Vanessa Mdee a.k.a V-Money: ijue historia yake, maisha yake, familia ya kishua aliyozaliwa

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,032
vanessamdee.jpg
UTANGULIZI

Wengi na vijana hasa wa kike kwa ujumla wanamtazama vanessa mdee kama role model wa maisha yao kutokana na umaarufu wake mkubwa alioupata kupitia muziki na maisha yake kwa ujumla kwa kuwa mfano wa kuigwa katika jamii hasa katika upande wa tabia iliyojengwa kwa kiasi kikubwa kwa kukuzwa katika familia inayojali malezi kwa misingi ya kidini.

Lakini watu wengi hawajui mitihani mikubwa ambayo binti huyu ameipitia mpaka kufika hapo alipo. Ukiitazama historia ya maisha yake, utaelewa kwa nini mwaka juzi binti huyu aliamua kuachana kabisa na masuala ya muziki na badala yake kuamua atulie nyumbani na mchumba wake na kulea familia.

Historia ya Vanessa na wanafamilia

Vanessa mdee amezaliwa tarehe 7 june mwaka 1988 akiwa ni mtoto wa sita katika familia ya watoto nane kwenye familia ya marehemu mzee sammy mdee. Kipindi mama yake vanessa anaolewa na marehemu mzee sammy mdee, tayari alikuwa amezaa na mwanaume mwingine mtoto mmoja anayeitwa adam. Lakini pia marehemu mzee sammy mdee naye alikuwa tayari ana watoto wawili wa kike anna na carol ambao alikuwa amezaa na mwanamke mwingine.

Kwa hiyo ukiacha watoto hawa ambao wazazi wao walikuwa tayari wamezaa na nje ya ndoa yao, ndani ya ndoa ya mzee mdee na mkewe bi. Sophia walifanikiwa kupata watoto wanne ambao ni Godfrey, Nancy Namtero, Vanessa hau na Marianne Namshali (msanii mimi mars). Pia marehemu mzee sammy mdee na mkewe wali-adopt mtoto mmoja wa kike anayeitwa samantha.

Baba Yake Vanessa kuwa balozi na Maisha ya nje ya nchi.

Kipindi cha mwalimu nyerere, marehemu mzee sammy mdee aliteuliwa kuwa mhariri mkuu wa magazeti ya daily news na sunday news. Baadae akapelekwa redio tanzania ambako nako alifanyakazi hiyo hiyo ya muhariri mkuu. Baada ya kufanya kazi nzuri huko daily news na redio tanzania, nyerere mwenyewe akamchukua na kumuajiri ikulu akiwa kama katibu wake wa masuala ya habari na mawasiliano.

Kipindi baba vanessa anafanyakazi kama katibu wa nyerere ndipo alikutana na bi. Sophia enzi za usichana wake, bi. Sophia alikuwa ni mwanamitindo na mzee mdee ndiye alimsaidia kumpeleka chuo kusomea masuala ya uhasibu.

Baada ya nyerere kuondoka madarakani, mzee mdee alifanyakazi kama mwenyekiti wa bodi wa mawasiliano. Mwaka 1989, ikiwa ni miezi michache tu baada ya vanessa kuzaliwa, baba yake aliteuliwa na rais mwinyi kwenda kuwa balozi mdogo katika ubalozi wa tanzania nchini marekani .

Kwa hivyo marehemu mzee sammy mdee, mkewe sophia na watoto wao wote wakahamia nchini marekani jiji la new york ambako waliishi kwa takribani miaka mitano, kuishi huku marekani mwanzoni kumemsaidia vanessa mpaka sasa anacharaza kingereza kizuri sana maana ndio ilikuwa lugha yake ya kwanza kuijua.

Baadae baba yake akateuliwa tena na rais mwinyi aende kukaimu nafasi ya ubalozi nchini ufaransa ambako huko ufaransa rais mwinyi alikuwa amemuhamisha balozi aliyekuwepo hapo (balozi christopher liundi) kwenda nchini ethiopia.

