Mtegee misumari anapotoka kwake au mahali anapokuoea lift halafu usipande yeye na wapambe wake uwapite njiani uwahi ofisini kuwaonyesha hata yeye anahitaji msaada kwani atazikwa nalo
vidole vya mkono havilingani na si wote tutakufa siku moja ww msubiri tu atajileta
Jamani leo naona jirani yangu niliyezoea kumuomba 'lift',
nadhani huenda baada ya 'kunichoka' kutokana na katabia
kangu ka kumuomba lifti wakati wa kwenda kazini.
Huenda aliamua kunitolea uvivu, au pengine nilikuwa namboa, au pengine
kwa mtazamo wake, anadhani ninao uwezo au labda ni ubahili
wangu.......hata sijui why....ila kifupi mara baada ya kupanda, akionekana
hana furaha, neno lake la kwanza likawa 'Hivi jirani kwa nini hununui
gari likusaidie usafiri wa kwenda na kurudi ofisini? Abiria wengine wawili walokuwa
ndani ya gari walibaki kuangaliana tu, maana nao kama wasaidiwa
huenda walihis hilo 'dongo' linawahusu pia
Kwa kuhisi huenda jamaa kanichoka, nililoweza kufanya ni
kuguna tu, mhhhhhh bila kujibu kitu huku nikiwa na aibu tele usoni.
Baada ya kwenda kama mita 70 hivi, nikajidai nimesahau simu na kumuomba jamaa
anishushe niirudie simu yangu nyumbani. Baada ya kushuka
nikapanda zangu daladala na kuelekea job.
Hapa kazini hii stori imekuwa gumzo kwani abiria wale wengine waliifikisha
hii skendo ofisini na imekuwa gumzo la siku. Kila mtu 'ananitania' kwa kurudia
kauli ya mshikaji, 'Hivi jirani kwa nini hununui gari'? Nabaki nacheka tu hapa
ofisini!
Gharama za kutunza au kuwa na gari.1. Ununuzi (capital tied up)2.Bima3. motor vehicle licence4. service ya kila mara5. Ununuzi wa matairi6. ununuzi wa vipuri7. mafuta ya gari8. gharama za maegesho9. n.kJe wewe unamsaidiaje mwenzako katika gharama hizi?Ungekuwa muungwana unajaza hata mafuta ya wiki moja kwa mwezi angekuwa anakupitia nyumbani kwako mwondoke.Acha kupendelea KITONGA ( MITEREMKO)
wako watu wanadai gari sio muhimu bora kujenga nyumba, ukiwa unakaa nyumba ya kupanga ukanunua gari wanakuona mwehu tu, sasa mvua ikinyesha unapandisha vioo hadi juu , walewale walio kucheka wananuna na kukuona una roho mbaya , si wapande nyumba zao sasa.
kakuambia jambo jema nawe tia hasira ununue lako
kuna watu kweli hata wakipewa lifti hata viatu hawakunguti mchanga unakuta umejpinda asbh au mke kaamka mapema kasafisha gari la mumewe na kutoa michanga watu wengine kazi yao lift za kila siku na kujaza michanga.hata mm iliniboa sana hii kitu
naona ulimboa labda kwa hilo.
Hahaha! Lazima angemtolea kwa dirishani lol!Wewe ungemchefua na wewe;sijaona umuhimu wa gari sasa hivi na mambo mengi muhimu ya kufanya kwanza.Halafu ndo ungeona