Tundu Lissu: Ubelgiji nchi Tajiri Msafara wa Waziri Mkuu una magari 3 tu, Tanzania nchi maskini Msafara wa Rais una magari zaidi ya 200!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,968
141,980
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu amesema Serikali ya Tanzania ina Matumizi ya anasa ya kodi za wananchi.

Amesema kwa mfano Ubelgiji Msafara wa Mkuu wa Nchi ambaye ni Waziri Mkuu una magari 3 tu na ni nchi Tajiri lakini hapa Tanzania Msafara wa Rais una magari zaidi ya 200.

Sasa piga hesabu ya mafuta, posho, upigaji nk, ni lazima tutaendelea kuwa maskini kwa kitambo kirefu.
 
Makamu mwenyekiti wa Chadema mh Tundu Lisu amesema Serikal ya Tanzania ina Matumizi ya anasa ya kodi za wananchi

Amesema kwa mfano Ubelgiji Msafara wa mkuu wa nchi ambaye ni Waziri mkuu una magari 3 tu na ni nchi Tajiri lakini Hapa Tanzania Msafara wa Rais una magari zaidi ya 200
Sasa piga hesabu ya mafuta, posho,upigaji nk ni lazima Tutaendelea kuwa maskini kwa kitambo kirefu
Population ya Ubeligiji na huku anapokulinganisha vikoje?
 
Kiongozi wa upinzani nchini ubelgiji anatumia baiskeli, huu hapa msafara wa mwenyeki wangu
download.jpeg
 
Makamu mwenyekiti wa CHADEMA mh Tundu Lissu amesema Serikali ya Tanzania ina Matumizi ya anasa ya kodi za wananchi

Amesema kwa mfano Ubelgiji Msafara wa mkuu wa nchi ambaye ni Waziri Mkuu una magari 3 tu na ni nchi Tajiri lakini Hapa Tanzania Msafara wa Rais una magari zaidi ya 200

Sasa piga hesabu ya mafuta, posho, upigaji nk ni lazima tutaendelea kuwa maskini kwa kitambo kirefu

Mikutano ya kisiasa itakuwa na maana viongozi wakiitumia kuhamasisha maendeleo badala ya kujenga chuki kati ya Watawala na Wananchi. Naamini waliohudhuria mkutano huo walipenda kusikia kiongozi huyo ana Sera na Mikakati ipi ya kuwaletea maendeleo badala ya Utawala ambao msafara wa Rais una msururu wa magari.

Du, kumekucha na malalamiko ya viongozi wa upinzani
 
Msafara unahusisha population?
Ndio, Kwa maana sisi nchi zenye high population tunatumia indirect democracy ambapo jamiii inawakilishwa na WAWAKILISHI kutoka vijiji, KATA, Hadi jimboo, hivyo haoviongozi wote lazima wawepo kwenyemsafara wa raisi kwani yapo mambo mengi raisi anaweza kuwauliza wao WAWAKILISHI wa maeneohusika.

Hakuna raisi anayetumia masafara wa magari 500, huo ni uongo, raisi anakuwa na gari lake Moja tuu, mengine yanakuwa na wawakilish wa MAENEO husikaaa. Wakuuu wa idara mbalimbali lazima waambatane naye. Ndio MAANA nimeuliza population ya ubeligiji na huku vikojee??
 
Ndio, Kwa maana sisi nchi zenye high population tunatumia indirect democracy ambapo jamiii inawakilishwa na WAWAKILISHI kutoka vijiji, KATA, Hadi jimboo, hivyo haoviongozi wote lazima wawepo kwenyemsafara wa raisi kwani yapo mambo mengi raisi anaweza kuwauliza wao WAWAKILISHI wa maeneohusika. Hakuna raisi anayetumia masafara wa magari 500, huo ni uongo, raisi anakuwa na gari lake Moja tuu, mengine yanakuwa na wawakilish wa MAENEO husikaaa. Wakuuu wa idara mbalimbali lazima waambatane naye. Ndio MAANA nimeuliza population ya ubeligiji na huku vikojee??
Kwanini Wakuu wa Idara wasipande Shabiby au Abood?
 
Ndio, Kwa maana sisi nchi zenye high population tunatumia indirect democracy ambapo jamiii inawakilishwa na WAWAKILISHI kutoka vijiji, KATA, Hadi jimboo, hivyo haoviongozi wote lazima wawepo kwenyemsafara wa raisi kwani yapo mambo mengi raisi anaweza kuwauliza wao WAWAKILISHI wa maeneohusika. Hakuna raisi anayetumia masafara wa magari 500, huo ni uongo, raisi anakuwa na gari lake Moja tuu, mengine yanakuwa na wawakilish wa MAENEO husikaaa. Wakuuu wa idara mbalimbali lazima waambatane naye. Ndio MAANA nimeuliza population ya ubeligiji na huku vikojee??
Tukichukulia kwa mfano huo wa msafara wa magari matatu kuwa kweli, unafikiri huko hakuna hao wakuu wa idara na wawakilishi wengine katika ngazi za utawala kiserikali?
 
Dunduka katika ubora wake, et magari zaidi ya 200!

Hizi kamba za ufipa
 
Back
Top Bottom