Hivi nani aliweza kuacha pombe kabisa?

Hivi nani aliweza kuacha pombe kabisa?

Mimi niliacha baada ya kuiba beer ya jamaa ambao nilikuwa nawavizia baa. Ni hivi, jamaa walikuwa wamechfua meza yao na beer za kila aina, mimi baada ya kuona vile nikaone gere. Jamaa walivyotoka kwenda kudansi nikachukua beer 3 na kuficha. Nikafungua moja na kunywa haraka haraka kumbe ilikuwa imetemewa makohozi na mimate pamoja na vipisi vya sigara humo....nikatapika na kuacha kabisa kunywa pombe toka mwaka 1995 na mpaka leo hiii nikisikia tu jina la pombe nawashwa mwili mzima.
Hahahahaha[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
haipiti siku duh......mimi sikumbuki kwa mwaka naweza kunywa mara 5 tu .....au 10 ...naweza kaa miezi mitatu hata sijagusa kabisa..yani sio issue hiyo ni maamuzi...hat mwaka naweza nisiguse......yani tangu 2009 mpaka 2018 sijapiga zaidi ya siku 30 na chini ya 20 kabisa
 
Hio ni kwenu walevi tu. Kwa sie wanywaji raha tu. Naweza kaa mwezi mzima sijanywa huwa nakunywa nikiwa na furaha tu.
 
Jina niliandika siku nying kabla sijaamua kuacha Bia, now nimepunguza kwa asilimia kubwa na nitaacha kabisa siku zijazo..
 
Mimi ni mmoja wa waioacha pombe . Kila nikipata pesa naweka heshima bar , ila kuna soku nilishukiwa na roho wa bwana akaniambia kila ninapokunywa niandike kumbukumbu . Nilipoona kiasi cha pesa kwa mwezi nimeacha kabisa hata harufu yake siipendi .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
haipiti siku duh......mimi sikumbuki kwa mwaka naweza kunywa mara 5 tu .....au 10 ...naweza kaa miezi mitatu hata sijagusa kabisa..yani sio issue hiyo ni maamuzi...hat mwaka naweza nisiguse......yani tangu 2009 mpaka 2018 sijapiga zaidi ya siku 30 na chini ya 20 kabisa
Wewe ni mlambaji tu mkuu.

Sio Mnywaji/mlevi.
 
Wazee wenzangu (mabibi na mabwana),
Natumaini mko wazima kabisa.

Mimi ni mwanaume, na nafikisha miaka 30 this year.

Unajua kwenye maisha kuna mambo mengi tunafanya kwa kukusudia yawe mazuri au mabaya, ila mara nyingi tunajutia yale mabaya.

Najuta sana kuwa addicted na Bia, na ninaona kabisa ni adui yangu ila haipiti siku bila kuuweka, this hurts me sana.

Kuna aliyeweza kuacha bia kabisa na aliwezaje?. Natamani niache, chaah! this too much.

NB: Ushauri wa kukaa mbali na vishawishi au mbali na washkaji nishajaribu na haujafaa, maana kiu ya bia hatari sana. Hata ukikaa mwenyewe utaitafuta.
Ukifanikiwa kuacha nakupa zawadi ya kret moja..mimi nipo kwenye mpango mkakati wa kufanya upembuzi yakinifu wa kuandaa mpango kazi wa namna gani ya kuishi bila kunywa
 
Zipo stage za ulevi ambapo unaweza kuacha mwenyewe bila msaada, Ila pia zipo stage hata kama una nia mwili unakuwa dhaifu unahitaji msaada.
Kutegemea unapoishi fika hospital ukutane na wataalum watakushauri.
Kama uko Dar fika Muhimbili, Kama Dodoma fika Milembe. Usiwaze kuhusu unyanyapaa.
Tafuta kuhusu kujua Alcoholic Anonymous ( AA) ambapo watu wenye na waliokuwa na matatizo ya pombe wanabadilishana uzoefu na kupeana support na mawazo. Unaweza kujifunza mengi na kuwasaidia wengine.
Hapa Tanzania unaweza kuwapata kupitia email address: aatanzania@gmail.com.
Watafute watakupa taarifa zaidi.
Kupitia simu yako; google - CAGE alcoholism screening, utapata ufahamu kuhusu stage uliyopo na wakati mwingine nini ufanye kuepukana nayo.
Unaweza pia kugoogle " alcohol medical related disorders" itakupa reinforcement ya nia yako ya kuacha ikiwa utajua kuwa yajayo katika pombe hayafurahishi.
Kimsingi pombe ni public heath problem na matatizo yatakanayo na pombe yanaongezeka, kuanzia kwenye ajali, kufukuzwa kazi, kutelekeza watoto/ familia mpaka matatizo ya kiafya.
Lakini kumbuka pia pombe ni genetic kuna wengine wamezaliwa mzazi yupo tungi hivyo kitoto adi kikiwa tumboni kimezaliwa kikiwa alcoholic



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom