HIV inanitesa

HIV inanitesa

Inabidi tuunde kikundi chetu sie waathirika wa HIV+ humu Jamii Forums ili kuweza kutambuana na pia kupambana na changamoto mbalimbali zinazotukabili kuhusu unyanyapaa kutoka kwa baadhi ya watu hasa wanawake wenzetu.

Madame B habari yako aisee!
 
Last edited by a moderator:
Mie ninao mume wangu....naomba nikifa usioe mke mwingine, hata ukioa jaribu kumzuia kuvaa baadhi ya vitu vyangu....
Ila kama utatangulia wewe ujue mie nitaolewa tu....sitaweza kuvumilia ukame

ha ha haaaaaaaaaaa
 
Mie ninao mume wangu....naomba nikifa usioe mke mwingine, hata ukioa jaribu kumzuia kuvaa baadhi ya vitu vyangu....
Ila kama utatangulia wewe ujue mie nitaolewa tu....sitaweza kuvumilia ukame

Binamu, umeongea kiurahisi sana...!
Nisindikize nami nikajue afya yangu...!
 
Niko serious matumbo.
Na kama kuna mtu alishawahi kuja pm kwa ajili ya kunitongoza na nikaamua kulala nae basi ajue nae amekwisha, maana humu nina Id zaidi ya 18 na karibia zote zilikuwa zinashinda jukwaa la Love connect.
Hivyo huwezi kujua kama nawe uko kwenye mkumbo wa kusubiri kuingia katika chama chetu au laaa!
mmmh.. hayo masihara yako utaacha watu wajikojolee saivi binamu...!
 
Ndio mkuu....
Unajua sie waathirika tunanyanyapaliwa sana mitaani hasa hasa baada ya kujitangaza.
Ndio maana tumeamua kuunda kikundi chetu.
Unakaribishwa mkuu

Hata kama sijajitangaza nakaribishwa Madame B?
 
Mie ninao mume wangu....naomba nikifa usioe mke mwingine, hata ukioa jaribu kumzuia kuvaa baadhi ya vitu vyangu....
Ila kama utatangulia wewe ujue mie nitaolewa tu....sitaweza kuvumilia ukame

Wife kwani ukiwa na Ukimwi ndiyo unakufa?
 
Niko serious matumbo.
Na kama kuna mtu alishawahi kuja pm kwa ajili ya kunitongoza na nikaamua kulala nae basi ajue nae amekwisha, maana humu nina Id zaidi ya 18 na karibia zote zilikuwa zinashinda jukwaa la Love connect.
Hivyo huwezi kujua kama nawe uko kwenye mkumbo wa kusubiri kuingia katika chama chetu au laaa!

Pole yako sana, ila maneno yanaumba pia ukumbuke.
 
Last edited by a moderator:
HIV ilikuwa ni death sentence maika iliyopita, siku hizi ukichanganya lifestyle na dawa uanweza kuishi vizuri na kutimiza maana ya ule wimbo wa zamani katika kipindi cha kusalimia wagonjwa cha "Pole" "Ajuaye bwana mola kwa mzima kuwa mfu, mgonjwa kuwa salamaaaa, leo tunawapa poleee".

Nakusihi sana usifanye maambukizo ya makusidi kwa maana hilo ndilo linamtenganisha binadamu na mnyama.

Kumbe siku nyingine unamtambua Mungu?!!Kweli Mungu ni mkubwa jamani.
 
Sikupi pole sababu sio kuwa ukiumwa UKIMWI ndio unakufa leo au kesho...Ni wewe mwenyewe kujipenda na kujua jinsi ya kuishi...Wapo wazima wanakufa, wapo wanaoumwa homa au malaria wanakufa kila kukicha wenye ukimwi wanabaki.

Mie nakupa hongera kwa kufikiria hili jambo la kupenda kuendelea na maisha baada ya kuupata, Ukimwi siku hizi ni sawa na Mwenye kisukari au pressure kwani mtu hutakiwa kufuata tuu taratibu unazoambiwa na doctor..

Ila ni kweli, watu wengi kwa kupitia tamaa zao, au kwa kujisahau hujikuta anapata maambukizi ya Ukimwi. kwani mtu hujikuta akiwa na mpenzi hawapimi mwanzo na kujidai kutumia condom amapo hudumu siku chache tuu na kuanza kuaminiana kuweka condom mbali....Hujui mtu huyu alikuwa na wangapi kabla yako....Hujui alikuwa na nani na huyo nani alikuwa na nani...Dahh inasikitisha...Na tabia pia ya kupanga wapenzi imekuwa ndio sifa kwa wengi.

Pili wapo hasa wanaume wengi wenye Ugonjwa wanaopenda kuambukiza wengine na hata watoto nikimaanisha mabinti wadogo kwa makusudi....Na wengi wao walioathirika wamekuwa ni wenye maneno matamu ..
Na wamekuwa ni wajanja sana hasa hawa wababa, ukitaka kupima anakuambia, ni kesho, ni kesho hiyo kesho ikifika anatajidai anadharura hapimi, anajaribu kukulaghai ukikataa atakuahidi tuu ni kesho tena haifiki siku ya siku unajikuta umeingia bila condom...

Dahhh kweli tumuogopeni Muumba wetu...Km wewe umeathirika Tubu, rudi kwa Muumba wako, Elimisha wenzio kama huyu HIV+....Kumbuka unapomfanyia kumuambukiza mwenzio kwa makusudi huna tofauti na yule anayemuekea mwenzie sumu bila kujua...Wanafunzi dah, nishashuhudia mwanafunzi binti mdogo anaenda kuukwa mtu ambaye sie nafsi iliuma sana nilimlaani sana baba huyo kwa jina kapuni....ila ndio hivyo ashaingia tena...

