Hivi Mgao umeanza tena kimyakimya?

Hivi Mgao umeanza tena kimyakimya?

Kwa siku nne sasa hapa Arusha kuna maeneo ambapo Umeme unakatwa saa tatu asubuhi mpaka saa moja usiku. Isitoshe usiku wa kuamkia leo umeme ulirudi saa moja usiku na kukatwa kati ya saa tano na saa sita. Umerudishwa asubuhi. Je huu si mgawo? Au kuna hujuma?
 
Tusubiri tuone hiyo tarehe 24 itakuwa mwisho wa marekebisho au la.
 
Nimejaribu kuangalia mwenendo wa kukatika umeme naona unakatika mara kwa mara tena bila taarifa yeyote na unaporudi mara nyingine unakuwa mwingi na kuunguza vifaa vya watu. Tunaomba angalau wawe wanatutaarifu tuwe tunajipanga na vijenereta vya kichina
 
Siyo mgao; Prof yuko serious na uzalendo wa nchi hii; ni maintenance ya kukarabati infrastruct.
 
Baada tu ya kushika wadhifa wa uwaziri wa Nishati na madini, Prof Sospeter Muhongo alitamka kwa Watanzania, tena kwa mbwembwe na kujiamini kabisa kwamba mgawo wa umeme sasa utakuwa historia, kwani ulikuwa unapikwa tu kutokana na ufisadi nk nk.

Leo hii asubuhi ktk kipindi cha Nipashe cha Radio One Stereo, akielezea kukatika katika kwa umeme mara kwa mara hivi sasa amenukuliwa kwamba hali hiyo ni kutokana na miundombinu ya Tanesco ya usamazaji umeme iliyochoka kabisa na Tanesco inalishughulikia suala hilo.

Nauliza: Hivi wakati ule alipowaahidi Watz kuwa mgao wa umeme utakuwa historia, hakuwa na habari kwamba miundo mbinu ya Tanesco imechakaa?

Mimi naona mambo yanarudi kuwa ni yale yale tu -- hawa mawaziri wanatoka katika mfumo ule ule wa chama kilichochoka na cha kifisadi.
 
Tumbo ovu huzaa matunda maovu. I tell you CCM will always produce rulers and not leaders. Ulevi wa madaraka na kutaka sifa ili JK amuone, jitu zima tena linajiita Prof.!
 
na wewe huna akili kabisa, sasa hapo kasema kuna mgao? fikiria kabla ya kuja na hoja mbovu mbovu hapa

Baada tu ya kushika wadhifa wa uwaziri wa Nishati na madini, Prof Sospeter Muhongo alitamka kwa Watanzania, tena kwa mbwembwe na kujiamini kabisa kwamba mgawo wa umeme sasa utakuwa historia, kwani ulikuwa unapikwa tu kutokana na ufisadi nk nk.

Leo hii asubuhi ktk kipindi cha Nipashe cha Radio One Stereo, akielezea kukatika katika kwa umeme mara kwa mara hivi sasa amenukuliwa kwamba hali hiyo ni kutokana na miundombinu ya Tanesco ya usamazaji umeme iliyochoka kabisa na Tanesco inalishughulikia suala hilo.

Nauliza: Hivi wakati ule alipowaahidi Watz kuwa mgao wa umeme utakuwa historia, hakuwa na habari kwamba miundo mbinu ya Tanesco imechakaa?

Mimi naona mambo yanarudi kuwa ni yale yale tu -- hawa mawaziri wanatoka katika mfumo ule ule wa chama kilichochoka na cha kifisadi.
 
Kweli Kabisa profesa Muhongo alisema bungeni kuwa mgawo utakuwa historia.
No research no Right to speak! Kwenye jina lake tukiondoa h kwenye muhongo,,atabaki kuwa muongo.:frusty:
 
Ila katakata ya umeme imezidi kama ni mgao waweke wazi.
 
Ndani ya serikali ya CCM na mautumbo yoote yale unategemea atafanya maajabu? Hata umlete malaika, kwa akili za magamba hamkuna kitu pale!
 
Baada tu ya kushika wadhifa wa uwaziri wa Nishati na madini, Prof Sospeter Muhongo alitamka kwa Watanzania, tena kwa mbwembwe na kujiamini kabisa kwamba mgawo wa umeme sasa utakuwa historia, kwani ulikuwa unapikwa tu kutokana na ufisadi nk nk.

Leo hii asubuhi ktk kipindi cha Nipashe cha Radio One Stereo, akielezea kukatika katika kwa umeme mara kwa mara hivi sasa amenukuliwa kwamba hali hiyo ni kutokana na miundombinu ya Tanesco ya usamazaji umeme iliyochoka kabisa na Tanesco inalishughulikia suala hilo.

Nauliza: Hivi wakati ule alipowaahidi Watz kuwa mgao wa umeme utakuwa historia, hakuwa na habari kwamba miundo mbinu ya Tanesco imechakaa?

Mimi naona mambo yanarudi kuwa ni yale yale tu -- hawa mawaziri wanatoka katika mfumo ule ule wa chama kilichochoka na cha kifisadi.
Kaka uwe unaangalia basi na vyombo vya habari ili usiwe mdaku, unajua ni aibu sana kuongelea kitu ambacho kila siku watu wanakisemea na kufafanua, naomba nikuope taarifa juu ya kukatikax2 umeme, ni kwa sababu hali ya hewa wametangaza kwamba kunaweza kuwa na mvua kubwa ambazo zinaweza zikaleta madhara, kwa hiyo Tanesco wanajiandaa kuweka nguzo ambao zimechoka na kuweka nguzo mpya zitakazohimili hali hiyo ya hewa, Pili, kuna miradi mingi ya ujenzi wa bara bara inaendelea karibu nchi nzima, kwa hiyo wanahamisha nguzo ili kupisha ujenzi wa barax2. na haya yanasemwa karibu kila siku kwenye matv na maredio, sasa ndg yangu hivi uko tz kweli au ni kwamba huna utamaduni wa kusikiliza vyombo vya habari vinavyoaminika>. pole kaka.
 
Kuna tofauti kati ya mgao wa umeme na katizo la umeme....la kwanza tumezoea kwaajili ya maji na vyanzo vya umeme kushindwa lakini hili la pili yaani Katizo ni kawaida miundombimu inachoka na inafanyiwa marekebisho inapowezekana hata nchi walizoendelea hukarabati miundombinu iliyochoka hawatupi yote maramoja; tuwape muda kama itakuwa mgao haujifichi tutajua
 
Hahaaahaaahaaa. Profesa Muhongo alisahau kuwa "Usitukane wakunga, uzazi ungalipo." Yeye akiwa bado si mwanasiasa mkongwe alitakiwa kusoma alama za nyakati kwanza na siyo kukurupuka na kusema hakutakuwa na mgao wa umeme tena!

Kaingizwa kwenye kapu la samaki waliooza kisha naye kuooza. Wizara ya Nishati na Madini anayoiongoza ni mahali ambapo shetani hupumzika. Ni sehemu yenye vishawishi vingi na ambapo macho,akili na masilahi ya wasio na uzalendo na nchi hii yameelekezwa.

Baada ya kupewa semina elekezi juu ya namna ya kusema na kuwadanganya Watanzania kama kawaida yao,Mheshimiwa waziri Profesa Muhongo anaogopa na kuona aibu kusema alikosea aliposema hakutakuwa na mgao wa umeme tena, na sasa kuna marekebisho katika miundombinu chakavu ya umeme Tanesco.

Waswahili tunasema,"Kwenye msafara wa Mamba na Kenge wamo." Mtoto wa mkulima yuko wapi? Alikuja moto moto hata kulilia watu wake! Sasa hivi kageuka na kuwa,"Liwalo na liwe!." Sisi watoto wa masikini tumezoa vibatari na vijinga vya moto.
 
Wizara inahitaji kuwa na waziri ambae ni strategic thinker na sio waziri wa kutoa matamko ambayo anajitokeza tena yeye mwenyewe kuyakanusha . Naamini kabisa RAISI wetu msikivu Jk atamtimua tu kwa maana matamko yake yanaharibia chama chetu
 
Baada tu ya kushika wadhifa wa uwaziri wa Nishati na madini, Prof Sospeter Muhongo alitamka kwa Watanzania, tena kwa mbwembwe na kujiamini kabisa kwamba mgawo wa umeme sasa utakuwa historia, kwani ulikuwa unapikwa tu kutokana na ufisadi nk nk.

Leo hii asubuhi ktk kipindi cha Nipashe cha Radio One Stereo, akielezea kukatika katika kwa umeme mara kwa mara hivi sasa amenukuliwa kwamba hali hiyo ni kutokana na miundombinu ya Tanesco ya usamazaji umeme iliyochoka kabisa na Tanesco inalishughulikia suala hilo.

Nauliza: Hivi wakati ule alipowaahidi Watz kuwa mgao wa umeme utakuwa historia, hakuwa na habari kwamba miundo mbinu ya Tanesco imechakaa?

Mimi naona mambo yanarudi kuwa ni yale yale tu -- hawa mawaziri wanatoka katika mfumo ule ule wa chama kilichochoka na cha kifisadi.

Ni vizuri ukatofautisha kati ya mgawo wa umeme na katizo linalotokana na hitilafu za kiufundi. Mgawo uliokuwepo ulitokana na uzalishaji mdogo na kuwa na vyanzo visivyoweza kuzalisha nishati ya kutosha. Kinachotokea sasa ni katizo la hapa na pale ambalo chanzo chake ni hitilafu za kimitambo na hiyo ni kutokana na kuchoka kwa miundombinu. Unahitaji kuzeekea darasani kulijua hili au kupambanua tofauti za mambo haya?
 
Wizara inahitaji kuwa na waziri ambae ni strategic thinker na sio waziri wa kutoa matamko ambayo anajitokeza tena yeye mwenyewe kuyakanusha . Naamini kabisa RAISI wetu msikivu Jk atamtimua tu kwa maana matamko yake yanaharibia chama chetu

Umesikika wakala wa mafisadi lakini hilo halitatokea kamwe!
 
Kauli ya Prof. Muhongo kuwa hakutakuwa na mgao wa umeme ilikuwa ni kauli ya kukukurupuka bila tathmini ya kutosha na matokeo yake ndiyo mgao tunaanza kuuona hivi sasa. Inawezekanaje mgao usiwepo wakati maji katika mabwawa makubwa ya kuhifadhia maji yamekwisha, bei za umeme ambazo TANESCO wanatoza hazikidhi kugharama za kuzalisha, kusafirisha na kusambaza umeme, uwezo wa Serikali kugharamia mafuta kwa ajili ya mitambo ya dharura ni mdogo, na TANESCO inakabiliwa na mzigo wa madeni kutoka kwa watoa huduma. Nadhani Prof. anadhani yupo darasani.
 
Back
Top Bottom