MSD kuleta dawa ya kuacha kunywa pombe

MSD kuleta dawa ya kuacha kunywa pombe

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
27,560
Reaction score
62,126
Bohari Kuu ya Dawa Tanzania (MSD) imesema ipo mbioni kuleta dawa ya kusaidia kuacha pombe, ili kusaidia wenye changamoto ya uraibu wa pombe.

alcohol and cancer risk.jpg

Meneja wa MSD Kanda ya Dodoma, Mwanashehe Jumaa amesema dawa hizo zitatibu uraibu wa pombe na si sigara.

MY TAKE:

Viwanda vya pombe ndo vinaongoza kwa kulipa Kodi. Je, MSD imedhamiria kumhujumu Samia?

Bado naamini hizo dawa zita-expire zikiwa Store. Nani kawaambia tunataka dawa?

Bora mnngeshauri wanywe Baltika
 
Sijui dili la nani hili na kutoka nchi gani.. Yaani wameona hii ndio suluhu ya kuacha pombe?

Mbona hajasema lolote kwenye kuwekeza kwenye elimu juu ya pombe? Faida madhara hasara nk

Wariruhusu uzalishaji mwingi wa pombe Kali za bei poa, halafu wakaruhusu uzalishaji mkubwa wa energy drinks..! Hiivi viwili vimewaunguza mabandama vijana mpaka basi

Sasa mtu aliyekwisha kuathirika mwilini na kemikali za pombe kali mixer energy unamuongezea dozi ya kemikali ya madawa.

Sumu zote hizo zinaingia kwenye mwili usio na lishe bora na uliojaa stress.

Huu mpango ni uhujumu uchumi 100%
 
Sidhani kama kuna dawa ya kuacha pombe, hii itakuwa ni dawa ya kukusaidia kuacha pombe.
Labda inakufanya ujisikie vibaya ukitumia vitu vyenye pombe au inakupunguzia ile hamu.

Wajuzi watuambie.
 
Biashara juu ya biashara, pombe inatupa Kodi nyingi Sana.

Unameza dawa ya kuacha pombe Huku unapiga pombe kama kawaida ukijisemea nitaacha Tu dawa si nakunywa! ...Kesho asubuhi unanunua dawa ya pombe unakula, jioni Una Bapa kubwa unasema ngoja ninywe kidogo Tu yaani kifuniko Tu kinanitosha Kwanza Haya mambo kuacha ni mdogo mdogo, waapi, unalipiga Bapa lote, unajifanya unajutia kinafiki Tu, Kesho tena hivyo hivyo.
 
Back
Top Bottom