Kwa hivyo familia ya kina vanessa ikahama tena kutoka marekani kwenda jiji paris nchini ufaransa ambako baba yake alifanyakazi kama balozi mpya wa tanzania.

Familia yao iliishi hapo ufaransa karibia miaka minne, na hii pia ndio sababu kwa nini vanessa mdee mpaka sasa anaweza kuzungumza kifaransa kwa ufasaha kabisa, kwa kuwa utotoni ameishi kwa muda mrefu jijini paris na pia amehudhuria mpaka shule za ufaransa.

Familia kurudi Tanzania.

Mwishoni mwa miaka ya tisini, serikali ilimrejesha baba yake nyumbani tanzania kuja kuwa mkurugenzi wa kituo cha kimataifa cha mikutano, aicc jiji arusha. Na hapo ndipo familia iliporejea nchini tanzania. Lakini japokuwa mzee mdee alirejeshwa kwenye jukumu hilo jipya ndani ya nchi, watoto wake waliendelea kusoma nje na hasa hasa nchini kenya.

Baada ya miaka kadhaa vanessa mdee alirejea nchini tanzania na kuhudhuria masomo yake ya sekondari katika shule ya arusha modern high school iliyoko jijini arusha. Na baada ya kumaliza elimu ya sekondari, baba yake akampeleka tena nchini kenya kusomea sheria kwenye moja ya vyuo bora na vya gharama kubwa nchini humo, catholic university of eastern africa.

Mpaka hapa maisha ya vanessa yalikuwa ya raha sana na yenye furaha kubwa. Alikuwa amezunguka nchi kibao, amehudhuria masomo katika shule bora kabisa africa, ulaya na marekani . Kila kitu kilikuwa kinakwenda kwenye mstari mnyoofu na kwa uzuri kabisa.

Lakini kipindi hiki akiwa chuo kikuu ndipo ambapo pigo zito likatua kwenye familia yao.

Kifo cha baba yake Vanessa Mdee

Kuna siku baba yake vanessa na mama yake waliamua wasafiri waende jijini nairobi kumtembelea vanessa chuoni. Lakini safari yao hii hawakupanda ndege badala yake walienda kwa gari yao wenyewe kutoka arusha mpaka nairobi.

Walifika nairobi salama kabisa, wakaonana na vanessa kisha wakakaa hapo nairobi kwa siku nyingine kadhaa kutembelea ndugu na marafiki ambao walikuwa wanaishi hapo. Hii ilikuwa ni mwaka 2007 mwezi march. Siku ya tarehe 9 mwezi huo huo march, baba yake na mama yake walianza safari ya kurejea tanzania kwa staili ile ile ya kurudi kwa gari yao wenyewe.

Wakavuka mpaka na kuwasili salama arusha mida ya jioni. Kutokana na uchovu wa safari, mama vanessa akashindwa kupika chakula cha jioni na hivyo wakaamua waende na mumewe kwenye moja ya hoteli hapo jijini arusha kwa ajili ya kupata chakula cha jioni.

Mama vanessa mpaka leo hii anakumbuka kwamba, walipofika hotelini kati ya vyakula ambavyo waliagiza kulikuwa na kuku pamoja na samaki. Baada ya kumaliza kula chakula, baba vanessa akagundua kwamba kulikuwa na mwiba wa samaki umekwama kooni. Sio kwamba ulikuwa mwiba mkubwa kumfanya pengine ashindwe kupumua au kuongea.. La hasha, ilikuwa ni kamwiba kadogo tu ka kawaida.

Kwa kawaida twajua kwamba mwiba mdogo wa samaki ukikaa kooni huwa unateremka wenyewe baada ya masaa machache na bila hata wewe mwenyewe kujua unashitukia tu haupo tena. Kwa hivyo baba vanessa hakuhofu sana. Lakini mpaka usiku walipokwenda kulala bado baba vanessa alikuwa analalamika mfupa bado ulikuwa haujateremka na uko umekwama kooni.

Kwa hivyo kulipokucha asubuhi wakaamua kwamba aende hospitali mfupa ukatolewe na daktari ili usije kumletea madhara kwa kukaa kooni muda mrefu. Moja ya marafiki zake akamwambia baba vanessa kwamba, wiki hiyo hospitali ya kcmc kulikuwa na daktari specialist wa ent (masikio, pua na koo) yuko hapo kwa wiki nzima akitoa huduma. Kwa hiyo baba vanessa akaendesha gari yeye mwenyewe kutoka arusha mpaka moshi hospitali ya kcmc kwa ajili ya kuonana na huyo daktari wa makoo.

Baba vanessa akawasili kcmc na kuonana na daktari. Baada ya daktari kumkagua, akamweleza kwamba itabidi aingize kifaa mdomoni kwa ajili ya kupanua njia ya koo ili aweze kutoa hako kamfupa. Na kwa kuwa hilo zoezi la kutumia hicho kifaa kuutanua mdomo linaweza kumletea maumivu kidogo kwenye taya, ni vyema achomwe sindano ya ganzi.

Jambo ambalo daktari alikuwa hafahamu ni kwamba mzee mdee alikuwa na matatizo ya presha. Na kwa bahati mbaya, nesi ambaye alikuja kumchoma mzee mdee sindano ya ganzi, hakumpima presha kama ambavyo inatakiwa kufanyika. Akamchoma ganzi moja kwa moja kitendo ambacho kilisababisha presha ya marehemu mzee mdee kuvurugika na kusababisha kupata mshtuko wa moya ambao ulisababisha mzee mdee afariki ndani ya dakika chache tu.

Kifo cha baba vanessa kilikuwa cha ghafla mno.. Sababu hakuwa anaumwa au labda mgonjwa mahututi.. Alifika hospitali akiendesha gari yeye mwenyewe kwa tatizo dogo tu la usumbufu wa kimfupa ambacho kilikuwa kimenasa kooni. Lakini badala yake sindano ya ganzi ikasababisha mshtuko wa moyo na kupelekea umauti wake.

Mzee mdee alikuwa ni kila kitu kwenye familia yake, kwa hiyo kifo chake kilikuwa ni pigo baya kwa familia kiasi kwamba kilifanya familia ipitie kwenye kipindi kigumu mno na cha simanzi ambayo ilidumu kwa miaka mingi na pengine mpaka sasa hivi bado wako na maumivu ya msiba huu.

Japokuwa familia nzima iliumizwa na huu msiba, lakini hakukuwa na watu ambao waliumia vibaya na msiba huu na kuwachanganya kama mama vanessa, vanessa mwenyewe na dada yake Nancy Namtero.

Kitendo cha kumpoteza mumewe, kilimfanya mama vanessa azame mno kwenye dini kutafuta faraja kiasi kwamba mpaka sasa hivi amekuwa ni muhubiri mwenye cheo cha apostle na amebadili hata jina lake siku hizi anaitwa apostle dorcas na sio tena sophia mdee.

Mdogo wake Vanessa - Narianne a.k.a MIMI MARS

Mdogo wake Vanessa anaitwa Narianne Namshali, wengi tunamjua kwa jina la Mimi Mars nae aliamua kufata nyayo za dada zake kwa kuingia kwenye muziki na kujizlea umaarufu kwenye sanaahii kwa vibao kama La La, Una , mua, n.k. Mimi Mars na msanii mwenzake maarufu Marioo wamewahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi.

Dada yake Vanessa - Namtero a.k.a Tero

Dada yake vanessa, huyo anaitwa Nancy Namtero mdee. Huyu yeye alikuwa anaishi nchini kenya. Na kwa miaka mingi pale kenya alikuwa ni moja ya watangazaji wa kike bora kabisa nchini humo. Wakenya wengi wanamfahamu kwa jina la tero katika kazi zake. Alikuwa ni mtangazaji wa kipindi cha muziki kinaitwa str8up ambacho kilikuwa kinarushwa na kituo cha televisheni cha ktn. Na pia alikuwa mtangazaji wa kipindi cha muziki kwenye stesheni ya homeboyz radio. Na sio tu kwamba nancy alikuwa moja ya watangazaji bora nchini kenya, bali binti huyu pia alikuwa ni moja ya pisi kali ambazo zilikuwa zinatingisha jiji la nairobi.

Lakini baada ya kifo cha baba yake nancy alipatwa na msongo wa mawazo ambao ulidumu kwa muda mrefu sana kiasi kwamba baadae nancy alikuja kufanya jambo la ajabu sana. Mwaka 2011 nancy aliondoka ghafla kenya na kutokomea kusikojulikana. Hakuandika barua ya kuancha kazi wala hakumuaga mtu yeyote yule hata bosi wake au wafanyakazi wenzake. Akapotea tu ghafla. Akakimbia kenya na kurudi tanzania. Hii ilikuwa ni habari kubwa sana nchini kenya miaka hiyo kiasi kwamba watu walishuku labda ametekwa au jambo baya zaidi limempata.

Lakini nancy mwenyewe anasema kwamba, tangu msiba wa baba yake na kipindi kirefu kilichofuata licha ya kwamba alikuwa anaonekana ni binti mwenye furaha akiwa anatangaza kwenye televisheni, lakini kiuhalisia alikuwa kwenye msongo mkubwa sana wa mawazo. Nancy anasema alikuwa kwenye depression (lindi la msongo wa mawazo) ya hatari kiasi kwamba ilifika kipindi alikuwa anataka kujiua. Na kwenye kujinusuru ndipo ikabidi aondoke kenya na kukimbilia tanzania kwa mama yake ili apate msaada wa kisaikolojia.

Mama yake akamsaidia kumpeleka kwenye maombi ambayo mwenyewe anadai yalimsadia kuwa sawa sawa tena, nancy kwa sasa hivi ameolewa na jamaa muhubiri yuko pale arusha anaitwa mchungaji hebroni.

Baada ya msiba Vanessa aacha chuo, aingia kwenye utangazaji.

Kama ambavyo msiba wa baba uliwaumiza vibaya dada yake na mama yake, ndivyo hivyo pia ambavyo vanessa naye kumpoteza baba yake kulimpotezea kabisa mwelekeo wa maisha. Baada ya baba yake kufariki vanessa aliacha chuo. Katika kutafuta faraja, mwezi mmoja tu baada ya kumzika baba yake vanessa akashauriwa na rafiki yake anaitwa sarah, kuingia kwenye shindano la channel maarufu ya mtv base linaloitwa mtv vj search, shindano lilikuja kufanyika hapa tanzania, na kama bahati vanessa alishinda na kupata nafasi ya kuwa mtangazaji katika kituo cha mtv base nchini afrika kusini.

Lakini licha ya fursa hii ya mtv kuwa ni kubwa lakini nyuma ya pazia ilikuwa na changamoto nyingi sana. Vanessa alikuwa anaishi tanzania lakini kituo cha mtv base kipo nchini afrika kusini. Mara nyingi ilikuwa ukifika muda wa kurekodi vipindi alikuwa hapewi hata tiketi ya ndege na ilimlazimu kuomba pesa kwa mama yake ili aweze kukata tiketi ye ndege kwenda afrika kusini. Mara nyingi mno vipindi ambavyo alikuwa anaviandaa alikuwa anapewa bajeti ndogo kiasi kwamba ili kufanikisha inabidi aingie mfukoni mwake mwenyewe kuongezea hela ili vipindi viweze kufanyika. Licha ya hizi changamoto, vanessa aliendelea kukomaa na mtv base akiamini kwamba uwepo wake pale utamfungulia fursa nyingine.

Changamoto hizi za mtv ndizo ambazo kwa kiwango kikubwa zilimsukuma kutafuta kazi ya ziada ili aweze kujikimu na ndipo akaanza kutangaza radio ya hapa kwetu tanzania inayoitwa choice fm kwenye kipindi cha the hitlist.

Vanessa aingia rasmi kwenye Muziki

Baada ya kulisoma vyema soko la muziki hatimaye vanessa mdee akaamua kuingia kwenye industry kama muimbaji. Na alipoamua kuwa msanii wa bongofleva ndipo akapata kujulikana zaidi ndani na nje ya nchi. Twafahamu ni kwa namna gani ambavyo katika kipindi chote ambacho vanessa alikuwa anaimba, akaibuka kuwa moja kati ya wasanii bora wa kike si tanzania pekee bali bara zima la afrika akiwa moja ya wasanii wakubwa wawakilishi wa ukanda wa nchi za afria mashariki.

Depression (Msongo wa Mawazo) na Ulevi

Lakini licha ya mafanikio yote ambayo vanessa aliyapata kupitia muziki, kulikuwa na upande ambao hatukuwa tukiufahamu kuhusu yeye. Katika muda wote huu ambao alikuwa anaimba.. Vanessa hakuwa na furaha. Ukitafakari kwa makini utapata jawabu kwamba vanessa hakuwahi kutoka kwenye msongo wa mawazo tangu alipompoteza baba yake. Alikuwa anafanya vitu vingi sana ili apate furaha lakini bado havikuweza kuziba shimo ambalo liliachwa na pigo la kumpoteza baba.

Na mbaya zaidi, ugumu wa soko la muziki uliongeza presha kwenye maisha yake ambayo ikafanya awe na msongo zaidi maradufu. Vanessa mwenyewe alikiri kwamba, soko la muziki tanzania lina vitu vingi sana vibaya kiasi kwamba vimemuumiza mno kisaikolijia na kumfanya awe na depression kwa muda mrefu ambayo alikuwa akiificha watu wasijue. Kuna muda ulifika, msongo wa mawazo kwa vanessa ulikuwa mbaya mpaka akawa analewa kila siku kupunguza mawazo. Alikuwa hawezi kulala usingizi bila kunywa pombe.

Vitu vyote hivi.. Msongo wa mawazo ambao alikuwa hajautibu tangu kumpoteza baba yake, ugumu na vita za soko la muziki, mahusiano mabovu ya kimapenzi, presha ya jamii, vyote hivi vikamfanya vanessa kuwa katika hali mbaya sana kisaikolojia. Na mwenyewe anakiri kwamba kama hali hii ya depression ingeendelea basi yawezekana kuna jambo baya sana lingemtokea na pengine hata kupoteza maisha yake.

Mahusiano na Jux na kwanini jamii haipaswi kumlaumu sana Jux

Penzi la Vanessa Mdee na Jux lilijizolea umaarufu sana hapa nchini na lilidumu kwa takribani miaka mitano (2014 - 2019), Na hakuna uhusiano ambao ulimuumiza sana kwa jinsi ambavyo uliisha vibaya kama uhusiano wake na msanii mwenake wa bongofleva juma mkambala maarufu kama jux.


Wengi walimlaumu Jux kwa kuachana na Vanessa lakini huenda Depression (msongo wa mawazo) aliyokuwa nayo Vanessa ndio ulikuwa chanzo kikuu kwa mahusiano yao kuharibika, kuishi na mtu mwenye depression inafaa uwe na elimu kidogo ya afya ya akili na kwa bahati mbaya haya mambo muhimu huwezi kuyakuta hata katika mitaala yetu ya elimu.

Nadhani Jux hata hakuweza kumsoma Vanessa vizuri. Kuna watu sio wepesi kuonyesha wanachopitia sababu muda wote wanatabasamu na kucheka utadhani wana furaha toka moyoni kumbe wanapitia mambo mazito sana. Vanessa ni aina hiyo ya mabinti ambao si rahisi kuwagundua, hivi hata wewe kwa ule uchangamfu, ucheshi na sura iliyojaa tabasamu ya Vanessa uliamini kwamba ana depression ?

yawezekana Jux hakuwa na ujuzi wa kujua namna ya kuimudu hali hii ya Vanessa, kwa miaka mitano huenda Jux alijitahidi hivyo hivyo kibishi na kujitoa kadri awezavyo ila ikafikia muda akaona jitihada zake zote zimegonga mwamba .

