Mbunge Nancy Nyalusi achangia Milioni 10 ujenzi wa zahanati Kilolo

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,903
945

MBUNGE NANCY NYALUSI ACHANGIA MILIONI 10 UJENZI WA ZAHANATI KUPUNGUZA VIFO VYA MAMA NA MTOTO KILOLO

MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa Mhe. Nancy Nyalusi ameshiriki zoezi la ujenzi wa jengo la huduma ya Mama na Mtoto kwenye Zahanati ya Kijiji cha Kimala kata ya Kimala katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo ambapo pia ametoa fedha Shilingi Milioni 10 kwenye ujenzi huo kama sehemu ya mchango wake binafsi kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya 6 katika kukabiliana na changamoto ya vifo vinavyotokana na uzazi kwenye Kijiji hicho na maeneo ya jirani.

Mhe. Nyalusi amefanya hayo katika ziara ya kibunge ambayo imefanywa kwa ushirikiano kati yake na Mbunge wa Jimbo la Kilolo Mhe. Justine Nyamoga katika kata ya Kimala wilayani Kilolo.

Akizungumza mara baada ya zoezi hilo la ujenzi wa jengo hilo la Mama na Mtoto, Mhe. Mbunge Nancy Nyalusi amesema binafsi amegusa na kadhia ya kutembea umbali mrefu kufuatakukosekana kwa huduma ya Mama na Mtoto wanayopitia wananchi wa Kijiji cha Kimala na maeneo ya jirani na hivyo kufikia uamuzi wa kutoa kiasi hicho cha fedha ili kusaidia kukamilisha ujenzi huo.

“Kiukweli huku Kilolo ni nyumbani na niliposikia juu ya changamoto ya huduma ya Mama na Mtoto niliguswa na nikaona nina wajibu wa kuwa mstari wa mbele kama mwanamke na kama kiongozi kutoa mchango wangu wa hali na mali ili kubioresha utoaji wa huduma za afya hasa katika eneo la Mama na Mtoto”-Amesema Mhe. Mbunge Nyalusi.

Mhe. Nyalusi, amesema ni wakati muafaka kwa watu binafsi na taasisi mbalimbali kuunga mkono juhudi za Serikali kwenye kukabiliana na changamoto mbalimbali ambazo zimekuwa katika jamii kwani tayari Serikali kwa upande wake imeonyesha dhamira ya dhati na utayari mkubwa kwenye juhudi hizo.

Aidha Mhe. Nyalusi amesema ofisi yake itaendelea kushiriki kikamilifu kwenye utatuzi wa changamoto mbalimbali katika jamii ya watu wa mkoa wa Iringa kwani kwa kufanya hivyo anakuwa ameonyesha kwa vitendo dhamira yake kwenye kuifanya jamii ya waTanzania kuwa jamii bora.

Katika hatua nyingine Mbunge Mhe. Nyalusi ametoa kiasi cha Shilingi Laki Mbili kwa uongozi wa Shule ya Sekondari J. Nyamoga iliyopo Kijiji cha Kimala kata ya Kimala ili zisaidie kununua vitu vidogovidogo kama vile chaki kwa ajili ya walimu kufundishia.

Serikali imeendelea kutoa kipaumbele katika huduma za afya zenye ubora na zinazowafikia wananchi wote ili kuboresha afya zao.

Serikali inatambua umuhimu wa afya bora kwa wananchi wake kwani afya bora ni raslimali muhimu kwa maendeleo. Maendeleo ya Taifa letu la Tanzania yataletwa na wananchi wenye afya na wenye uwezo wa kuzalisha mali.

Katika kuhakikisha kuwa wananchi wana afya bora, Serikali imeendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kutoa huduma za afya kwa kuzingatia sera na miongozo iliyopo.

#KaziIendelee
#KiloloYaSamia
#IringaYaSamia
#TanzaniaYaSamia

WhatsApp Image 2023-07-20 at 13.44.15.jpeg
WhatsApp Image 2023-07-20 at 13.42.38.jpeg
WhatsApp Image 2023-07-20 at 13.40.21.jpeg
WhatsApp Image 2023-07-20 at 13.39.41.jpeg
WhatsApp Image 2023-07-20 at 13.39.16(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-07-20 at 13.39.16.jpeg
 
Back
Top Bottom