Hoja ya Shossi juu ya sh. 500/- ya babu

Hoja ya Shossi juu ya sh. 500/- ya babu

wajameni samahani....!

mi nashauri tuachane na mjadala wa bikira,turejee kwenye mjadala husika wa babu wa loliondo
 
Nakubaliana na haya maneno yako hasa kwenye kipengele cha kujikweza, NI kweli tunaishi kwa Neema ya Mungu tuuuuuuuu!!!
Sio kweli kwamba kama hujaanguka kwenye uzinzi kimatendo ni kwa sababu ya ujanja wako hapana ni kwa sababu ya Neema ya Mungu inayokulinda na kukuhifadhi.

Kuna watu tume/wamejikuta wanaingia kwenye mahusiano ya mapenzi bila hata kutarajia kwa sababu tuna miili na tupo duniani. Roho i radhi lakini mwili ni dhaifu. ILa tunayeweza yote katika MUNGU. Miss Judy, nyenyekea na itukuze Neema ya MUngu tuuuuu!!!

Hayo mengine ya babu, umeshasema vya kutosha.
TUOMBE SASA, cha Mungu kijulikane ni kipi.

Afu sasa na ninyi ndo nini kuhamishia thread kwenye BIKIRA jamani,
Au hoja zimeisha?
Haya kwa herini.
ILa MSIACHE KUOMBA, OMBENI BILA KUKOMA!!!

Usiondoke, ona majibu yako uliyouliza
 
Jamani tujadili kama dawa inaponya au la..na mambo mengine kama side effect nk..mambo ya imani ni magumu na yana jukwaa lake...ila tiba ni tiba na haina dini na mgonjwa ndo hufuata tiba sio tiba kumfuata mgonjwa.sioni tija kuijadili 500 wakati hata soda haitoshi wala daladala kwenda na kurudi posta haitoshi
 
maanake mi nimeshangaa kidogo kuna story zinamuhusisha BABU na freemasons
 
Maswali yako yooote yameegemea kwanza kwa KUNISEMEA NIMEFIKA KWA BABU.
Kwanza naomba usiwe unanikadiria, niulize kwanza kama nilifika Loliondo au la then ndio utaandalia validity ya hayo maswali yako

Unatakiwa ufahamu ya kwamba Babu yuko pale kutibu, sio kubadilisha imani za watu. Na hata ukipata dawa zake ukapona bado pia hakuchagulii imani. Yeye ameongozwa na Mungu akaponye watu wote wenye imani na wasio na imani.
Kwa hiyo imani inabaki kuwa ya mtu mwenyewe binafsi, kabla na baada ya kupata dawa.

Halafu then naona umeingiza Jina la Yesu hapa ili ionekane kuna utofauti.
Kwangu mimi mkristo, na hata kwa imani ya Walutheran uponyaji kwa Jina la Yesu, kwa Jina la Mungu bado ni kule kule tu.
Yaani Yesu, Mungu bado njia ni ile ile kwa Muumba wa Mbingu na Dunia. Maana Yesu ni Mwana wa Mungu, hivyo na yeye pia ni Mungu
Au wewe mwenzetu una separate vp hayo majina?????
Mkuu sipiyuuu shida mi mwenyewe nashindwa kuelewa, yeye anaamini kabisa yesu ni mungu, ila haamini mtu akiponywa kwa jina la mungu ila tu mpaka utamke Yesu!
 
Nimekusoma vizuri mpendwa,

Bikira inakuwa ni muhimu kuitaja kwa kuwa ukimsoma vizuri judith utamuona kwamba anajisifia kuwa na bikira katika umri wake wa miaka 26, kwa maneno mengine ni kama anajina kwamba amemaliza kazi, yuko kwenye njia sahihi lakin akasahau kwamba muda mfupi uliopita alikuwa anatoa darasa la kidunia-kutongoza, maandiko matakatifu hayatufundishi mbinu za kutongoza, yanatufundisha kuwa wanyenyekevu na upendo kwa binadamu wenzetu. Maandiko yanatuambia tutawezaje kusema tunampenda Mungu tusiyemuona ilihali tunawachukia majirani zetu tunaowaona kila siku??

btw, tuko pamoja tuanajribu kuwekana sawa.

Mkuu

Tatizo LD ameanza kuiona hii thread huku mwishoni, hajui chanzo cha watu kuzungumzia hiyo bikira.
Halafu tukieleza ukweli wa mienendo yake hapa JF wanasema tunamshambulia yeye binafsi.
Sasa sielewi mtu mwenye kujiita anauelewa mzuri wa neno la Mungu na maandiko yake anajitenganisha vipi na mienendo yake????
ANAEJIONA MSAFI AWE WA KWANZA KUMRUSHIA JIWE BABU
 
wajameni samahani....!

mi nashauri tuachane na mjadala wa bikira,turejee kwenye mjadala husika wa babu wa loliondo
Teamo huyu kaja kutukera hapa, hiyo bikira yake ina manufaa gani kwenye jamii hii si bora huduma ya babu watu wengi wanapona
 
Yeye kaoteshwa uponyaji na sio kuhubiri neno kama maandiko yanavyowafundisha. Kumbuka yeye hajaoteshwa kupitia maandiko, ameoteshwa kupitia ndoto.

Msiwe wachoyo kwa kuona imani zenu na yale mliyofundishwa ni bora kuliko imani za wengine. Msimhukumu babu mchungaji, Mungu ndiye mwenye kujua yote na si binadamu.
Yesu ni yule yule jana, leo na hata milele (Heb 13:8), neno la Mungu haliwezi kujipinga kwahiyo hawezi leo kusema eti mponywe miili tu bila roho. Ndiyo maana tunatakiwa kujua maandiko kwasababu kama hatujui yule mwovu atatushinda. Tunaambiwa kuwa mtu hataishi kwa mkate tuu (mambo ya kimwili kama uponyaji) bali katika kila neno.. (matayo 4:4). Sasa itakuwaje Mungu leo ajigeuke na kutaka kuponya tuu. Kumbuka mwili hauna thamani kama roho ndiyo maana shetani yeye hulenga roho zetu, angekuwa analenga miili tu mbona tungeipata.
 
eti wakuu...........!

is it possible babu akawa ni AGENT wa freemasons?...

kwa kuangalia ile alama ya TANO:
-anatibu magonjwa makubwa MATANO
-KWA GHARAMA YA SH 500
 
Mkuu sipiyuuu shida mi mwenyewe nashindwa kuelewa, yeye anaamini kabisa yesu ni mungu, ila haamini mtu akiponywa kwa jina la mungu ila tu mpaka utamke Yesu!

Mkuu
Hii tunaita ni confusion yenye kipaji
 
Yesu ni yule yule jana, leo na hata milele (Heb 13:8), neno la Mungu haliwezi kujipinga kwahiyo hawezi leo kusema eti mponywe miili tu bila roho. Ndiyo maana tunatakiwa kujua maandiko kwasababu kama hatujui yule mwovu atatushinda. Tunaambiwa kuwa mtu hataishi kwa mkate tuu (mambo ya kimwili kama uponyaji) bali katika kila neno.. (matayo 4:4). Sasa itakuwaje Mungu leo ajigeuke na kutaka kuponya tuu. Kumbuka mwili hauna thamani kama roho ndiyo maana shetani yeye hulenga roho zetu, angekuwa analenga miili tu mbona tungeipata.

una uhakika gani kama uponyaji ni mambo ya kimwili (mkate tu). Tatizo tunaweka tafsiri zetu, kwa matamanio yetu au ya wale waliotufunza. Tunasahau kuwa hatujui yote ya Mungu, hatujui nani mwovu na nani mwema, hatujui nani anafanya ya Mungu na nani anafanya ya shetani. Tumeemegemea kuhukumu.

Tukeshe tukiomba.
 
Ninachosema ni kuwa waangalifu kwani kama Babu anamwamini Mungu wa Abrahamu, Isaka na Yakobo basi kwanini asiwape neno kuwaelezea kwanini Yesu alikuja na kwanini hao watu wanatakiwa kumfuata yeye. Kama babu atasema yeye ni mganga mimi wala sita kuwa na shida. lakini kama ni mchungaji ni wajibu wake kuchunga kondoo wa bwana

Chamoto kama umesoma post zangu kabla nilisema "Binafsi sina uhakika na dawa anayotoa babu lakini sitotenda haki kuisema negatively kwa vile isije ikawa kwa kufanya hivyo ukawa unashindana na Mungu mwenyewe".

Ninapinga watu ku-conclude kwamba anachofanya yule babu si cha Mungu bila kuonyesha kimaandiko kwamba si cha Mungu. Binadamu tunadhani tunaweza kumchagulia Mungu nani amtumikie na amtumikie vipi. Ni vipi kama kweli mtu akinywa dawa na akapona undhani sifa atampa Mungu yupi hata kama hakuhubiriwa injili siku hiyo??? Kama Rahabu kahaba alikuwa ni mtumishi wa Mungu, Mchungaji mstaafu je??

Tuseme tu kwamba TUSIHUKUMU maana nani ajuaye kama afanyacho babu ni Kazi ya Mungu, ni nani yuko tayari kushindana na Muumba wake?? Eti chungu kimwambie mfinyanzi hujui kazi yako wewee... thubutuuuuu!!!!!!!!!!!!!!!!
 
nianze kwa kuweka wazi kuwa sina hakika na imani ya huyu ndugu yetu Mohamedi Shossi, sijui kama ni mwislamu, mkristo ama muumini wa dini nyinginezo.

aliweka wazi kuwa babu si size ya Yesu na alisema kuwa Yesu ni "world icon" na babu hawezi kulinganishwa naye hata kidogo. baadhi walimkosoa kumwita Yesu "world icon" na walikuwa na sababu zao. pia ametoa michango mingi tu mingine ila hapa nataka niungane naye na kumpongeza kwa kuhoji hiyo bei ya babu.

Mungu wetu afikie mahali apange bei!! tena ya huduma itokanayo na karama aliyotoa mwenyewe? kweli hapo pagumu kuingia akilini. tena mungu wake huyo akampa na mchanganuo wa namna atakavyozigawa hizo pesa, eti 300/- kwakanisa, yatima na wajane na 200/- za wahudumu wanaomsaidia kazi! kwa kweli naona kama hizi ni kashfa kwa Mungu wetu.

neema ya Mungu wetu ni kubwa na pana sana, na kamwe huyu babu asiichezee kiasi hiki. yeye atangaze kuwa ni mganga aliyekuja na dawa ya mti wa mrigariga, afuate taratibu za serikali za kujisajili kisheria ili serikali itambue kazi zake na aweke bei yake kama wawekavyo waganga wengine na tutamchukulia kama tunavyowachukulia waganga wengine.

hongera tena Mohamed Shossi, hoja yako ni njema na ya kweli. Mungu wetu hahitaji hata senti yetu moja. karama zake hutoa bure. michango kwa ajili ya kazi ya Bwana ni ya hiyari na kadiri mtu alivyojaaliwa kutoa.

ukishaweka bei (hata kama ni sh.10/-) maana yake ni kwamba asiye nayo hapati huduma! kumbuka madukani kuna pipi za sh.10/- na usipokuwa na hiyo sh.10/- hupati hiyo pipi. ndiyo maana ya bei. sasa babu anasema kama huna sh. 500/- kaa pembeni mwenye hela aje apate kikombe! hata akiamua kuwasamehe wengine kulipa, manake atakuwa kakiuka utaratibu wa huyo mungu wake anayedhibiti bei! sasa hii nayo bado ni huduma ya kiroho kweli kwa mujibu wa dini ya kikristo? mungu gani huyu anayepanga hesabu hivi?

tuendelee kutafakari na kuliombea kanisa

Mungu akubariki sana ndugu Mohamedi Shossi,

Glory to God!

Kimsingi hata Yesu alihitaji hela kwa ajili ya kujikimu yeye na wanafunzi wake. Ushahidi ni kuwa Yuda Iskarioti alikuwa mtunza hazina. Walipata wapi fedha ilhali kina Petro walikuwa wameacha kazi ya kuvua samaki? Babu kutoza 500 si jambo la ajabu. Haiwezekani utoe nauli 80,000shs halafu ukose 500 ya dawa.
Be Jealous!
 
eti wakuu...........!

is it possible babu akawa ni AGENT wa freemasons?...

kwa kuangalia ile alama ya TANO:
-anatibu magonjwa makubwa MATANO
-KWA GHARAMA YA SH 500
Hommie naona unaanzisha ligi nyingine hapa!!
 
Maswali yako yooote yameegemea kwanza kwa KUNISEMEA NIMEFIKA KWA BABU.
Kwanza naomba usiwe unanikadiria, niulize kwanza kama nilifika Loliondo au la then ndio utaandalia validity ya hayo maswali yako

Unatakiwa ufahamu ya kwamba Babu yuko pale kutibu, sio kubadilisha imani za watu. Na hata ukipata dawa zake ukapona bado pia hakuchagulii imani. Yeye ameongozwa na Mungu akaponye watu wote wenye imani na wasio na imani.
Kwa hiyo imani inabaki kuwa ya mtu mwenyewe binafsi, kabla na baada ya kupata dawa.

Halafu then naona umeingiza Jina la Yesu hapa ili ionekane kuna utofauti.
Kwangu mimi mkristo, na hata kwa imani ya Walutheran uponyaji kwa Jina la Yesu, kwa Jina la Mungu bado ni kule kule tu.
Yaani Yesu, Mungu bado njia ni ile ile kwa Muumba wa Mbingu na Dunia. Maana Yesu ni Mwana wa Mungu, hivyo na yeye pia ni Mungu
Au wewe mwenzetu una separate vp hayo majina?????

Nimeshakuelewa cpu, ubarikiwe na nisamehe kwa kukuambia umefika kumbe hujafika. Ila pia nashukuru kwa sababu sasa nimekuelewa vizuri sana.
 
There you err again, there are five fold ministries.
Kuhubiri neno la Mungu sio kipimo cha kuwa mtumishi wa Mungu. Hebu tukumbushane kidogo maana babu kaingilia huduma za watu (1Cor 12:.....New Translation)..
Mimi sijakataa usemayo ila babu hata kuwaambia waliopokea uponyaji kwamba ni Mungu ndiye aliyewaponya ili jina lake litukuzwe?
 
Hommie naona unaanzisha ligi nyingine hapa!!

hahahaha!
UEFA CUP hiyo.....

lakini nimepata storiiz chini ya carpet kwamba BABU NI FREEMASONS live...

nasikia hata dawa wanakunywa watu watano watano....
 
Back
Top Bottom