Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,014
- 144,371
Viongozi wa nataifa mbalimbali wakitembelea nchi yetu, magari husimamishwa kupisha msafara na Rais wa Taifa kama Marekani ndio kabisa mji mzima unaweza kusimama (nakumbuka kufuru ya msafara wa George W. Bush kutoka KIA kwenda Arusha miaka ya 2000 mwanzoni).
Miaka ya nyuma bila shaka walikuwa wanapewa hizo heshima kwa malengo ya kiusalama, ila kwa miaka hii nawaza kama maraisi wetu bado wanapewa heshima za aina hiyo hasa kwa marais kutoka mataifa machanga ya kiafrika ingawa hadhi ya Rais wa nchi haitegemei ukubwa au udogo wa Taifa lake mradi tu ni Raisi wa nchi.
Swali langu ni je, marais wa nchi zetu hizi za kiafrika kama Tanzania, Rais akiwa safarini huko Marekani au Ulaya, anakuwa na msafara na magari husimamishwa kupisha msafara wake?