Hivi kwanini Kibaha isiwe Dar es Salaam?

Hivi kwanini Kibaha isiwe Dar es Salaam?

Huwa najiuliza, viongozi wa hii nchi wana akili timamu kweli? Yaani wanajua kabisa raia wao wengi hawana elimu na wamejirundika Dar es Salaam kwa ajili ya jina. Kwanini wasiifanye wilaya ya Kibaha kuwa ndani ya Dar es Salaam ili watu wasambae kujenga huko?

Maana naona kutoka Kibaha mpaka Mbezi Magufuli ni karibu kuliko kutoka Kariakoo mpaka Mbezi Magufuli, ambapo ndio kituo kikubwa cha mabasi Tanzania. Aisee, namuomba Rais wetu Samia aipanue Dar es Salaam kwa kuchukua ardhi ya Kibaha, maana hata daladala zinapandisha nauli kila siku kwa kigezo cha Kibaha kuwa mkoa mwingine, wakati unakuta umbali ni mdogo tu.
Rahisi ni kufanya Dar es Salaam kuwa kibaha. Siyo rahisi kibaha kuwa dar es Salaam.
 
Kama ni mipango endelevu
Basi wilaya za Mkuranga, kisarawe,Bagamoyo,Mafia , kibaha na Bagamoyo ziwe Dar es salaam.

Ili iundwe Metropolitan city yenye kuunganisha wilaya zote na BRT na Reli.

Inawezekana tukiwa na Nia ila sio sababu za kipuuzi za mleta mada kisa wilaya moja ipo karibu na stand.

Anauliza Kisenvule Kuna maendeleo gani, viwanda kule mkuranga unafikiri vimejengwa kimbwanindi?
 
Tatizo sio kuongeza ardhi.. Bali mipango Miji.. Dar Ina ardhi kubwa tu lakini imetumiwa vibaya kwa ujenzi holela na ukosefu wa mipango miji. Yaani TZ kila mtu anataka apate ardhi ajenge ndio maana Miji yetu inatanuka horizontally.

Suluhisho ni kuweka mipango Bora ya makazi.. Serikali inaweza kuingia ubia na mashirika ya makazi wakajenga nyumba za makazi kwa mfumo mzuri ili kuongeza density. Mfano Ukijenga Jengo moja la ghorofa 10 lenye nyumba(apartments) 20 ukawauzia watu kwa mkataba labda wa miaka ishirini huku wakilipa kidogo kidogo utaokoa ardhi kubwa. Maana hao watu Kama kila mtu angejenga vibanda vyake wangetumia ardhi kubwa kujenga nyumba 20.

Hapo tunasema mji una expand vertically sio horizontally. Pia hii itasaidia hata shida za Usafiri na kufuata huduma kupungua. Sio Kama Sasa mtu anaishi kilometa 40 from City center, na kila siku inabidi aende huko kwenye utafutaji.

Hitimisho Ni kwamba naona Miji yetu inapaswa ku-limit horizontal expansion.. bila hivyo miaka 50 au 100 ijayo tutajikuta tumetumia ardhi yote.. hatuna pa kujenga Wala kulima Wala kuwekeza.
 
Mkoa wa Pwani ugawanywe

Kibaha, Bagamoyo, Kisarawe na Mkuranga ziunde jiji la Dar Es Salaam.

Rufiji, Kilwa, Mafia na Kibiti ziunde Mkoa wa Pwani/Rufiji/Kilwa.

Mikoa miwili ya Tanzania bara yaani Morogoro na Tabora iwe mikoa ya Viwanda vikubwa/vizito zaidi na technologia ya majeshi yetu na taasisi nyingine kama za matibabu.

Hapa naamanisha Viwanda vizito vyote visiendelee kujengwa Mkoa wa Pwani tena bali vielikezwe Morogoro na Tabora na Viwanda vyepesi viendelee kujengwa Mkuranga kama eneo la rasmi la Viwanda, huku Bagamoyo, Kibaha na Kisarawe yawe makaazi tu lakini serikali ipime maeneo hayo yote ili kuepuka ujenzi holela wa makaazi, hii inalenga upanuzi wa Jiji la Dar Es Salaam.

