Hivi lini hii dunia wajinga wataisha? Hivi msomi nae anaweza kuwa na vivyo hivyo ukawa mjinga! Dada Betty ujinga umekufanya upoteze maisha

Chawa wa lumumbashi

JF-Expert Member
Nov 19, 2022
793
1,749
MAREHEMU BETTY AJENTA CHARLES:

Hadithi ya Betty Ajenta Charles (pichani), inasikitisha. Mwili wake umefukuliwa baada ya kufunga mpaka kufa katika sakata linaloendelea nchini Kenya la Mchungaji Paul Mackenzie ambaye anawafungisha Wakenya hadi umauti ("Fasting to Death") ili wafike Mbinguni kirahisi.

Mwili wake ni kati ya miili 73 iliyofukuliwa katika zoezi la kiuchunguzi linaloendelea kwenye jimbo la Kilifi - Kanisa la Shakahola. Marafiki na ndugu za Betty wamepata mshtuko mkubwa sana.

Betty alikuwa mfanyakazi wa Shirika moja kuubwa la ndege duniani, ambaye aliamua kuacha kazi yake, akauza ardhi yake kwa Kshs 7,000,000 = Tzs 121,170,000 na kumkabidhi "Mchungaji Wakala wa Shetani" Paul Mackenzie wa Malindi - Kenya.

Betty alirejea Kenya kutoka ughaibuni baada ya mtoto wake aitwaye Jason kulazimishwa kufunga hali iliyopelekea mtoto huyo aage dunia. Wakati mtoto huyo wa Betty anafunga kula hadi kufariki, Betty alikuwa nchini Qatar. Mtoto wa Betty, Jason, alikuwa akiishi na babu na bibi yake wakati huo. Haijulikani ni nani alimfungisha mtoto huyo hadi kufa.

Baada ya kupokea taarifa za kifo cha mwanaye, inaelezwa Betty alifunga safari kutoka Qatar hadi Kenya kwa ajili ya mazishi ya mwanaye lakini akapotea na hakujulikana alipo tena.

Dada ya Betty anayeishi eneo la Umoja - Nairobi, anasema Betty aliacha barua ya hisia kali kwa Mume wake akionesha asingelirejea tena milele. Baada ya kuandika barua hiyo Betty aliondoka na wanaye kuelekea Malindi.

Inaonekana alifuta akaunti zake zote za mitandao ya kijamii, akauza vitu vyake vyote kabla ya kupanda Ndege kuelekea Malindi - Kenya.

Rafiki ya Betty anasema, Betty alimuaga akimjulisha kuwa anaenda kuonana ana kwa ana na Yesu siku ya tarehe 08 Aprili 2023 na kwamba alilazimika kuondoka tarehe 07 Aprili 2023. Rafiki ya Betty alipoifuatilia tiketi yake ya ndege akagundua ni tiketi ya moja kwa moja na siyo ya nenda rudi.

Katika msako unaoendelea katika eneo la ekari 800 linalomilikiwa na "Mchungaji Feki" Paul Mackenzie, polisi wamemkamata Mchungaji mwenza anayejulikana kama "Zablon wa Yesu". akiwa anasoma Biblia akieleza yeye angelianza kufunga Juni 2023!
 
Ujinga hautegemei na elimu ya mtu
20230425_212350.jpg
 
Mm nikiona mtu yyte anashadadia dini na wengine hadi hasira juu ujue hao ni wagonjwa wa akili.

Kila kitu kina kiasi na watu wenye mihemko kupitiliza ni sawa na mwanamke mrahisi kila mwanaume yeye twende tu au mwanaumwe ambaye yy kila mwanamke anatongoza tu.
 
Wanangu wanaangamia kwa kukosa maarifa, hata maana ya kufunga hawajui hao, na wanaenda motoni
 
Back
Top Bottom