Hivi kwanini wali wa mkaa ni mtamu kuliko ule wa 'rice cooker'?

amu

JF-Expert Member
Aug 8, 2012
13,417
2,000
Huwezi amini sasa hivi kupika wali kwenye mkaa siwezi natoa bokoboko, ila kwa rice cooker natoa kitu konki na ukoko laini wa chini.
 

Kamgomoli

JF-Expert Member
May 3, 2018
994
1,000
Hahahaa uwiiiiii,hii ndo raha ya jamiiforum
MATANDU.

Muda wa kupakuliwa Chakula, ni raha pale yanapoanza kuondolewa MATANDU.

Hiyo kama upo karibu na Mpishi lazima uombe kuonja MATANDU.

Kama ni Mpishi mwenye gubu, anakutimua, "toka,"mtoto wa KIUME unaleta HILA jikoni" "toka".

MATANDU yakimwagiwa MCHUZI, au MAHARAGE na ROJO yake, acha tu.

Jamani
Sent using Jamii Forums mobile app
 

Thebroker

JF-Expert Member
Aug 26, 2016
791
1,000
Bahati mbaya sijawah kula wali wa mkaa au wa rice cooker....nimekula wa mchele tu.

The good, the bad and the ugly.
 

mwandende

JF-Expert Member
Feb 16, 2017
2,799
2,000
Kwanza WALI MWENZIO ni NAZI,,na sio mafuta,,, wali wa NAZI NI BALAA,,,halafu JUU lazima uwe na MATANDU. ,AU MAHABA (watu wa tanga tunaita hivyo)na lazima uwekewe mkaa juu ya sufuria au chungu.,,HALAFU unapata na SAMAKI WA CHUKUCHUKU,,,hatari MKUU ,,,haya mambo ya GESI,,MAJIKO YA UMEME,,,huwezipata LADHA HALISI YA WALI,,

Sent using Jamii Forums mobile app
 

amu

JF-Expert Member
Aug 8, 2012
13,417
2,000
Nami pia ndo nachokiona hiko.
Lakini kwa karne hii matumizi ya kuni nia adhabu sana kuzipata hizo kuni na pia ile harufu ya Moshi ukijumlisha na macho kutoa machozi mhhhh.

Last Christmas nilipika biriani kwenye kuni.
Haloooo moto wa kuni nao ni mkali tu kama gas ila niliipata pata.
Lakini biriani ilitoka poa sana.
Naona kama Chungu mwenzie Kuni.
 

amu

JF-Expert Member
Aug 8, 2012
13,417
2,000
Kisamvu nakielewa sana.
Kwanza nikikichemsha naweka saum na kitunguu kiiiva naweka ile top layer ya maziwa fresh.
Kinalala.
Kesho yake naweka nazi na siagi ya karanga.
Kinaliwa ila ni lazima kibaki tena .
Keshokutwa kinapashwa na siagi ya karanga.
Maharage yaliyolala, pembeni kisamvu na dagaa mchele au samaki wa kukaanga na fresh wali(si kiporo)
+ kisamvu kilicholala

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Top Bottom