Hivi Kiongozi anaepeleka mtoto wake Shule ya Milioni 10 atatoa Mawazo Gani ya Maana ya kuendeleza shule za Serikali?

Katika pitapita zangu nimekutana na video ya Anthon Mtaka akizungumza kuhusu Elimu, hii hapa chini View attachment 2289897
Nikaona kaongea ukweli fulani ,Hivi wana JF ,mtu ambae hajawahi somesha mtoto shule ya serikali hasa ya kata anawezaje akawa na mipango ya maana kuhusu hizi shule?
Hizi ni aina ya hotuba ya viongozi waliosimama katika ukweli
 
Shule sio kufaulu tu ni pamoja na networking na connection. Wewe kasome kanumba na wa Feza wako tofauti wakianza maisha mtaani.Mwenzio for that 11m akitoka pale ananetwork ya walala hoi wenzie na sio choka mbaya ni mtazamo wangu tu
 
Wajinga ndiyo waliwao na msingi wa utumwa umejengeka kichwani mwa mtumwa mwenyewe.
Mtu ambaye shule hazimhusu (watoto wake hawasomi huko) hawezi kujali hata kidogo.
Yawapasa wananchi kujua hilo, vinginevyo uhuru hauna maana kwa kuwa hawajiamulii mambo yao wenyewe.
Shule ziboreshwe ili watoto wa mawaziri wasome humo humo.
Waziri ambaye watoto wake wanasoma shule za serikali, atajitahidi kuziboresha kwa kuwa zinamhusu.
 
Katika pitapita zangu nimekutana na video ya Anthon Mtaka akizungumza kuhusu Elimu, hii hapa chini View attachment 2289897
Nikaona kaongea ukweli fulani ,Hivi wana JF ,mtu ambae hajawahi somesha mtoto shule ya serikali hasa ya kata anawezaje akawa na mipango ya maana kuhusu hizi shule?
Kiongozi wa namna hii siku zote huitwa "mnafiki" na kamwe hawezi kuwa na mawazo yenye tija na yenye matokeo endelevu..!

Kwa sababu ni ngumu sana kumwelewa na kukubaliana na kiongozi anayetoa mawazo fulani ili yazingatiwe na kutendwa na watu ili hali yeye mwenyewe hayaishi hayo anayotaka wengine watende!!

Zamani zile za Biblia ya kale, hizi ndo zilikuwaga za wale viongozi maarufu wa zama hizo waliokuwa wanajulikana kama "waandishi" na "mafarisayo". Hawa walikuwa wanawahimiza wanawaongoza kufanya mambo ambayo wao wenyewe walikuwa hawawezi kufanya...

Yesu Kristo aliwachana chanaga hawa LIVE bila chenga, kwani walikuwaga wakihubiri haki lakini wao wenyewe na haki ilikuwa ni mbalimbali kabisa kama ilivyo mashariki na magharibi...!

Yesu Kristo aliwaita viongozi wa dizaini hili kwa jina la "vwanafiki" kwani waliwabebesha wananchi mizigo mizito ambayo hata wao wasingeweza kuibeba kwenye mabega yao kisha wakastahimili kutembea japo kwa hatua chache tu mbele yao..

Leo hii, hawa hawa kina Samia, Mwigulu Nchemba, Januari Makamba na wenzao top seeds huko serikali ndiyo waandishi na mafarisayo wetu leo...!

Ni tozo, tozo na kodi kandamizi kwa kwenda mbele ili wao kutoka humo wapate mapesa kupeleka watoto na ndugu zao kwenye shule za ada ya 10m, 20m na hata 45m...!

Hawa ni Wanafiki watupu hakika...!!
 
Kusomesha mtoto mahela mengi siyo ubora wa elimu ni ulimbukeni tu na kutaka kujenga social classes hakuna kingine. Ktk matokeo ya form six mwaka huu miongoni mwa shule kumi bora zipo shule za kata mfano Ziba Sekondari iliyoko Mkoa wa Tabora Wilaya ya Igunga, Dareda Sekondari iliyoko Mkoa wa Manyara Wilaya ya Babati.

Wakifika Vyuo vikuu wale waliosoma shule za gharama kubwa wanapigwa mbaya sana na wale waliotoka shule za serikali tena mnazoita za kata. Mi nachoomba serikali mboreshe shule zetu za serikali waache wajinga wachezee pesa zao sana sana wataambulia kujua zaidi lugha ya wakoloni.

..shule ya kata ina sifa zake, na moja wapo ni mazingira mabaya kwa waalimu na wanafunzi.

..shule ambazo umezitaja kuwa ni za kata na zimeshika nafasi za juu kitaifa maana yake ni kuwa zilishajikomboa / kombolewa toka kundi la shule za kata.

..uwezekano mkubwa ni kwamba shule hizo ziliboreshwa kwa kupewa miuondombinu mizuri, vifaa, na waalimu wa kutosha, ndio maana zimeweza kupata matokeo mazuri.

..shule yoyote ile ukiipatia waalimu wazuri wa kutosha, vifaa, miundombinu, na ukasisitiza nidhamu, lazima utapata matokeo mazuri.
 
Katika pitapita zangu nimekutana na video ya Anthon Mtaka akizungumza kuhusu Elimu, hii hapa chini View attachment 2289897
Nikaona kaongea ukweli fulani ,Hivi wana JF ,mtu ambae hajawahi somesha mtoto shule ya serikali hasa ya kata anawezaje akawa na mipango ya maana kuhusu hizi shule?
Na huyu jamaa baada ya hotuba hiyo alishambuliwa sana kwa kusema ukweli huu!

Bahati yake bado yupo kama Mkuu wa Mkoa!
 
Shule sio kufaulu tu ni pamoja na networking na connection. Wewe kasome kanumba na wa Feza wako tofauti wakianza maisha mtaani.Mwenzio for that 11m akitoka pale ananetwork ya walala hoi wenzie na sio choka mbaya ni mtazamo wangu tu
Pointi ya msingi ndiyo hiyo mkuu UPOPO Why, viongozi wetu wenye akili timamu, wanaamua kuwafanya mazuzu-maji Watanzania zaidi ya milioni 60?

Imagine wanasifu kwenye vyombo vya habari day in and day out kwamba elimu hakuna kulipa ada, at the same time tunashuhudia wao wakilipa millions kuwasomesha watoto wao!

Hakuna tusi kubwa kuliko hilo siasani! The fact that they afford to pay millions worth of money yearly in order to secure such an expensive, exclusive, partial education, despite having free government schools is very telling at best, and mostly threatening, at worst.

Solution: Education has to be declared one of the basic commodities which every citizen is entitled to. Then standardize the affordability.

Do our leaders know where sustainable development really come from? Viongozi wetu, the way wanavyolichukulia suala la elimu, ni sawa na mkulima aliye mikono mitupu.

Au tumeshauzwa tayari? Usikute ule ubashiri wa Job Ndugai ulishagatimia siku nyingi kitambo huko!
 
Nyerere alisema vyema kwamba nchi yetu inakabiliwa na maadui ^war-tar-two:^ UJINGA, MARADHI, na UMASKINI. Ujinga ni mama na baba yao, maradhi ni watoto wake identical twins!)
Dah!

Hii imekaa vizuri sana:
"Nchi yetu inakabiliwa na maadui watatu: Ujinga, maradhi na umaskini; UJINGA ni mama na baba wa maradhi na umaskini ambao ni watoto pacha 'identical twins.'"

Sasa hivi UJINGA umerudi kwa kasi sana, kwa hiyo watoto mapacha wanaongezeka kwa kasi kubwa.
Na watawala wanaipenda sana hali hii.
 
Wajinga ndiyo waliwao na msingi wa utumwa umejengeka kichwani mwa mtumwa mwenyewe.
Mtu ambaye shule hazimhusu (watoto wake hawasomi huko) hawezi kujali hata kidogo.
Yawapasa wananchi kujua hilo, vinginevyo uhuru hauna maana kwa kuwa hawajiamulii mambo yao wenyewe.
Shule ziboreshwe ili watoto wa mawaziri wasome humo humo.
Waziri ambaye watoto wake wanasoma shule za serikali, atajitahidi kuziboresha kwa kuwa zinamhusu.
Uko vizuri
 
Katika pitapita zangu nimekutana na video ya Anthon Mtaka akizungumza kuhusu Elimu, hii hapa chini View attachment 2289897
Nikaona kaongea ukweli fulani ,Hivi wana JF ,mtu ambae hajawahi somesha mtoto shule ya serikali hasa ya kata anawezaje akawa na mipango ya maana kuhusu hizi shule?
Wanasiasa na wasomi wenye maamuzi wa Tanzania, wengi ni useless! Wanahubiri elimu bure, ila watoto wao wanawapeleka shule za mamilioni! Yaani wanatuona kama hatuna akili vile.

Siku ikitungwa sheria rasmi ya watoto wa viongozi wa kisiasa, na wale wa kiserikali kusoma shule za serikali, na hasa kutoka darasa la 1 mpaka kidato cha 4! Naamini elimu yetu itakuwa bora kwa wote. Ila kwa sasa, naona tunadanganyana tu
 
Kusomesha vizuri na kusomesha vibaya kupoje?

Umaanisha kwamba shule zisizotoza ada (serikali) zina elimu duni na zile zinazotoza ada kubwa zina elimu bora?

Kumbe hujui? Elimu bora siku hizi ni ghali sana dunia nzima. Shule za serikali hazina hela ya kushindana na shule zinazokusanya ada kubwa.
 
Ningependa kujua upande wa pili, yani kusomesha vibaya. Halafu mimi, nita 'correlate' na hiyo video hapo juu.

Shule inayokosa vyombo vya maabara vya kisasa, kompyuta, vitabu vya kutosha, mambo ya ziada (extracurricular) naweza kusema kwa dunia ya leo inasomesha vibaya.
 
Tunaishi kwenye zama za ubepari
Usipopambania watoto wako utajua mwenyewe
Acheni kutumia akili za wanasiasa tumieni akili zenu wenyewe
 
Back
Top Bottom