Hivi gesi yetu inayochimbwa Mtwara inatumika wapi?

Hivi gesi yetu inayochimbwa Mtwara inatumika wapi?

hako kajamaa ni ka zezeta mkuu kasikuumize kichwa kwanza angalia jina analotumia ni michosho


Mkuu utaumia bure kubishana na hawa tahira
Mkuu hvi ww ni wa nchi gani??

Tunalia mgao wa umeme na gesi tuko nayo ww una sema matahira...

Wewe Utakuwa ni mwafrika , na siyo mtanzania....watanzania hatuko ivo aisee...
 
"ya songosongo ndo inazalishwa tangu 2010"????000000

Mkuu hapo sija kuelewa aisee...km ilianza kuzalishwa muda huo,, ilisafirishwa kwa njia gani hadi dar??

Kwani mabomba yamekamilika 2015..sasa hyo 2010 au kulikuwa na means nyingine ya kusafirisha??

Afu songo songo iko mtwara??
Error, visiwa vya songo songo vipo chini ya mkoa wa lindi
 
Unajua mkuu, hujajibu maswali hapo juu...naona unaongea kisiasa na wakati ni masuala ya kitaalam.....

Hivi wakati wananchi wa mtwara wanapigwa sababu ilikuwa ni nini hasa??
Mbona unauliza swali la kizezeta sana we unataka wakutafunie then wakupige fimbo umeze
 
lindi kuna gesi ya visiwa vya songo songo na Mtwara ya offshore (baharini) huko Msimbati, ipo mtwara. Hii inayokuja Dar inatoka Songo songo


Unaelewa kuwa kuna mabomba mawili moja la 1998 toka songosongo na lingine hili la 2014 toka Mtwara? Hapa tunajadili hili la pili.
 
Nasubiri hili jibu chief maan mabomba yamelazwa mpaka Mtwara halafu gesi itoke Songosongo je, tangu gesi ianze kuchimbwa Songosongo imehamia Mtwara?
Kumbuka,ukiacha hiyo gesi ya Msimbati huko mtwara ambayo haijaanza kuchimbwa, pia kuna ya Mnazi bay huko huko mtwara, ambayo most likely inachangia kiwango kikubwa cha gesi inayokuja Dar
 
Shabushaaaaa kwahiyo ili bomba halina kazi yoyote from madimba to dar waje waling'oe tu tupme viwanja
Huki Mtwara kuna Mnazi bay gas fields ambazo nazo zinachangia kiasi kikubwa cha gesi inayokuja Dar, hivyo hilo bomba ni muhimu
 
Hapo kuna mawili, either bomba lililotoka Songo songo kuja Dar limechepushwa kuja Mtwara ili mradi wa Mtwara utakapokamilika litumike kuleta gesi dar, au inawezekana gesi ya Songo songo imeletwa Mtwaravkwa ajili ya kuzalisha umeme huko mtwara.
Mkuu nilijua ww unahakika na unacho changia hapa...kumbe unadhani..

N.way...tunashukuru kwa mawazo yako.
 
Transmission losses??? Power Plant ikiwa Dar, Mtwara wakaungwa kwenye grid, umeme utakuwa unawafikiaje? Hakutakuwa na transmission losses?
Transmission losses za kusafirisha umeme wa kuhudumia watu milioni 5 sio sawa na TL za kusafirisha umeme wa kuhudumia watu 50,000
 
Gesi ilyogunduliwa juzi juzi ya Mtwara bado haijaanza kuchimbwa, inaweza kuchukua hata miaka 10 kuanza kuchimbwa. Ile iliyogunduliwa miaka ya 1970 ya Songas ndio inayotumika Kinyerezi power plant na ubungo power plant kuzalisha umeme, pia imesambazwa baadhi ya viwanda jijini Dar. Na kwasasa umeme wa gesi unaozalishwa Ubungo na Kinyerezi I power plants bado hautoshi kwani mahitaji ya umeme yanaongezeka kwa kasi, na ndio maana serikali iko mbioni kukamilisha na kuwasha mitambo ya Kinyerezi II power plant ili kusaidia kupunguza uhaba, pia nadhani patakuwa na Kinyerezi III na Kinyerezi IV power plants zitafuata ili kuendelea kupambana na uhaba. Stiegler's gorge ndio baba lao kabisa, muwe waelewa na sio watu wa kulia lia kama kuku wanataka kutaga.
mbona wewe jamaa upo kila kona ile expansion joints bado hujajibu chochote umerudi kwenye umeme au bado capacity charges zimepata expansion joints ndo maana upo mgao ?
 
Nimeshawajibu kwa kirefu watu humu mara kadhaa na nimegundua watu wengi hawana taarifa juu ya gesi ya mtwara. Wengi wanafahamu kwamba kujengwa kwa lile bomba basi na ile hifadhi kubwa ya gesi kule ndani ya maji mtwara imekwishaanza zalishwa wasijue kwamba lile bomba linapitisha gesi ya madimba ambayo ni kiasi kidogo na imegunduliwa miaka mingi kabla ya hii ambayo wanasiasa waliiongelea sana hapo nyuma.
Lakini nafikiri ni tatizo la serikali yenyewe kutotoa taarifa ya kuwaelewesha wananchi.
Hivi unafahamu MADIMBA wanatoa gesi wapi?
 
Gesi inatumika, masaki ,mbezi, ikulu, huko,msoga, Yaani sehemu zote za kishua ,shangani hukoo Yaani sehemu kama izoo
 
Gesi ilyogunduliwa juzi juzi ya Mtwara bado haijaanza kuchimbwa, inaweza kuchukua hata miaka 10 kuanza kuchimbwa. Ile iliyogunduliwa miaka ya 1970 ya Songas ndio inayotumika Kinyerezi power plant na ubungo power plant kuzalisha umeme, pia imesambazwa baadhi ya viwanda jijini Dar. Na kwasasa umeme wa gesi unaozalishwa Ubungo na Kinyerezi I power plants bado hautoshi kwani mahitaji ya umeme yanaongezeka kwa kasi, na ndio maana serikali iko mbioni kukamilisha na kuwasha mitambo ya Kinyerezi II power plant ili kusaidia kupunguza uhaba, pia nadhani patakuwa na Kinyerezi III na Kinyerezi IV power plants zitafuata ili kuendelea kupambana na uhaba. Stiegler's gorge ndio baba lao kabisa, muwe waelewa na sio watu wa kulia lia kama kuku wanataka kutaga.
Muongo MKUBWA USIYE NA HAYA... Madimba gas plant wanapata wapi gesi yao?
Umeme wa mtwara unazalishwa kwa gesi gani?
Artumas wakati wapo hapa Tanzania, walikuwa wanafanya nini kama si kuchimba gesi ya Mtwara?
 
"ya songosongo ndo inazalishwa tangu 2010"????000000

Mkuu hapo sija kuelewa aisee...km ilianza kuzalishwa muda huo,, ilisafirishwa kwa njia gani hadi dar??

Kwani mabomba yamekamilika 2015..sasa hyo 2010 au kulikuwa na means nyingine ya kusafirisha??

Afu songo songo iko mtwara??
Visiwa vya Songo songo ni lindi sorry, kabla ya kujengwa kwa bomba kubwa la gesi kuja Kinyerezi Dar es salaam, kulikuwa na bomba lingine dogo lililokuwa limeshajengwa na Songas wenyewe kwenda Ubungo power plant ambako ndiko umeme wa Songas ubungo ukaanza kuzalishwa, hili bomba la juzi ambalo ni kubwa zaidi ndio la Kinyerezi, pia linachukua gas toka Mnazi bay mtwara
 
Sasa, viwanda vpo mtwara tu??

Huku tuliko tunadunduliza ili tufikshe mtaji wa viwanda vidogo, kukimbizana na lengo la kila mkoa viwanda 100,.. Sasa huu mgawo unatukata steam aisee..
Vibatari ndo vitatumika kendesha viwanda
Pia serikali mambo mengi inafafanua kisiasa....hawataki kuwaelimisha wananchi kiundani.
 
lindi kuna gesi ya visiwa vya songo songo na Mtwara ya offshore (baharini) huko Msimbati, ipo mtwara. Hii inayokuja Dar inatoka Songo songo. Ila pia inawezekana bomba hili limechepushwa kuja huko mtwarakwa ajili ya kuwasaidia kukuza na kuendeshea viwanda kama cha Dangote
We hujui lolote wewe kuhusu gesi ya Mtwara... Kule Mnazibay kuna visima vitano.. kimoja ndo mkinachopeleka gesi mtwara mjini kwa ajili ya umeme wa Mtwara na kwingineko... Visima vingine vinalisha plant ya serikali ya MADIMBA ambao wanapeleka DAR... usidanganye watu.. DAR WANAGESI TOKA MNAZIBAY (MTWARA) NA SONGOSONGO (LINDI)
 
Ninachokiona kwny huu mjadala ni kukosa taarifa sahihi na kukosa maarifa ya kupata taarifa sahihi.

Ni hivi, kuna gas reserves katika makundi matatu. Kundi la kwanza ni gesi iliyogunduliwa miaka ya 1970s/80s kwny kisiwa cha Songo Songo kilichopo Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi. Songo Songo haipo Mtwara. Mwaka 2004 gesi ya Songo Songo ilianza kutumika baada ya mitambo ya Songas iliyopo Ubungo kuanza kutumika. Hivyo, kuna mtambo wa kuchakata gesi Songo Songo unaomilikiwa na Songas pamoja na bomba la kusafirishia gesi toka kisiwani hadi Songas Ubungo kwenye mitambo ya kuzalisha umeme kwa kutumia gesi.

Aidha, kundi la pili ni reserve ya gesi iliyogunduliwa katika vijiji vya Mnazi Bay na Madimba mkoani Mtwara. Kampuni ya Artumas na baadae Maurel et Prom ilijenga mtambo mdogo wa kuchakata gesi katika kijiji cha Mnazi bay na bomba lenye urefu wa 27km miaka ya 2006. Gesi hiyo ndiyo inayotumika kuzalisha umeme kupitia mitambo ya Tanesco iliyopo Mtwara Manispaa na kusambaza umeme kwenye mikoa miwili ya Mtwara na Lindi.

Kundi la tatu ni gesi iliyogunduliwa kwenye kina kirefu cha bahari miaka ya 2010s. Ugunduzi wa gesi ya kina kirefu cha bahari ulifanyika yapata km 100 away from onshore. Pia, inakadiriwa kati ya km 2 - 3 chini ya bahari ndipo visima vyenye kina cha kati ya km 2-3 vimechimbwa.

Ukweli ni kwamba gesi ya kina kirefu haijaanza kuchimbwa, ambayo ndio nyingi. Kinachowachanganya wengi ni kwamba ugunduzi wa gesi kwny kina kirefu cha bahari ulienda sambamba na ujenzi wa bomba la inchi 36 kutoka Madimba hadi Kinyerezi. Gesi ambayo inasafirishwa kupitia bomba hili ni ile ya Mnazi Bay na Madimba. Kilichofanyika ilikuwa ni kuunganisha bomba kwny visima vya onshore vipya na vya zamani ili kufikisha gesi Kinyerezi.

Hivyo, kuna mabomba mawili yanayosafirisha gesi. Mosi, ni lile la kutoka Songo Songo hadi Ubungo (2004). Pili, ni lile linalotoka Madimba hadi Kinyerezi (2015).

Naweza kuwa nimesaidia kidogo kutoa ufafanuzi maana niliona watu wanachanganya mambo kwa kukosa taarifa sahihi/uelewa.

Nawasilisha.
 
Unaelewa kuwa kuna mabomba mawili moja la 1998 toka songosongo na lingine hili la 2014 toka Mtwara? Hapa tunajadili hili la pili.
Yes naelewa hilo la kwanza ni dogo na lilikuwa linaendesha mtambo wa Songas Ubungo,na hili la pili linalopeleka Kinyerezi.
 
Naomba nichangie kidogo huu mjadala mtamu.

Moja, 1974, serikali kupitia kampuni ya Agip/TPDC ndio waliogundua uwepo wa gesi katika visiwa vya Songo songo vilivyoko wilaya ya Kilwa. Kwa kuwa lengo lao lilikuwa mafuta, mpango ukaishia hapo. Kwa hesabu za wakati za wachumi, ikaonekana gesi iachwe kwanza.

Wakaenda Mtwara, kama sijakosea miaka 1980 hivi, pia wakapata gesi pale Msimbati, pia wakaacha kile kisima kwa kuwa Agip walilenga mafuta zaidi.

Mwaka 2003 mradi wa kuvuna gesi ya Songosongo ulianza, na mwaka 2004 kwa mara ya kwanza gesi ilifika Ubungo na kuanza kuzalisha umeme badala ya mafuta mepesi/Jet. Bomba limetoka kisiwani na kufika Ubungo. Ile gesi pale Ubungo inazalisha Umeme na nyingine imesambazwa viwandani. Wenye umri mkubwa watakumbuka hata simbonyi walitumia gesi ya Songo songo kuzalisha umeme.

Miaka michache baadae, Gesi ya Msimbati ilianza kuvunwa kupitia ile kampuni ya ATUMAS, kupitia generator zao pale Mtwara, umeme ulisambazwa Mtwara na Lindi, mpaka hapo hakukuwa na bomba la gesi toka Mtwara kwenda Dar. Miaka ya baadaye ndio ikaonekana ktk mwambao wa Mtwara ndani ya bahari kuna gesi nyingi sana. Mpaka hapa tuna mabomba mabomba mawili yanayokuja Dar, moja linatokea Songo songo na lingine linatokea Mtwara. Nina hakika na hili la Songo songo sababu linaleta gesi kiwandani kwetu TBL, mpoooooooo wajuba !!!!!, hili la Mtwara linaishia pale Kinyerezi, nenda mwenyewe kaone.
 
Yes naelewa hilo la kwanza ni dogo na lilikuwa linaendesha mtambo wa Songas Ubungo, hili la pili linalopeleka Kinyerezi nalo linatumia gesi ya Songo songo, huko mtwara lilichepushwa tu ili kuwapelekea gesi ya kuendeshea viwanda kama cha dangote na vingine.
WE KAMA HUJUI ULIZA USIDANGANYE uma MCHANA KWEUPE...
 
Back
Top Bottom