Hivi kwanini Kibaha isiwe Dar es Salaam?

Ngoja niwaoneshe majimbo yatavyokua

Dar State - Dar,Pwani,Tanga,Morogoro.
State 2 - Mwanza,Kagera,Geita, Simiyu.
State 3 -Kigoma,Tabora,Shinyanga,Singia.
State 4 -Mara,Arusha,Manyara,Kilimanjaro.
State 5-Katavi,Rukwa,Mbeya.
State 6 - Njombe,Ruvuma,Lindi,Mtwara.

Dodoma ibaki na hadhi yake ya makao makuu ya nchi na serikali.

tutapunguza sana matumizi ya serikali na tutaongeza ufanisi sana wa utandaji wa serikali.Wakurugenzi wabaki kama walivyo, awepo tu mkurugenzi mkuu wa jimbo na wakurugenzi wachini yake katika maeneo ambayo yalikua mikoa.
 
Mimi nashauri Pwani yote iungane na Dar halafu irudishiwe jina lake la Mzizima, kisha Sinza iwe manispaa na iwe ndio makao makuu ya Mzizima, na manispaa za Ilala na Ubungo zirudi kuwa kata pamoja na kata zao zote ziwe ndani ya manispaa ya Sinza, yani kwa kifupi Mzizima iwe na manispaa na wilaya kama ifuatavyo: Sinza, Kinondoni, Kigamboni, Kibaha, Temeke, Bagamoyo, Kisarawe, Chalinze, Mkuranga, Rufiji, Kibiti, halafu wilaya ya kisiwa cha Mafia iwe Lindi basi tunakuwa tumemaliza mchezo
 
Miji iende vertical badala ya horizontal. Dar ingeenda vertical inavyotakiwa huenda isingekuwa imepita Manzese tukasave ardhi kwa matumizi mengine muhimu badala ma-slums kuenea hadi Mlandizi huko.
Kwahiyo unataka watu waishi kama kuku wa kwenye cage, kaeneo kadogo watu utitiri

Tz bado ni kubwa sana tembea uone usiishie hapo manzese tuu
 
Miji iende vertical badala ya horizontal. Dar ingeenda vertical inavyotakiwa huenda isingekuwa imepita Manzese tukasave ardhi kwa matumizi mengine muhimu badala ma-slums kuenea hadi Mlandizi huko.
Hakika Skyscraper including maghorofa ya floor 5 kuendelea zinasaidia mno ku conserve space
 
Huwa najiuliza, viongozi wa hii nchi wana akili timamu kweli? Yaani wanajua kabisa raia wao wengi hawana elimu na wamejirundika Dar es Salaam kwa ajili ya jina. Kwanini wasiifanye wilaya ya Kibaha kuwa ndani ya Dar es Salaam ili watu wasambae kujenga huko?

Maana naona kutoka Kibaha mpaka Mbezi Magufuli ni karibu kuliko kutoka Kariakoo mpaka Mbezi Magufuli, ambapo ndio kituo kikubwa cha mabasi Tanzania. Aisee, Bora i Dar es Salaam ipanuliwe kwa kuchukua ardhi ya Kibaha, maana hata daladala zinapandisha nauli kila siku kwa kigezo cha Kibaha kuwa mkoa mwingine, wakati unakuta umbali ni mdogo.
Kama tatizo ni nauli nakushauri ununue baiskeli
 
Ila ukitokea mtikisiko kama wa juzi Myanmar na Thailand plus expansion joints za ma-engineer wa kibongo na ratio zao wanazozijua wenyewe taifa litaomboleza hatari!
Watafute ma engineer kutoka Japan ni wataalamu kidogo wamezoea matetemeko
 
Ngoja niwaoneshe majimbo yatavyokua

Dar State - Dar,Pwani,Tanga,Morogoro.
State 2 - Mwanza,Kagera,Geita, Simiyu.
State 3 -Kigoma,Tabora,Shinyanga,Singia.
State 4 -Mara,Arusha,Manyara,Kilimanjaro.
State 5-Katavi,Rukwa,Mbeya.
State 6 - Njombe,Ruvuma,Lindi,Mtwara.

Dodoma ibaki na hadhi yake ya makao makuu ya nchi na serikali.

tutapunguza sana matumizi ya serikali na tutaongeza ufanisi sana wa utandaji wa serikali.Wakurugenzi wabaki kama walivyo, awepo tu mkurugenzi mkuu wa jimbo na wakurugenzi wachini yake katika maeneo ambayo yalikua mikoa.
Kabisa mkuu
 
Huwa najiuliza, viongozi wa hii nchi wana akili timamu kweli? Yaani wanajua kabisa raia wao wengi hawana elimu na wamejirundika Dar es Salaam kwa ajili ya jina. Kwanini wasiifanye wilaya ya Kibaha kuwa ndani ya Dar es Salaam ili watu wasambae kujenga huko?

Maana naona kutoka Kibaha mpaka Mbezi Magufuli ni karibu kuliko kutoka Kariakoo mpaka Mbezi Magufuli, ambapo ndio kituo kikubwa cha mabasi Tanzania. Aisee, Bora i Dar es Salaam ipanuliwe kwa kuchukua ardhi ya Kibaha, maana hata daladala zinapandisha nauli kila siku kwa kigezo cha Kibaha kuwa mkoa mwingine, wakati unakuta umbali ni mdogo.
Baada ya hapo, Morogoro pia itakuwa jirani na Dar, hivyo Moro ihamishiwe Dar. Kisha, Dodoma itakuwa jirani na Dar, nayo Dodoma ihamishiwe Dar, hivyo hivyo, Singida, Iringa na kwingineko.

Kwa lugha rahisi, Tanzania/Afrika yote iitwe "Daslam"
 
Wewe kibaha iliwahi kuwa ndani ya dar ndio maana nasema hivyo Sasa huko morogoro lini ilowahi kutambulika ndani ya dar
 
Hoja yako ni ukaribu... Na umesema, "Kwanini wasiifanye wilaya ya Kibaha kuwa ndani ya Dar es Salaam ili watu wasambae kujenga huko?" Hoja yako hujaijenga vizuri...
 
Tufanye haitowezekana basi Ili ufurahi maana umekuja kupinga Sina mda wa kubishana
 
Huwa najiuliza, viongozi wa hii nchi wana akili timamu kweli? Yaani wanajua kabisa raia wao wengi hawana elimu na wamejirundika Dar es Salaam kwa ajili ya jina. Kwanini wasiifanye wilaya ya Kibaha kuwa ndani ya Dar es Salaam sababu ilishawahi kuwa ndani ya dar es salaam ili watu wasambae kujenga huko?

Maana naona kutoka Kibaha mpaka Mbezi Magufuli ni karibu kuliko kutoka Kariakoo mpaka Mbezi Magufuli, ambapo ndio kituo kikubwa cha mabasi Tanzania. Aisee, Bora i Dar es Salaam ipanuliwe kwa kuchukua ardhi ya Kibaha, maana hata daladala zinapandisha nauli kila siku kwa kigezo cha Kibaha kuwa mkoa mwingine, wakati unakuta umbali ni mdogo.
Kwani kinachowazuia watu kujenga kibaha ni Kwa kua kibaha haiko dar?,hoja Yako Haina mashiko kwaiyo hata Tunduma iwe Zambia sababu ni karibu na Zambia au horohoro iwe Kenya sababu ya ukaribu na Kenya?
 
Back
Top Bottom