Baada tu ya kushika wadhifa wa uwaziri wa Nishati na madini, Prof Sospeter Muhongo alitamka kwa Watanzania, tena kwa mbwembwe na kujiamini kabisa kwamba mgawo wa umeme sasa utakuwa historia, kwani ulikuwa unapikwa tu kutokana na ufisadi nk nk.
Leo hii asubuhi ktk kipindi cha Nipashe cha Radio One Stereo, akielezea kukatika katika kwa umeme mara kwa mara hivi sasa amenukuliwa kwamba hali hiyo ni kutokana na miundombinu ya Tanesco ya usamazaji umeme iliyochoka kabisa na Tanesco inalishughulikia suala hilo.
Nauliza: Hivi wakati ule alipowaahidi Watz kuwa mgao wa umeme utakuwa historia, hakuwa na habari kwamba miundo mbinu ya Tanesco imechakaa?
Mimi naona mambo yanarudi kuwa ni yale yale tu -- hawa mawaziri wanatoka katika mfumo ule ule wa chama kilichochoka na cha kifisadi.
hapo kwa blue si kila umeme ukikatika ni mgao! na miundombinu kuchakaa si kitu cha ajabu! na ili kurekebisha inabidi kuzima, acha watu wafanye kazi mwaka 2015 sii mbali utaweka hao unaowataka umeme uszimike milele! na nchi itakuwa kama ahera!