Serikali ichore ramani mpya ya Dar Es Salaam ikiunganisha Halmashauri hizo katika miundombinu ya Barabara za kisasa, Reli, umeme, Maji, pia serikali itenge eneo kubwa zaidi kule Kisarawe kwa ajili ya ujenzi wa uwanja mwingine wa ndege, yawezekana miaka 50 mpaka 70 ijayo kutoka leo uwanja wa ndege wa Mwalimu Julias Nyerere utazidiwa kutokana na maendeleo makubwa na upanuzi wa miundombinu ya usafiri wa Anga.

Viwanda vyote ambavyo vimejengwa tayari Mkoa wa Pwani vibakie hivyo hivyo na/au vinaweza kuhamishwa hasa vile vizito na kuelekezwa Morogoro na Tabora.

Morogoro iwe sehemu ya kilimo cha kimkakati na Viwanda vikubwa/vizito ikiwemo na taasisi za utafiti wa kisayansi za majeshi yetu na technologi nyingine zielekezwe Morogoro na Tabora.

Na, Nicolas J Clinton Gabone
Yaani sielewi kama wtaalamu wa mipango miji kama wanaishauri serikali au vipi. Natamani wawe wanaitwa kweye media serious tuwalize haya maswali
 
Kibaha hadi Bagamoyo, yaani Chukua Kiluvya, Kibaha, Bagamoyo, Kisarawe, yote ingefaa iwe Mkoa wa Dar es Salaam
 
Huwa najiuliza, viongozi wa hii nchi wana akili timamu kweli? Yaani wanajua kabisa raia wao wengi hawana elimu na wamejirundika Dar es Salaam kwa ajili ya jina. Kwanini wasiifanye wilaya ya Kibaha kuwa ndani ya Dar es Salaam ili watu wasambae kujenga huko?

Maana naona kutoka Kibaha mpaka Mbezi Magufuli ni karibu kuliko kutoka Kariakoo mpaka Mbezi Magufuli, ambapo ndio kituo kikubwa cha mabasi Tanzania. Aisee, namuomba Rais wetu Samia aipanue Dar es Salaam kwa kuchukua ardhi ya Kibaha, maana hata daladala zinapandisha nauli kila siku kwa kigezo cha Kibaha kuwa mkoa mwingine, wakati unakuta umbali ni mdogo tu.
Rudi kwenu na huo ushamba wako
 
alafu tunataka mapinga iwe dar.magari ya bunju yafike.
tuwakomoe bajaj wanaopandisha bei usiku
 
Kama ni mipango endelevu
Basi wilaya za Mkuranga, kisarawe,Bagamoyo,Mafia , kibaha na Bagamoyo ziwe Dar es salaam.

Ili iundwe Metropolitan city yenye kuunganisha wilaya zote na BRT na Reli.

Inawezekana tukiwa na Nia ila sio sababu za kipuuzi za mleta mada kisa wilaya moja ipo karibu na stand.

Anauliza Kisenvule Kuna maendeleo gani, viwanda kule mkuranga unafikiri vimejengwa kimbwanindi?
Huko porini kwenu kisemvule utafananisha na kibaha hivi unaakili timamu kweli
 
Huwa najiuliza, viongozi wa hii nchi wana akili timamu kweli? Yaani wanajua kabisa raia wao wengi hawana elimu na wamejirundika Dar es Salaam kwa ajili ya jina. Kwanini wasiifanye wilaya ya Kibaha kuwa ndani ya Dar es Salaam ili watu wasambae kujenga huko?

Maana naona kutoka Kibaha mpaka Mbezi Magufuli ni karibu kuliko kutoka Kariakoo mpaka Mbezi Magufuli, ambapo ndio kituo kikubwa cha mabasi Tanzania. Aisee, namuomba Rais wetu Samia aipanue Dar es Salaam kwa kuchukua ardhi ya Kibaha, maana hata daladala zinapandisha nauli kila siku kwa kigezo cha Kibaha kuwa mkoa mwingine, wakati unakuta umbali ni mdogo tu.
Maana naona kutoka Kibaha mpaka Mbezi Magufuli ni karibu kuliko kutoka Kariakoo mpaka Mbezi Magufuli,
"J'3 KWENDA J'PILI V/S J'PILI KWENDA J'3"
 
Back
Top Bottom