Sasa kama unakubali kwamba uthibitisho hautanyi jambo kuwepo mbona mnasema hakuna uchawi kwa sababu hakuna uthibitisho?
Kudai kitu ni jambo moja ila kuweza kuthibitisha hicho unachodai ni jambo lengine, na ndio maana zipo tiba za mitishamba ambazo waafrika tunatumia kutibu maradhi mbalimbali ila hadi sasa hakuna uthibitisho wenye kuweza kuthibitisha ni kwa jinsi gani hiyo mitishamba ni kwa vp inatibu hayo maradhi, wenzetu pia wana wana tiba ambazo hazijathibitika kisayansi ila wanazitumia kama energy healing. Mfano Reiki, crystal healing, chakra healing, healing touch n.k
Nishawahi kutolea mfano kuhusu meditation nikasema sayansi imekuja kueleza faida za meditation kisayansi juzi tu ukilinganisha na hiyo meditation yenye watu wameanza kupractice thousands of years ago.