Hivi, jirani kwanini hununui gari? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi, jirani kwanini hununui gari?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by ndyoko, Feb 22, 2012.

 1. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #1
  Feb 22, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  Jamani leo naona jirani yangu niliyezoea kumuomba 'lift',
  nadhani huenda baada ya 'kunichoka' kutokana na katabia
  kangu ka kumuomba lifti wakati wa kwenda kazini.

  Huenda aliamua kunitolea uvivu, au pengine nilikuwa namboa, au pengine
  kwa mtazamo wake, anadhani ninao uwezo au labda ni ubahili
  wangu.......hata sijui why....ila kifupi mara baada ya kupanda, akionekana
  hana furaha, neno lake la kwanza likawa 'Hivi jirani kwa nini hununui
  gari likusaidie usafiri wa kwenda na kurudi ofisini? Abiria wengine wawili walokuwa
  ndani ya gari walibaki kuangaliana tu, maana nao kama wasaidiwa
  huenda walihis hilo 'dongo' linawahusu pia

  Kwa kuhisi huenda jamaa kanichoka, nililoweza kufanya ni
  kuguna tu, mhhhhhh bila kujibu kitu huku nikiwa na aibu tele usoni.
  Baada ya kwenda kama mita 70 hivi, nikajidai nimesahau simu na kumuomba jamaa
  anishushe niirudie simu yangu nyumbani. Baada ya kushuka
  nikapanda zangu daladala na kuelekea job.

  Hapa kazini hii stori imekuwa gumzo kwani abiria wale wengine waliifikisha
  hii skendo ofisini na imekuwa gumzo la siku. Kila mtu 'ananitania' kwa kurudia
  kauli ya mshikaji, 'Hivi jirani kwa nini hununui gari'? Nabaki nacheka tu hapa
  ofisini!
   
 2. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #2
  Feb 22, 2012
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 476
  Trophy Points: 180
  Ila swali linabaki pale pale ''hivi jirani kwa nini hununui gari''?? au mipango haijakaa sawa kwasasa??
   
 3. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #3
  Feb 22, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Hata kavitz kanakushinda?
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Feb 22, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Gari siyo hitaji la lazima!
  Msicomplicate maisha kiasi hiki jamani!...mtachochea hata ujambasi mitaani, kisa VITZ!
   
 5. Asabaya

  Asabaya JF-Expert Member

  #5
  Feb 22, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 1,317
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Mwenzangu mtu atakupa lift siku moja imezidi tatu sio kila siku bora ununue yako,siunajua nguo yakuazima haistiri mwili.
   
 6. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #6
  Feb 22, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Mkuu ndyoko,

  Duh mkuu nimebaki nacheka tu vipi unaishi mitaa ipi ?.
   
 7. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #7
  Feb 22, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Jirani yako mtu mzuri anakupenda sana.
   
 8. Twilumba

  Twilumba JF-Expert Member

  #8
  Feb 22, 2012
  Joined: Dec 5, 2010
  Messages: 6,148
  Likes Received: 878
  Trophy Points: 280
  Aisee kwa kweli ni dalili ya kushoshwa na kuomba kwako lift,
  Lakini huyo nae anadhani gari ni kipaumbele kwa kila mmoja,
  Naamini ni limbukeni wa magari maana hata kama angekupa lift mwaka mzima bado alitakiwa kujua kuwa kila kitu kinafanyika kwa mipango.

  Kwa kifupi huyo bwana amekosa Busara na zaidi inawezekana hana maarifa.
  Pole sana Mkuu.
   
 9. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #9
  Feb 22, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Ndyoko kumbe twafanya ofisi moja, Aisee bonge la sooo
   
 10. obsesd

  obsesd JF-Expert Member

  #10
  Feb 22, 2012
  Joined: Nov 23, 2011
  Messages: 1,226
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  uwiiiii! jirani kweli kakuchoka mkuu!
  alikuwa nakuhesabia tu unavyocut down expenses zako hata wese huchangii teh!
  swali la ziada, umepanda io lift kwa muda gan mkuu?? hehehe usiniambie mwaka duuh!
   
 11. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #11
  Feb 22, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,227
  Trophy Points: 280
  huwezi kununua gari kwa sababu tu jirani amesema, ila pale mambo yako yatakapokaa shwari...

  pia kutokuwa na gari haina maana daily unadandia lifti, mtu akose hata privacy, kama ana kinyumba ndogo chake ashindwe kukipitia kuogopa jirani atamuona.

  au unaishi nyumba ya kupanga ya bei ghalii? ndo maana jirani kashangaa unalipa kodi kubwa halafu kutwa kwenye magari ya watu?

  ila chukulia hiyo kama challange...
  jipange
   
 12. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #12
  Feb 22, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,470
  Likes Received: 5,847
  Trophy Points: 280
  Yaani watu wa ofisi moja mko mtaa mmoja pia?......na wote hamna gari?..hiyo ofisi yenu hiyo
   
 13. g

  gongolamboto JF-Expert Member

  #13
  Feb 22, 2012
  Joined: Feb 21, 2011
  Messages: 509
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 45
  Huyo ni jirani mwema sana. Kama gari siyo hitaji muhimu hukuwa na haja ya kuomba lift.
   
 14. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #14
  Feb 22, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Hii mada pia ni ya hapa MMU!!! Anyway, kwa kuwa umeposti hapa ngoja tuchangie! Kwa kifupi jamaa inaonekana kachoshwa na tabia yako ya kuomba lifti, so anauliza indirectly kukupa meseji tu kuwa kachoka.

  Kimtazamo si tabia njema aliyoionyesha, maana kila mtu ana priorities zake katika maisha na pia kununua gari kunategemea na other factors ukiacha hizo priorities kama uwezo nk.

  Ni vizuri kupanda kidala dala na kuachana na lifti yake, itakutesa kisaikolojia.
   
 15. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #15
  Feb 22, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  Kwa sasa najenga, hivyo nimeona ni vyema nijenge kwanza wakati huu ambao bado nakaa nyumba za bure za ofisi, then ikiisha niipangishe, then hela itakayotokana na kodi ya pango nichanganye na nyingine ndo ninunue gari. Unajua nini nisingependa mwanangu atakapo-join university mwakani basi hiyo kodi ya nyumba ndiyo itumike kumlipia tuition fees maana nataka asome kozi yenye future na sio ile atakayochaguliwa na TCU. Sipendi asome kwa mkopo wa HESLB.

  Kwa kuwa dodoma nyumba ya kupanga sasa si chini ya 350,000 kwa mwezi, nadhani kodi ya mwaka ya millioni 4, katoto kataweza kusomeshwa na kodi ya nyumba tofauti na kama nikinunua gari ambalo litakuwa linavyonza tu mfuko wangu.
   
 16. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #16
  Feb 22, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  Ujumbe ulifika the very moment ulipotolewa, na ndiyo maana nilishuka aisee. I felt humiliated to the maximum!
   
 17. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #17
  Feb 22, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,276
  Trophy Points: 280
  Kwani hii mada haiusiani na Urafiki? au MMU ni kwa ajili ya Mapenzi na Mahusiano tu?
   
 18. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #18
  Feb 22, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  bado sijajua why alitoa maneno yale.
   
 19. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #19
  Feb 22, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  miezi minne sasa. lakini sio kila siku, maana kuna wakati huwa napotezea ili nami niende kivyangu ofisini
   
 20. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #20
  Feb 22, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  asante mkuu
   
Loading...