Hivi gesi yetu inayochimbwa Mtwara inatumika wapi?

Hivi gesi yetu inayochimbwa Mtwara inatumika wapi?

Muongo MKUBWA USIYE NA HAYA... Madimba gas plant wanapata wapi gesi yao?
Umeme wa mtwara unazalishwa kwa gesi gani?
Artumas wakati wapo hapa Tanzania, walikuwa wanafanya nini kama si kuchimba gesi ya Mtwara?
Madimba wanatumia gesi ya mnazi bay na sio ya Msimbati ambayo ndiyo ipo kwa wingi na bado haijaanza kuzalishwa.
 
Hata wachimbe uranium tatizo la mgao litaendelea hadi tutapofika mwisho wa dunia, bado ujajiuliza tuna viwanda takribani sita vya sukari lakini sukari ya kutoka nje ni rahis kuliko ya viwandani. Wanasiasa sio watu wa kuaminika sana
mkuu naskia tatizo la sukari ya hapa kuwa juu ni system ama utaratibu mbovu wa kiwanda/viwanda ambapo mara baada ya kuzalishwa kwa sukari huingia mkataba na msambazaji/mfanyabiashara mmoja tu... so huyo ndiye anayehodhi sukar yote ya kiwanda hicho ilyokwisha zalishwa,,, yeye ndiye atakayepanga bei na mengineyo...

utakuta sukar inazalishwa kilombero lakini cha ajabu baada ya kuzalishwa ni lazima ije mpaka morogoro mjini then ndiyo irudi nyuma hadi kwa wakazi kilombero,, wakazi wakilombero watainunua wakiwa tayari wamejumuishiwa na bei ya usafiri(Bei sawa na ya mjini)... so faida ya kukaa karibu na kiwanda hakuna.

hawa wasambazaji naskia pia wamegawanyika kikanda/zone,, zone ya dar, kaskazini, kusini kat, magharibi n.k...

solution nadhani wenye viwanda kama wangekuwa wanaruhusu kuwauzia watu wengine(watu wengi) ingechangia sana ushindani, kama vile yalivyo makampuni ya simu...

stail ya sasa ya huu mfumo wa usambazaji sukari wa kuwa chini ya watu wa chache ni sawa na system ya bongo movie na wadosi... hawa nao ndiyo wanyonyaji kupita maelezo...
 
Gesi iliyogunduliwa juzi juzi ya Msimbati Mtwara bado haijaanza kuchimbwa, inaweza kuchukua hata miaka 10 kuanza kuchimbwa. Ile iliyogunduliwa miaka ya nyuma ya Songas na Mnazi bay ndio inayotumika Kinyerezi power plant na ubungo power plant kuzalisha umeme, pia imesambazwa baadhi ya viwanda jijini Dar. Na kwasasa umeme wa gesi unaozalishwa Ubungo na Kinyerezi I power plants bado hautoshi kwani mahitaji ya umeme yanaongezeka kwa kasi, na ndio maana serikali iko mbioni kukamilisha na kuwasha mitambo ya Kinyerezi II power plant ili kusaidia kupunguza uhaba, pia nadhani patakuwa na Kinyerezi III na Kinyerezi IV power plants zitafuata ili kuendelea kupambana na uhaba. Stiegler's gorge ndio baba lao kabisa, muwe waelewa na sio watu wa kulia lia kama kuku wanataka kutaga.
Aiseeeeeeeeeee
 
Transmission losses za kusafirisha umeme wa kuhudumia watu milioni 5 sio sawa na TL za kusafirisha umeme wa kuhudumia watu 50,000
Transmission line inapokuwa ni moja, iwe inahudumia 5000k au 50k, ukubwa wa losses unakuaje? Unatokana na nini?

Kama plant watazalisha, mfano 33.5kV au niseme watazalisha 11kV, stepping it up to 33.5kV na kuisafirisha kwenda kwenye substation kupitia transmission line, hizi substation zianze kugawa kwa end users; loss ipi inayoogopwa hapo au kuzingatiwa?
 
Madimba wanatumia gesi ya mnazi bay na sio ya Msimbati ambayo ndiyo ipo kwa wingi na bado haijaanza kuzalishwa.
Weweee Sikia, wauzaji wa gesi yote huku mtwara ni M&P.
1. Wana visima vitano namely MB1 (kipo baharini), MB2, MB3, MB4 na MS-1X. MB1 kiligunduliwa toka mwaka 1978 na watafuta mafuta, Nyerere akawaambia wasifukie, wakizibe tu juu hadi hapo tutakapopata akili ya kuchimba gesi (KAZI YA BABA WA TAIFA) na ndo kisima hiki pekee kinalisha gesi majenereta ya Mtwara... Na hayo majenereta yanakula gesi kidogo sana ukilinganisha na uwezo wa kisima hicho. Gesi inayotoka hapo inachakatwa Mnazibay na kupokelewa Mtwara kupitia mashine nyingine ya kuchakata iliyo mtwara mjini (magharani) kabla ya kuingia TANESCO
2. Visima vingine vyote (VINNE) vinapeleka gesi yake MADIMBA na wao wanapeleka Dar

NB. Visima vyote vimechimba sehemu mbalimbali ndani ya Msimbati na Mnazibay. Jumla, kama nilivyosema ni vitano
We endelea kudanganya watu... GESI HUKO INACHIMBWA, HAKUNA AMBAYO HAIJAANZA KUCHIMBWA KWAMBA IPO KWENYE EXPROLATION LEVEL
 
We hujui lolote wewe kuhusu gesi ya Mtwara... Kule Mnazibay kuna visima vitano.. kimoja ndo mkinachopeleka gesi mtwara mjini kwa ajili ya umeme wa Mtwara na kwingineko... Visima vingine vinalisha plant ya serikali ya MADIMBA ambao wanapeleka DAR... usidanganye watu.. DAR WANAGESI TOKA MNAZIBAY (MTWARA) NA SONGOSONGO (LINDI)
Sawa, ila elewa msingi wa hoja, gesi tuliyoambiwa itafanya Tanzania tuwe uchumi wa kati ni hiyo ya mnazi bay? No! Si hiyo, na haijaanza kuzalishwa, maana ndiyo inayouliziwa hapa.
 
Gesi iliyogunduliwa juzi juzi ya Msimbati Mtwara bado haijaanza kuchimbwa, inaweza kuchukua hata miaka 10 kuanza kuchimbwa. Ile iliyogunduliwa miaka ya nyuma ya Songas na Mnazi bay ndio inayotumika Kinyerezi power plant na ubungo power plant kuzalisha umeme, pia imesambazwa baadhi ya viwanda jijini Dar. Na kwasasa umeme wa gesi unaozalishwa Ubungo na Kinyerezi I power plants bado hautoshi kwani mahitaji ya umeme yanaongezeka kwa kasi, na ndio maana serikali iko mbioni kukamilisha na kuwasha mitambo ya Kinyerezi II power plant ili kusaidia kupunguza uhaba, pia nadhani patakuwa na Kinyerezi III na Kinyerezi IV power plants zitafuata ili kuendelea kupambana na uhaba. Stiegler's gorge ndio baba lao kabisa, muwe waelewa na sio watu wa kulia lia kama kuku wanataka kutaga.
Kule msimbati maurel Prom kampuni ya ufaransa walishaanza kuzalisha muda mrefu tangu 2015,na wanaipeleka mpaka pale Process plant ya Madimba iliyopo chini ya TPDC kwa ajili ya kuileta Dsm.
 
Ninachokiona kwny huu mjadala ni kukosa taarifa sahihi na kukosa maarifa ya kupata taarifa sahihi.

Ni hivi, kuna gas reserves katika makundi matatu. Kundi la kwanza ni gesi iliyogunduliwa miaka ya 1970s/80s kwny kisiwa cha Songo Songo kilichopo Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi. Songo Songo haipo Mtwara. Mwaka 2004 gesi ya Songo Songo ilianza kutumika baada ya mitambo ya Songas iliyopo Ubungo kuanza kutumika. Hivyo, kuna mtambo wa kuchakata gesi Songo Songo unaomilikiwa na Songas pamoja na bomba la kusafirishia gesi toka kisiwani hadi Songas Ubungo kwenye mitambo ya kuzalisha umeme kwa kutumia gesi.

Aidha, kundi la pili ni reserve ya gesi iliyogunduliwa katika vijiji vya Mnazi Bay na Madimba mkoani Mtwara. Kampuni ya Artumas na baadae Maurel et Prom ilijenga mtambo mdogo wa kuchakata gesi katika kijiji cha Mnazi bay na bomba lenye urefu wa 27km miaka ya 2006. Gesi hiyo ndiyo inayotumika kuzalisha umeme kupitia mitambo ya Tanesco iliyopo Mtwara Manispaa na kusambaza umeme kwenye mikoa miwili ya Mtwara na Lindi.

