SOARES
Senior Member
- Jul 6, 2007
- 146
- 57
Gesi iliyogunduliwa juzi juzi ya Msimbati Mtwara bado haijaanza kuchimbwa, inaweza kuchukua hata miaka 10 kuanza kuchimbwa. Ile iliyogunduliwa miaka ya nyuma ya Songas na Mnazi bay ndio inayotumika Kinyerezi power plant na ubungo power plant kuzalisha umeme, pia imesambazwa baadhi ya viwanda jijini Dar. Na kwasasa umeme wa gesi unaozalishwa Ubungo na Kinyerezi I power plants bado hautoshi kwani mahitaji ya umeme yanaongezeka kwa kasi, na ndio maana serikali iko mbioni kukamilisha na kuwasha mitambo ya Kinyerezi II power plant ili kusaidia kupunguza uhaba, pia nadhani patakuwa na Kinyerezi III na Kinyerezi IV power plants zitafuata ili kuendelea kupambana na uhaba. Stiegler's gorge ndio baba lao kabisa, muwe waelewa na sio watu wa kulia lia kama kuku wanataka kutaga.
Kwa Stiegler Gorge, ionabidi tufikiri upya. Mabadiliko ya tabia nchi yatatuathiri kwenye mradi huu, huenda hata kabla ya kurudisha gharama. Pili tujifunze toka Kidatu, kwetu sisi hydropower si ya kutegemewa sana. Tatu tuweke mipango yetu kwa kuona mbele. Kenya ambao sidhani kama wana urani, wana malengo ya umeme wa urani. Ni mara mia tungeongeza nguvu kwenye umeme wa upepo pale Singida, tuanzishe mashamba ya umeme jua, umeme toka mawimbi ya bahari. Hivi ni vyanzo vyenye kuonyesha mategemeo ya kuwepo kwa muda mrefu zaidi. Hiyo Stiegler ilikuwa inakadiriwa kuzalisha Megawati 4500 hadi 6000 wakati inafikiriwa kipindi cha awamu ya kwanza. Sasa leo imekuwa chini ya 3000 hii ni kuonyesha kuwa uwezo utazidi kupungua hadi sufuri. Hizi data zilikuwa kwenye magazeti ya nyakati fulani fulani.