HIV inanitesa

HIV inanitesa

pole sana dada yangu. usijihukumu wewe mwenyewe wala kujinyanyapaa hivyo unayo nafasi ingine ambayo itaweza kukubadilisha maisha yako unayoishi sasa na kuwa mwingine, mtegemee Mungu kuwa mtu wa maombi na jua kuwa Mungu
unapomuendea yeye anasikia kwani sikio lake si zito wala asiweze kusikia na kutenda jambo jipya kwako

Kinachotakiwa kwako ni kumwamini na kumtegemea na kumpa maisha yako afanyike mtawala moyoni mwako soma
warumi 10:9 vile vile mwite yeye anayeponya atakuponya na utakuwa mzima usiwe na hofu wala mashaka kwa
M,ungu yote yanawezekana anaponya magonjwa yote yawe ya kufisha, kawaida yeye ni mponyaji kwani ulituma neno
lake la uponyaji na kukuponya pale utakapomwamini na kukubali na kumruhusu awe Bwana na Mwokozi wako utapata uponyaji
 
...Asante,sitanii

Aisee Madame B hili ni tatizo kwenye jamii yetu,kwenye familia zetu...na wengine tumeguswa kabisa kwenye familia zetu bado tuna machungu si la kufanyia mzaha pliz...
 
Last edited by a moderator:
I LOVE U HIV+, Mungu akupe Umri, akuzidishie imani.....na akunyooshee maisha yako yawe mepesi

Ila wanaume huwa nawashangaa sana sana...Utakuta mwanaume anakutaka...Huwezi kumueleza uhalisia wa afya yako kwani ni siri yako wewe utakachoamua ni kumkataa Basi yeye atakung'ang'ania na ukizidi kumkataa atakuwekea hasiri/chuki...
Hawatambui wkt mwingine kila likuepukalo lina kheri na wewe..
Wengine hawapendi kuambukiza na wengine wanapenda kuambukiza ukimtongoza tuu imekula kwako..
Ndo tuache kukurupuka, unakutana na mtu jf..Leo Jioni mnavuana tena bila kinga. Nimejifunza mengi..hisia zangu nimea ha nyumbani
 
Duh kwa jinsi ulivyoji xpress nimesononeka saana, pole Mungu akutie nguvu ili uzidi kuwa imara. Ukijilinda unakuwa umetulinda sote. Naona hata mkuu wa Kaya hapa kati kati ya miguu kanywea kabisaaaa.
 
Aisee Madame B hili ni tatizo kwenye jamii yetu,kwenye familia zetu...na wengine tumeguswa kabisa kwenye familia zetu bado tuna machungu si la kufanyia mzaha pliz...

Kwa hiyo shoga yangu huamini kama nimeathirika?
 
Last edited by a moderator:
mtafute +ve mwenzako then muanze kuishi maisha yenu kwa raha kabisa
 
I LOVE U HIV+, Mungu akupe Umri, akuzidishie imani.....na akunyooshee maisha yako yawe mepesi

Ila wanaume huwa nawashangaa sana sana...Utakuta mwanaume anakutaka...Huwezi kumueleza uhalisia wa afya yako kwani ni siri yako wewe utakachoamua ni kumkataa Basi yeye atakung'ang'ania na ukizidi kumkataa atakuwekea hasiri/chuki...
Hawatambui wkt mwingine kila likuepukalo lina kheri na wewe..
Wengine hawapendi kuambukiza na wengine wanapenda kuambukiza ukimtongoza tuu imekula kwako..

Private hospital gani zinatoa huduma ya wagonjwa wa ukimwi? Kupima na kutoa dawa.
 
Niko serious matumbo.
Na kama kuna mtu alishawahi kuja pm kwa ajili ya kunitongoza na nikaamua kulala nae basi ajue nae amekwisha, maana humu nina Id zaidi ya 18 na karibia zote zilikuwa zinashinda jukwaa la Love connect.
Hivyo huwezi kujua kama nawe uko kwenye mkumbo wa kusubiri kuingia katika chama chetu au laaa!

hahahaaaaaaaa daaaa
 
Last edited by a moderator:
unajua haya mambo ni rahisi kuyaandika lakini ni mahimu sana tena sana kuyaangalia kwa ukaribu wake....
 
Pole sana HIV+. Mimi huwa nawaambia wagonjwa wangu kati ya magonjwa sugu, HIV ni bora kuliko Kisukari au Shinikizo la damu. Wagonjwa wa hayo magonjwa watakusimulia. Cha muhimu, kama umeanza kutumia dawa tumia vizuri na fuata ushauri mwingine toka kwa madaktari au wataalamu wa afya unaowatembelea mara kwa mara.
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom