Hivi, jirani kwanini hununui gari?

Waswahili wanasema "Cha mtu mavi". Uso umeumbwa na haya, hata kabla ya jirani kukuambia hilo uliona au ulitakiwa kuona alama kwamba hutakiwi kuwa tegemezi hivyo.

Wabongo wengi tunapenda dezo sana. Tunakuwa mzigo. Nilichogundua ni kwamba hizi habari za "carpooling" zipo hata nchi zilizoendelea, kwa sababu si kila mtu ana gari, au hata kama kila mtu ana gari mara nyingine inakuwa hai-make sense watu wawili mnaenda ofisi moja na kukaa mtaa mmoja mchukue magari mawili, kwa hiyo mnaamua kuchukua gari moja. Lakini wenzetu wanaogopa sana vya bure. Kuitwa "freeloader" ni tusi kubwa sana. Kwa hiyo mara nyingi unakuta watu wana "chip in" mtu hata kama hana gari, anatoa hata hela ya mafuta.

Sina hakika kama ulikuwa ukitoa hata hela ya mafuta, lakini uzoefu wangu na lifti za kibongo sijaona mtu kuchangia hela ya mafuta hata ndogo tu ya "token gesture".

Unaweza kumlaumu mwenye gari kwa kuwa blunt, lakini mara nyingine uwazi ndio unatakiwa zaidi. Sasa hapo mtu kapewa challenge ajitegemee.

Ndiyo maana nasema "Ujamaa na Kujitegemea" umetuharibu.
 
tatizo ulikuwa ukipanda unakaa mbele alafu unaanza kubadili redio station mara wafu fm, mara kiss fm wakati mwenzio kajiwekea redio tanzania anasiliza kipindi cha jambo, akahisi siku nyingine utapiga honi
 
Hii mada pia ni ya hapa MMU!!! Anyway, kwa kuwa umeposti hapa ngoja tuchangie! Kwa kifupi jamaa inaonekana kachoshwa na tabia yako ya kuomba lifti, so anauliza indirectly kukupa meseji tu kuwa kachoka.

Kimtazamo si tabia njema aliyoionyesha, maana kila mtu ana priorities zake katika maisha na pia kununua gari kunategemea na other factors ukiacha hizo priorities kama uwezo nk.


Ni vizuri kupanda kidala dala na kuachana na lifti yake, itakutesa kisaikolojia.

'Hivi jirani kwa nini hununui gari?' Aisee hi kali sana,yaani kila nikikaa maneno yananijia .. kama nakuona vile ila jamani tuacheni utani yaani kuna watu wengine bana wamezidi yaani unatoka tu home jamaa unamkuta nje anajidai anaibuka eti kama vile ndio katokea... unatoka ofisini huyu hapa... daa.... nadhani hapa lazima siku aulizwe tu.... 'Hivi jirani kwa nini hununui gari?'
 
Ungejibu swala la kununua gari lipo kwenye mchakato na ninayo furaha kukuarifu wafadhili washapatikana.
 
Ndiyo maana mimi nilishamkatalia wife lift, niliwahi kukaa na washikaji zangu fulani wakaanza kumsema mshikaji kwamba anapenda lift, mimi ni mgeni tu maeneo haya nilivyojua hayo nikamwambia wife hakuna kuomba lift hata wakikuta njiani wambie bado upoupo kwanza wala hutapungukiwa na kitu ukipanda daladala na wanaona maisha yanaenda bomba kabisa. Uswahilin bwana kuna mambo acha tu
 
Ndiyo, nunua gari lako, jamaa kajipinda kavuta chombo halafu design hata pesa ya mafuta haumchangiagi, vuta Chombo na wewe mkuu!!
 
Sasa mkuu umepangaje kwaanzia kesho??

Itabidi uwe unawahi sana kuondoka au uchelewe wakati jamaa kishasepa zake....

Na je akikukuta njiani kabla hujachukua daladala utamtolea nje??

huyo jamaa yako ni mshamba sana, inabidi umuonyeshe umasikini jeuri tu!

Nilikuwa nadoea lift ya jamaa yupo na mke wake asubuhi, uh nilipanda siku mbili tu baada ya hapo nikaona isiwe shida bwana, wakawa wakinikuta nakataa hivihivi macho makavu "nitaenda na daladala"
 
jamani leo naona jirani yangu niliyezoea kumuomba 'lift',
nadhani huenda baada ya 'kunichoka' kutokana na katabia
kangu ka kumuomba lifti wakati wa kwenda kazini.

Huenda aliamua kunitolea uvivu, au pengine nilikuwa namboa, au pengine
kwa mtazamo wake, anadhani ninao uwezo au labda ni ubahili
wangu.......hata sijui why....ila kifupi mara baada ya kupanda, akionekana
hana furaha, neno lake la kwanza likawa 'hivi jirani kwa nini hununui
gari likusaidie usafiri wa kwenda na kurudi ofisini? Abiria wengine wawili walokuwa
ndani ya gari walibaki kuangaliana tu, maana nao kama wasaidiwa
huenda walihis hilo 'dongo' linawahusu pia

kwa kuhisi huenda jamaa kanichoka, nililoweza kufanya ni
kuguna tu, mhhhhhh bila kujibu kitu huku nikiwa na aibu tele usoni.
Baada ya kwenda kama mita 70 hivi, nikajidai nimesahau simu na kumuomba jamaa
anishushe niirudie simu yangu nyumbani. Baada ya kushuka
nikapanda zangu daladala na kuelekea job.

Hapa kazini hii stori imekuwa gumzo kwani abiria wale wengine waliifikisha
hii skendo ofisini na imekuwa gumzo la siku. Kila mtu 'ananitania' kwa kurudia
kauli ya mshikaji, 'hivi jirani kwa nini hununui gari'? Nabaki nacheka tu hapa
ofisini!

hapo kaka inabidi ujipange upate kausafiri chako,hata siku ukikutana nae bahati mbaya utajisia upweke sana kupanda kwenye usafiri wake.
 
Pole sana, yawezekana kakuambia hivyo ama amekuchoka kwa kuomba lift kwa muda mrefu, au kwa nia nzuri ya kuona unapata taabu wakati uwezo wa kununua unao.

Wapo walioamua kununua mfano TV baada ya kuona watoto wao wanapigwa makonzi wanapoenda kuangalia tamthilia kwa majirani.

Kwako iwe ni changamoto, baada ya kumaliza ujenzi nunua hata gari kama ya Mr. Bean uepukane na hayo mambo.
 
siyo kwenu tu hata kwetu wapo,
kuanzia leo usipande lift ya mtu yeyote
jitaabishe kwanza,
omba MUNGU na wewe siku moja utakuwa na magari.

na siku akipata shida asaidiwe na gari lake.
 
kakuambia jambo jema nawe tia hasira ununue lako
kuna watu kweli hata wakipewa lifti hata viatu hawakunguti mchanga unakuta umejpinda asbh au mke kaamka mapema kasafisha gari la mumewe na kutoa michanga watu wengine kazi yao lift za kila siku na kujaza michanga.hata mm iliniboa sana hii kitu
naona ulimboa labda kwa hilo.
 
Huenda labda nina makengeza, lakini hiyo bold naona kama ulikuwa unaomba lifti kila siku na ndio maana kakuchoka au..................!?

Najaribu kutafuta maneno kila siku, bado siyaoni. Ngoja nifuate darubini.............agrrrrrrrrrrrr na jamaa sijui bado wako kwenye mgomo wao?
 
... kumuomba 'lift',
nadhani huenda baada ya 'kunichoka' kutokana na katabia
kangu ka kumuomba lifti wakati wa kwenda kazini...[/
QUOTE]

Mkuu hapa wewe mwenyewe umefanya watu waamini kila siku unaomba lift, by the way unaomba wala husubiri kupewa. Namna umeeleza katabia kako kalivyo na kwamba ni wakati wa kwenda kazini tunaamini unakwenda kila siku ya kazi hivyo ni jambo linalotokea kila mara

tuseme niliomba kwa siku 6 kwa nyakati tofauti wakati wa kwenda kazini, hapo ulitaka niseme wakati wa kwenda sokoni, au?
 
i bado na-question nilikosema hayo maneno 'kila siku' bado nayatafuta. Ninachoona watu wanaongea kwa hisia zaidi kuliko uhalisia
 
Sasa mkuu umepangaje kwaanzia kesho??

Itabidi uwe unawahi sana kuondoka au uchelewe wakati jamaa kishasepa zake....

Na je akikukuta njiani kabla hujachukua daladala utamtolea nje??

huyo jamaa yako ni mshamba sana, inabidi umuonyeshe umasikini jeuri tu!

Nilikuwa nadoea lift ya jamaa yupo na mke wake asubuhi, uh nilipanda siku mbili tu baada ya hapo nikaona isiwe shida bwana, wakawa wakinikuta nakataa hivihivi macho makavu "nitaenda na daladala"

hiyo ya kukutwa stendi simpo, namwambia tu namsubiri mtu anakuja nchukua
 
'Hivi jirani kwa nini hununui gari?' Aisee hi kali sana,yaani kila nikikaa maneno yananijia .. kama nakuona vile ila jamani tuacheni utani yaani kuna watu wengine bana wamezidi yaani unatoka tu home jamaa unamkuta nje anajidai anaibuka eti kama vile ndio katokea... unatoka ofisini huyu hapa... daa.... nadhani hapa lazima siku aulizwe tu.... 'Hivi jirani kwa nini hununui gari?'

haya bwana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom