Hivi Mgao umeanza tena kimyakimya?

Hivi Mgao umeanza tena kimyakimya?

Takribani wiki moja hapa mjini Arusha sijui maeneo mengine umeme unakatika mara kwa mara hasa nyakati za jioni.Ikumbukwe waziri wa nishati na madini aliahidi mgao wa umeme basi! Shirika limekaa kimya hakuna taarifa kwa umma shughuli nyingi za kiuchumi zinazotegemea umeme haziendi vizuri..... nawasilisha
 
WanaJF, kwa muda sasa tumeshudia umeme ukikatika bila sababu na kwa muda mrefu hadi masaa kumi bila kupewa taarifa yeyote na Tanesco. Naomba kujua,je, wameamua kuendesha mgao kimyakimya? Ikumbukwe kuwa viongozi wa wizara ya nishati wa sasa walishatamka hadharani kuwa mgao sasa utakuwa historia. Inawezekana ndoo sababu wanashindwa kutangaza?
Tuelezane
 
hii nchi ni kama imeuzwa, wangetupa pesa zetu kila mtu asepe kivyake! ukute washaniuzia hadi wanangu na mwenyewe sina taarifa, laanakhum!
 
nchi mgawo huwa hautangazwi mara zote huja kimyakimya
 
Prof Muhongo ni muongo kama waongo wenzake huwezi kuingia kwenye chaka la wezi,utendaji zero ukasimama bungeni bila aibu ukasema umeme kamwe hautakatika tena ,sasa ndio tunaipata joto ya jiwe ni wiki ya tatu tumeingia kwenye mgao,Kikwete yuko Kenya ana enjoy tuu wenziwe hatujawaona wakija Tanzania kuzurura yeye na laana zake kutwa kwenye Ikulu za watu sijui tumfanye nini huyu bwana hatuelewe kelele zote hizi kawa kiziwi
 
tumeshazoee kupigwa promo kila kukicha taa zangu za kichina pamoja na jenereta sijauza wala kutupa vipo maana ninajua nchi hii ilivyo
 
Leo wamedai eti "Kuna marekebisho makubwa ya miundombinu ili kukabiliana na madhara yanayoweza kuletwa na mvua za vuli!" kwahiyo umeme utakuwa unakatika katika kwa kipindi cha wiki mbili kuanzia sasa. Mi naona ni danganya toto tuu
 
Nimesikitika kuona mgao wa umeme ukiendelea licha ya waziri kusema mgao sasa utakuwa historia.kwa muda wa wiki mbili sasa mkoa kilimanjaro kumekuwa na ukatikaji wa umeme kwa siku nzima na kwa maeneo tofauti, mwanzo walisingizia wanaondoa nguzo zilizooza ila kadiri siku zinavyo kwenda naona tatizo likiongezeka na hao mafundi wanaobadili nguzo hatuwaoni na wala hakuna nguzo zilizo badilishwa.nilipojaribu kufuatilia TANESCO mtu mmoja akaniambia ni kweli upo mgao wa kimyakimya sasa najiuliza wapi kauli ya kihistoria ya waziri Muongo?
 
Ccm na akili mgando, kumdanganya mwenye macho na akili kuwa mchana ni usiku tena saa sita na jua linawaka inahitaji ujasiri wa kifisadi.

Wanadanganya hata katika vitu visivyowezekana. Nidhahili mgawo upo na unaendelea.

HIYO NDIYO MITAMBO YA KIKWETE KUPIKA UWONGO.
 
siyo kweli،hakuna mgao،tatizo ni uboreshaji wa njia،siyo lazima zi
rekebishwe eneo ulilipo,.
 
Hakuna mgawo bwana. Watanzania tufike mahali tuwaamini viongozi wetu. Siyo kila wakati kulalamika tu.
 
Tukiweka propaganda kando hata hapa Dsm kuna mgao unaendelea. Zaidi ya wiki tatu sasa.
 
subiri, wape mda. mgao hakuna, na haiwezekani ulalamike wewe wa K'njaro tu. Mgao ukiwepo waathirika wa kwanza huwa ni DSM
 
siyo kweli،hakuna mgao،tatizo ni uboreshaji wa njia،siyo lazima zi
rekebishwe eneo ulilipo,.

Yap mkuu hakuna mgao kabisa,mtoa sredi kabla haujapost fanya udadisi kwanza,tanesco wametoa matangazo mda mrefu sana kwamba wanafanya marekebisho ya miundombinu yake kwasababu na taarifa waliyopata kutoka TMA kwamba kutakua na mvua nyingi kuanzia september hadi december so wanajidhatiti kukabiliana na mvua hizo,marekebisho yataisha tar 26 mwezi huu,kama hadi tar 27 umeme ukiendelea kuzima basi hauna budi kupiga cm call center hili kupata info zaidi.
 
tatizo letu watanzania tumezoeshwa kukubali kila kitu na kuwa na nidhamu za woga. ki uhalisia kuna ka mgao fulani. ila wanasiasa hawataki kukubali kwa sababu zao za kisiasa, hata hivyo hatuna haja ya kulumbana kwani ukweli utakuja kujianika muda si mrefu. binafsi sina haja ya kuongea kauli za kinafiki kuwasifia ccm, hawa jamaa wameshashindwa muda mrefu, ninachotaka kwa sasa ccm waje kwa vitendo sio kuendeleza blaa blaa wakati ni kweli kuna dalili za mgao na watu hawapati umeme japo kwa masaa machache.
 
Yap mkuu hakuna mgao kabisa,mtoa sredi kabla haujapost fanya udadisi kwanza,tanesco wametoa matangazo mda mrefu sana kwamba wanafanya marekebisho ya miundombinu yake kwasababu na taarifa waliyopata kutoka TMA kwamba kutakua na mvua nyingi kuanzia september hadi december so wanajidhatiti kukabiliana na mvua hizo,marekebisho yataisha tar 26 mwezi huu,kama hadi tar 27 umeme ukiendelea kuzima basi hauna budi kupiga cm call center hili kupata info zaidi.

Ingependeza kama Pro. Muhongo angetoa kauli yake mwenyewe kuhusu hili; issue ndogo ndogo za 'box la misumari' hatuna shida nazo!
 
Ulitegemea nini mwenye kiwanda cha kutengeneza uongo Kikwete amefuzu kozi akawaachia akina Pinda Muhongo bila aibu bungeni walisema hakutakuwa na mgao lakini Dar es Salaam kuna mgao wa umeme ni masaa matano mpaka kumi na mbili kila siku ,nchi ya wagagagigogo
 
Back
Top Bottom