingi sana nimetoa majibu mengi sana tofauti. tatizo kuna mtu hukurupuka kuweka post bila kusoma zilizotangulia. kwa hiyo kama hoja fulani imejirudia na mimi nilishaijibu silazimiki kujijibu upya.

pia kuna wale wanaoniuliza wakinitaka nisemee mfano madhehebu yangu ya KKKT ama huduma zinazojitegemea kama za akina rwakatale, mwingira, kakobe, mwakasege, lusekelo nk, mimi si msemaji wa KKKT wala huduma nyingine yoyote ila nikiona kitu hakiendi kama maandiko yanavyosema mimi hufafanua namna maandiko yanavyotaka na si kusemea kanisa. hata huyu babu naye ni m-KKKT kama mimi, ninamkosoa kwa kuwa shughuli zake zina maswali mengi sana kwa mujibu wa maandiko.

kuna wengine wananishambulia mimi binafsi. naweza kuafafanua pale ninapoona kuna haja ya kufanya hivyo, vinginevyo naziacha tu hoja zao waendelee wenyewe.

halafu mmeona wengine wameanza kuchat na marafiki zao hapa kwenye thread kama wafanyavyo kwenye thread za jukwaa la MMU, sijui watu watabadilika lini!?

we jadili hoja nami nipo kufafanua hoja.

you are welcome.

kwa neema ya Mungu nitazikabili hoja zenu zote

Glory to God
 
msitoke nje ya mada wapendwa! ubikira si mada ya kujadiliwa kwenye thread hii. najua mabikira ni adimu sana hapa duniani, hapa tunamjadili babu na sh. 500/- yake . please turudi kwenye mada

Glory to God

Huyu asiyetaka Bikra ana lake jambo maana inaonekana hata maana yake haijui. Walewaleeeeee! Kesho atakuambia hataki mke! Tusubiri tutaona mengi mbeleni
 
haijaniuma hata kidogo mpendwa.

kuna watu hapa JF wanatangaza kuwa wa hisia za u-lesbian, sijaona ukiwakaripia, wengine wanafagilia tigo, nao sijasikia ukiwakaripia, nk. uliposikia kuna mtu kaukabidhi mwili wake kwa Mungu kwa uaminifu kwa miaka 26, umegeuka mbogo!

naijua roho inayokutesa. nitakuombea. ubarikiwe

Glory to God

Wazinzi huku wengi! Inawauma sana roho, shetani kawapa kazi sasa wanaona kwako wamefeli wanatafuta jinsi ya kukuvunja moyo usijione shujaa.
 
Kwanza tukubaliane, kutoa sadaka sio lazima yaani kama huna kipato sio lazima kutoa.
Na sadaka pia sio lazima kutoa pesa(nirekebishwe kama nimekosea)
Na pia hiyo 10% uliyoitaja hapo nayo pia inategemea na kipato cha mtu(tunarudi pale palee)
Kama kuna askofu, padri au mchungaji anayesema sadaka ni lazima utoe kiasi fulani huyo ANAKOSEA.
Kuhusu biblia;
Kesi ya biblia hapa ni tofauti kabisa.
wapo wanaouza biblia kwa bei ya juu, wapo wanouza kwa bei ya chini na wapo pia wanaotoa bure.
Hawa wote hawajaoteshwa na Mungu.

Turudi kwenye tiba ya babu.
Mungu anapoagiza mtu anayetaka tiba yake ni lazma atoe sh 500/- ili apone na asiyekuwa nayo je?
Tiba iliyoelekezwa na Mungu!!
kama mimi uwezo wangu ni sh 100/- je inamaana nife? Mungu yupo fea kweli hapo?
Ndio maana hata kwenye kutoa sadaka Mungu alielekeza kutoa kadiri ya uwezo wako, hakusema fixed amount.

asante kwa kuongeza sauti.

zama za makuhani ndio hiyo 10% iliamuriwa na labda hili nalo lahitaji mjadala wake unaojitegemea.

lakini kwa siku zetu kutoa ni hiyari na kulingana na uwezo na moyo wako unavyojisikia. kumyima mgonjwa huduma kwa vile tu hela aliyonayo haifiki aliyoamuru mungu fulani, huo ni uganga tu kama wa wengine wanaodai kiasi fixed cha pesa ama mifugo kama kuku, mbuzi nk. Mungu wetu hawezi kutunyima rehema na uponyaji wake kwa kuwa kaweka bei na tumeshindwa kuimudu.

mbarikiwe sana

Glory to God
 
kuna post nyingi sana nimetoa majibu mengi sana tofauti. tatizo kuna mtu hukurupuka kuweka post bila kusoma zilizotangulia. kwa hiyo kama hoja fulani imejirudia na mimi nilishaijibu silazimiki kujijibu upya.

pia kuna wale wanaoniuliza wakinitaka nisemee mfano madhehebu yangu ya KKKT ama huduma zinazojitegemea kama za akina rwakatale, mwingira, kakobe, mwakasege, lusekelo nk, mimi si msemaji wa KKKT wala huduma nyingine yoyote ila nikiona kitu hakiendi kama maandiko yanavyosema mimi hufafanua namna maandiko yanavyotaka na si kusemea kanisa. hata huyu babu naye ni m-KKKT kama mimi, ninamkosoa kwa kuwa shughuli zake zina maswali mengi sana kwa mujibu wa maandiko.

kuna wengine wananishambulia mimi binafsi. naweza kuafafanua pale ninapoona kuna haja ya kufanya hivyo, vinginevyo naziacha tu hoja zao waendelee wenyewe.

halafu mmeona wengine wameanza kuchat na marafiki zao hapa kwenye thread kama wafanyavyo kwenye thread za jukwaa la MMU, sijui watu watabadilika lini!?

we jadili hoja nami nipo kufafanua hoja.

you are welcome.

kwa neema ya Mungu nitazikabili hoja zenu zote

Glory to God
Mi nakuuliza naomba unipe ushuda mmoja wa Wokovu ulioshuhudia na ukadhibitisha kweli huu wokovu unatoka kwa Mungu huyo unaemwamini! na nini kilikufanya uamini?
 
kama mimi uwezo wangu ni sh 100/- je inamaana nife? Mungu yupo fea kweli hapo?
Ndio maana hata kwenye kutoa sadaka Mungu alielekeza kutoa kadiri ya uwezo wako, hakusema fixed amount.

Sina hakika kama ni kwa kujua ama la, lakini naona unaharibu hoja yako/yenu yote.

Mbona watu wanakufa tu.....ina maana Mungu ameshindwa kazi? Kuna wengine wamekufa jana kwa ajali ya gari...lakini mimi na wewe tupo na keyboard! Ina maana sisi ni bora kuliko wao mbele za Mungu? Kama sisi sio bora kuliko wao, ina maana Mungu hayupo fair? La hasha! Hata hao wanaokunywa dawa hiyo ya Babu siku moja watakufa tu!

Kwa ujumla hoja ya kwamba eti kwa sababu Babu anatoza/ameagizwa kutoza sh 500 basi hilo halitoki kwa Mungu ni hoja legelege ambayo kwa maoni yangu inatokana na kutoelewa vizuri au kushindwa kutafsiri vizuri maandiko na pia kutofahamu uwezo wa Mungu na jinsi anavyotenda kazi.
 
Nisaidieni kidogo. Kuna mtu alienda akawa hana 500 akakataliwa kupewa huduma?

Na kuna sehemu babu amesema ameoteshwa kutoza 500?

swali zuri sana.
Naomba niaze kujibu swali la pili.
Kwa mujibu wa baubu mwenyewe alisema ameoteshwa gharama ya matibabu ni SHILINGI 500/- hilo alilitamka yeye mwenyewe ene ameambiwana Mungu mpaka jinsi ya kuigawa hiyo 500/- inayopatikana.

Swali lako la kwanza naomba nikujibu kwa swali.
Kuna siku babu alishawahi kutangaza kuwa asiye na 500/- aende tu atatibiwa?
 
Kwanza tukubaliane, kutoa sadaka sio lazima yaani kama huna kipato sio lazima kutoa.
Na sadaka pia sio lazima kutoa pesa(nirekebishwe kama nimekosea)
Na pia hiyo 10% uliyoitaja hapo nayo pia inategemea na kipato cha mtu(tunarudi pale palee)
Kama kuna askofu, padri au mchungaji anayesema sadaka ni lazima utoe kiasi fulani huyo ANAKOSEA.
Kuhusu biblia;
Kesi ya biblia hapa ni tofauti kabisa.
wapo wanaouza biblia kwa bei ya juu, wapo wanouza kwa bei ya chini na wapo pia wanaotoa bure.
Hawa wote hawajaoteshwa na Mungu.

Turudi kwenye tiba ya babu.
Mungu anapoagiza mtu anayetaka tiba yake ni lazma atoe sh 500/- ili apone na asiyekuwa nayo je?
Tiba iliyoelekezwa na Mungu!!
kama mimi uwezo wangu ni sh 100/- je inamaana nife? Mungu yupo fea kweli hapo?
Ndio maana hata kwenye kutoa sadaka Mungu alielekeza kutoa kadiri ya uwezo wako, hakusema fixed amount.

Kwanza naona unajileta we mwenyewe.
Umesema Biblia inapatikana sehemu nyingi, hivyo bei ni tofauti. Dawa ya Babu inapatikana wapi na wapi???
Huko zinapotoka Biblia bei ni fixed au????
Unaweza ukatuletea sehemu ambayo Babu amesema alioteshwa hiyo 500/-??

Turudi kanisani.
Ni kweli sadaka sio lazima pesa, ni chochote, lakin unafahamu kwamba zile bahasha za kutolea sadaka zimeandikwa umetoa kiasi gani kwa pesa tu na sio vinginevyo???
Kama unafahamu kwamba kutoa sadaka sio lazima, je kutafuta tiba ni lazima????
Babu alisema ni lazima utibiwe na yeye???
Kuna mtu alikosa 500/- akaomba asaidiwe ikashindikana???
Huyu Mungu alisema NA ASIYEFANYA KAZI ASILE, je kutayakumbuka haya maneno kweli???
Wewe uliyekuwa na 100/- uliomba kusaidiwa na Babu au mtu yeyote ikashindikana???
Je ni kweli haiwezekani kusaidiwa???

Bado hujasema, tunapoambia tuchangie ujenzi wa kanisa ili ifike kiasi fulani sio fixed amount??
Sare za kwaya je?? Kitatakiwa kiasi chochote kuzipata???
 
mpendwa kiby, kinachokustaajabisha ni nini?

wakristo hawatongozi? hawatongozwi? watumishi wa Mungu hawatongozi/tongozwa? sasa cha ajabu ni nini pale? kutongoza ni njia ya kujenga mawasiliano na mahusiano. si lazima mahusiano haya yaishie kwenye uzinzi au ngono. kama una maswali kuhusu hoja hizi, ziulize kwenye thread inayohusika, usitutoe kwenye mstari wa mada yetu hapa.

kuhusu kanisa ninaloshiriki ibada nimeishamjibu, inaonekana hujafuatilia post zote. rudi ukurasa wa nyuma utaona jibu langu kwake.

hayo ya mtumishi msagaji au fataki kwanza nimeshangaa baadaye nikakuelewa. kuwa wewe unaamini kuwa mtumishi ana haki na anaweza kukuburuza kuelekea kokote anakotaka, ili mradi tu kajiita au kaitwa "mtumishi"! kumbe basi ndio maana uko na babu kama chanda na pete bila kuona umuhimu wa kuhoji biashara yake na kama inakubaliana na maandiko matakatifu ya Mungu!

ushauri wangu kwako na kwa wengine ni kuwa usimtegemee mwanadamu bali mtegemee Mungu. soma neno lake nalo lifanyike taa na mwangaza miguuni mwako. imeandikwa, amelaaniwa yoyote amtegemeaye mwanadamu.

glory to God

.
Hebu nisaidie dadangu wewe unawatongoza wanaume ili nini? Hebu nitofautishie mwonekaniko wako wakati wa kutongoza na wakati wa kumshuhudia mtu habari za Yesu. Wewe kama unavyodai ni mkristo ulieokolewa na kwa mujibu wa biblia ni mwanamume ndie anaemtafuta mke na akiisha kumpata, humlipia mahari kwa wazazi wake ili iwe haki kwake.
Mbona weye dada wayapindua maandiko? Hata hivyo turudi nyuma wewe ni wakala wa nani? Maana kama ni wa Yesu umefungwa katika mipaka ya neno lake na sii vinginevyo.
Unaponishauri kutomtumainia mwanadamu unamaanisha nini haswa? Maana katika posti zangu zote hakuna mahali nimemtegemea babu wala kumfanya kinga yangu zaidi ya kumchukulia kama mtu(chombo) cha Mungu, aliyepata neema ya kipawa cha karama ya kuponya kimiujiza kutoka kwa Mungu. Kwanini una kawaida ya kumtangulia mtu na kujaribu kumwazia anayowaza badala ya kuyaamini yale anayotamka kwako?
Hata hivyo nakupongeza kwa kukomaa kutolea majibu kwa kila jambo. Siwezi nikakuita mshupavu wa kidini, kwani bado sijawa na uhakika huo.
Zaidi ya ya yote ubarikiwe na Mungu miss jude.
.
 
Miss Judith! Mi baada ya kupitia post yako na kwa jinsi ninavyosoma sikuzote,Ghafla nimepitiwa na maneno ya kuandika. Nitarudi baadae pls!
 
Back
Top Bottom