Ziara ya Rais wa China nchini Marekani yaongeza utulivu katika uhusiano wa nchi hizo mbili

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,034
VCG111378067918.jpg

Mwezi uliopita, rais Xi Jinping wa China alifanya ziara rasmi nchini Marekani, ambako pia alihudhuria mkutano wa Ushirikiano wa Kiuchumi wa Asia na Pasifiki (APEC) uliofanyika mjini San Fransisco.

Katika ziara hiyo, rais Xi alikutana na mwenyeji wake, rais Joe Biden wa Marekani, na kufanya mazungumzo ya ana kwa ana, ambayo ni ya pili kati ya viongozi hao baada ya rais Biden kuingia madarakani. Mazungumzo hayo yamefuatiliwa sana na jamii ya kimataifa, ikizingatiwa kwamba, China na Marekani ni nchi mbili kubwa kiuchumi duniani, na uhusiano kati ya nchi hizo ni muhimu kwa mustakabali wa dunia.

Wachambuzi wa nchini China wanaona kuwa, kwa sababu China kwa sasa imeonyesha njia sahihi ya kufuata kuhusu jinsi ya kuendeleza uhusiano kati ya nchi hiyo na Marekani, ni wakati sasa wa kuona jinsi gani Marekani itafanya na kwa kiwango gani wasiwasi wa nchi hiyo utaathiri mustakabali wa siku za baadaye wa uhusiano kati ya China na Marekani. Wakati wa mkutano wa APEC, dunia pia iliona uaminifu na uwazi wa China katika kuchangia ufufukaji wa uchumi wa dunia, ili dunia ambayo inakabiliwa na hali ya wasiwasi na vurugu katika baadhi ya maeneo, inaweza kunufaika na faida zinazotokana na soko la China kwa uaminifu zaidi.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la China, Xinhua, alipokuwa nchini Marekani akiwa katika msafara wa ziara ya rais Xi, Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, aliongea na wanahabari kuhusu mazungumzo kati ya rais Xi na rais Biden, na kusema ziara ya rais Xi nchini Marekani imevutia ufuatiliaji wa kimataifa, na hivyo kuongeza utulivu katika uhusiano kati ya China na Marekani, na kuleta chachu mpya katika ushirikiano wa Asia na Pasific, na kuleta nguvu chanya katika mazingira ya kikanda na kimataifa.

Wang Yi amesema, katika mazungimzo yake na rais Biden mjini San Francisco, rais Xi alisema kuwa nchi hizo mbili, China na Marekani, zinapaswa kuchukua kuwa na malengo mapya, na kwamba zinapaswa kuendeleza mtazamo sahihi, kwa pamoja kusimamia tofauti zao kwa ufanisi na kuheshimu kanuni na mipaka ya kila nchi. Pia rais Xi alisema nchi hizo mbili zinapaswa kubeba wajibu kama nchi kubwa kiuchumi duniani na kwa pamoja kuboresha mawasiliano kati ya watu na watu. Ameongeza kuwa, kauli hiyo imejenga kwa pamoja misingi mitano kwa uhusiano wa China na Marekani.

Wang Yi aliwaambia wanahabari kuwa, kutokana na juhudi za pande zote mbili, zaidi ya matokeo 20 yalipatikana katika mkutano kati ya marais hao, ikiwemo kuanzishwa kwa kikosi kazi cha ushirikiano wa kupambana na dawa za kulevya, makubaliano ya kuanzisha tena, katika msingi wa kuheshimiana na usawa, mawasiliano ya ngazi ya juu na majadiliano ya kitaasisi kati ya majeshi ya nchi hizo mbili, na kwa pamoja kuboresha mafanikio ya Mkutano wa 28 wa Hali ya Hewa wa Umoja wa Mataifa utakaofanyika mjini Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu.

Lu Xiang, mtaalamu wa elimu ya Marekani na mtafiti mshiriki kutoka Akademia ya Sayansi ya Jamii ya China anasema, kwa kutoa misingi hiyo mitano, rais Xi ameuambia upande wa Marekani jinsi ya kuendeleza kwa njia sahihi uhusiano wa pande mbili, na huu ni mwongozo unaoweza sio tu kuhakikisha kuishi kwa masikilizano kati ya pande hizo mbili, lakini pia kufanya ushirikiano wa kunufaishana kuwa kiini cha maslahi ya watu wa pande hizo mbili. Hata hivyo, Lu amesema, kama uchokozi na shughuli za kijeshi za Marekani katika maeneo kama Taiwan na Bahari ya Kusini ya China vitaendelea, ni wazi kwamba mvutano na mgogoro kati ya nchi hizo mbili utaibuka tena na tena.

Profesa Li Haidong wa Chuo Kikuu cha Masuala ya Kigeni cha China anasema, mazungumzo kati ya rais Xi na rais Biden yamethibitisha kwamba makundi yasiyotaka kuona uhusiano kati ya China na Marekani unatulia hayatanyamaza baada ya mkutano huo, na kwamba kama kawaida, vyombo vya habari vya nchini Marekani vitaelewa vibaya umuhimu wa mkutano huo na haja ya pande zote mbili kusimamia tofauti zao.

Msaidizi wa mkuu wa Shule ya Elimu ya Kimataifa katika Chuo Kikuu cha Renmin nchini China, Jin Canrong anasema, ingawa bado kuna changamoto na matatizo katika upande wa Marekani, ni muhimu kwa China kuonyesha uwajibikaji wake na kutoa majibu kwa dunia na kwa historia ya kudhibiti mvutano kati ya China na Marekani.

Pia anasema, mkutano kati ya rais Xi na rais Biden umeleta nafuu kubwa katika mazingira ya nchi hizo mbili, na kwamba huu ni msingi kwa nchi hizo kubwa duniani kusimamia uhusiano wao katika njia sahihi, kujenga tena uaminifu na pia kutafuta uwezekano wa ushirikiano.
 
Back
Top Bottom