Kundi la tatu ni gesi iliyogunduliwa kwenye kina kirefu cha bahari miaka ya 2010s. Ugunduzi wa gesi ya kina kirefu cha bahari ulifanyika yapata km 100 away from onshore. Pia, inakadiriwa kati ya km 2 - 3 chini ya bahari ndipo visima vyenye kina cha kati ya km 2-3 vimechimbwa.

Ukweli ni kwamba gesi ya kina kirefu haijaanza kuchimbwa, ambayo ndio nyingi. Kinachowachanganya wengi ni kwamba ugunduzi wa gesi kwny kina kirefu cha bahari ulienda sambamba na ujenzi wa bomba la inchi 36 kutoka Madimba hadi Kinyerezi. Gesi ambayo inasafirishwa kupitia bomba hili ni ile ya Mnazi Bay na Madimba. Kilichofanyika ilikuwa ni kuunganisha bomba kwny visima vya onshore vipya na vya zamani ili kufikisha gesi Kinyerezi.

Hivyo, kuna mabomba mawili yanayosafirisha gesi. Mosi, ni lile la kutoka Songo Songo hadi Ubungo (2004). Pili, ni lile linalotoka Madimba hadi Kinyerezi (2015).

Naweza kuwa nimesaidia kidogo kutoa ufafanuzi maana niliona watu wanachanganya mambo kwa kukosa taarifa sahihi/uelewa.

Nawasilisha.
Okay, kwahiyo gesi inayokuja Kinyerezi inachukua gesi ya mnazi bay peke yake au linasaidiwa na gesi toka songo songo?
 
Point of correction, hilo la mtwara ni linatoka mnazibay gas fields na sio msimbati.Hiyo ya Msimbati ambayo ndio nyingi sana ni bado.
We baba (sijui mama!) acha UWONGO...
1. Umeshawahi kwenda Msimbati?
2. Unakujua Mnazbay?

KAMA HUJUI ULIZA
 
hili ni janga letu nadhani sasa ni muda wa kuokoa vizazi vyetu sasa
 
Sawa, ila elewa msingi wa hoja, gesi tuliyoambiwa itafanya Tanzania tuwe uchumi wa kati ni hiyo ya mnazi bay? No! Si hiyo, na haijaanza kuzalishwa, maana ndiyo inayouliziwa hapa.
NILICHOGUNDUA
1. Hujui kitu kwenye gesi ya Mtwara
2. Unaleta stori ulizozisikia vijiweni
3. Unabisha huna data
 
Transmission line inapokuwa ni moja, iwe inahudumia 5000k au 50k, ukubwa wa losses unakuaje? Unatokana na nini?

Kama plant watazalisha, mfano 33.5kV au niseme watazalisha 11kV, stepping it up to 33.5kV na kuisafirisha kwenda kwenye substation kupitia transmission line, hizi substation zianze kugawa kwa end users; loss ipi inayoogopwa hapo au kuzingatiwa?
Kwenye kusafirisha umeme kuna kuwa na resistance kwenye wire, jinsi watumiaji wanavyokuwa wengi hata resistance inakuwa kubwa hivyo umeme mwingi utapotea kama joto
 
Alafu kuna Madiwani na Wabunge eti wanajiuzuru nafasi zao kumuunga Mkono..

Hii iko Bongo tu..

Wakati Raslimali ya Gesi ilivyokuwa inapigiwa chapuo huwezi amini haya yanayoendelea..
 
Weweee Sikia, wauzaji wa gesi yote huku mtwara ni M&P.
1. Wana visima vitano namely MB1 (kipo baharini), MB2, MB3, MB4 na MS-1X. MB1 kiligunduliwa toka mwaka 1978 na watafuta mafuta, Nyerere akawaambia wasifukie, wakizibe tu juu hadi hapo tutakapopata akili ya kuchimba gesi (KAZI YA BABA WA TAIFA) na ndo kisima hiki pekee kinalisha gesi majenereta ya Mtwara... Na hayo majenereta yanakula gesi kidogo sana ukilinganisha na uwezo wa kisima hicho. Gesi inayotoka hapo inachakatwa Mnazibay na kupokelewa Mtwara kupitia mashine nyingine ya kuchakata iliyo mtwara mjini (magharani) kabla ya kuingia TANESCO
2. Visima vingine vyote (VINNE) vinapeleka gesi yake MADIMBA na wao wanapeleka Dar

NB. Visima vyote vimechimba sehemu mbalimbali ndani ya Msimbati na Mnazibay. Jumla, kama nilivyosema ni vitano
We endelea kudanganya watu... GESI HUKO INACHIMBWA, HAKUNA AMBAYO HAIJAANZA KUCHIMBWA KWAMBA IPO KWENYE EXPROLATION LEVEL
Hapa tunaongelea gesi iliyopo off-shore baharini iliyogunduliwa recently, sio ya enzi za nyerere, na hiyo gesi ndio tuliambiwa iko kwa wingi kiasi itakapoanza kuchimbwa itatufanya Tanzania tuingie uchumi wa kati, hii gas ya baharini ndio inayouliziwa hapa, na ni kwamba bado sana kuchimbwa.
 
