Hivi Rais wa Tanzania akienda nchi kama Marekani, magari husimamishwa kupisha msafara wake?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
42,928
2,000
Viongozi wa nataifa mbalimbali wakitembelea nchi yetu, magari husimamishwa kupisha msafara na Rais wa Taifa kama Marekani ndio kabisa mji mzima unaweza kusimama (nakumbuka kufuru ya msafara wa George W. Bush kutoka KIA kwenda Arusha miaka ya 2000 mwanzoni).

Miaka ya nyuma bila shaka walikuwa wanapewa hizo heshima kwa malengo ya kiusalama, ila kwa miaka hii nawaza kama maraisi wetu bado wanapewa heshima za aina hiyo hasa kwa marais kutoka mataifa machanga ya kiafrika ingawa hadhi ya Rais wa nchi haitegemei ukubwa au udogo wa Taifa lake mradi tu ni Raisi wa nchi.

Swali langu ni je, marais wa nchi zetu hizi za kiafrika kama Tanzania, Rais akiwa safarini huko Marekani au Ulaya, anakuwa na msafara na magari husimamishwa kupisha msafara wake?
 

Chaliifrancisco

JF-Expert Member
Jan 17, 2015
16,631
2,000
Hakuna kitu kama hicho mzee. Hayo mambo yapo TZ tu. Kwa wenzetu hakuna foleni za kijinga.

Sana sana wana cordon baadhi ya streets tu kwaajilo ya usalama ila mambo ya kuzuia magari eti kupisha msafara hamna.
 

JABALI LA KARNE

JF-Expert Member
Apr 19, 2021
1,254
2,000
Ukienda kijijini na gari lako vs jirani yako wa kijijini akija mjini na pikipiki yake kuna utofauti gani?
 

stateman_

New Member
Jan 20, 2021
2
45
Anapewa heshima zote kama Mh.Rais pale anapotembelea nchi husika kwa ziara ya kiofisi. Kumbuka lazima kuna mwaliko na sheria za mwaliko kidiplomasia mwenyeji lazima atimize mahitaji ya mgeni, hapa tunazungumzia malazi yake na wasaidizi wake wote pia hiyo kazi inafanywa na balozi pamoja na wasaidizi wa Rais wanaohusika na ziara za nje ya nchi.

Si vema sana kuweka wazi ila kwa wenzetu wapo very systematic in such a way kustukia tukio kama hilo ni nadra kutokanana mazingira pamoja na wenzetu kujali sana muda na usalama wa wageni ni kitu kwao cha msingi na hawapo kutafuta attention. Kumalizia anapewa heshima zote zinazopaswa kupewa kiongozi wa nchi akiwa ziarani
 

Earthmover

JF-Expert Member
Sep 28, 2012
18,024
2,000
Akienda kwa shughuli binafsi no vimulimuli yaani kaladi tu kama raia only VIP LOUNGE ..vimulimuli mpaka mwaliko rasmi yaani official escorts
 

Criss

JF-Expert Member
Mar 19, 2011
858
250
Tofauti kubwa huwa kwenye miundombinu tu lakini kwa heshima huwa ni yakiwango sawa bila kujali utofauti wa ukubwa wa Taifa lake au Uchumi wake.

Kwetu wanatumia barabara zaidi na mbaya zaidi hatuna barabara mbadala tofauti na zile zinazotoa huduma kwa uma , kwa wenzetu hali huwa tofauti kidogo.

Moja huwa na barabara mbadala au wakati mwingine kupokewa kwa helicopter inategemea na maeneo aliyoshukia na anakotaka kuelekea.

Wenzetu issue ya muda na haki za raia wanazichukulia very seriously .
 

Lakasa chika7

JF-Expert Member
Jan 7, 2017
378
1,000
Viongozi wa nataifa mbalimbali wakitembelea nchi yetu, magari husimamishwa kupisha msafara na Raisi wa Taifa kama Marekani ndio kabisa mji mzima unaweza kusimama( nakumbuka kufuru ya msafara wa George W. Bush kutoka KIA kwenda Arusha miaka ya 2000 mwanzoni)...
Zipo njia special za viongozi ambazo raia hawapiti.
 

Hero

JF-Expert Member
Aug 20, 2010
3,721
2,000
Viongozi wa nataifa mbalimbali wakitembelea nchi yetu, magari husimamishwa kupisha msafara na Raisi wa Taifa kama Marekani ndio kabisa mji mzima unaweza kusimama( nakumbuka kufuru ya msafara wa George W. Bush kutoka KIA kwenda Arusha miaka ya 2000 mwanzoni)...
Ndio maana Dr. JPM hakutaka kwenda kwao maana hakupenda dharau 😜 Lakini yule mwingine alikuwa kama raia wa huko, anatukanwa yumo tu😡! Alifanya nchi yetu kudharirika sana isee!? RIEP our great African hero Hon Dr JPM 🙏👊💪!
 

Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
11,061
2,000
Swali langu ni je, maraisi wa nchi zetu hizi za kiafrika kama Tanzania, Raisi akiwa safarini huko Marekani au Ulaya,anakuwa na msafara na magari husimamishwa kupisha msafara wake?
Thubutu!

Nani atakubali upuuzi huo.

Sana sana patakuwepo na askari wawili watatu kuhakikisha usalama, basi; na hasa kama kuna maandamano ya wananchi wake walioko huko wakipinga siasa zake.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom