Historia fupi ya Mchungaji Paul Nthenge ambaye aliwaanisha waumini kufunga bila kula kwa siku kadhaa ili kumuona Yesu. Huyu ni Paul McKenzie Nthenge

Mwigunejacob

New Member
Apr 25, 2023
2
2
Historia fupi ya Mchungaji Paul Nthenge ambaye aliwaanisha Waumini kufunga bila kula kwa siku kadhaa ili kumuona Yesu.

Huyu ni Paul McKenzie Nthenge wakati kanisa lake la Good News International huko Malindi lilipoimarika miaka michache iliyopita. Hakuwa mtu aliyechanganyikiwa, kama alivyochanganyikiwa anavyoonekana katika runinga leo.

Alianza kanisa hili mwaka 2003 kama kituo kidogo cha kiinjilisti pamoja na Mkewe Joyce Mwikamba.Kisha walihamia kijiji kiitwacho Migingo huko Malindi ambako alianzisha kanisa katika boma lililozungukwa na ukuta, ambamo familia yake bado inaishi hadi sasa. Mkewe Joyce anamsaidia katika kuhubiri kama Mchungaji mwenza huku McKenzie akidai kuwa na uwezo wa kuzungumza na Mungu MOJA KWA MOJA. Katika mahubiri yake, alidai kutoa maneno kama yalivyotolewa na Mungu mwenyewe. Ikiwa inamaana kwamba alitumia maneno ya Mungu katika mahubiri na fundisho yake.

Mwaka wa 2016, Mckenzie alipata kituo cha televisheni baada ya mmoja wa wafuasi wake Kennedy Mwacharo kumuuzia mali yake huko Lamu yenye dhamani. Mali hiyo na biashara hiyo ya runinga inasemekana kwamba Mckencie alinuwa shilingi Milioni 20 na kumkabidhi pesa zote, huku muuzaji Kennedy Mwacharo akiacha familia na majukumu yake. Mali hiyo ilikuwa na thamani ya zaidi ya Milioni 100 wakati huo. Kennedy Mwacharo alifariki miezi miwili baadaye katika hali isiyoeleweka.

Kesi kadhaa za watu kuuza mali zao na kumpa McKenzie wakati wakingojea ujio na kukutana na Yesu zilizidi kuwa nyingi, moja ya hivi karibuni ikiwa Betty, Muhudumu wa ndege za usafiri ambaye aliacha kazi aliyokuwa ameifanya miaka 11.

Alimwacha Mumewe na kuuza mali na vitu alivyokuwa amenunua na kuwekeza wa maisha yote kwa bei chini ya milioni 7 na kuelekeza fedha hizo katika kanisa la McKenzie la Shakaola. Betty anashukiwa kuwa miongoni mwa maiti zinazookotwa kwenye makaburi huko Shakahola.

Inadaiwa kuwa McKenzie alitumia pesa ambazo Kennedy Mwacharo alimpa kununua vipande vya ardhi huko Malindi na Mombasa, magari mawili na kuanzisha kituo cha runinga. Kupitia kituo chake cha TV, Mckenzie aliwafikia watu wengi sana na mafundisho yake kimsingi yalikuwa juu ya nyakati za mwisho, uovu wa njia za maisha za kimagharibi kama vile huduma za matibabu, elimu, chakula, michezo, muziki n.k.

Mackenzie alikaa juu ya ubatili wa maisha na alisisitiza juu ya maisha ya baadaye. Alihubiri kuhusu ujio wa pili wa Kristo ambao kulingana naye ulikuwa upesi sana - kalenda yake ya ujio wa mara ya pili wa Yesu Kristu ilikuwa daima chini ya mwaka mmoja. Pia alikazia fikira ghadhabu iliyowangojea wale ambao wangekuwa hai kufikia wakati huo. Hofu inayotokana na dhana hii potovu huenda ikawa chanzo cha wafuasi wake kutaka kufa ili siku hiyo isije ikawapata wakiwa hai.

Mwaka 2018 Dkt. Ezekiel Mutua kupitia Baraza la Kenya la kuainisha Filamu KFCB aliamuru kufungwa mara moja kwa kituo hicho cha runinga, hii ilikuwa mwaka mmoja baada ya Mckenzie na Mkewe kufikishwa mahakamani kwa itikadi kali za kidini, kufunza visivyo na kukiuka uhalali mfumo wa imani uliokithiri kwa madhumuni ya kurahisisha itikadi na kuleta mabadiliko ya kidini na kijamii.

Haijafahamika ni jinsi gani kesi hii ilivyoendeshwa licha ya maagizo ya kufungwa kwa kituo cha hicho cha runinga, McKenzie aliendelea nayo jambo lililoonyesha jinsi alivyokuwa na usemi siku hizo. Kumbuka wakati fulani, alimtishia aliyekuwa Mbunge wa Kilifi wakati huo Aisha Jumwa alipotilia shaka baadhi ya mafundisho yake na jinsi alivyowaweka wagonjwa katika boma lake badala ya kuwapeleka hospitalini.

Mwaka 2019, McKenzie aligonga vichwa vya habari tena wakati ndugu wanne kutoka magharibi mwa Kenya sehemu ya Mumias walipoondoka nyumbani kujiunga na Mckenzie, watatu kati yao walirudi huku mmoja asijulikane aliko. Hili, pamoja na baadhi mashinikizo yaliyowekwa juu yake kufunga shule aliyokuwa akiendesha katika boma lake bila leseni, ikampelekea kuhama kutoka Migingo hadi Shakaola. Alifunga kanisa, akauza baadhi ya magari yake kisha akanunua shamba la Shakaola kwa jina la kuanzisha biashara ya kilimo.
Watu waliokwenda kumuona ambapo kanisa lake la awali lilikuwa Migingo walipewa rufaa ya kwenda shambani kwake Shakaola na kulingana na majirani, watu wengi walienda huko lakini wachache wangeoneka baadaye hukuwengi wao wakipotelea mbali.

McKenzie alikuwa na Wasaidizi ambao wangewafutilizia watu waliokuwa wamefunga kula kwa sababu za ujio wa Yesu mfungo ambao wangefuatilia roho za watu masikini msituni. Hawa pia ni watu wale wale wanaofanya kazi ya kuzika kwa ajili yake. Inadaiwa kuwa wakati akitoka Migingo na kufunga kanisa lake, aliuza kituo cha TV (vifaa) na gari lake moja kwa Mchungaji Ezekiel wa New Life na hata baadhi ya zana zake za uinjilisti. Kumbuka kuwa Mchungaji McKenzie haishi na familia yake huko Shakaola, familia hiyo inaishi katika kijiji cha Migingo katika eneo la lango alimokuwa na kanisa lake na amekuwa na nyumba nyingine nzuri ya familia umbali mfupi kutoka mji wa Malindi.

Huku akiwaongoza watu na watoto wao kufa ili kukutana na Yesu, familia yake inaishi bora zaidi kutokana na wanachompa wanapojitayarisha kwa Safari 'takatifu'. Kumbuka wengi wa watu hawa wanafunga porini mchana na usiku, huku wakikabiliwa na hali mbaya ya hewa na hatari nyinginezo.

Habari hii imetayarishwa na Mwana habari Paul Gregory. Mswali machache kwetu sote.

1. Je hii ni sawa na kujitia kitanzi

Toa maoni yako
#MvanoHabari
#MvanoMtangazaji
#M31
 
Acheni wafe wameamua wenyewe

INSTAGRAM @dollrubii_decors
 
Situlikubaliana kuwa wafuasi wa Yesu wana elimu na akili kuliko wafuasi wa Mood!
 
Jamaa ni mporaji anaetumia dini, ukiingia kwenye 18 zake anakufilisi anakutupa porini huko.

Ukikutwa ataambia raia kua alifunga hadi akafa ili akamuone yesu, hakuna ataemuona ana hatia bali kumlaumu marehemu kua hana akili.
 
Ni ujinga wa watu wengi tu kuwaamini haraka wachungaji/manabii wanaohubiri miujiza na upuuzi mwingi mwingine.

Hawashtuki kwamba hao wachungaji / manabii wanatajirika haraka kwa Jasho lao, au hata madhara kwa afya zao.
 
Pana mmoja mwanza aliitwa Babagodi huyu Mchungaji laiti asingekiuka masharti ya kichawi angekuja kuleta kilio kikubwa Sana kwa wakaazi wa Mwanza alikuwa na nguvu za kichawi kuliko zumaridi. Sema ndo hivyo Mungu aliingilia kati kuepusha madhara.
 
Pana mmoja mwanza aliitwa Babagodi huyu Mchungaji laiti asingekiuka masharti ya kichawi angekuja kuleta kilio kikubwa Sana kwa wakaazi wa Mwanza alikuwa na nguvu za kichawi kuliko zumaridi. Sema ndo hivyo Mungu aliingilia kati kuepusha madhara.
Alijuwaje Mzee?
 
Back
Top Bottom