Hivi Mgao umeanza tena kimyakimya?

toka saa 3 ndio umeme unarudi sahizi, yaani saa 12 na robo, his is terrible, afazali wangesema tu...kuwa kuna mgawo.
 
Hata huku mbeya, mfano maeneo ya sayi hadi uyole jana had leo kuanzia jion saa 12 hakuna umeme.
 
Zitto aliwaambia Mmeliwazwa kwa Maneno matamu mkapitisha Bajet kwa mbwembwe kumbe watu walikuwa wanagombea tender ya Kukausha mabwawa ili wauze mafuta!
 
Nafikiri mgao upo,tena ni mkali sana kupita maelezo. Tanesco wamekuwa WasengeNyaji sana kupita maelezo. Wanatusengenyaaa tu utafikiri umeme wenyewe wanatugawia bure.

Hapo kwenye red unamaanisha *******?
Yes i too thing so. They really are
 
Nani alisema inji hii haitakuwa na mgawo wa umeme? Sijui labda kwa kuwa wawekezaji mabepari wataendelea kuja kuwekeza(kuchukua na kuiba) malighafi ikiwemo madini,labda watafikiria(wawekezaji) kuboresha uzalishaji wa umeme ili kufanikisha malengo yao.

Tanesco imeamriwa na mahakama kuilipa Dowans shilingi bilioni 96 ambalo ni deni lililotokana na kufuliwa au kutofuliwa umeme,kulikotokana na mkataba wenye utatanishi mkubwa! Maendeleo bila umeme yatawezekana? Profesa Mhongo alisema hakutakuwa na mgawo wa umeme tena kwa kupinga hoja ya Zitto Kabwe ya kuwa mgawo wa umeme ni ndoto kumalizika! Je,ni nani msema kweli?
 
Hapa Tanzania, mgao wa umeme haukwepeki. Waliotangaza kuwa hakuna mgao wa umeme, nadhani hawaijui Tanzania. Na sasa nadhani wanajikia aibu kuutangaza mgao wenyewe! Ukiwapo hesabu kuwa ni mgao wenu wa umeme na usipokuwapo ni mgao wenu wa giza.
 
Hali hii inashangaza, sisi tulio maeneo ya kinondoni tunapata tabu ya umeme kila siku asubuhi kwa masaa kama 4 hivi. toka jana, ikifika saa 3 kasoro robo wanakata na kurudisha kama saa 6 hivi. hiyo imetokea jana na leo tena imetokea,
Je kuna mgao wa kimyakimya? mbona hawatangazi?

Ni kweli kuna tatizo la umeme lakini sio mgao rasmi. Mafuta ya kuendeshea mitambo ya IPTL yaliisha na wahusika hawakuwa wameandaa kuleta stoock nyingine kwa wakati hivyo kusababisha upungufu kwenye gridi. Mtu wa ndani ya Tanesco anasema wanafuatiliia delivery ya mafuta na hali itarudi kawaida kabla ya mwishop wa wiki hii.

Labda tumwombe Engineer Nsiande atupe ufafanuzi zaidi.
 
Last edited by a moderator:
Ni kweli kuna tatizo la umeme lakini sio mgao rasmi. Mafuta ya kuendeshea mitambo ya IPTL yaliisha na wahusika hawakuwa wameandaa kuleta stoock nyingine kwa wakati hivyo kusababisha upungufu kwenye gridi. Mtu wa ndani ya Tanesco anasema wanafuatiliia delivery ya mafuta na hali itarudi kawaida kabla ya mwishop wa wiki hii.

Labda tumwombe Engineer Nsiande atupe ufafanuzi zaidi.
kwani mpaka hayo mafuta yaishe wao hawajui consumption ya hizo machine ili wafanye kuagiza mengine kabla ya stock iliypo kuisha? au ndio yale mambo ya wafanyakazi wa serikali kukalia kucheza karata na kuchck faceboob bila kuangalia majukumu yao? this is terrible!
 
Huko nitokako nao wamenipa taarifa umeme umekatika!! Mambo ya udhaifu maana bora liende. Hakuna notice hakuna lolote.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom