ukwaju_wa_ kitambo
Senior Member
- Sep 15, 2024
- 147
- 167
HISTORIA FUPI YA MSANII BAB LEE KATIKA TASNIA HII YA MUZIKI WA BONGO FLEVA..
"Bab lee jina langu halisi naitwa "Ally Omary " kiukweli mimi kwenye mambo ya muzuki nimeanza toka mwaka 2000 kwahiyo mpaka sasa nina Takribani miaka 24 katika game hii ya Bongo fleva.
Tangu nilipoanza Muziki nikiwa Bado mdogo sana , maana nilianza kufanya muziki nikiwa Bado nipo shuleni... wasanii ambao walini inspire kufanya muziki Enzi hizo alikuwepo msanii kama Dully sykes a.k.a mr misifa alikuwa kama brother yangu yule kwenye upande wa muziki , professor jay , juma nature . Hao ndio wasanii ambao walini inspire " nyani Enzi hizo nilikuwa napenda sana muziki na kwa kipindi hicho cha udogo wangu nilikuwa sijui nini maana ya Muziki, namna ya kuandika lycris nk. lakini nilitokea kupenda kile walichokifanya wasanii hao.
na kipindi hicho tulikuwa hatujuani na wala nilikuwa sina wazo kama siku moja na mimi nitakutana nao.
Nami nikajikuta nimeanza najifunza kuandika lycris za nyimbo , nikaanza kujifunza hadi nikafahamu kumbe napaswa kuandika nyimbo Kwa kwa style hii na kwa kufuata vina kwa style kama hii , basi na mimi nikawa majaribu mara kwa mara kuandika lycris za nyimbo nikiwa Bado nipo shuleni kiukweli Enzi hizo nilichafua sana madaftari yangu ya shule hasa kwenye suala nzima la kujifunza namna sahihi na nzuri ya uandishi wa nyimbo.
Tukija katika Tasnia hii ya muziki wa Bongo fleva hapa Bongo au ya burudani kwa ujumla mimi nina Amini siku zote wanasanaa au wanamuziki siraha kubwa kwetu ni lazima tuwe na ukaribu..
nikijizungumzia mimi kwa upande wangu. mimi kwa kiasi kikubwa nimeshirikiana na wasanii wengi sana kwaajili ya kutengeneza "unit " kwa maana umoja , wale wasanii wote, mara zote wasanii mnapokuwa pamoja tumekuwa na Desturi moja ya kupeana mawazo , idea na connection , mimi nilikutana na wasanii ambao katika mzunguko wangu katika safari yangu ya muziki ni wengi sana ..
wasanii hao kama vile msanii H. Baba mpaka leo ukimpingia H . Baba simu ukimuuliza unamjua Bab lee atakueleza A - z kuhusu mimi Kwa kifupi ananifahamu vyema.
Lakini pia na muomba Mungu wangu aweze kumrehemu ndugu na rafiki yangu kipenzi marehemu H. Mbizo huyu nimeshiriki nae vitu vingi sana katika sanaa na maisha binafsi ( private) maana mimi na yenye Enzi hizo tulikuwa tunaishi nae mtaa moja..
kuna msanii mwengine kutoka Nzega anaitwa j.i a.k.a mtoto wa nzega ile ni Damu yangu kabisa yule hata mimi nikipata shida ama safari ya kwenda nchini kenya sehemu anayoishi j.i kwa sasa mara zote ama mara nyingi nimekuwa nikifikia kwake ( nyumbani kwake). huko nchini kenya nae hata akipata dhalula na kufanya maamuzi ya kuja hapa Bongo jijini Dar es salaam kwaajili ya kufanya project zake za muziki na inshu zingine nje ya muziki nae mara nyingi ama mara zote amekuwa akifikia kwangu hapa jijini Dar es salaam..
Ni Damu yangu kabisa mpaka kesho, kuna wasanii wengine kama kina Ali kiba, ambao tulikuwa nao kwenye Record label moja Enzi hizo ya " G records" kina hakeem 5, pasha & abby skills tulikuwa pamoja nao pale kwa G lover katika studio za " G records " hawa ni watu baadhi ambao nilifight nao kutafuta nafasi ya kung'aa katika muziki , ingawa kila mtu ana maisha yake kwa sasa.m tukirudi Tena huku unakutuna na msanii kama Daimond plantnumz, producer & msanii bob jonior nyani wote Hawa ni familia yangu kabisa nimeshirikiana nao vitu vingi sana kusema na ukweli Enzi hizo nikiwa naanza Muziki..
Kwa upande wangu kwenye inshu au suala la changamoto siwezi kulizungumzia sana , Kwa sababu kwanza changamoto katika maisha ni kitu ambacho kipo kwa kila mtu ndio maana kuna ile kauli wanapenda kuisema kuwa " ukubwa ni jalala" kwahiyo kupitia changamoto ni jambo la kawaida sana kwa mwanadamu kupitia hasa ukifikia lika la uutuuzima lakini pia ni upeo wa akili , nyani kwa kifupi ni kujifunza zaidi , unapopatwa na changamoto cha kwanza uwe unafahamu chanzo cha changamoto uliyoipata , lakini pia ni sehemu ya kujifunza ili kwa mara nyingine jambo kama hilo lisije kukutokea na hata kama likikutokea Tena uweze kulikabili , kwahiyo siwezi kusikataa Sana changamoto za maisha..
Changamoto nilizopitia katika muziki cha kwanza ilikuwa ni inshu ya studio , sikuweza kupata ile production ( kwa wakati sahihi) baada ya mimi kupata idea / mawazo ya kufanya kitu hiki sasa naanzaje..
Kingine fedha nilikuwa sina kwa kipindi hicho kutokana na umri mdogo niliokuwa nao lakini pia familia yangu ilikuwa imeishika sana Dini ( imeshika Dini ya kiislamu) ilikuwa haikubaliani kabisa na mambo ya kidunia kama hayo , hasa muziki wa kidunia ambao mimi nilitamani sana kuufanya Enzi hizo , kama unavyojua wazee wetu Enzi hizo walikuwa wanachukulia suala la muziki kama ni vile chaka ama ni sehemu ya vijana kujifunza uhuni .
Kwahiyo hiyo ni changamoto nyingine niliyoipitia nikawa najitahidi tahidi kufanya hivi na vile mpaka pale nilipopata chance ya kwenda kufanya Kazi kwa mara ya kwanza project ya wimbo wangu kwanza unaitwa
"Kizizi" project hiyo sikuifanyia Hapa Bongo, project hii niliifanya katika mji mkuu wa "zambia" lusaka kule zambia kuna kaka yangu ambaye anaishi kule.. kwahiyo bi mkubwa wangu alikuwa ni mtu ambaye alinisuport kwa kiasi kikubwa sana katika muziki wangu , na maisha yangu kwa ujumla , ukiachana na watu wengine wote walikuwa hawana Muda / time ya kunisupport upande wa baba , ni watu ambao hawataki kabisa kunisupport , mimi Dini naifahamu vyema kwa maana nimesomea Dini katika shule ya kiislamu ( islamic knowledge) kwahiyo Hali kama hiyo ilinipa changamoto kubwa sana katika kutimiza ndoto zangu lakini bi mkubwa wangu aliweza kuendelea kunishika mkono , sikiliza mwanangu si una kaka yako yupo huko lusaka zambia , basi nenda kule maybe nae yenye Kaka Yako anaweza kukusaidia kwa namna moja ama nyingine..
kweli mimi nikaamua kufanya safari ya kuelekea huko nchini Zambia uamuzi huu niliufanya baada ya kupatiwa ushauri na bi mkubwa wangu nikasafiri nikaenda zangu hadi zambia na nikafanikiwa kufanya project yangu ya wimbo wangu wa " kizizi ".
nilivyofanya project hii kiukweli nina mshukuru Mungu kwakuwa Mungu sio Athumani watu Ngoma yangu ya kizizi watu wakaipenda na kuipokea kwa mikono miwili vituo vya radio na Television vilicgeza sana Kazi yangu na baada ya mimi kurudi kutoka zambia nikafika hapa Bongo .
Ndio producer G lover ambaye ni ni producer wa " G records" alivyonisikia kupitia nyimbo yangu ya kizizi ndio akawa amefanya uamuzi wa kunitaka mimi niwe sehemu ya wasanii wake nyani niwe chini ya Record label yake ya G records..
kwahiyo katika makubaliano yangu na producer G lover ndio nikawa nimefikia katika "label ya G records" ndio nikapata fursa ya kukutana na wasanii kama kina Ali kiba , kwahiyo changamoto yangu ya pili ilikuwa ni hiyo . Kwanza kushindwa kupata nafasi ya kurekodi lakini pia nyani nilikuwa sina support , nyani sio support ya fedha na maanisha support ya kimawazo zaidi tu.. kikubwa ni ushauri niliyopatiwa na bi mkubwa na mama yangu Mdogo Enzi hizo . Mama yangu Mdogo anaitwa bi hondo ndie aliyefikia uamuzi wa kunipa jina hili la " bab lee" nyani bab lee maanake ni " babu ally"
Enzi hizo nikiwa mdogo walikuwa wananiita babu ally , kwahiyo mama mdogo akaamua kulifanya jina la babu lee litamkwe kifupi " in short cut ( bab lee) .
Lakini nitoe ushauri kwa wasanii wadogo ambao Bado wanatafuta chance kwenye Muziki ni kwamba Unapokuwa under Ground itakupindi upinge show hata kwenye ma bar ili uweze kuonyesha kipaji chako kwa jamii , ili watu kwenye jamii Yako waweze kukufahamu kipaji chako.
Katika harakati za muziki jambo hili kwa msanii yoyote anayeanza muziki kantu hawezi kukipinga , Uwezi kutokea tu from no where ukawa msanii mkubwa bila kupitia njia hizo za kushiriki matamasha mbalimbali na matukio mengine kama hayo .
Mimi Enzi hizo nilikuwa naishi mbezi .. mbezi beach kabla hata ya kuwa " bab lee nilikuwa naishi kwa mama yangu Mdogo nilikuwa na wanangu kule ( washigaji zangu kibao) kama wote kuna kundi moja la muziki Enzi hizo lilikuwa linaitwa " East mbezi' kuna mwangu / msela wangu mmoja alikuwa anajulikana pale kitaa kwa jina la " Ema" huyu Ema alikuwa kama ndio kiongozi wetu katika hiyo crew ya "East mbezi'" yenye ndio alikuwa ngwiji wa kuandaa matamasha , alikuwa ni mtu fulani hivi anayependa kuandaa andaa matamasha mbalimbali mara kwa mara ..
sometimes matamasha ya kusaka mamiss hapo kitaani kwetu " shindano la miss mbezi" nk. Mara tengeta vitu kama hivyo kwahiyo kupitia yale matamasha tulikuwa pamoja kama washigaji wa karibu kila mmoja wetu katika lile kundi aliweza kuonyesha Uwezo wake , uwe una cheza, ama unafanya kitu chochote kinachohusu inshu za sanaa pale ulikuwa unaruhusiwa kuonyesha kipaji chako kupitia hayo majukwaa ya sanaa na matamasha yaliyokuwa yanaandaliwa na jamaa yetu bwana Ema enzi hizo .
Na mimi pale niliingia kwa tiketi ya uimbaji maana nilikuwa napenda kuwa mwana muziki na ninashukuru sana ndugu zangu ( washigaji zangu) walikuwa wananipenda na kunipa ushirikiano katika mambo mbalimbali tukikaa kama crew ya "East mbezi'" , na mimi niliendelea kuonyesha kipaji changu kwa jamii nilichopewa na mwenyezi Mungu , sometime nilikuwa naingiza fedha , ( napewa malipo) na mara nyingine nilikuwa nafanya for free na enzi hizo nilikuwa sitangulizi sana fedha mbele maana nilikuwa na kiu moja tu ya kutaka mimi na jamii yangu waweze kuelewa ni nini ama ni jambo lipi ninalolifanya katika sanaa tofauti na wasanii wengine Enzi hizo.
Kwahiyo nilishapita sana kwenye haya matamasha madogo madogo na niliweza kufanya vizuri kuliko wengine na mimi kuanzia wakati huo nikaanza kujiamini kupitia hii crew yetu ya "East mbezi'"
Baadhi ya members waliunda crew hiyo ambao mimi bado nawakumbuka ni wawili tu alikuwepo huyo Ema , Peter dah wengine nimewasahau maana imekuwa kitambo sana ..
ilikuwa ni mwaka 1999 kabla ya 2000 maana kwenye 2000 hiyo hiyo 2001/2002 mpaka na 2003 kwahiyo ni muda mrefu sana lakini kumbukumbu yangu huku ndipo nilipopitia mimi katika safari yangu katika huu muziki..
Mimi Nimezaliwa Dar es salaam mtaana wa mwananyamala lakini mimi chimbuko langu ni mtu wa Tanga , Dar es salaam ndio Tanzania , lakini Asili yangu ni mtu wa Tanga ...
Kwanza mimi namshukuru Mungu na mama yangu na mshukuru pia na kaka yangu maana wote walitoa ushirikiano ama support katika muziki wangu Tangu nikiwa Zambia , kwa sababu siwezi kukisia ama kusema Uongo kwa kipindi hicho maana hapa nazungumzia mwaka 2004 maana project ya kizizi imetoka mwaka 2004 mwishoni .kwahiyo kama yangu ndio alikuwa mhusika mkuu kwenye kila kitu kinachonihusu mimi kwenye upande wa muziki , kwahiyo kwa miaka ile kutokana na umri wangu nafasi yangu ya kuweza angalau kumuuliza alikuwa anatoa ghalama kiasi Gani studio kwaajili ya kurecord nyimbo ...
Eti producer umemlipa tsh Gapi hiyo ilikuwa ni siri ya kaka yangu na producer , kaka yangu aliamua tu kunisaidia hakutaka hata cent 50 kutoka kwenye Muziki mpaka sasa hivi nilipopata mafanikio. Yenye cha zaidi alikuwa ananipa support na ushauri ama mawazo ili ndugu yake niweze kufanikisha ndoto zangu katika muziki .
Lakini yenye hakuwa sehemu ya meneja eti kwa lengo la kutaka manufaa kupitia muziki wangu katika hilo kiukweli ni hapana alifanya tu kama sehemu ya mapenzi ya kunisaidia mdogo wake ,
Msanii kama Dully sykes alinifanya niwe kama low model wake, ingawa mimi nilikuwa mdogo kwa kipindi hicho , mtu mwingine alikuwa ni mr blue kwakuwa mr blue na Age yangu ilikuwa kama sawa hivi..
Ndio watu nikiwazungumzia kibongo bongo nikienda ki mbele mbele nakutana na kina lil bow wow , lakini nikija bongo mtu ambaye nilipenda sana kufanya nae challenge alikuwa ni mr blue .
Mimi kwenye upande wa Elimu sijasoma sana , lakini mimi kwenye Elimu yangu niliishia kidato cha nne ( form four) nimetoa ujinga wa Dunia Elimu ndogo ya kuniwezesha kufahamu hili na lile..
Nyimbo kiukweli nilikuwanazo nyingi ila zilizopata Airtime kwenye radio zilikuwa chache
Nilifanikiwa hadi kuuza Album , lakini Album hiyo ilikuwa chini ya Record label ya G lover huyu meneja wangu .
Lakini kwakuwa nilikuwa sina usoefu na taharuma kuhusu muziki ( industry) mimi nilikuwa naona ni sawa tu , zilikuwepo nyimbo nyingi nyingi kama.
Kuna wimbo kama mara Saba , nilifanya wimbo huo nilifanya kwa marehemu producer roy pale katika studio za G 2 lakini pia
Kuna wimbo mwingine unaitwa "maisha ni siri"
Lakini kuna wimbo wangu mmoja unaitwa " changua mmoja " ni true stori ambayo ilinitokea mimi Enzi hizo nikiwa Bado shuleni wakati nafikia ile Age ya kuingia Kwa mara ya kwanza kwenye inshu ama masuala ya mapenzi..
Nikawa namwambia yule Dem Enzi hizo Ebu changua mmoja kwanini unataka huku huku ebu eleweka upo upande upi? Basi mwambie kuwa upo na mie ila yenye asikusumbue lakini kama wewe umeamua kuwa nae basi pia niambie mimi ili nami niache kuwa nakusumbua..
Wimbo kama "kizizi" ilikuja tu kama idea , idea ambayo inaishi mpaka kesho ,
Kwakuwa mimi huwa napenda kufanya jambo ama kuandika lycris za nyimbo za vitu ambavyo vimetokea katika jamii zetu ama vitakuja kutokea huko mbeleni katika jamii zetu.
Kwa maana ujumbe utakaokuwepo katika huo wimbo uendelee kuishi kizazi na kizazi..
Mara nyingi nilikuwa naimba vitu ambavyo vimetokea katika jamii zetu na kuna baadhi ya watu vimekwisha kuwatokea katika maisha yao . Na hao watu wanaoguswa na ujumbe huo , hao hao ndio wanakuja kuwa mashabiki zangu na kupenda kufuatilia nyimbo zangu ..
Kwenye upande wa mafanikio niliyoyapa kwenye Muziki ni makubwa mno , kwanza nimshukuru Mungu , mafanikio niliyoyapata katika muziki yamenifanya niwe na ukaribu na kufahamiana na watu wengi na wa aina mbalimbali katika sekta mbalimbali hapa nchini ndani ya sanaa ya muziki na nje sanaa Kwa ujumla..
Watu ambao mnaweza kusaidiana , mkaweza kufanya vitu vingine vya msingi nje muziki ingawa muziki ndio kitu ambacho kimewafanya kukutana..
Kwa maana ya mashabiki ndio utajiri wangu , nafahamika kwa mfano kama sasa hivi mimi nina studio yangu , muziki umepelekea kunipa taharuma ya kuniwezesha kutengeneza production mwenyewe , kwa maana natengeneza muziki mzuri mwenyewe , nikimtaka kwa mfano producer estukizzy anakuja kwenye studio yangu..
Na mafanikio mengine niliyoyapata katika muziki ni fursa naweza kupata dili kwa mfano kupitia muziki labda inshu za matangazo au hata ajila kwa maana watu wanakuamini na ajila yenyewe itakuwa inafanana au inaendana na inshu za internterment
" Kwenye upande wa je? Matamanio ya wasanii wengi wa zamani kutamani muziki huu kufikia level fulani ..
Iko hivi hata ma babu zetu Enzi hizo waliimba nyimbo hizo kitambo mpaka sasa kuna baadhi ya wasanii wanazirudia Tungo hizo..
Kwahiyo Takwimu ama Dunia inavyokwenda kutokana na karne zinavyokwenda na kubadilika kila kunapoitwa leo , kwahiyo haiwekani tu , kwa mfano kuna mazingira fulani kwenye jamii zetu ambayo hapo mwanzo yalionekana kama ni mapori lakini kwa sasa ni mjini ( town) kwa sababu Gani, jibu ni kwamba karne inazindi kukua , technologia inaongezeka na idadi pia ya watu pia vile vile inaongezeka ..
Na hata muziki nao pia unaenda hivyo hivyo huwezi kantu kustack na muziki huo huo miaka na miaka ,
Nikisema muziki kama wa Dully sykes maybe salome sijui nyambizi au nyimbo kama za professor jay wimbo kama zali la mentali ama juma nature wimbo kama vile sitaki dem nk.
Muziki unaenda na sio kwamba hizo nyimbo nimekutajia hazina maana hapana!!
Ni muziki mzuri ambao hata leo ukiuplay utafurahi na kuenjoy kwa wale wachache wanaoelewa..
Kwahiyo muziki ndio unavyokwenda hata Hawa wasanii tunawaita "new Generation" nao baada ya miaka 5 au 10 huko mbeleni nao watakuja kuongelewa hivyo hivyo...
Kwa mfano Taifa kama Afrika ya kusini muziki wao mkubwa Enzi hizo ulikuwa ni muziki aina ya "kwaito" lakini kwa sasa Afrika ya kusini Wana aina nyingine ya muziki inayofahamika kwa jina la "Amapiano" muziki ambao umeenea Dunia kote mpaka sasa hivi...
Kadri siku zinavyokwenda nao watakuja na Aina nyingine ya muziki kutokana na nyakati ama muda KWA kipindi hicho huko mbeleni tutakuja kushuhudia kama Mungu ataendelea kutupa pumzi ..
Sisi hapa Tanzania tuna muziki aina ya Bongo fleva kwenye hiyo Bongo fleva kuna majina mengine pia utakuta labda Arabic , bey bunda commercial na vitu vingine kama hivyo..
Siwezi kuzungumzia kwanini wasanii wa sasa Wana hit Kwa maana ndio muda wao sasa.
Kwa mfano msanii kama mr nice na style yake ya uimbaji iliyojulikana kwa jina la "tekeu style" kwa kipindi kile kulikuwa hakuna aina nyingine ya muziki zaidi ya "tekeu style" ambao ulikuwa unasikilizwa hapa Bongo Enzi hizo..
Mpaka wakaja kina marehemu mez b Mungu amlaze pema nao wakataka kuingia huko huko kwenye "tekeu style" nyimbo kama "kikuku" nk
Maana yangu mimi kila jambo au kitu kina muda wake hususani maybe muziki kama Bolingo ,
Enzi hizo zilikuwepo band za muziki wa Dansi kama vile twanga pepeta , kina mwinjuma kina banza stone
Walisumbua sana soko la muziki hapa Tanzania .
Ikafika hadi mahala bongo fleva ikawa haisikiki kabisa..
Lakini kwa sasa hivi kitu kama hicho hakuna .
Wakaja waimbaji wa nyimbo za Taarabu kina mzee yusupuh na kundi lake la jahazi, 5 stars na makundi mengi ya Taarabu nayo pia yalisumbua soko la Muziki Tanzania kwa nyakati tofauti tofauti..
Kama msanii saida karoli Enzi hizo sijui ule muziki wake ulikuwa unaitwaje
Lakini ni Aina ya muziki ambao hata leo ukiamua kuufanya ndio maana hata msanii kama Diamond aliufanyia muziki wa saida karoli kupitia ule wimbo wa "chambua kama kalanga"
Kwahiyo ni inshu ya timeming tu ya generation iliyopo kwa sasa , kwa mfano hata mimi nyimbo yangu kama kizizi mpaka leo namshukuru mumgu kila mmoja Bado anausema muziki huo ni mzuri kuanzia beat ( instrumental) maandishi ( lycris) zinaeleweka hata mtu mzima anaweza kusikiliza wimbo huo ...
Kwahiyo hata mimi kupitia wimbo ule ule naweza kufanya maamuzi ya kumchukua msanii kama vile mario au ndugu yangu alikiba tufanye muziki ama rmx kama alivyofanya diamond wimbo wa mr blue mapozi ..
Unakuwa una switch nyimbo zako kutokana na uhutaji wa generation iliyopo kwa wakati huo , kwa sababu muziki walaji wa kwanza ni Huwa ni sehemu za starehe kama club , bar .
Kwenye suala la Haki miliki linatokana na muhisika mwenyewe , kwa maana ya msanii mwenyewe jinsi ya ufuatiliaji wa Haki zake Enzi za uhai zilikuwaje? Je? Zilikuwa sehemu husika je marehemu alifuata Taratibu zake , inshu za usajili ili kutambulika kama msanii na kupata Haki miliki ya Kazi zake sanaa..
Inshu ya mambo ya Haki miliki ni inshu ya private baina yake na mamlaka husika kama Basata kujiandikisha na kutambulika nk..
UKWAJU WA KITAMBO
0767 542 202