The Phylosopher
JF-Expert Member
- Mar 11, 2015
- 1,503
- 2,046
Kwa nijuavyo mimi siasa ni mchezo wa kusoma vizuri alama za nyakati, tangu wanasiasa wakomavu hata wachanga hutafuta mambo mazito na magumu anayokabiliana nayo mwananchi siku kwa siku.
Hayo mambo ndiyo hutangulizwa mbele kuwa chambo cha kampeni yoyote mnayopiga. Nakumbuka kwa mfano CHADEMA walikuja na hoja ya kupambana na ufisadi, hoja ambayo wananchi tuliielewa vizuri kwani kila raia aliumizwa na vitendo vya ufisadi hivyo CHADEMA walipokuja na hoja hiyo ilipokelewa kwa hisia na kueleweka vizuri na kwa urahisi sana.
Yapo matatizo mengi yanayo muumiza mwananchi moja kwa moja ambayo ni mtu mwenye upeo wa juu kidogo atakayekua na uwezo wa kuhusuanisha hayo matatizo na mapungufu ya kikatiba.
Vinginevyo watu wengi wanaona ni kama kelele zoote mnazopiga kuhusu katiba mpya ni ili ziwasaidie kuingia ikulu.
Nitoe wito kwa wapinzani fanyeni utafiti wa matatizo ya watu na angalieni upeo wa walio wengi kujua wanaamini yatatatuliwaje.
Imani yangu ni kwamba ukiweka chat yenye nafasi kumi yaani, 1...10 ya mambo ambayo mwananchi wa kawaida anayataka huenda katiba mpya ikaambulia 2% kwani wengi wa wnaoongelea katiba ni wale wenye elements za siasa ndani yao!
Wakati katika mchakato wa kupiga kura tunawahitaji wote.
Ni kwa sababu hiyo munahitaji kuja na hoja zitakazoeleweka na kuvutia makundi yote ili kupata uungwaaji mkono wa kutosha kwenye hoja yenu!