Jamii ilimchukulia Jux vibaya kwa kudhani kamuacha kikatili Vanessa ambae tulidhani hakuwa na tatizo lolote kumbe uhalisia ni kwamba Vanessa alikuwa akipitia kipindi kigumu sana cha depression.


Uchumba - Vanessa na Rotimi muigizaji wa marekani

Kwa bahati nzuri sana, iko siku moja ya kipekee kabisa ambayo ilibadili kabisa maisha ya vanessa mdee.

Mwaka 2019 mwezi july, vanessa mdee alialikwa kutumbuiza kwenye jukwaa la tamasha la essence festival lililofanyika jijini new orleans nchini marekani . Tamasha hili lilikuwa linawakutanisha waimbaji wengi mahiri kutoka kila kona ya dunia.

Kama kawaida vanessa akapiga show na akaua vibaya sana. Sasa, baada ya tamasha kuisha, kampuni maarufu ya kusikiliza mziki ya spotify walikuwa wameandaa party maalumu kwa ajili ya mastaa ambayo ilikuwa inafanyika kwenye nyumba fulani la kifahari hapo hapo new orleans. Vanessa alikuwa ni moja ya staa ambaye alialikwa kwenye hii party.

Hili jumba ambalo party ilikuwa linafanyika lilikuwa kama limegawanyika sehemu mbili alafu katikati kuna swimming pool. Wakati party inaendelea, muigizaji wa hollywood nchini marekani anaeitwa rotimi aliwasili akiwa amechelewa sana, party ilikuwa imeanza kitambo. Kimsingi rotimi hakutaka kuudhuria hii party lakini wasanii wenzake wa tamthilia maarufu ya power ambayo yumo msanii maarufu 50 cent walimsisitiza asikose.

Sasa, wasanii wa power pamoja na mastaa wengine wakubwa wa marekani walikuwa wametengewa upande wao kwenye lile jumba. Lakini kutokana na rotimi kuchelewa sana hakuelewa akae upande gani kwa hiyo akajikuta ameenda kukaa upande ambao vanessa mdee na watu wengine walikuwa wamekaa. Moja ya waandaaji wa hii party akamtambulisha rotimi kwa vanessa na stori zikaendelea. Baada ya stori kunoga sana kama ilivyo kawaida kwa mtoto wa kiume kumtikisia taya binti, rotimi akaomba namba ya simu ya vanessa, na bidada bila hiyana akatoa namba.

Rotimi akabiliana na depression ya Vanessa kwa njia sahihi

Huenda Vanessa kukutana na Rotimi ndio ilikuwa njia sahihi zaidi ya kutuliza msongo wake wa mawazo, Serikali ya marekani imelipa uzito mkubwa sana suala la afya ya akili, maswala a afya ya akili yameingizwa hadi kwenye mitaala ya elimu, vitu kama elimu ya mbinu za kukabiliana na depression vipo katika mitaala ya elimu, hivyo hata Rotimi huenda alifaidika na hii elimu ambayo aliitumia kumsaidia Vanessa.

Baada ya Vanessa kumpa namba Rotimi wakaendelea kuwasiliana kwa wiki kadhaa. Katika haya mawasiliano yao, rotimi akagundua jambo kwamba Vanessa alikuwa ni mtu anayefanya kazi mno muda wote kuliko kawaida. Katika kumdodosa dodosa akagundua kwamba vanessa alikuwa anafanyakazi muda wote ikiwa kama njia ya kuondokana na msongo wa mawazo alionao. Vanessa alikuwa anahofia kukaa bila shughuli sababu ataanza kuzama kwenye mawazo aliyonayo pamoja na ulevi.

Rotimi akamshauri kwamba hilo jambo ni baya sana analolifanya. Sababu kujichosha kupitiliza na kazi sio suluhisho, akamuuliza ni lini mara ya mwisho vanessa alijipa likizo ya kupumzika hata kwa wiki mbili tu. Vanessa akamueleza rotimi kwamba tangu ameacha chuo (tangu baba yake afariki) hakumbuki kama amewahi kujipa likizo kupumzika hata kwa wiki moja tu asifanye kazi. Rotimi akamsihi sana ajitahidi ajipe likizo.

Baada ya kumbembeleza kwa siku kadhaa hatimaye Vanessa akakubali kujipa likizo ya muda mfupi. Akasafiri mpaka marekani ambako rotimi alimpokea na kumpeleka mapumziko kwenye jiji la Miami.

Kwa muda wa siku tatu za kwanza ambazo walikuwa huko Miami, Rotimi alitoa wazo la kuzima vifaa vyao vyote vya mawasiliano. Yaani kwa siku tatu wakazima simu na laptop. Yaani kwa siku tatu hizo ikawa ni kama wao wawili tu ndio wako duniani peke yao wamegandana kama kumbikumbi. hapa unaona wazi kabisa Rotimi alikuwa na elimu ya haya mambo kwa hio ikawa msaada mkubwa kwa Vanessa tofauti na huku bongo ambako hata watu wa karibu kama marafiki zake, ex wake (Jux) na watu wa karibu walikuwa hawana elimu ya afya ya akili maana hata kwenye mitaala yetu hivi vitu hakuna.

Vanessa anakiri kwamba, kwa mara ya kwanza baada ya miaka mingi sana akajisikia amani moyoni. Akajihisi kama kuna mzigo mzito ameutua. Akajihisi kama amevuta pumzi mpya ya kwanza ya maisha yake.


Uchumba hadi ndoa, kupata mtoto na kufunga ndoa

Na ni siku hiyo ambayo alijisikia amani moyoni, Vanessa akakata shauri kwamba Rotimi ndiye atakuwa mwanaume wa mwisho kwenye maisha yake.

Na hakutaka kuipoteza amani hii mpya ambayo alikuwa anajisikia, kwa hiyo akaamua kwamba ataachana na vitu vyote ambavyo anaviona vinamnyima furaha kwenye maisha. Na kitu kikubwa ambacho kilikuwa kinamnyima furaha ilikuwa ni muziki. Yaani japo alikuwa anapenda kuimba, lakini industry ya muziki aliiona kama ni jinamizi ambalo linaweza kumfanya apotee. Na ndipo hapo akakata shauri la kuachana kabisa na masuala ya muziki na awekeze maisha yake kwenye furaha yake na familia yake ambayo anataka kuijenga na rotimi.

Mpaka sasa mwenyezi mungu amewajalia kupata mtoto wao wa kwanza, na tayari rotimi amemvalisha vanessa pete ya uchumba na tunategemea mwaka huu huu tutakwenda upareni kula pilau la harusi.

Tunamtakia cash madame, vee money, vanessa mdee kila la heri na maisha yenye furaha na mafanikio.
 
Picha sasa.

Halafu mbona kama walikiwa na ubini mwingine au wachaga ndio utaratibu wenu huu??.mfano jina la mimi mars lina ubini
 
Asante Sana hii info inasikitisha na kufundisha pia,unajua watu wengi huwa hatujui uapnde wa pili wa Maisha ya mtu,mara nyingi huwa tunaona mafanikio Tu lkn hutujui upande wa pili ukoje.

Lkn pili huenda TUNAWEZA mlaumu jux lkn huenda Vanessa mwenyewe kutokana na msongo wa mawazo aliokuwa nao huenda ndio ukasababisha hata mahusiano Yao kuharibika, ilihitaji akili kubwa kujua jinsi ya kumhandle v money,so jux hakuwa ktk level hizo
 
Wanasema amtegemeaye mwanaadam ameangamia…siku mambo yakibadilika kwa Rotimi itabidi!
 
Nimejifunza kwamba sisi wababa tuwe tuna simulate maisha ya endapo hatupo duniani familia inaweza ku exist namna gani? tusiwe one man show.

Jaribu kuwafanya watoto na mama yao kuwa jasiri, tumia muda kuongea nao if your not there what you expect them to do, behave etc... !! inasaidia sana hasa hivi vifo vya ghafla.

Watoto hata mama yao watakuwa wanasema.. "hata baba alisema wakati wa uhai wake....."
 
Back
Top Bottom