Dar yenye heshima, hadhi inawezekana

Dar yenye heshima, hadhi inawezekana

Miss Halima

Senior Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
198
Reaction score
439
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila ametamka kuwa lazima wairejeshe Dar es Salaam yenye hadhi, heshima na kwamba kila kitu kikae mahali pake.

Kwa mujibu wa Chalamila, hali ya uholela kwa kila kitu Dar es Salaam imetosha na aliahidi katika hili hataki mzaha. Ametamka haya baada ya kutangaza kuchukua hatua dhidi ya malori yanayoegeshwa kiholela, hasa katika barabara ya kutoka bandarini kupitia Nelson Mandela kwenda mikoani kupitia Barabara ya Morogoro.

Na si hilo la malori pekee. Katika kurejesha hadhi ya Dar es Salaam pia amekuja na agizo la mabasi yote kuanzia na kumalizia safari zao katika Stendi Kuu ya Magufuli Mbezi Louis badala ya kuwa na vituo kila kona ya mkoa.

Kimsingi, mkuu wa mkoa ana hoja za msingi kutokana na ukweli kuwa mkoa sasa umekuwa na ‘vurugu’ zinazotokana na mabasi na malori hayo kuegeshwa sehemu zisizoruhusiwa na mji umekuwa na foleni zisizo za lazima na kuhatarisha maisha ya watumiaji wa barabara.

Kwa Tanzania, Dar es Salaam ndio kioo cha nchi, hivyo kama hakutakuwa na mpangilio unaoeleweka katika mji basi utakuwa unahatarisha uwekezaji, kwani wageni watajionea vurugu zisizo za lazima katika mitaa ya mji.

Na pengine hili la mkuu wa mkoa limekuja kwa wakati mwafaka, hasa ikizingatiwa kuwa miezi michache ijayo Tanzania itakuwa mwenyeji wa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2027) zitakazoandaliwa kwa pamoja na majirani Kenya na Uganda.

Hivyo, uwepo wa wageni wengi mwakani ina maana lazima mji uwe katika mpangilio wake ili kurahisisha usafiri na ukazi wa wageni wataokuja kushuhudia fainali hizo. Katika siku za karibuni, Dar es Salaam imekuwa na uholela wa watu kujichukulia sheria na taratibu zisizofaa na kufanya mji uwe na mambo mengi yasiyopangwa.

Watu wamevamia maeneo ya wazi, maeneo ya watembea kwa miguu, vituo vya daladala, maeneo ya burudani na mengineyo na hivyo kusababisha usumbufu kwa wananchi wanaotumia maeneo hayo kama yalivyotengwa.

dar.png
 
Back
Top Bottom