Pili kweli kama dada anavyosema Wengine huwanyanyapaa na kujiona wapweke...Tubadilike, tuwaone nisawa na kuwa na mgonjwa wa kisukari ndani, au pressure....Tuwajali kwani ukiwajali anaishi hata miaka 20 mbeleni na kusaidia katika familia kujenga taifa na familia...Tuwapendee...Mimi kitokea kwa upande wangu nahakika nitampenda sana...

Me ni hayo tuu

Hongera sana HIV+

Habari zenu wana jamvi.
Naombeni maoni yenu /michango yenu.
Mie ni Mdada wa miaka 30 nima MBA ya UDSM na nimebahatika nimeajiriwa hapa DSM mitaa ya post mpya.Pia nina ishi na Virus visababishavo ukimwi (HIV)

Naisha maisha ya kawaida kabisa nimejenga na nina kiusafiri cha kunifikisha popote napotaka kwenda.Vile vile ni Mrembo nimeumbika haswaa maji ya kunde umbo la kibantu haswaa hakuna mwanaume akutane na mie asigeuke mara mbili mbili kuniangalia.

Niliishi maisha ya kawaida tu hapo awali adi mwaka 2008 mwishoni nilipata mchumba kwenda kupima mie nikangundulika nimeathirika wapendwa.kweli ilikuwa hali ngumu sana kwa upande wangu.Nikakaa kimya adi leo sijawambia mtu ndo naweka wazi hapa Jamii leo hii.Namshukuru Mungu nina afya njema sana sina hapa uwezi kujua hata ukiambiwa uwezi kukubali.

Shida ni hii hapa Unyanyapaa kwa baadhi ya jamaa zetu katika jamii zinazotuzunguka umekuwa mkubwa sana.
Hali hii uwa inanipelekea kutaka kuambuka kwa makusudi wanaume wanaojigonga kwangu.Na wakati mwingine mie kama binadamu uwa najikuta kwenye mahusiano kama mjuavyo mara ya kwanza mtatumia kinga ya pili njema inataka kavu hapo ndo uwa napatwa na ngazi mwili mzima.

Jamani napenda kutoa wito kwa waathirika mwenzangu hapa Jamii forum tujiunge walau tufanye ka network ketu ili tuangalie namna ya kupambamba na Maradhi+Unyanyapaa na kukumbusha jamii UKIMWI upo nna pia hauchagui.Maana sie wagonjwa ndo tunajukumu la kuwalinda hawa wanao tunyanyapaa.

Tukichukulia Hasira unyanyapaa nawaaambia waTanzania wengi watapoteza maisha yao kwa HIV.
Na ninajutia sana Kwa kuwaambukiza wengine kwa taama zao za kimwili.
Asante
HIV+
 
I LOVE U HIV+, Mungu akupe Umri, akuzidishie imani.....na akunyooshee maisha yako yawe mepesi

Ila wanaume huwa nawashangaa sana sana...Utakuta mwanaume anakutaka...Huwezi kumueleza uhalisia wa afya yako kwani ni siri yako wewe utakachoamua ni kumkataa Basi yeye atakung'ang'ania na ukizidi kumkataa atakuwekea hasiri/chuki...
Hawatambui wkt mwingine kila likuepukalo lina kheri na wewe..
Wengine hawapendi kuambukiza na wengine wanapenda kuambukiza ukimtongoza tuu imekula kwako..

Habari zenu wana jamvi.
Naombeni maoni yenu /michango yenu.
Mie ni Mdada wa miaka 30 nima MBA ya UDSM na nimebahatika nimeajiriwa hapa DSM mitaa ya post mpya.Pia nina ishi na Virus visababishavo ukimwi (HIV)

Naisha maisha ya kawaida kabisa nimejenga na nina kiusafiri cha kunifikisha popote napotaka kwenda.Vile vile ni Mrembo nimeumbika haswaa maji ya kunde umbo la kibantu haswaa hakuna mwanaume akutane na mie asigeuke mara mbili mbili kuniangalia.

Niliishi maisha ya kawaida tu hapo awali adi mwaka 2008 mwishoni nilipata mchumba kwenda kupima mie nikangundulika nimeathirika wapendwa.kweli ilikuwa hali ngumu sana kwa upande wangu.Nikakaa kimya adi leo sijawambia mtu ndo naweka wazi hapa Jamii leo hii.Namshukuru Mungu nina afya njema sana sina hapa uwezi kujua hata ukiambiwa uwezi kukubali.

Shida ni hii hapa Unyanyapaa kwa baadhi ya jamaa zetu katika jamii zinazotuzunguka umekuwa mkubwa sana.
Hali hii uwa inanipelekea kutaka kuambuka kwa makusudi wanaume wanaojigonga kwangu.Na wakati mwingine mie kama binadamu uwa najikuta kwenye mahusiano kama mjuavyo mara ya kwanza mtatumia kinga ya pili njema inataka kavu hapo ndo uwa napatwa na ngazi mwili mzima.

Jamani napenda kutoa wito kwa waathirika mwenzangu hapa Jamii forum tujiunge walau tufanye ka network ketu ili tuangalie namna ya kupambamba na Maradhi+Unyanyapaa na kukumbusha jamii UKIMWI upo nna pia hauchagui.Maana sie wagonjwa ndo tunajukumu la kuwalinda hawa wanao tunyanyapaa.

Tukichukulia Hasira unyanyapaa nawaaambia waTanzania wengi watapoteza maisha yao kwa HIV.
Na ninajutia sana Kwa kuwaambukiza wengine kwa taama zao za kimwili.
Asante
HIV+
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom