Hoja ya Katiba Mpya inawapotezea muda wapinzani. Mbona yapo mengi yanayoeleweka kirahisi!

The Phylosopher

JF-Expert Member
Mar 11, 2015
1,018
2,000
Kwa nijuavyo mimi siasa ni mchezo wa kusoma vizuri alama za nyakati, tangu wanasiasa wakomavu hata wachanga hutafuta mambo mazito na magumu anayokabiliana nayo mwananchi siku kwa siku.

Hayo mambo ndiyo hutangulizwa mbele kuwa chambo cha kampeni yoyote mnayopiga. Nakumbuka kwa mfano CHADEMA walikuja na hoja ya kupambana na ufisadi, hoja ambayo wananchi tuliielewa vizuri kwani kila raia aliumizwa na vitendo vya ufisadi hivyo CHADEMA walipokuja na hoja hiyo ilipokelewa kwa hisia na kueleweka vizuri na kwa urahisi sana.

Yapo matatizo mengi yanayo muumiza mwananchi moja kwa moja ambayo ni mtu mwenye upeo wa juu kidogo atakayekua na uwezo wa kuhusuanisha hayo matatizo na mapungufu ya kikatiba.

Vinginevyo watu wengi wanaona ni kama kelele zoote mnazopiga kuhusu katiba mpya ni ili ziwasaidie kuingia ikulu.

Nitoe wito kwa wapinzani fanyeni utafiti wa matatizo ya watu na angalieni upeo wa walio wengi kujua wanaamini yatatatuliwaje.

Imani yangu ni kwamba ukiweka chat yenye nafasi kumi yaani, 1...10 ya mambo ambayo mwananchi wa kawaida anayataka huenda katiba mpya ikaambulia 2% kwani wengi wa wnaoongelea katiba ni wale wenye elements za siasa ndani yao!
Wakati katika mchakato wa kupiga kura tunawahitaji wote.

Ni kwa sababu hiyo munahitaji kuja na hoja zitakazoeleweka na kuvutia makundi yote ili kupata uungwaaji mkono wa kutosha kwenye hoja yenu!
 

Anita Kajembe

JF-Expert Member
Jun 29, 2021
215
500
Katiba iliyopo ndiyo ilituletea Rais mwenye absolute power aliyeweza kuamrisha uchafuzi badala ya uchaguzi 2020. Katiba mpya itawasaidia wananch kuongozwa na viongozi waliowachagua na si waliochaguliwa na CC ya CCM

Furaha na amani ya wananch itaanzia hapo na furaha na amani ndiyo kiini cha mafanikio.
 

Tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
44,464
2,000
Wakati wananchi wamehamasika na madai ya katiba mpya 2010-2015 hawakuwa wanajua hizo agenda nyingine? Isitoshe mambo yanayofanyiwa kazi ni yale yenye utashi wa viongozi, au yenye msukumo hasa wa wanasiasa. Kama ingekuwa mahitaji ya wananchi ndio yanafanyiwa kazi na sio ya viongozi, ndege zisingenunuliwa huku wananchi wengi wakiwa na matatizo ya maji. Ni hivi tunataka katiba mpya, hizi porojo zenu bakini nazo.
 

PTER

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
17,239
2,000
Unawezaje kupambana na ufisadi wakati Katiba inawalinda mafisadi wakuu?

Suluhisho ni katiba itakayowawezesha wananchi kumwajibisha kiongozi fisadi badala ya kusubiri hisani ya rais.
 

Lord OSAGYEFO

JF-Expert Member
Feb 19, 2021
2,059
2,000
HATUDANDANYIKI KAMA NI MUDA TUMEOPOTEZA MIAKA 60 ILIYOPITA NA KAMA NI KUPOTEZA MUDA CCM WASINGEOMBA WASUBIRIWE
 

mgaka12

JF-Expert Member
Mar 19, 2017
582
1,000
Tanzania ni moja ya nchi yenye katiba bora kabisa mm naona DJ Mbowe na Wafuasi wake wapambanie katiba hii ifatwe (itekelezwe) japo kwa 90% tu wataona changes kubwa sana ni upuuzi kudai nguo mpya tukiwa watupu japo tuvae hizi nguo chakavu wkt tunadai nguo mpya
 

Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
53,822
2,000
Katiba iliyopo ndiyo ilituletea Rais mwenye absolute power aliyeweza kuamrisha uchafuzi badala ya uchaguzi 2020. Katiba mpya itawasaidia wananch kuongozwa na viongozi waliowachagua na si waliochaguliwa na CC ya CCM

Furaha na amani ya wananch itaanzia hapo na furaha na amani ndiyo kiini cha mafanikio.
Good
 

Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
53,822
2,000
Katiba mpya siyo mali ya CCM wala CHADEMA, ni mali ya wananchi hivyo tunaitaka
 

cariha

JF-Expert Member
Apr 9, 2015
20,780
2,000
Kuna matatizo mengi yanayogusa wananchi kuliko katiba hata huku mtaani watu hawazungumzii ila Kuna matatizo ka ajira kwa vijana, utitiri wa Kodi unaoumiza wananchi wengi na huduma ka za afya Sasa hyo katiba ni njaa za wananchi wapi na wapi. CDM waje na agenda zinazogusa wananchi direct sio kutaka uraisi wa wao kupata madaraka ka ccm
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom