Wengine hawapendi kutoa lift kwa kuwa mara nyingine wanahitaji privacy. Kuna jirani yangu mmoja mara nyingi hupenda lift wakati wa kutoka kazini; atapiga simu na kuuliza: "unaondoka saa ngapi mkuu?". Sasa shida ni kwamba mara nyingi mie nina mizunguko yangu, ikiwemo ya nyumba ndogo, kwa hiyo inakuwa ngumu kufuatana na mtu kwenye mambo yako private. Ukimwambia nitachelewa leo, anasema naye atachelewa kwa hiyo umshitue wakati wa kuondoka. Mambo gani haya? Mimi nadhani kama kuna watu wanaona kununua gari sio muhimu basi wawe tayari kupanda daladala.