Hivi nani aliweza kuacha pombe kabisa?

Hivi nani aliweza kuacha pombe kabisa?

Wazee wenzangu (mabibi na mabwana),
Natumaini mko wazima kabisa.

Mimi ni mwanaume, na nafikisha miaka 30 this year.

Unajua kwenye maisha kuna mambo mengi tunafanya kwa kukusudia yawe mazuri au mabaya, ila mara nyingi tunajutia yale mabaya.

Najuta sana kuwa addicted na Bia, na ninaona kabisa ni adui yangu ila haipiti siku bila kuuweka, this hurts me sana.

Kuna aliyeweza kuacha bia kabisa na aliwezaje?. Natamani niache, chaah! this too much.

NB: Ushauri wa kukaa mbali na vishawishi au mbali na washkaji nishajaribu na haujafaa, maana kiu ya bia hatari sana. Hata ukikaa mwenyewe utaitafuta.

Sijaacha pombe kabisa, so this is a little bit off.

Mimi niliweza kuacha pombe kwa mwakamzima mwaka juzi, na hata sasa nikiamua kuacha naacha.

Na nikiamua kuacha, sharti langu ni kwamba niwe na mizinga ya Scotch Whisky isiyopungua mitatu ndani, na bia ziwe kwenye friji.

Halafu naamua kuacha huku naziona hizo pombe kila siku.

Hapondipo najua nimeamuakuacha.

Nikiwa sina pombe ndani, halafu nasema nimeacha, nakuwa sina uhakika kama nimeacha kweli, au nimeishiwa pombe tu.
 
Mimi niliwahi kuwa kama wewe nilianza kunywa bia nikiwa high school nikawa mnywaji wa kudumu nikiwa chuo kuna kipindi nilikua siwezi kupitisha siku sijanywa.
Nilifika hatua nikawa natetemeka yani miaka 29 lakini tayari nimekua mnywaji nikiyekubuhu sasa how niliacha hapa ndipo palinitesa sana.

Nilianza kupunguza kwenda maeneo niliyopendelea kwenda sana nikawa nakunywa bia 3 kila baada ya siku mbili lakini kinywaji changu kikubwa kilikua malta na maji aisee nilikua nakunywa maji vibaya sana.

Nikafanikiwa kuwa nakunywa bia 3 kwa wiki sasa nikaanzisha saving kwa ajili ya kufanikisha jambo flani nilifanikiwa kutoigusa Bia muda sana hatimae nikafanikiwa kabisa kuto gusa bia kwa takriban miezi minne nikawa nikitoka na washkaji nakunywa tonic water mwisho nikazoea hali yangu nikawa naona kawaida kabisa.

Nikashinda mwisho nikawa nimefanikiwa na mpaka leo nasikia watu wanakunywa so sasa naitawala na sitaki itawale mwili wangu tena so far tangu mwaka jana mwezi wa pili mpaka leo sijagusa pombe

So nikwambie inawezekana but you need very high burning desire
Hongera ndugu ,
Nami nadhamiria kuacha kabisa,
Mungu atusaidie katika hili,

Pombe inaharibu bajeti na mipango mingi sana.

Ukinywa bia 4 elfu 10 imekutoka na bado hujachangamka.

Kila siku unakunywa zaidi ya bia nne hapo kwa mwezi ni zaidi ya laki 3, ambayo kwa baadhi ya watumishi ni mishahara ya mwezi na wanamudu majukumu yao ya kila siku.

Unajikuta hupigi hatua kumbe kinachorudisha nyuma ni pombe.

Hakika haifai. Kama utakunywa mara moja moja hasa weekend sidhani kama ni shida Ila kama ni daily hapa ni shida na ndipo tunapotakiwa kujiepusha.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee pombe acha tu, ilifika mahali nikinywa namuota marehemu mamaangu ananionya kwamba " mwanangu acha pombe unaelekea kubaya" nikiamka napatwa na uchungu nakaa kitandani nalia weeee!! Halafu naenda kazini,

Kuna kipindi kikafika mizimu yangu ikagoma kuwa nisijaribu tena pombe, nikaacha nilikuja kujaribu ikawa kero nikaacha mazimaaa!!

Pombe sio jambo la maana ikikuzidi ni utumwa, unaweza kuharibu future yako kizembe sana.
Kaabiiisaa mkuuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wazee wenzangu (mabibi na mabwana),
Natumaini mko wazima kabisa.

Mimi ni mwanaume, na nafikisha miaka 30 this year.

Unajua kwenye maisha kuna mambo mengi tunafanya kwa kukusudia yawe mazuri au mabaya, ila mara nyingi tunajutia yale mabaya.

Najuta sana kuwa addicted na Bia, na ninaona kabisa ni adui yangu ila haipiti siku bila kuuweka, this hurts me sana.

Kuna aliyeweza kuacha bia kabisa na aliwezaje?. Natamani niache, chaah! this too much.

NB: Ushauri wa kukaa mbali na vishawishi au mbali na washkaji nishajaribu na haujafaa, maana kiu ya bia hatari sana. Hata ukikaa mwenyewe utaitafuta.
Mkuu INAWEZEKANA KABISA kama UKIAMUA.
Mimi nilianza kinywa pombe nikiwa na miaka 14,nilikunywa aina mbalimbali zza pombe,(za kienyeji na zenye TBS)
Unywaji ulikiwa ni wa Kiwango cha KULEWA.
Unywaji wangu ulichanganya na uvutaji sigara bangi.
Baada ya miaka 7 nikiwa na miaka 22, NILIACHA VYOTE NDANI YA SIKU MOJA.
Nilienda kwenye IBADA kanisa la WALOKOLE na mwishoni mwa IBADA waliita watu KUOKOKA,nikafanya hivyo.
Kuanzia hapo KIU ya vyote hivyo iliisha,leo ni mwaka wa16 nimeachana na ULEVI!
ASANTE YESU kwa muujiza huu.
 
Nilianza pombe 2000 hadi kufikia 2010,siku ambazo sikunywa pombe hazizidi 5,

ha ha ha,

leo ni miaka 6,tangu 2012 sijaweka pombe mwilini,
inahitaji uamzi tu,

na lazima uteseke kwa miezi miwili mitatu wakati alicohol ikitoka ndani ya mwili

Well said ndugu... Ukiamua unaacha, hakuna kitu kinachoshindikana
 
Mi nilianza kunywa pombe (beer) mwaka 2001 baada ya kupata ajira kwenye taasisi moja ya kiserikari,hii ilitokana na kuambatana na marafiki ambao walikuwa mapampula.Ila nilikuwa na matatizo yafuatayo: nikilewa nakuwa mkorofi kupindukia,pia nikishalewa nashindwa kuvuka barabara hii ya kigogo pale landa bar pamenitesa sana hasa usiku gari iko kigogo mwisho ikinipiga mwanga tu hata nipo katikati ya barabara nitarudi kuanza upya,mwisho asbh nilikuwa nikiamka kichwa kinauma hatari naambiwa dawa yake nikazimue tena pombe. Nikafikiria mwisho nikaamua kuachana na marafiki pampula na kuanza maisha kivyangu mpaka bia naiona kama tako la mama mkwe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hujaamua bado,hata sober house hawamuachishi mtu urahibu Ila wanamsaidia kuacha baada ya yeye kuamua kuwa anataka kuacha,we kisaikolojia hata uandishi wako unaonyesha bado unaipa kipaimbele pombe.Wewe ukiamua hakuna lililo gumu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi mvinyo nayo ni kundi la pombe? Teh teh, mara moja kwa mwaka angalau napooza koo na chupa ya mvinyo kidogo.
 
Back
Top Bottom