pole jamani...... ila ni tabia mbaya sana, cha\fu kabisa... tena ya kufisha... ya kutia kinyaaa sana. janani!!!!!!!!!!! """NA ALAANIWE ALALAYE NA UMBU LAKE, BINTI YA BABAYE, AU BINTI YA MAMAYE. NA WATU WOTE WASEME, AMINA. Kumbukumbu la Torati 27:22""" ukiweza waweza kusoma sura nzima ya 27. au tena ngojeni::: HII HAPA JAMANI SIO MIMI MSIJESEMA NIMETUNGA BURE:-
Madhabahu katika Mlima Ebali Mose na wazee wa Israeli wakawaagiza watu: Yashikeni maagizo haya yote ninayowaagiza leo. 2Mtakapokuwa mmevuka mto Yordani na kuingia katika nchi awapayo BWANA Mungu wenu, msimamishe mawe makubwa na mkayatie lipu. 3Andikeni juu yake maneno yote ya sheria hii wakati mtakapokuwa mmevuka na kuingia katika nchi awapayo BWANA Mungu wenu, nchi itiririkayo maziwa na asali, kama vile BWANA Mungu wa baba zenu, alivyowaahidi. 4Mtakapokuwa mmevuka Yordani, simamisheni mawe haya juu ya Mlima Ebali, kama ninavyowaagiza leo, mkayatie lipu. 5Huko mjengeeni BWANA Mungu wenu madhabahu, madhabahu ya mawe. Msitumie kifaa cho chote cha chuma juu yake. 6Jengeni madhabahu ya BWANA Mungu wenu kwa mawe ya shambani na mtoe sadaka za kuteketezwa juu yake kwa BWANA Mungu wenu. 7Toeni sadaka za amani juu yake, mkizila na kufurahia mbele za BWANA Mungu wenu. 8Nanyi mtaandika juu yake kwa wazi sana maneno yote ya sheria hii juu ya mawe haya ambayo mmesimamisha.
Laana kutoka Mlima Ebali.
9Kisha Mose na makuhani, ambao ni Walawi, wakawaambia Israeli wote, Nyamaza Ee Israeli, sikiliza! Sasa umekuwa taifa la BWANA Mungu wako. 10Mtii BWANA Mungu wako na kufuata amri zake na maagizo ninayokupa leo.
11Siku ile ile Mose akawaagiza watu:
12Mtakapovuka mto Yordani, makabila haya yatasimama juu ya Mlima Gerizimu kubariki watu: Simeoni, Lawi, Yuda, Isakari, Yosefu na Benyamini. 13Makabila haya yatasimama juu ya Mlima Ebali kwa kutamka laana: Reubeni, Gadi, Asheri, Zabuloni, Dani na Naftali.
14Nao Walawi watawasomea watu wote wa Israeli kwa sauti kubwa:
15Alaaniwe mtu afanyaye sanamu ya kuchonga au mwenye kusubu sanamu, kitu ambacho ni chukizo kwa BWANA, kazi ya mikono ya fundi stadi na kuisimamisha kwa siri.
Kisha watu wote watasema,
Amen!
16Alaaniwe mtu amdharauye baba yake na mama yake.
Kisha watu wote watasema, Amen!
17Alaaniwe mtu asogezaye jiwe la mpaka wa jirani yake.
Kisha watu wote watasema,
Amen!
18Alaaniwe mtu ampotoshaye kipofu njiani.
Kisha watu wote watasema,
Amen!
19Alaaniwe mtu apotoshaye haki ya mgeni, yatima au mjane.
Kisha watu wote wataseme,
Amen!
20Alaaniwe mtu akutanaye kimwili namke wa baba yake, kwa maana anadharau malazi ya baba yake.
Kisha watu wote watasema,
Amen!
21Alaaniwe mtu akutanaye kimwili na mnyama ye yote.
Kisha watu wote watasema,
Amen!
22Alaaniwe mtu akutanaye kimwili na dada yake, binti wa baba yake au binti wa mama yake.
Kisha watu wote watasema,
Amen!
23Alaaniwe mtu akutanaye kimwili na mama mkwe.
Kisha watu wote watasema,
Amen!
24Alaaniwe mtu amwuaye jirani yake kwa siri.
Kisha watu wote watasema,
Amen!
25Alaaniwe mtu apokeaye rushwa ili kumwua mtu asiye na hatia.
Kisha watu wote watasema,
Amen!
26Alaaniwe mtu ambaye hatashika maneno haya ya sheria hii kwa kuyafanya.
Kisha watu wote watasema,
Amen!