Okay, kwahiyo gesi inayokuja Kinyerezi inachukua gesi ya mnazi bay peke yake au linasaidiwa na gesi toka songo songo?

Kuna jambo sikulitaja kwny uzi wangu. Wakati gas processing plant ya Madimba inajengwa pamoja na bomba la kusafirishia gesi kuja Kinyerezi, mradi huu ulienda sambamba na ujenzi wa processing plant nyingine kule Songo Songo. Gesi inayochakatwa na mtambo wa serikali wa Songo Songo inasafirishwa kupitia bomba lenye urefu wa km 25 hadi Somanga Fungu (Kilwa) na kuingiza gesi yake kwny bomba linalotoka Madimba (Mtwara) kuja Kinyerezi.

Hivyo, Songo Songo kuna gas processing plants mbili. Moja inamilikiwa na Songas (2004) na plant ya pili ni ile ya Serikali chini ya TPDC. Pia, kutoka Songo Songo kuna mabomba mawili. Lile la Songas limekuja moja kwa moja Ubungo na lile la Serilikali limeunganishwa Somanga Fungu kwny bomba la kutoka Madimba kuja Kinyerezi.

Nadhani nimejibu swali lako.
 
Hapa tunaongelea gesi iliyopo off-shore baharini iliyogunduliwa recently, sio ya enzi za nyerere, na hiyo gesi ndio tuliambiwa iko kwa wingi kiasi itakapoanza kuchimbwa itatufanya Tanzania tuingie uchumi wa kati, hii gas ya baharini ndio inayouliziwa hapa, na ni kwamba bado sana kuchimbwa.
Unaweza ukasema nani wamefanya exprolation ya hiyo gesi unayodai haijaanza kuchimbwa huko Msimbati?
 
Kuna jambo sikulitaja kwny uzi wangu. Wakati gas processing plant ya Madimba inajengwa pamoja na bomba la kusafirishia gesi kuja Kinyerezi, mradi huu ulienda sambamba na ujenzi wa processing plant nyingine kule Songo Songo. Gesi inayochakatwa na mtambo wa serikali wa Songo Songo inasafirishwa kupitia bomba lenye urefu wa km 25 hadi Somanga Fungu (Kilwa) na kuingiza gesi yake kwny bomba linalotoka Madimba (Mtwara) kuja Kinyerezi.

Hivyo, Songo Songo kuna gas processing plants mbili. Moja inamilikiwa na Songas (2004) na plant ya pili ni ile ya Serikali chini ya TPDC. Pia, kutoka Songo Songo kuna mabomba mawili. Lile la Songas limekuja moja kwa moja Ubungo na lile la Serilikali limeunganishwa Somanga Fungu kwny bomba la kutoka Madimba kuja Kinyerezi.

Nadhani nimejibu swali lako.
Swadakta, kwahiyo nikisema Kinyerezi power plant inatumia gas ya Songo songo na mnazi bay nitakuwa sijakosea?
 
Hivi unafahamu MADIMBA wanatoa gesi wapi?
Madimba ni kijiji ambacho kina plant ya kuchakata gas na kui-feed kwenye bomba linaloanzia kijijini hapo hadi somanga Lindi ambapo linaungana na bomba lingine dogo la kutoka songo songo gas field.
Jibu kwa swali lako, wanatoa wapi gas: gas inatoka kwenye visima vya mnazi bay vinavyomilikiwa na wawekezaji(kampuni) wawili ambao ni Wentworth na maurel et prom. TPDC wanamiliki 20% tu za uzalishaji. Hawa wawekezaji wanaiuzia serikali gas kwa kupitia pipes hadi hapo madimba kwenye processing plant na mtwara-dar pipeline ambavyo vyote ni vya serikali na vilijengwa na kampuni ya kichina kwa mkopo kupitia bank ya exim bank of china. Mkopo ni US$1.2bn na ili mradi wote ukamilike(bomba na plant) TPDC ilichangia US$274.92.
 
Back
Top Bottom