Kibongobongo haya ni Mafanikio Makubwa kwako Kijana ukiwa nayo. Furahia Maisha

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,900
KIBONGOBONGO HAYA NI MAFANIKIO MAKUBWA KWAKO KIJANA UKIWA NAYO.

Anaandika, Robert Heriel

Siandiki kukusifia, au kukufanya uridhike. Najaribu kukueleza kuwa lazima ukubali kuwa umepambana na ufurahie matunda ya Kazi ya mikono yako. Usiposhukuru Kwa hayo uliyonayo hutokuja kushukuru Kwa Yale usiyonayo unayoyahangaikia.

Mwaka juzi nikiwa katika ofisi yangu, Kihonda Morogoro, alikuja kijana mmoja akiwa amebeba viatu anauza(alikuwa Machinga) akawa anaikagua ofisi yangu akitazama huku na huku. Nikamuona akigeuzageuza macho yake kuangalia ofisi yangu; Akaangalia shelfu zilizokuwa na vitabu, akaangilia sofa mbili za ngozi zilizokuwa mule ndani, akaiangalia meza kubwa ya kiofisi, akacheki Laptop yangu, kisha akaiangalia meza nyingine ndogo ambayo ilikuwa na laptop nyingine pamoja na Printer na cut-paper machine, Chini likiwelo Zulia la plastiki, pamoja na Kiti cha kisiasa cha ofisini cha kuzunguka, aliyekaa juu ya Kiti hicho alikuwa ni Mimi Taikon huku nikipepewa na Upepo mzuri wa Feni.

Kwake aliiona ni ofisi nzuri Sana. Lakini vipi kuhusu Mimi mwenye Ofisi, je niliiona kama alivyoiona? Hasha! Mimi niliiona yakawaida, tena yenye mapungufu meeengi mno.

Lakini Jambo moja pekee ambalo nililiamini ni kuwa nilikuwa nimefanikiwa. Na nilishukuru Kwa Mafanikio Yale. Hata kama kuna Wakati niliona kuwa ninahitaji maboresho na kuongeza uzuri na Mvuto WA ofisi ili iwe na hadhi ninayoitaka.

Yule kijana alinisimulia Historia fupi ya Maisha yake. Kiumri alikuwa na miaka 19 nikiwa nimemzidi miaka kama sita hivi.

Katika umri huo nikagundua tayari anauzoefu wa Maisha katika kiwango Fulani. Anajitegemea katika makazi kwani alikuwa amepanga chumba kimoja, anajilisha na kujivalisha na Wazazi wake Huko Sumbawanga wanategemea hivyo anawatumia Pesa nyingi mno, kila wiki Anawatumia elfu kumi.

Nilipomdadisi zaidi, nikagundua alinionea wivu Kwa kuona ati Mimi kazi yangu ni kukaa tuu ndani ya ofisi, kuandikaandika, na sipati shida. 😀😀 Nikacheka Sana.

Lakini wivu wake ulikuwa mzuri kwani alisema anatamani siku moja naye afanye kazi akiwa katulia sehemu moja, kutembeza vitu Kwa mguu inachosha Sana. Nikamuambia kila Jambo ukiliwekea Nia utafanikiwa kama utalifanya Kwa juhudi, Akili, uthubutu na nidhamu.

Nikamuambia, hata Mimi kuna Wakati nafanya kazi ya kutembeza bidhaa, ni kweli nikiwa na shida ya Pesa ya haraka nilikuwa naagiza mzigo WA dagaa, nafunga kwenye pakti, natembeza nyumba Kwa nyumba, Sako kwa Bako. Kuanzia saa tatu Asubuhi mpaka saa Saba Mchana hapo nitakuwa nimeuza pakti zisizopungua 40 ambayo ni Sawa na Tsh 40,000/= mauzo faida hapo ni Tsh 20,000/=. Ni masaa manne tuu ya mateso lakini nimeweka kibindoni elfu 20 kama faida.

Nilikuwa na Sababu tatu za kufanya biashara ya Umachinga (kutembeza dagaa) sababu hizo;

1. Kuondoa kiburi, kujiona na kuondoa Aibu.
Kwa wasiomjua Taikon, Mimi ni Msomi tena sio Msomi oyaoya! Namaanisha Msomi haswa hata kama nimesomea shule za kata lakini nilisoma kuelewa na kuipa Akili yangu Uhuru. Nisiwe mjinga.

Niliuza dagaa ikiwa ni misheni ya kuondoa Aibu, kiburi na majivuno na kuji- neutralize niwe mtu wa kawaida.

Wasomi tukimaliza shule tunabeba dhana ya ukubwa, hadhi na hatustahili kazi zenye vipato vidogo. Jambo hilo linaathiri utendaji wetu.

Pia, Muonekano wangu kama kijana barubaru ungeweza kuniathiri kuzidharau baadhi ya Kazi. Kusifiwa na Wanawake kuwa Mimi ni kijana Mzuri Kwa muonekano na kutosumbuliwa na Wanawake katika harakati za kuwatongoza, pengine ingeniathiri na kujiona Mimi ni Mwanaume spesho, sina haja ya kujitesa kutafuta Pesa Kwa Njia ngumu ilhali ninauwezo wa kuzipata Kwa Wanawake. Jambo ambalo baadhi ya Vijana WA siku hizi wamejikuta katika hatari hiyo.

Kufanya kazi zilizodharauliwa kwangu ilikuwa mkakati sahihi Kabisa wa kuitengeneza tabia na mtazamo wangu kuhusu Maisha. Na katika hilo nimefanikiwa.

Taikon habagui kazi, Taikon anaiheshimu Pesa. Taikon hawezi kuwekwa ndani na Mwanamke akalishwa, kwani Taikon ni Mwanaume Halisi. Lazima afanye majukumu yake.

2. Kupata uzoefu wa kuanzia Chini.
Nisingeweza kusubiri Ajira. Mimi sio MTU wa kusubiri. Ninapenda kuona mambo yakifanyika.
Hivyo kuanzia Chini ndio mbinu pekee ambayo itakupatia uzoefu.

3. Kutaka kupuuzwa na kutokuzingatiwa.
Naipenda Hii Kanuni na mara nyingi ninaitumia Sana. Sio tuu kwenye utafutaji Bali hata kwenye mahusiano ya kawaida.

Jamii tayari inajua Mimi ni Msomi, kuniona ninafanya kazi zenye kipato cha Chini wengi wao watanipuuza na kutokunizingatia. Hata baadhi ya Wachumba😀😀. Watakaobaki hata kama ni mmoja hao ndio nitawachukulia seriously.

Kwa Watu wanaonifahamu, Taikon ni kijana simple, sio MTU wa kuvaa Sana, hiyo hunifanya niwe comfortable kusoma uhalisia wa Watu vile wanionavyo.

Kimsingi nisipozingatiwa na watu itanisaidia kufanya mambo yangu pasipo kuingiliwa na kusikia milunzi mingi.

Hii inafanya kazi Kwa Watu wanaoanza Maisha wakiwa Hawana kitu chochote.

Hata katika mapambano iwe Ngumi au ushindani wa kibiashara, anayeanzia Low Key au anayeanzia Chini ni rahisi kushinda na kufanya vizuri kuliko Yule anayejitutumua.

Maelezo hayo nilimpa Yule kijana aitwaye Moses.

Mafanikio huanza polepole Kwa uhakika.
Kidogokidogo mpaka yanakuwa makuubwa! Mpaka Watu wanashangaa.

Nilimuambia Dogo Moses, Hii ofisi haikuanza hivi kama unavyoiona, ilianza kidhalili, kifukara, kinyonge, lakini niliyeinzisha sikuwa mnyonge, sikuwa dhalili na wala sikuwa fukara ndio maana unaiona hivi ilivyo. Hata kama ningeianzisha kifalme, kitajiri na kibingwa kama Mimi muanzilishi ningekuwa mnyonge, fukara na dhalili basi ungeikuta Ipo vibaya Sana.

Ninachotaka kukuambia, hata wewe unayefanya Umachinga wa viatu, mtaji wako au namna biashara yako ilivyo sasa, itabadilika kulingana na wewe jinsi ulivyo Kwa Ndani.

Nilimuambia, nilianza na meza na Kiti tuu na hii laptop moja unayoiona. Lakini kidogokidogo ndani ya mwaka mmoja na Nusu ndivyo unaiona hivi ilivyo. Ni kubwa?

Nikamuuliza, akatabasamu kisha akasema ni kubwa, ilhali moyoni mwangu nikiwa nimeadhimia itakuwa kubwa mara kumi ya vile aionavyo.

Sijui kama naeleweka!

Kijana, hapo ulipofika ni umefanikiwa Sana. Yote uliyonayo ni Mafanikio.

Lazima ushukuru, lazima ujivunie! Haijalishi wengine wanayaona na kuyatafsirije hayo Mafanikio. Hayo ndio Mafanikio yako.

Amini kwamba kuna Watu wanakuona kama Role model wao. Wanatamani wawe kama wewe. Jivunie mafanio yako.

Siongei kama Motivesheni Spika hapa, nazungumzia uhalisia.

KIBONGOBONGO ukiwa na haya basi umefanikiwa;

1. Ukiwa na Ghetto na ukiwa unajitegemea.

Ni dhahiri wengi tumetoka familia masikini.
Kitendo cha wewe kujitegemea mwenyewe Kwa makazi, chakula na mavazi na unalipa Bills zako. Hayo ni Mafanikio makubwa Sana. Ambayo unatakiwa umshukuru MUNGU.
Kujitegemea kunamaanisha kuwa huru, kutompa MTU mzigo.

Hata kama bado hujafikia kiwango cha kuwahudumia wazazi wako, shukuru! Shukuru! Nao wanatakiwa washukuru kwani hauwategemei.

Endelea kupambana, kadiri unavyojitegemea ndivyo unavyoweka msingi WA kutegemewa, kuwa tegemeo.

2. Kujiajiri au kuajiriwa.

Ni Mafanikio makubwa kujiajiri au kuajiriwa. Kwamba unaouwezo wa kuhudumia Watu wengine nao wanakupatia malipo Kwa Huduma yako.

Kuwa MTU mzalishaji mwenye manufaa ndani ya jamii yako ni Mafanikio hayo.

Jitahidi usikae Kae hivi bila kuihudumia jamii yako.
Ihudumie Kwa yote uliyonayo. Hayo ndio Mafanikio yenyewe.

Haufurahi Watu wakifurahia na kuzipenda kazi zako?
Kama unaimba, imbia Watu hata kama ni burebure imbia, imbia!
Hudumia Watu mpaka pumzi yako ya mwisho.
Jitahidi Huduma zako zilenge kuleta manufaa chanya ndani ya jamii.

Nakupa mfano, Taikon ninapoandika hapa, ninafurahi kuihudumia jamii. Sina Pesa za kuwapa, labda sina chochote cha kutoa katika Maisha yangu Kwa jamii yangu. Sasa Niishi kama sipo, hapana! Taikon hayupo hivyo.

Nitaandika Kwa maana Hilo ndilo nililojaliwa na Mwenyezi Mungu, pale pumzi yangu itakapokoma basi nitapumzika nikiwa nimeridhika, nami nitajiona nilifanya Jambo Fulani hata kama ni Kwa kiwango kidogo.

Nawe Fanya. Fanya Kwa sehemu yako.
Iwe ni Kwa malipo au Kwa kujitolea. Ila kamwe usikubali kukaa vivihivi!
Huko ni kushindwa, ni Kufa. Hautokuwa na maana yoyote ya kuishi.

3. Kumiliki na Kutumia Mashine.
Mafanikio ni pamoja na kumiliki zana au vyombo zinazokurahisishia kufanya kazi ambazo huitwa Mashine.
Kumiliki magari, Simu, Luninga, Mashine za kufulia, Majiko ya kisasa ya kupikia n.k.
Hayo ndio Mafanikio yenyewe.

Mafanikio yanahusu kukufanya kuwa Huru. Kukuondolea utumwa na ugumu WA Maisha hayo ndio Mafanikio.

Huwezi ukawa umefanikiwa ikiwa bado unaugumu wa Maisha.
Kumiliki mashine ni sehemu ya Mafanikio.
Mfano, badala ya kutembea Kwa mguu wewe unaendesha Gari. Hayo ni Mafanikio.
Upo Moshi unataka kuwasiliana na MTU wa Mwanza umuone Live/mubashara yaani moja Kwa moja. Badala ya kusafiri Kutoka Moshi kumfuata Mwanza, unachukua simu yako unampigia kupitia Zoom, telegram, au WhatsApp n.k mnaonana. Hayo ndio Mafanikio yenyewe.

Unataka kupika chakula, sio mpaka upasue Juni au uwashe mkaa. Unachukua Jiko la Pressure Cooker, unaweka chakula chako unaseti muda, kisha unaendelea na mambo mengine huku chakula kikiiva bila usimamizi wako. Hayo ndio Mafanikio.

Unataka kufua, unamashine ya kufulia, unaweka nguo na sabuni kisha unaziacha kwenye Mashine, unaendelea na mambo mengine. Ukija unatoa unaanika au unapiga pasi. Hayo ni Mafanikio.

Mafanikio yapo kifikra na kifizikali. Ni muhimu Kwanza kuwa na Mafanikio ya kifikra ili iwe rahisi Kupata Mafanikio ya kifizikali.

Ninatoa mfano mwingine, Kwa Vijana.
Taikon amemaliza CHUO, Hana hili la lile. Anataka kujitegemea, anataka kazi, anataka mahusiano, anataka Maisha mazuri. Kipi kinatangulia?

Chochote kinaweza kutangulia inategemea na kipi kipo Mbele YAKO.

Taikon huwaga natumia Kanuni isemayo; tumia kilichopo Kupata ambacho hauna.

Ngoja nipumzike alafu tutaendelea, Pole Kwa andiko Refu. Hata hivyo sijadhamiria kukukera au kukuumiza, zaidi nilitaka kusema yote Ila muda ni mchache

Ni yule Mtibeli Kutoka Nyota ya Tibeli yenye mbawa mbili irukayo Kutoka Ulimwengu mmoja Hadi mwingine.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Mafanikio yanahusu kukufanya kuwa Huru. Kukuondolea utumwa na ugumu WA Maisha hayo ndio Mafanikio.
Huwezi ukawa umefanikiwa ikiwa bado unaugumu wa Maisha.💯💯💯💯💯

Ni yule Mtibeli Kutoka Nyota ya Tibeli yenye mbawa mbili irukayo Kutoka Ulimwengu mmoja Hadi mwingine.
 
Mafanikio yanahusu kukufanya kuwa Huru. Kukuondolea utumwa na ugumu WA Maisha hayo ndio Mafanikio.
Huwezi ukawa umefanikiwa ikiwa bado unaugumu wa Maisha.💯💯💯💯💯


Ni yule Mtibeli Kutoka Nyota ya Tibeli yenye mbawa mbili irukayo Kutoka Ulimwengu mmoja Hadi mwingine.


Naam Mkuu
 
Mm nina nyumba mbili ila najihis sijafanikiwa bado vp hapo bwana Taikon na nna umri wa miaka 31 mwaka huu

Jifunze kushukuru ndipo utajua Mafanikio ni kitu gani.
Kitu chochote ambacho ulipanga kukitimiza aladu ukakitimiza hayo ni Mafanikio.
Furaha haitokani na kutimiza Jambo Fulani, furaha inatoka ndani vile unavyoyachukulia Maisha katika fikra chanya.

Kuwa bilionea au kufanikiwa hakukufanyi ufurahi.
Hata Mimi Wakati nasoma nilidhani nikifika CHUO nitakuwa nafuraha au nitajiona nimefanikiwa lakini haikuwa hivyo.

Furaha ni maamuzi, uchaguzi wa kujipa Raha
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom