Hivi gesi yetu inayochimbwa Mtwara inatumika wapi?

Hivi gesi yetu inayochimbwa Mtwara inatumika wapi?

Kule msimbati maurel Prom kampuni ya ufaransa walishaanza kuzalisha muda mrefu tangu 2015,na wanaipeleka mpaka pale Process plant ya Madimba iliyopo chini ya TPDC kwa ajili ya kuileta Dsm.
Je, hii ndio ile ambayo ipo 100km off shore na imegunduliwa just recently, na ambayo ni nyingi sana kiasi cha kutupeleka uchumi kati, ndio hiyo?
 
Naomba nichangie kidogo huu mjadala mtamu.

Moja, 1974, serikali kupitia kampuni ya Agip/TPDC ndio waliogundua uwepo wa gesi katika visiwa vya Songo songo vilivyoko wilaya ya Kilwa. Kwa kuwa lengo lao lilikuwa mafuta, mpango ukaishia hapo. Kwa hesabu za wakati za wachumi, ikaonekana gesi iachwe kwanza.

Wakaenda Mtwara, kama sijakosea miaka 1980 hivi, pia wakapata gesi pale Msimbati, pia wakaacha kile kisima kwa kuwa Agip walilenga mafuta zaidi.

Mwaka 2003 mradi wa kuvuna gesi ya Songosongo ulianza, na mwaka 2004 kwa mara ya kwanza gesi ilifika Ubungo na kuanza kuzalisha umeme badala ya mafuta mepesi/Jet. Bomba limetoka kisiwani na kufika Ubungo. Ile gesi pale Ubungo inazalisha Umeme na nyingine imesambazwa viwandani. Wenye umri mkubwa watakumbuka hata simbonyi walitumia gesi ya Songo songo kuzalisha umeme.

Miaka michache baadae, Gesi ya Msimbati ilianza kuvunwa kupitia ile kampuni ya ATUMAS, kupitia generator zao pale Mtwara, umeme ulisambazwa Mtwara na Lindi, mpaka hapo hakukuwa na bomba la gesi toka Mtwara kwenda Dar. Miaka ya baadaye ndio ikaonekana ktk mwambao wa Mtwara ndani ya bahari kuna gesi nyingi sana. Mpaka hapa tuna mabomba mabomba mawili yanayokuja Dar, moja linatokea Songo songo na lingine linatokea Mtwara. Nina hakika na hili la Songo songo sababu linaleta gesi kiwandani kwetu TBL, mpoooooooo wajuba !!!!!, hili la Mtwara linaishia pale Kinyerezi, nenda mwenyewe kaone.

Wewe ndio umeongea sasa!
 
We hujui lolote wewe kuhusu gesi ya Mtwara... Kule Mnazibay kuna visima vitano.. kimoja ndo mkinachopeleka gesi mtwara mjini kwa ajili ya umeme wa Mtwara na kwingineko... Visima vingine vinalisha plant ya serikali ya MADIMBA ambao wanapeleka DAR... usidanganye watu.. DAR WANAGESI TOKA MNAZIBAY (MTWARA) NA SONGOSONGO (LINDI)
Sasa kulikuwa kuna haja ya kutoa povu? kama unajua unasema tu watu waelewe, DON kaelezea kengi kama kuna mengine kasahu au kakosea ilikuwa ni kuongeza maelezo tu sasa unakuja na mipasho ya taarabu hapa
 
Hongera...
Ila ujuwe anadanganya sana.. na ukifuatilia kila nayemkwoti unaona kabisa kuwa anarekebishwa lakini anabisha tu... Unaweza ukasema natoa POVU as if NENO mipasho ya taarabu siyo POVU...
 
NILICHOGUNDUA
1. Hujui kitu kwenye gesi ya Mtwara
2. Unaleta stori ulizozisikia vijiweni
3. Unabisha huna data
Asante mkuu, kwa kutusaidia...huyo jamaa katudaganya hapa..nilipo jua kua ana majibu ya "nadhani" nikajua napoteza muda..

Asante kwa kuja na kunifungua kuwa gesi ipo na inachimbwa..

Sasa km gesi ni nyingi kiasi hicho, mbona bado umeme ni wa mgao???
Tuanzia kwanza hapo mkuu
 
Siasa mkuu...
Mfano, pale Mtwara kuna majenereta 9, ambayo wakati yanaendeshwa na Artumas, yote yalikuwa mazima na tayari kwa kutembea... na wakati huo hakukuwa na kitu kinaitwa MGAO huko Mtwara. Lakini baada ya majenereta yale kuchukuliwa na TANESCO, LEO hii yanayotembea kila siku hayazidi matano.. Kila siku lazima moja litoke kwenye operation na wakati mwingine huzima yoooteeee.... KUNA MMOJA NIMEMSIKIA AKISINGIZIA GESI NDO INASHIDA... huyo naye ni muongo kabisa

Si uliona hata waziri alipokwenda Mtwara, ETI WAFANYAKAZI WAKATWE POSHO....!!!!!!!!
 
Sasa kulikuwa kuna haja ya kutoa povu? kama unajua unasema tu watu waelewe, DON kaelezea kengi kama kuna mengine kasahu au kakosea ilikuwa ni kuongeza maelezo tu sasa unakuja na mipasho ya taarabu hapa
Afu, ww jamaa una matatizo siyo kidogo...ww ni kujeli tu majibu ya wengine.....sijui una nn humo kichwani!!![emoji57]
 
Madimba ni kijiji ambacho kina plant ya kuchakata gas na kui-feed kwenye bomba linaloanzia kijijini hapo hadi somanga Lindi ambapo linaungana na bomba lingine dogo la kutoka songo songo gas field.
Jibu kwa swali lako, wanatoa wapi gas: gas inatoka kwenye visima vya mnazi bay vinavyomilikiwa na wawekezaji(kampuni) wawili ambao ni Wentworth na maurel et prom. TPDC wanamiliki 20% tu za uzalishaji. Hawa wawekezaji wanaiuzia serikali gas kwa kupitia pipes hadi hapo madimba kwenye processing plant na mtwara-dar pipeline ambavyo vyote ni vya serikali na vilijengwa na kampuni ya kichina kwa mkopo kupitia bank ya exim bank of china. Mkopo ni US$1.2bn na ili mradi wote ukamilike(bomba na plant) TPDC ilichangia US$274.92.
Asante kwa nyongeza ..
Hvyo hyo gesi ya bahari, ikianza kuchimbwa, bomba hlo hlo litatumika kuisafirisha??
 
Sawa, ila elewa msingi wa hoja, gesi tuliyoambiwa itafanya Tanzania tuwe uchumi wa kati ni hiyo ya mnazi bay? No! Si hiyo, na haijaanza kuzalishwa, maana ndiyo inayouliziwa hapa.
Na tuliambiwa hapo awali 2015 kuwq imenza kufanya kazi..na kuwa mgao wa umeme sasa basi tanzania..kumbe zilikuwa ni siasa tu.
 
Asante kwa nyongeza ..
Hvyo hyo gesi ya bahari, ikianza kuchimbwa, bomba hlo hlo litatumika kuisafirisha??
Sifahamu vizuri kuhusu hilo ndugu, ila kidogo ninachofahamu ni kwamba hiyo gasi nyingi ya ndani ya bahari(offshore) itatolewa baharini kutoka kwenye visima na kupitishwa kwenye mfumo wa mabomba hadi nchi kavu ambapo kutakuwa na advanced processing plant itakayoibadili gas kuwa kimiminika(LNG, liquefied natual gas). Na baada ya hapo itapakiwa kwenye meli maalum(tankers) sababu mradi huu utahusisha na bandari kubwa kuliko ya mtwara ambavyo itahusika na meli za gas tu.
Matumizi yetu yatakuwa madogo kuliko uzalishaji na hivyo kiasi kikubwa kitapelekwa katika masoko ya far east hasa China. Ila gharama za uwekezaji ni kubwa sana zaidi ya US$15bn(zaidi ya trillions 60 za Tanzania) na ndio maana wawekezaji ambao ni statoil na exon mobbil wanachelewa kuanza mradi kwa haraka. Inahitajika uchambuzi makini ili kurudisha gharama za uzalishaji kwa wakati.
Mara nyingi hawa investors huwa wanataka incentives kubwa kutoka serikalini na hichi ndio kinachochelewesha mradi wa miaka mingi wa mchuchuma coal na liganga iron.
 
Wanasubiri nn kuanza kuchimba??

Kasa cha kuingia gharama zote hzo za mabomba wakati uzalishaji kumbe bado kilikuwa ni cha nn??

Huoni km ni hasara , kwa kuingia gharama nyingi kiasi hicho kwa ajili ya kuweka mabomba ya gesi wakati gesi yenyewe inayopita ni kiduchu??

Na hzo gharama za mabomba ni za serikali au mwekezaji??

Kuanza kuchimba itachukua kuanzia miaka 10,?? nn kinasubiriwa wakati watu wanahitaji umeme kwa ajili ya viwanda...na gesi ipo??
Ninavyojua mimi kwa sasa mazungumzo yanaendelea juu ya kitu kinaitwa Host Government Agreemy(HGA),ambayo ni makubaliano ambayo yatasimamia kwa ujumla hiyo ishu ya hiyo gesi huko baharini na uvunaji wake.

Ili hiyo gesi ianze kutumika lazima ijengwe gas plant ambayo ndio itakua inachakata hiyo gesi na kutengeneza bidhaa za mwisho mbalimbali.

Na hapo upatikanaji wa mwekezaji wa kujenga hiko kiwanda cha gas processing utategemea na hiyo HGA itakavyokua.Ikiwa mbaya inaweza ikachukua muda zaidi wawekezaji kuja na kuendeleza utafutaji katika vitalu vingine
Wanasubiri nn kuanza kuchimba??

Kasa cha kuingia gharama zote hzo za mabomba wakati uzalishaji kumbe bado kilikuwa ni cha nn??

Huoni km ni hasara , kwa kuingia gharama nyingi kiasi hicho kwa ajili ya kuweka mabomba ya gesi wakati gesi yenyewe inayopita ni kiduchu??

Na hzo gharama za mabomba ni za serikali au mwekezaji??

Kuanza kuchimba itachukua kuanzia miaka 10,?? nn kinasubiriwa wakati watu wanahitaji umeme kwa ajili ya viwanda...na gesi ipo??
Ninavyojua mimi kwa sasa mazungumzo yanaendelea juu ya kitu kinaitwa Host Government Agreemy(HGA),ambayo ni makubaliano ambayo yatasimamia kwa ujumla hiyo ishu ya hiyo gesi huko baharini na uvunaji wake.

Ili hiyo gesi ianze kutumika lazima ijengwe gas plant ambayo ndio itakua inachakata hiyo gesi na kutengeneza bidhaa za mwisho mbalimbali.

Na hapo upatikanaji wa mwekezaji wa kujenga hiko kiwanda cha gas processing utategemea na hiyo HGA itakavyokua.Ikiwa mbaya inaweza ikachukua muda zaidi wawekezaji kuja na kuendeleza utafutaji katika vitalu vingine.

[emoji116] [emoji116]
Maelezo zaidi na "complicated" kidogo,ila ukipenda ipitie.
Screenshot_20171208-204720.jpg

Screenshot_20171208-204740.jpg
 
Attachments

Sababu ilikuwa ni kwamba wananchi walitaka mitambo iliyop Kinyerezi ipelekwe huko huko gesi inapotoka ili umeme uzalishwe huko na kusafirishwa kuja Dar,ila hiyo ilikuwa ngumu sababu ya Transmission losses ambazo zingeweza kutokea, ni bora zaidi kusafirisha gesi kuliko umeme
Jibu lako para ya mwisho inaonesha hujui unacho ongelea.
Unababaisha na kupotosha watu humu ndani. Kwa nini unakomaa na upotoshaji...achia wenye uweledi waelezee.
 
Hata kama tukibadilishana na marekani.
Yaani wa Tanzania tukaishi marekani na wamarekani waje kuishi Tanzania. Baada ya miaka 5.
TANZANIA ITAGEUKA KUWA MAREKANI.
NA MAREKANI ITAGEUKA KUWA TANZANIA.
Sure. Tatizo sio rasilimali tatizo ni brain zetu. No kutumia akili no maendeleo. Inakera sana mtu unadanganywa wakati unajua kuwa unadanganywa na anaekudanganya anajua kuwa unajua anakudanganya na alakulazimisha umpigie makofi halafu unaexpect maendeleo! Ngoja tusubiri
 
Gesi iliyogunduliwa juzi juzi ya Msimbati Mtwara bado haijaanza kuchimbwa, inaweza kuchukua hata miaka 10 kuanza kuchimbwa. Ile iliyogunduliwa miaka ya nyuma ya Songas na Mnazi bay ndio inayotumika Kinyerezi power plant na ubungo power plant kuzalisha umeme, pia imesambazwa baadhi ya viwanda jijini Dar. Na kwasasa umeme wa gesi unaozalishwa Ubungo na Kinyerezi I power plants bado hautoshi kwani mahitaji ya umeme yanaongezeka kwa kasi, na ndio maana serikali iko mbioni kukamilisha na kuwasha mitambo ya Kinyerezi II power plant ili kusaidia kupunguza uhaba, pia nadhani patakuwa na Kinyerezi III na Kinyerezi IV power plants zitafuata ili kuendelea kupambana na uhaba. Stiegler's gorge ndio baba lao kabisa, muwe waelewa na sio watu wa kulia lia kama kuku wanataka kutaga.
Unajifanya muelewa kumbe hakuna kitu kabisa. Kikwete alishatangaza kufikia 2012 kutakuwa na full capacity ktk uzalishaji wa umeme na alisema tutakuwa tunauza nje km megawatt 200(maana yangu ni kwamba asingiweza kusema kitu ambacho sio plani ya Tanesco, otherwise na vingine tunavyoambiwa inawezekana havipo kwenye plan). Sasa ww ukiendelea ku rely kwenye plan badala ya implementations na unajiona ni muelewa basi sawa!
 
Duuh..., nini hiki? Una comment uzi huu au umepotea njia?
 
Back
Top Bottom